Na. MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inalengo la uzalishaji endelevu wa kibiashara na wenye kuzingatia mazingira hususan uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji wa viumbe maji kwa kuzingatia uwezeshaji kinamama na ushiriki wa vijana.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara Mkoani Pwani ya kutembelea na kuona eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki na kuona utayari wa Halmashari na Jamii katika kupokea Mradi huo.
Aidha Waziri Ummy amesema Programu hiyo inatekelezwa katika Halmashauri 44 zilizo kwenye Mikoa 11 ya Tanzania Bara pamoja na Unguja na Pemba ambapo inatarajiwa kunufaisha watu takribani Milioni moja na laki 3 ikiwemo kaya za wakulima wadogo, wazalishaji wadogo na kati wa mbegu wafanyabishara wa pembejeo za kilimo, wavuvi wadogo, wafanyabiashara wa samaki na wafugaji wa samaki pamoja na viumbe maji (mwani).
"Lengo la kutembelea ni kukagua na kuangalia yale maagizo mahususi yakuendeleza kilimo tuliambiwa tuwe na ghala la chakula lakini nia ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ni maono yake kuwa Tanzania tuwe mstari wa mbele kwenye kilimo, uvuvi, uvuvi wa Bahari Kuu, uvuvi wa kisasa kwa vijana wetu ili kuendelea kutoa ajira lakini tunawaona waheshimiwa mawaziri na Manaibu na viongozi wote wa Wizara hizi mbili jinsi wanavyopambana kuhakikisha dhamira ya Mheshimiwa Rais inakamilika"."Alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Mussa Kunenge amesema katika Mkoa wake shughuli za uvuvi zinafanyika zaidi katika halmashauri za wilaya zilizopakana na bahari pia uwepo wa mabwawa ya asili unafanya Mkoa kuwa na Fursa kubwa ya Uvuvi.
"Katika Mkoa wa Pwani mazao makuu yatokanayo na Bahari, Mito na Mabwawa ni samaki, mwani na Dagaa, pia tunaanzisha ufugaji wa Jongoo bahari ekari nane katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na kwa mwaka 2022/2023 jumla ya kilo 612 zilivunwa na lengo la mkoa ni kuongeza uzalishaji hadi 1,200 kwa Mwaka hivyo tunawashauri watu wetu waacha mazoea na watafute biashara zilizo na tija kwao ." Alisema Mhe. Kunenge.
=MWISHO=
CAPTIONS
P1.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akiwa katika ziara yake Mkoani Pwani ya kutembelea na kuona eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki na kuona utayari wa Halmashari na Jamii katika kupokea Mradi huo unaotarajiwa kujengwa Bagamoyo Mkoani Pwani.
P 2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa ziara yake Mkoani Pwani ya kutembelea na kuona eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki na kuona utayari wa Halmashari na Jamii katika kupokea Mradi huo unaotarajiwa kujengwa Bagamoyo Mkoani Pwani.
P 3
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Mussa Kunenge akieleza namna Mkoa wake ulivyojipanga katika kukuza na kuendeleza mradi wa AFDP wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani).
P 4
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda wakati akiwasilisha Taarifa ya Mradi wa eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki linalotarajiwa kujengwa katika halamashauri hiyo.
P 5
Eneo ambapo ujenzi wa Vichanja vya samaki vitakapo jengwa katika halamashauri hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Home »
» PROGRAMU YA AFDP YALETA MATOKEO CHANYA SEKTA YA KILIMO UVUVI.
0 Comments:
Post a Comment