Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,DK.John Jingu amezindua mradi wa mzunguko wa saba wa Mfuko wa Dunia (Global Fund Circle7)ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia sasa kwaaijili ya kutokomeza Ukimwi,Kifua kikuu na Malaria nchini Tanzania ili kutokomeza Magonjwa hayo ifikapo Mwaka 2030.
DK.Jingu amezindua mradi huo,Machi 21 Jijini Dodoma, ambapo amewataka wanaotekeleza Mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza tija katika kutokomeza magonjwa hayo.
“Ni muhimu sana sisi ambao tunatekeleza Mradi huu kuhakikisha tunatumia fedha ambazo tumefadhiliwa na Mfuko huu wa Dunia kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuwa na huduma bora kwa Wananchi,”Amesema Dk. Jingu
Amefafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dk. Samia imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika Sekta ya afya kwa Lengo la kuboresha afya za Wananchi wake na Kuwataka watumishi hai kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa.
Kwa upande Wake,Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Dk.Tumaini Nagu amesema wapo kwaajili yakujipima na kuangalia walipotoka na walipo ili kufikia malengo ya Kidunia namba tatu kwa kutekeleza Strategic Plan ya afya namba tano.
“Serikali imeona umuhimu katika kutokomeza magonjwa haya ambayo ni Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria ili kuhakikisha inatokomeza magonjwa hayo ifikapo Mwaka 2030,”Amesema Profesa Nagu
Awali Mwakilishi wa Serikali ya Marekani ambao Pia wanatekeleza Mradi wa PEPFAR,GETRUDE TEMBA amesema wanatambua mchango wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Magonjwa hayo huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa umakini katika kuhakikisha rasilimali wanazopatiwa wanazitumia kwa usahihi.
MWISHO
Home »
» UKIMWI,KIFUA KIKUU NA MALARIA MBIONI KUTOKOMEZWA.
0 Comments:
Post a Comment