Na Moreen Rojas,
Dodoma
Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda ameiomba Serikali kupunguza bei ya Nishati ya gesi ili wanawake Waweze kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa kwenye shughuli za mapishi.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo leo Machi 9 , 2024 kwenye kongamano la wanawake la ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia jijini Dodoma,ambapo amesema sasa wanawake wanakwenda kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa hali itakayopelekea utunzaji wa mazingira katika jamii.
Amesema Bei ya Nishati safi ya Gesi ya kupikia ikipungua tofauti na ilivyo kwa sasa basi wananchi wengi wakiwemo wanawake wataweza kununua majiko na kuachana na Matumizi hatarishi ya kuni.
"Bei ya gesi ikipunguzwa madukani wanawake watakuwa na uwezo wa kununua kila yanapoisha na yatakuwa yanatumika nasio kuwa mapambo majumbani kwetu kama ilivyo sasa," Amesema
Na kuongeza " Ninaimani baada ya kongamano hili wanawake wote tuna kwenda kuwa mabarozi wazuri juu ya Matumizi ya mishati safi ya kupikia na sio kuni na mkaa, " Amesema Komredi Chatanda
Aidha amewapongeza waandaaji wa kongamano hilo ambao ni wizara ya Nishati kwa kuwaalika wanawake zaidi ya 10,000 kutoka mikoa tofauti tofauti na kuwapatia elimu na vitendea kazi vya nishati.
"Tunashukuru kwa elimu,mitaji na vitendea kazi kwani tupo kwenye maadhimisho ya wiki ya wanawake tunashukuru kwa kutukumbuka wanawake, "Amesema Chatanda
Na kuongeza "Na sisi tunaahidi Kwenye ziara zetu za Kata kwa Kata tunakwenda kuhamasisha matumizi sahihi ya gesi safi ya kupikia na wanawake wote kuachana na kuni ili kutunza mazingira kwani kunamsemo usemao mwanamke ni mazingira CCM hoyeeee, "Amesema
Amesema serikali imeongeza bajeti mwaka wa fedha 2023/24 ambapo fedha hizo za ruzuku ziliweza kusaidia makampuni ya usambazaji wa gesi kusambaza Nishati hiyo kwa Baraka na wepesi hadi pembezoni.
Hata hivyo kufuatia fedha hizo aliyataka makampuni hayo kwenda kusimamia makubaliano waliokubaliana na serikali kwa kuhakikisha Nishati hiyo inamfikia kila mtu Hali itakayosaidia kumtua mzigo wa kuni mama kichwani.
Mwisho
Home »
» SERIKALI IMEOMBWA KUPUNGUZA BEI YA NISHATI YA GESI YA KUPIKIA.
0 Comments:
Post a Comment