Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

MCH.MARKO AMEWATIA MOYO WAKRISTO MSIKATE TAMAA

 Na. Kadala Komba ,Dodoma

Wakiristo wametakiwa kuachana na hali ya kukata tamaa na kuishiwa nguvu hasa pale wanapokutana na changamoto mbalimbali katika maisha yao kwa maana tumaini lipo katika Mungu.

Hayo yamebainishwa na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania Assembles of God(TAG),Nazarath Internatinal Church(NIC) Mchungaji Zephania Marko katika ibada ya jumapili ya tarehe 29,10,2023 kanisa hapo.

Amesema kuwa kutokana na kuwa na mambo mbalimbali na changamoto mbalimbali zinapelekea watu kuishiwa nguvu  hata kama  wameokoka au kuwa na nguvu nyingi,hivyo kuwaomba wasikate tama wanapokutana na changamoto hizo.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania Assembles of God(TAG),Nazarath International Church Zephania Marko akihubiri katika ibada ya jumapili ya tarehe 29,10,2023 

WAZAZI NA WALEZI WAKUMBUSHWA KUPELEKA WATOTO SHULE.

 

Na Mwandishi Wetu- Kilimanjaro

Wazazi  na walezi nchini  wametakiwa kuhakikisha watoto wao waliofikia umri wa kwenda shule wanapelekwa ili kupata elimu itakayowawezesha kuwa wataalam wa fani mbalimbali pamoja na kutimiza ndoto zao.

Wito huo umetolewa na  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi wakati akizungumza katika  mkutano wa hadhara Kata ya Mroe, Jimbo la Same Mashariki ikiwa ni ziara yake katika Jimbo hilo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.

Mwenyekiti huyo amesema baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakizuia watoto wao kwenda shule huku wanaume wakitumikishwa katika shughuli za kilimo au kuchunga ng’ombe na wale wa kike wakilazimishwa kuolewa.

“Wazazi na walezi pelekeni watoto shule Serikali inahitaji wataalam wengi zaidi katika fani mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, barabara na nyinginezo. Pia mkumbuke juhudi hizi zinafanywa na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kila mtoto apate elimu bora na ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chma chetu,”Amesema Mwenyekiti huyo.

Vilevile amewasisitiza wanafunzi kuepuka vishawishi kwa kuwa na msimamo, kutojihusisha na makundi mabaya hatua itakayowafanya kushindwa kutimiza ndoto zao na hatimaye kujiingiza katika matendo ya uhalifu na kuzalisha jamii tegemezi.

“Msikubali kukatishwa tamaa na marafiki wabaya, watoto wakike wapewe fursa ya kusoma watimize ndoto zao hapo tutapata wakurugenzi, madaktari, Mawaziri msiwafanyie hayo mnayoyafanya ni machukizo mbele ya Chama, Serikali na hata Mwenyezi Mungu,”Ameeleza.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo ametoa kadi za Chama kwa baadhi ya wanachama waliorudi CCM wakitoka katika vyama vingine wakisema lengo la kufanya uamuzi huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ummy Nderiananga amesema Serikali ya Awamu ya Sita  inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo iko ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kukuza uchumi wa Taifa.

“Sisi Serikali kupitia Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaendelea kutekeleza ilani na  niwahakikishie kazi inaendelea vizuri hakuna kitakachosimama, tunafanya kazi usiku na mchana kwa sababu nyinyi wananchi ndiyo mmetupa kazi. Pia niwatoe hofu mnapoona wageni wanakuja kuwekeza nchini ni kutokana na mahusiano mazuri aliyonayo Rais wetu na Nchi zingine na wadau wa maendeleo,”Amefafanua Mhe. Ummy.

Naye Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anna Kilango amebainisha kwamba Serikali inaendelea kuboresha miradi mikubwa ya maji akisema kuwa licha ya changamoto kubwa ya maji katika Jimbo la Same Mashariki bado Serikali ina nia njema ya kumtua ndoo mama kichwani  ili wananchi wake waendelee kufanya shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi.

“Nikiri Jimbo langu linakabiliwa na uhaba wa huduma muhimu ya maji lakini bado Serikali haijatuacha inatoa fedha za kuboresha miundo mbinu ya maji hatua itakayosaidia wananchi wangu wa Same Mashariki kufanya kazi zao kwa amani. Pia tunamshukuru sana mama kwa kuendelea kupigania na kuhubiri amani katika Nchi yetu,”Amepongeza Mbunge huyo.

Aidha Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro, Adam Simba amehimiza kufanywa kwa ufuatiliaji wa karibu wa miradi inayofanya na Serikali ili  kubaini hatua iliyofikiwa, changamoto  na namna ya kuzitatua kwa maendeleo ya Taifa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi  akizungumza katika  mkutano wa hadhara Kata ya Mroe, Jimbo la Same Mashariki ikiwa ni ziara yake katika Jimbo hilo akiwa ameongozana na Kamati ya Siasa ya Mkoa huo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.

 


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Maore na Kata ya Mtii katika Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro wakisikiliza mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi pamoja na Kamati ya Siasa ya Mkoa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ummy Nderiananga akisalimiana na  wananchi wa Kata ya Maore katika Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro  wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa huo Patrick Boisafi.

SERIKALI IMETUTUPA,HAITUTAMBUI WANANCHI ZEPISA WATEMA NYONGO.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Wananchi wa kijiji cha ZEPISA Dodoma jiji wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwatimizia huduma muhimu kama maji,umeme,miundombinu ya barabara pamoja na kituo cha afya.

