Na Moreen Rojas
Dodoma.
OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa idadi ya Watalii kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Agosti Mwaka 2023 imeongezeka na kufikia 1,131,286 ikilinganishwa na Watalii 900,182 walioingia kwa kipindi kama hicho Mwaka Jana sawa na ongezeko la asilimia 25.7
Mkurugenzi wa Takwimu za uchumi kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)DANIEL MASOLWA ameyaelwza hayo Oktoba 9 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema ongezeko hilo limechagizwa na filamu ya Royal tour alayoifanya Mhe Rasi Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN.
Aidha amebainisha kuwa kati ya Watalii wote waluoingia nchini katika kipindi hicho,Watalii236047 waliingia nchini kupitia Zanzibar ambao ni sawa na asilimia 31.1 ya Watalii wote.
"Watalii walioingia Nchini Mwezi Agosti Mwaka 2013 p3kee wqliongez3ka hadi 186,030ikilinganishwa na Watalii158,049walioingia nchini MwwziAgosti2022 sawa na ongezeko la asilimia 17.7,"Amesema Masolwa
Pamoja na hayo,Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa Wataluu 336203kati ya Watalii wote walioingia Nchini Mwezi Agosti Mwaka 2023 waliingia kupitia Zanzibar sawa na asilimia 29.7ya idadi ya Watalii wote.
Akielezea Watalii walioingia Nchini kwa mchanganuo wa Utaifa,Januari hadi Agosti kutoka nje ya Bara la Afrika Januari hadi Agosti walitoka Marekani ikiwa ni watalii84541.
"Nchi nyingine zilizokuwq na idadi kubwa ya Watalii ni Ufaransa72,009,Ujerumani watalii57798,Uingereza Watali51,505 na Italia walikuwa Watalii 51056,"Amesema
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo amesema kuwq katika kipindi cha Januari hadi Agosti2023 Tanzania ilipokea Watalii kutoka katika Bara la Afrika ambapo idadi kubwa ya Watalii walitokw Kenya128,753,Burundi walikuwa 12319,Zambia 6,649,Rwanda5,124 na Uganda 4,052
MWISHO
Home »
» IDADI YA WATALII KUTOKA NJE YA NCHI IMEONGEZEKA.
0 Comments:
Post a Comment