This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
*WIZARA YA KATIBA KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA KIDIJITALI – DKT NDUMBARO*
ASKOFU KINYAIYA "WAZAZI PELEKENI WATOTO SHULE"
RAIS SAMIA ATEMBELEA JENGO LA MAKUMBUSHO YA HAYATI DKT.JOHN POMBE MAGUFULI,AKAGUA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA CHATO MKOANI GEITA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua kwenye Kaburi la Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
KAMPASI YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUJENGWA KAGERA-WAZIRI MKENDA
Na Mathias Canal, WEST-Kagera
Katika kuboresha huduma za upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi nchini Serikali imepanga kujenga Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Mkoani Kagera.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema hayo mbele ya Mgeni rasmi-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan tarehe 13 Octoba 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera.
Amesema kuwa Kampasi hiyo itajengwa kwenye vijiji vya Itahwa na Kangabusharo kwenye eneo la ekari 323.45. Kati ya ekari 323.45 zilizotolewa, ekari 231.36 ziko katika kijiji cha Itahwa na ekari 92.09 katika kijiji cha Kangabusharo.
Akizungumza kuhusu Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera, Waziri Mkenda amesema chuo hicho chenye hadhi ya Kimataifa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa thamani ya Yuani za Kichina Milioni 60.18 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 22.4, Fedha hizo zinajumuisha shughuli za ujenzi, uwekwaji wa baadhi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia, mashine na samani katika majengo.
Waziri Mkenda amesema kuwa Chuo hicho chenye karakana, vifaa na miundo mbinu ya kisasa kilichojengwa kwa msaada wa Serikali ya China kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma.
Waziri Mkenda amesema kuwa Chuo hicho cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera kilichozinduliwa na Mhe Rais ni hatua nyingine muhimu katika mpango wa kukamilisha ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya ngazi ya Mikoa.
“Mheshimiwa Rais Tulibakisha mikoa michache sana. Kwa sasa, mikoa mingine ambayo ujenzi unaendelea ni Njombe, Simiyu, Rukwa na Geita na mpango wa ujenzi wa chuo cha Mkoa wa Songwe unaendelea kukamilishwa ili ujenzi uanze” Amekaririwa Prof Mkenda
Prof Mkenda amesema kuwa serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya ngazi ya wilaya ambavyo hadi sasa Wilaya 77 zina vyuo na ujenzi wa vyuo katika Wilaya 62 unatarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha 2022/23 ambapo Serikali imetenga shilingi bilioni 100.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
UZINZI NA UASHERATI NI VYANZO VYA VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA KWENYE MAISHA YA MTU
SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA ULINZI NA UFUATILIAJI MIENENDO YA WANYAMAPORI
Na. Mwandishi wetu Morogoro
![]() | |||
BODI YA MAZAO MCHANGANYIKO NCHINI [CPB] IMEWATOA HOFU WAKULIMA WA MAZAO YA KUNDE
Na. Mwandishi wetu Simiyu
Bodi ya mazao mchanganyiko nchini (CPB) imesema kuwa wakulima nchini wenye mazao aina ya kunde, hawana sababu ya kuhangaika na soko la mazao yao kwani Bodi hiyo inao uhitaji mkubwa wa mazao hayo.
Ofisa Masoko wa Bodi hiyo Frank Bubelwa Akizungumza katika maonyesho ya wiki ya Chakula nchini yanayoendelea Mkoani Simiyu, amesema kuwa wakulima hawana sababu ya kuangaika na kutafuta wapi watauza mazao yao. Amesema serikali kupitia wizara ya kilimo, mazao na nafaka tumeona tuingie, tufungue milango kwa wakulima kwa kuweza kununua mazao yao yote ambayo wanalima na kuleta kwetu sisi inamaana kwa lugha nyepesi tunawasaidia kutoka katika changamoto ambayo walikuwa wananung’unika kupata masoko.
Aidha ameongeza kuwa mbali na Bodi hiyo kununua mazao kutoka kwa wakulima, bado bei ambazo wamekuwa wakinunulia mazao hayo ni rafiki kwa wakulima Lakini pia katika swala zima la bei za nafaka sisi kama taasisi sio taasisi kandamizi mkulima anapewa fursa na tunampa fedha inayoendana na bei ya sokoni mara nyingi wakulima wanakuwa na changamoto hiyo kubwa, unakuta mkulima anakuja kudalaliwa na mtu wakati kwa bei ya chini ambayo inamfanya yeye hasipate hamu au mtaji wake unaguswa kwaiyo anashindwa kufanya shughuli za kilimo. Sambamba na hilo afisa masoko Frank Bubelwaa amesema kuwa katika msimu wa kilimo bodi ya nafaka huwa tunaangalia pande zote mbili mkulima hasiumie pia sisi tusipate hasara kwaiyo mara nyingi tunanunua mali kutokana na bei iliyo sokoni kama kwamfano kilo moja ya mahalage ni silingi elfu mbili sokoni sisi tutakuja kununua kwa bei hiyohiyo hatuwezi tukashuka Zaidi ya hapo. Hivyo basi sisi tupo kwaajiri ya kuhakikisha kuwa kilimo kinaendelea kukua lakini pia kwaupande mwingine kuongeza uchumi wa nchi.
MIAKA 7 YA BMH: MKURUGENZI AELIMISHA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE
![]() |
WAZIRI WA SHERIA DKT DAMAS NDUMBARO AMETOA UFAFANUZI KUHUSU WANAFUNZI WA SHERIA KUFELI MAFUNZO KWA VITENDO































