Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Rais wa UTPC Deogratius Nshokolo amesema katika kipindi cha 2023_2025 UTPC inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya wanachama na wadau wengine wa habari nchini.
Rais wa UTPC ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi na mpango mkakati wa UTPC kwa mwaka 2023_25 jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania Ms.Charlotta Ozak .
Aidha amesema kuwa wadau wa habari nchini ni pamoja na vyombo vya habari,taasisi za habari,asasi za kiraia na serikali,ili kufanya kazi pamoja kufanikisha malengo kwa ufanisi zaidi.
"Ni vyema nikatumia nafasi hii kutoa wito kwa wanachama wa UTPC(Press Clubs) kote nchini kuunga mkono mpango mkakati na kuchukua jukumu kubwa la kufanya kazi kwa Juhudi ili kuleta mabadiliko ambayo UTPC imejiwekea,kwa pamoja tuna nafasi ya kipekee ya kujenga tasnia ya habari iliyoimarika zaidi na kuwa chombo nguvu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu" Amesisitiza Ndg.Deogratius
"Tunapojikita katika uzinduzi wa ofisi hii mpango mkakati wa UTPC leo pia tunasherekea miaka 60 ya ushirikiano wa kimaendelea baina ya nchi ya Sweden na Tanzania,ushirikiano huu umekuwa wa thamani kubwa katika kusaidia maendeleo ya nchi yetu na tasnia ya habari,tunatoa shukrani zetu za dhati kwa serikali ya Sweden kwa mchango wao kujenga na kuimarisha sekta mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania ikiwemo sekta ya habari ambapo UTPC na klabu zake ni wanufaika"
Aidha ameongeza kuwa mpango mkakati wa UTPC unazingatia malengo makuu matano ambayo ni kukuza uwezo wa kitaaluma wa waandishi wa habari,Kukuza Uhuru wa kupata taarifa na Uhuru wa habari,kuhakikisha klabu za waandishi wa habari zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kuweka mifumo mizuri na thabiti ya usimamizi wa klabu,kuhakikisha ulinzi na usalama wa waandishi wa habari na maslahi yao unazingatiwa pamoja na kuhakikisha UTPC inakuwa na mifumo mizuri inayochangia utekelezaji wa shughuli za UTPC kwa ubora zaidi.
"Tunafahamu jukumu letu kama waandishi wa habari ni kuleta mabadiliko chanya kwa jamii yetu,hasa kwa kuwa sekta ya habari ina jukumu kubwa katika kutoa habari za ukweli na kujenga jamii yenye taarifa na maarifa ili iweze kufanya maamuzi sahihi"
UTPC kwa kushirikiana na wadau wadau wa habari,ikiwemo serikali,wadau wa maendeleo kama vile ubalozi wa Sweden,Uswis na Marekani na wadau wengine ndani ya nchi,itaendelea kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanaendelea kupiga hatua katika kufanya kazi zao kwa Uhuru zaidi bila vitisho wala kuingiliwa.
Naye Zamaradi Kawawa ambaye ni afisa wa Serikali akizungumza kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa serikali na mkurugenzi idara ya habari Maelezo amesema kuwa wanaishukuru UTPC kwa kuwa na ofisi zake makao makuu ya nchi kwani itawasaidia waandishi wa Dodoma kuweza kutatua changamato mbalimbali kwani wataweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo viovu na kuhakikisha kunakuwa na usawa huku waandishi wakifanya kazi yao kwa uadilifu bila kuingiliwa na mamlaka yeyote hivyo uwepo wa UTPC utasaidia kulinda maadili ya sekta ya habari kwa makao makuu ya nchi.
Home »
» UTPC KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA WANACHAMA NA WADAU.
0 Comments:
Post a Comment