Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Shirika la Maendeleo la Kimataifa UNDP limezindua wazo la kibunifu la matumizi bora ya Nishati nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi 15,2024 jijini Dodoma Mtaalamu mshauri wa Shirika hilo Robert Washaija amesema kuwa mradi huu ni wa kimkakati kuhusu matumizi bora ya Nishati na unafadhiliwa na umoja wa Ulaya na Ubalozi wa Ireland na wanafanya kazi pamoja na Wizara ya Nishati.
Washaija amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha kwamba Tanzania kama nchi inakuwa na matumizi bora ya Nishati kwa sababu nishati ni kitu bora katika maendeleo ya viwanda
"Mradi huu kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na wafadhili wetu umoja wa Ulaya tunafanya Kazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Viwanda, Tunafanya Kazi na Shirika la Viwango Tanzania TBS, Tunafanya Kazi na Takwimu NBS, Tunafanya Kazi na taasisi ya elimu DIT na ni mradi ambao ni mpana sana na unalenga maeneo makubwa Sana"Amesema Washaija
Aidha amesema kuwa moja ya matunda ya mradi huo ni Kujenga uwezo nchini na kuwa na wataalamu wa kisasa ambao wataweza kutoa huduma mbalimbali pale zinapohitajika kuhusu matumizi bora ya Nishati,na kuzijengea uwezo Taasisi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake.
" Tunatambua kwamba eneo hili ni geni kwani tukianzia majumbani ni wengi wanapoteza nishati kwa kushindwa kutumia nishati kwa usanifu na kuweza kutumia nishati kubwa na kuipoteza kwani tungekuwa tunafuata matumizi bora ya nishati tusingekuwa na mgao wa umeme kama tungekuwa na matumizi rasmi ya umeme"Amesisitiza Washaija
Kwa upande wake Afisa Mahusiano (habari) wa UNDP Jolson Masaki amesema kuwa kwenye shindano hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati nchini wanalenga zaidi vijana wakike na wakiume wenye mawazo ya kibunifu yanayoenda kutoa mchango mkubwa katika kupunguza matumizi ya Nishati
"Ninaposema kupunguza matumizi ya Nishati ina maana kwamba kuna Nishati ambayo tunaitumia vibaya,sasa kupitia mawazo hayo ya kibunifu tutaenda kupokea maoni kutoka kwa Watanzania"Amesema Masaki
Aidha amesema kuwa ili uweze kushiriki katika shindano hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati kitu cha Kwanza lazima uwe na wazo la kibunifu ambalo linahusiana na matumizi bora ya Nishati,Lazima uwe Mtanzania na washindi kumi watachaguliwa ambapo katika hao washindi watapata Milioni Ishirini na tano kwa kila mmoja.
Ameongeza kuwa katika mawazo hayo ya kibunifu wanatazamia kupokea mawazo ambayo yanaweza kupunguza matumizi ya Nishati na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa yakiathiri nchi zetu.
Pia Masaki amesema kuwa wazo hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati ambalo limezinduliwa leo litakuwa ni la mda wa mwezi mmoja kuanzia leo Siku ya Uzinduzi hadi mwishoni mwa mwezi wa nne.
Kuhusu mwendelezo wa hili shindano la kibunifu la matumizi bora ya Nishati Masaki amesema kuwa huu mradi ni wa muda wa miaka mitatu.
Naye Mhandisi Collins Lwanga Kutoka Wizara ya Nishati amewaomba watanzania wote kuchangamkia fursa hii ya wazo la kibunifu la matumizi bora ya Nishati.
"Tumekuja kushuhudia uzinduzi wa shindano la wazo la kibunifu kuhusu matumizi bora ya nishati nchini ningependa kuwaalika watanzania wote kuweza kushiriki na kuendelea kubuni bunifu zenye tija kwani kila mmoja anatambua umuhimu wa sekta hii ya nishati"Ameongeza Lwanga
Home »
» UNDP YAZINDUA WAZO LA KIBUNIFU LA MATUMIZI BORA YA NISHATI NCHINI.
0 Comments:
Post a Comment