Subscribe Us

SERIKALI IMETIA SAINI YA MKATABA WA UPEMBUZI YAKINIFU

 Na Moreen Rojas,
Dodoma


Serikali imetia saini ya mkataba wa upembuzi yakinifu na ununuzi wa meli za uvuvi wa bahari kuu na ujenzi wa viwanda viwili vya kuchakata samaki(kilwa na  fungurefu)kupitia programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi itakayogharimu jumla ya Dola za kimarekani 77.4 millioni.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa shughuli za Serikali wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Salimu Mwinjaka wakati wa utiaji saini wa hafla hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Ngome jijini Dodoma.

Aidha programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi (AFDP)ni programu ya miaka 6 kuanzia 2021/22 hadi 2027/28 na itagharimu jumla ya Dola za kimarekani 77.4 milioni,kati ya fedha hizo,Mkopo toka IFAD ni Dola za Marekani millioni 58.8,Serikali Dola za Marekani milioni 7.8,Sekta binafsi Dola za Marekani milioni 8.5 na Wananchi Dola za Marekani millioni 2.4.

"Lengo kuu la programu ni kuwa na uzalishaji endelevu wa kibiashara na wenye kuzingatia mazingira hususani uzalidhaji wa mbegu za mazao ya kilimo(Mahindi,Alizeti,Maharagwe na Mimea jamii ya mikunde),uvuvi na ufugaji wa viumbe maji,ukizingatia uwezeshaji wakinamama na ushiriki wa vijana,programu hii inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu(SBU) na kutekelezwa na Wizara ya mifugo na Uvuvi,Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi_Zanzibar kupitia Taasisi ambazo ziko chini ya Wizara hizo ikiwa ni pamoja na TAFICO,ZAFICO,Wakala wa mbegu _ASA,Taasisi ya utafiti wa kilimo,Tanzania TARI,na Taasisi ya udhibiti wa ubora wa mbegu_TOSCI"

Aidha ameongeza kuwa programu inatarajia kuwanufaisha watu takribani 1,300,000 ikiwemo kaya za wakulima wadogo 200,000 ambao watakuwa wanapata mbegu bora za mahindi,alizeti na maharage,wazalishaji wadogo na kati wa mbegu na wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo takribani 1,000 ambao watapata mbegu bora na mafunzo,wavuvi wadogo na wafanyabishara wa samaki takribani 48,000,na wafugaji wa samaki na viumbe maji pamoja na mwani 21,000 .

"Programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi inatekeleza sehemu ya Ilani ya chama cha mapinduzi ambapo imesema wazi kuwa Serikali inakusudia kununua meli name(8) kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu ikijumuisha meli 4 kwa ajili ya TAFICO na Meli nyingine 4 kwa ajili ya ZAFICO,meli hizi zinakusudia kutumia jumla ya Tsh 30,413,275,427.00 ambapo zitanunuliwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza kutakuwa na meli tatu(3) na meli tano(5) zilizobakia zitanunuliwa katika awamu ya pili,meli hizi zinakusudiwa kuendeshwa kwa njia ya PPP"

Aidha Serikali ya Muungano wa Tanzania(SMT) na mfuko wa kimataifa wa kilimo Duniani (IFAD) zimekubaliana maeneo muhimu ya msingi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa kina kabla ya ununuzi/ujenzi wa meli hizo,maeneo hayo ni pamoja na (i)Tathmini ya athari ya kimazingira na kijamii(ESIA)kwa meli ambazo zitavua katika Bahari kuu na (ii)upembuzi yakinifu wa meli za uvuvi na bahari kuu,kazi zote hizi mbili nilazima zikamilike ndipo ununuzi /ujenzi wa meli uweze kuanza.

Sanjari na hayo upembuzi yakinifu wa awali tayari umefanyika na kubainisha kuwa meli hizi za uvuvi zitaleta tija kwenye uchumi,litaongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa,kuboresha lishe na kipato kwa wananchi mmoja mmoja hususani wale ambao wapo katika eneo la mradi,upembuzi yakinifu wa awali pia umependekeza meli hizo ziwe na urefu mita 26,hata hivyo ili kujiridhisha na matokeo haya ya awali kumekuwepo na haja kubwa na upembuzi yakinifu kamili ambapo kandadasi yake Leo ndio inategemewa kuingia mkataba na mkandarasi DMG Ltd.

"Katika eneo la upembuzi yakinifu linalenga zaidi kuangalia faida na hasara za uwekezaji tunaokusudia kwani tayari urefu wa meli Serikali imeamua uwe ni kuanzia mita 25 kwa kuangalia urefu wa meli ambazo zinavua katika EEZ yetu kutokana na Takwimu za DSFA,hivyo feasibility study itajikita zaidi kwenye kuangalia hasara na faida financial modeling kama PPP Act inavyoelekeza,hata hivyo SMT na IFAD zinekubaliana kuwa urefu wa meli maamuzi yanafanyika kupitia feasibility study ambapo pia itapendekeza msawazo wa meli pamoja na kutoa Hadidu za rejea zitakazotumika kutafuta mshiriki katika kuendesha meli hizo kwa njia ya PPP"


Kwa upande Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na UratibuDkt.Jim Yonazi  programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ni ya kimkakati katika kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi, hivyo, katika zoezi hili la upembuzi yakinifu walatalisimamia kwa karibu ili kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi unaotakiwa ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zote zitakazojitokeza.

" Mkataba huu tunaoingia leo utatekelezwa kwa muda za siku zisizozidi 45 kwa gharama ya Shilingi milioni 348, ni mategemeo yangu kuwa mtafanya kazi hii kwa weledi mkubwa na kumaliza kwa wakati"Amesisitizi Dkt.Yonazi


"Ninawasihi kuwa, wakati wa utekelezaji wa zoezi hili la Upembuzi Yakinifu, mara mtakapopata changamoto yoyote, tafadhali msisite kuwasiliana na ofisi yangu kwa utatuzi wa haraka ili tuweze kukamilisha zoezi ndani ya muda tuliokubaliana, kukamilika kwa upembumbuzi yakinifu kwa wakati kutawezesha Serikali kuanza taratibu za ujenzi wa meli za uvuvi katika bahari kuu pamoja na viwanda vya kuchakata samaki,ni matarajio yetu kuwa hamtachelewesha utaratibu huo kuanza kwa wakati"Ameongeza Dkt.Yonazi




0 Comments:

Post a Comment