Subscribe Us

RC SENYAMULE TUMEJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema azima ya Serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto za wananchi na kuleta maendeleo kwa watu wake.

Mhe.Senyamule ameyasema hayo alipotembelea Kijiji cha Mpwayungu kilichopo katika Wilaya ya Chamwino ikiwa ni katika utaratibu aliojiwekea wa kusikiliza kero za wananchi wa Dodoma ambapo amebaini changamoto mbalimbali za Wananchi hao ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme, na Barabara. Mhe. Senyamule amezipokea kero hizo na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kuja hapa leo ni kuhakikisha matamanio ya Rais wetu yanatimia kwa kusikiliza changamoto mlizonazo na kuzipatia ufumbuzi na zinazo muhusu yeye  kuziwasilisha kwake kwa ajili ya utekelezaji " amesema Mhe. Senyamule

Katika Hatua nyingine, akiwa katika mradi wa mashamba ya pamoja ya  'Bulding a Better Tomorrow '(BBT), ametoa shime kwa  wasimamizi wa mradi huo kuchukua hatua kwa Changamoto zinazojitokeza zinazopelekea  mradi huo kutokwenda kwa kasi iliyokusudiwa.

"Hakikisheni tarehe ambayo imepangwa kwa  kazi hii kuwa tayari inatimia ,hivyo basi fanyeni utaratibu wa kuweka mashine za  kufyatulia matofali sehemu ya mradi ifikapo Jumatano, mashine ziwe sehemu ya kazi ,pia ongezeni nguvu kazi ili kusadia mradi ukamilike kwa wakati "Amesisitiza Mhe. Senyamule

Kwa Upande Wake, Mkuu wa Wilaya ya chamwino Mhe. Gift Msuya, amemshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kufanya mambo ya maendeleo katika Tarafa ya Mpwayungu pamoja na mradi wa Kilimo cha pamoja, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Nkhambako na mengine.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambapo ziara hiyo ametembelea mradi wa Mashamba ya Kilimo cha pamoja, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Nkhambako na kusikiliza changamoto za wananchi wa tarafa ya Mpwayungu na kuzipatia ufumbuzi.


0 Comments:

Post a Comment