Na. Anselima Komba Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema kuwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kupambana na rushwa zimeanza kuzaa matunda, ambapo Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika viwango vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji.
Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Waziri Simbachawene amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa Transparency International wa mwaka 2024, Tanzania imepata alama 41 kati ya 100 katika Corruption Perception Index (CPI) na kushika nafasi ya 82 kati ya nchi 180 duniani. Hii ni hatua ya kupanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 87 mwaka 2023, ambapo nchi ilipata alama 40.
“Tanzania imeendelea kushika nafasi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kiashiria hiki cha rushwa, jambo linalothibitisha juhudi za serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha sekta zote zinakuwa safi na zinatoa huduma bora kwa wananchi,” alisema Simbachawene.
Maboresho ya Sheria na Kuimarishwa kwa TAKUKURU
Waziri huyo pia alieleza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha misingi ya kisheria kwa kupitia upya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura 329, ambapo maboresho hayo yameongeza uwezo wa TAKUKURU kushughulikia rushwa kwenye michezo, michezo ya kubahatisha na uchaguzi wa kisiasa.
“Hii ni hatua kubwa sana kwa nchi yetu. Si kila nchi duniani imeweza kupanua wigo wa mapambano dhidi ya rushwa hadi maeneo haya. Ni jambo la kujivunia na linaonyesha dhamira ya dhati ya Serikali yetu,” alisema Waziri Simbachawene.
Kuimarishwa kwa Rasilimali na Miundombinu ya TAKUKURU
Katika hatua nyingine, Serikali imeboresha uwezo wa kiutendaji wa TAKUKURU kwa kuongeza rasilimaliwatu na fedha. Kati ya mwaka 2022 hadi 2024, Serikali imetoa vibali vya ajira 1,190 kwa taasisi hiyo, pamoja na kugharamia mafunzo ya weledi kwa watumishi wake.
Pia Serikali imewekeza katika ujenzi wa majengo ya ofisi za TAKUKURU katika Mikoa na Wilaya mbalimbali ili kuimarisha huduma kwa wananchi.
Hitimisho
0 Comments:
Post a Comment