Na Mwandishi Wetu- Kilimanjaro
Wazazi
na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha watoto wao waliofikia umri wa
kwenda shule wanapelekwa ili kupata elimu itakayowawezesha kuwa
wataalam wa fani mbalimbali pamoja na kutimiza ndoto zao.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Kilimanjaro, Patrick Boisafi wakati akizungumza katika mkutano wa
hadhara Kata ya Mroe, Jimbo la Same Mashariki ikiwa ni ziara yake katika
Jimbo hilo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.
Mwenyekiti
huyo amesema baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakizuia watoto wao
kwenda shule huku wanaume wakitumikishwa katika shughuli za kilimo au
kuchunga ng’ombe na wale wa kike wakilazimishwa kuolewa.
“Wazazi
na walezi pelekeni watoto shule Serikali inahitaji wataalam wengi zaidi
katika fani mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, barabara na
nyinginezo. Pia mkumbuke juhudi hizi zinafanywa na Rais wetu Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan ili kila mtoto apate elimu bora na ni sehemu ya
utekelezaji wa Ilani ya Chma chetu,”Amesema Mwenyekiti huyo.
Vilevile
amewasisitiza wanafunzi kuepuka vishawishi kwa kuwa na msimamo,
kutojihusisha na makundi mabaya hatua itakayowafanya kushindwa kutimiza
ndoto zao na hatimaye kujiingiza katika matendo ya uhalifu na kuzalisha
jamii tegemezi.
“Msikubali
kukatishwa tamaa na marafiki wabaya, watoto wakike wapewe fursa ya
kusoma watimize ndoto zao hapo tutapata wakurugenzi, madaktari, Mawaziri
msiwafanyie hayo mnayoyafanya ni machukizo mbele ya Chama, Serikali na
hata Mwenyezi Mungu,”Ameeleza.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti huyo ametoa kadi za Chama kwa baadhi ya
wanachama waliorudi CCM wakitoka katika vyama vingine wakisema lengo la
kufanya uamuzi huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu
ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ummy Nderiananga amesema
Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya
maendeleo ambayo iko ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na
kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kukuza uchumi wa Taifa.
“Sisi
Serikali kupitia Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaendelea
kutekeleza ilani na niwahakikishie kazi inaendelea vizuri hakuna
kitakachosimama, tunafanya kazi usiku na mchana kwa sababu nyinyi
wananchi ndiyo mmetupa kazi. Pia niwatoe hofu mnapoona wageni wanakuja
kuwekeza nchini ni kutokana na mahusiano mazuri aliyonayo Rais wetu na
Nchi zingine na wadau wa maendeleo,”Amefafanua Mhe. Ummy.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anna Kilango amebainisha kwamba
Serikali inaendelea kuboresha miradi mikubwa ya maji akisema kuwa licha
ya changamoto kubwa ya maji katika Jimbo la Same Mashariki bado Serikali
ina nia njema ya kumtua ndoo mama kichwani ili wananchi wake waendelee
kufanya shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi.
“Nikiri
Jimbo langu linakabiliwa na uhaba wa huduma muhimu ya maji lakini bado
Serikali haijatuacha inatoa fedha za kuboresha miundo mbinu ya maji
hatua itakayosaidia wananchi wangu wa Same Mashariki kufanya kazi zao
kwa amani. Pia tunamshukuru sana mama kwa kuendelea kupigania na
kuhubiri amani katika Nchi yetu,”Amepongeza Mbunge huyo.
Aidha
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro, Adam Simba amehimiza
kufanywa kwa ufuatiliaji wa karibu wa miradi inayofanya na Serikali ili
kubaini hatua iliyofikiwa, changamoto na namna ya kuzitatua kwa
maendeleo ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick
Boisafi akizungumza katika mkutano wa hadhara Kata ya Mroe, Jimbo la
Same Mashariki ikiwa ni ziara yake katika Jimbo hilo akiwa ameongozana
na Kamati ya Siasa ya Mkoa huo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani
ya Chama hicho.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Maore na Kata ya Mtii katika Jimbo la Same
Mashariki mkoani Kilimanjaro wakisikiliza mkutano wa hadhara wakati wa
ziara ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro,
Patrick Boisafi pamoja na Kamati ya Siasa ya Mkoa.
.jpg) |
| Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ambaye pia ni
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ummy Nderiananga akisalimiana na wananchi wa
Kata ya Maore katika Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro wakati
wa ziara ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa huo Patrick
Boisafi. |