Home »
» UONGOZI DOREFA WAAGIZWA KUFUTILIA MAENEO YALIYOTENGWA KWAJILI YA MICHEZO
UONGOZI DOREFA WAAGIZWA KUFUTILIA MAENEO YALIYOTENGWA KWAJILI YA MICHEZO
Na Kadala Komba Dodoma
Wanamichezo nchini waaswa kupambania tasnia ya michezo ikiwa ni agenda ya kuhakikisha tasnia hiyo inapewa thamani na kipaumbele kama sekta zingine.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa michezo Nchini Ndg.Ally Mayai Tembele wakati akizungumza na wadau wa soka kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mpira wa miguu jijini Dodoma(DOREFA) uliofanyika ukumbi wa dear mama hotel.
Mayai amesema kuwa ili tasnia hii ya michezo iendelee kukua ni wajibu wa kila mwanamichezo kuwajibika kwa nafasi yake na hii itasaidia kukua kwa tasnia hii bila kusahau kuwa na nidhamu kwa kila mmoja kumuheshimu mwenzake bila kujali cheo.
Nawapongeza chama cha soka cha Mkoa wa dodoma kwa kuweza kufanya kazi bila kuwa na tofauti katika utendaji na hii itasaidia soka la Dodoma kuweza kukua kwa kasi kwani maendeleo bora huletwa na viongozi bora"Amesisitiza Ndg.Mayai
Aidha ameongeza kuwa anawapongeza Dodoma kwa kuwa na programu ya vijana chini ya miaka 20 kwani itawasaidia vijana kukua kisoka na kuweza kuvumbua vipaji wakiwa bado na umri mdogo.
"Milango ya serikali ipo wazi kwa yeyote mwenye nia njema na tasnia hii na tunawakaribisha wadau wote kuweza kujitokeza kusapoti vipaji vya watoto wetu kwani kila mtu anaelewa mpira ni ajira kwa ajili ya kukuza uchumi na kuondokana na umasikini na kila mtu ameshuhudia namna ambavyo familia nyingi zimejikwamua kiuchumi kupitia michezo"
Aidha ametoa rai kwa wadau wa mpira wa miguu kuingia mitaaani kwenda kusaka vipaji,kwani huko ndiko kwenye chimbuko la mpira wa miguu na hata historia ya watu wengi maarufu waliofanikiwa kwenye soka historia yao inaonyesha wametokea mitaani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu jijjni Dodoma (DOREFA) amesema kuwa anawashukuru wadau wa soka jijini hapa kwa kuendelea kutoa maoni na ushauri ili kuhakikisha wanaboresha sekta ya michezo haswa mpira wa miguu jijini Dodoma.
Naye mwakilishi wa wanamichezo jijini Dodoma amesema sekta ya michezo iko vizuri ila wanaiomba serikali chini ya Waziri wa michezo Mohamed Ncheregwa kutatuliwa changamoto inayojitokeza mara kwa mara ya uwanja wa jamuhuri kufungiwa mara kadhaa kutokana na matumizi mengine ambayo ni tofauti na michezo hivyo kufanya wapenzi wa soko jijini hapa kukosa burudani ya mpira wa miguu na kutumia viwanja vingine vilivyopo nje ya Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa michezo Nchini Ndg.Ally Mayai Tembele wakati akizungumza na wadau wa soka kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mpira wa miguu jijini Dodoma(DOREFA) uliofanyika ukumbi wa dear mama hotel.
mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu jijjni Dodoma (DOREFA)Mohamed All Akiwashukuru wadau wa soka kwa kuendelea kutoa maoni na ushauri
MATUKIO YA PICHA ZA WAJUMBE MKUTANO MKUU NA WAALIKWA
PICHA YA PAMOJA MGENI RASMI NA WAJUMBE WA SOKA
Related Posts:
BILIONI 1.7 ZIMETUMIKA KUJENGA BWENI LA WANAFUNZI WA KIKE Na. Moreen Rojas, Dodoma.Taasisi ya Afrika ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela inadhamiria kupendekeza ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike wenye watoto wadogo na mahitaji maalum ambapo kiasi cha shilingi bili… Read More
BAHI YAFUNGUA MILANGO KWA WANAFUNZI WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU. Na Kadala Komba- Dodoma Diwani wa Kata ya Mpamatwa, Sosthenes Mpandu amewataka wanafunzi kusoma kwa juhudi na kujiamini ili kufanya vizuri katika mitihani yao hatimaye waweze kujiunga na masomo ya elimu ya juu.… Read More
ULAJI WA VYAKULA VYENYE SUMUKUVU UNAVYOATHIRI AFYANa mwandishi wetu , SimiyuMADHARA ya sumukuvu huweza kujitokeza ndani ya muda mfupi, baada ya muda mrefu kutegemea na kiasi cha sumukuvu hiyo iliyopo kwenye chakula kilicholiwa,idadi ya milo ya chakula kilichochafuliwa… Read More
NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAJI ATEMBELEA MKOA WA KIGOMA Na Mwandishi wetu Kigoma Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma. Mradi huu unatumia ziwa Tanganyika kama chanzo cha maji, katik… Read More
JUMUIYA YA MARIDHIANO YAMTUNUKU RAIS SAMIA TUZO YA HESHIMANa. Kadala Komba DodomaJUMUIYA ya Maaridhiano mkoa wa Dodoma imemkadhi Tuzo Rais Samia Suluhu Hassani,kutokana na kuutambua mchango wake mkubwa wa kuiongoza nchi pamoja na Watanzania kwa amani. Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu … Read More
0 Comments:
Post a Comment