Pendo Wilson ambaye ni mwanakijiji wa ZEPISA amesema kuwa maji yamekuwa changamoto kubwa kwao hadi kupelekea ndoa majumbani hazidumu kwani kina mama hutoka nyumbani saa 12 asubuhi hadi saa 2 usiku ambapo kisima kimechimbwa lakini hakuna kinachoendelea hali inayopelekea hata zahanati ya kijiji wahudumu kuondoka mapema hivyo wanaiomba serikali iwasaidie kwani vijiji vya karibu kama zaka kuna huduma zote lakini kwao zinashindwa kuwafikia pamoja na wanafunzi kukutana na changamoto ya barabara na maji shuleni hali inayopelekea usalama wa vyoo kuwa mdogo.

 Naye Yona Dickson ambaye ni katibu wa tawi  chama tawala(CCM)amesema kama kiongozi anapata wakati mgumu wa kuzungumza na wanakijiji kwani wanaona serikali iliyopo inaongea uongo na hakuna kinachotekelezwa kwani kijiji hicho kimesahaulika hivyo  wanaiomba serikali na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mbunge Mhe.Anthony Mavunde pamoja na Mkuu wa mkoa Mhe.Rosemary Senyamule wawakumbuke kwa kutembelea eneo husika ambapo kero kubwa ni miundombinu ya barabara kwani hakuna muunganiko mzuri kutoka ZEPISA mpaka hombolo bwawani.

"Miundombinu ya maji ni changamoto,kituo cha afya changamoto,miundombinu ya barabara changamoto,hospitali ya kijiji haina umeme tumeshachoka viongozi wanakuja wanaongea tu hakuna utekelezaji,wanasubiri karibia na uchaguzi tunawapigia kura baada ya miaka mitano hawaonekani kiukweli tumechoka na tunaomba serikali kama haitutambui tujue kwasababu haiwezekani kijiji hiki pekee ndio huduma muhimu hazifiki je sisi ni wakimbizi au watanzania?" Amehoji Ernest Mchano mwanakijiji Zepisa.

" Maji ndio kero ya kwanza kwani hakuna kabisa kina mama wanatoka asubuhi wanarudi saa sita usiku,kwa upande wa barabara kutoka mwaka 1972 barabara haieleweki licha ya TARURA kuja kuchonga barabara hali inayopelekea mvua ikinyesha kushindwa kutoka sehemu moja hadi nyingine,kuhusu suala la umeme hili nalo ndio tatizo kuu kwani hospitali ipo lakini hakuna umeme hali inayopelekea wahudumu kufanya kazi mchana tu na jioni wanaondoka na kusababisha kina mama kujifungulia njiani,na kwa upande wa shule changamoto kubwa ni vyoo vya wanafunzi ni shida tunamuomba Rais kuja kutembelea na kutatua kero hizi kwani sisi ni watanzania"Amesisitiza Mzee Emily Makasi Mwanakijiji na mwanaharakati wa kujitegemea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ZEPISA B Ndugu.Musa Rashidi amesema ni kweli kero walizozisema wananchi zipo,vyoo mashuleni havitoshi na kumekuwa na ahadi bila matokeo kwani amekuwa akiwasiliana na viongozi husika bila matokeo chanya.

"Kama kiongozi na mwananchi naumia kuona toka kijiji hiki kianzishwe hakuna umeme wala hakuna vitendo vyovyote vinavyoendelea naiomba serikali itambue kwamba sisi tuko Dodoma jiji,ukitizama kwa upande wa visima kuna vya kiasili ambavyo havina uwezo wa kusambaza maji kote na tumekuwa tukifuatilia RUWASA bila kufua dafu na hali hii kama kiongozi inanikatisha tamaa kuona wananchi wangu hawafurahishwi na viongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao kama walivyoahidi" Amesisitiza Mwenyekiti Zepisa B Ndugu Rashidi.

"Hakuna muunganiko kati ya serikali na viongozi wa chama ifike kipindi Serikali itambue kwamba kunawatu waliowachagua kwani kitendo cha kuto kututambua sisi inafika kipindi serikali ikiitisha mkutano wananchi hawafiki kwasababu wanachoka kudanganywa,hakuna huduma zozote muhimu wakati tupo Dodoma jiji na Zepisa inafahamika na Serikali na kama haifahamiki basi watutafutie sehemu ya kutupeleka" Ameongeza Abi Mwanza mwanakijiji Zepisa.

Naye Ndugu Daudi Kamunya ambae ni mwenyekiti wa ZEPISA A amesema kuwa umeme kwenye kituo cha afya Zahanati bado ni changamoto kwani huwezi kufanya kazi bila umeme,hivyo amewaomba wananchi kuwa wa pole kusuburi huduma hiyo kwani changamoto ya umeme iko mbioni kutatuliwa.










𝗧𝗨𝗞𝗢 𝗧𝗔𝗬𝗔𝗥𝗜 𝗞𝗨𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗦𝗘𝗞𝗧𝗔 𝗕𝗜𝗡𝗔𝗙𝗦𝗜: 𝗲-𝗚𝗔

 

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeahidi kushirikiana na Benki ya NMB ili   kuimarisha, kukuza na kuendeleza ujuzi na vipaji kwa vijana wa Kitanzania wabunifu na wale wanaosoma fani ya TEHAMA, katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, kupitia programu maalum ya mafunzo kwa vitendo inayotolewa na e-GA kupitia Kituo chake cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC).

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mha. Benedict Ndomba, wakati wa kikao cha pamoja kati ya e-GA na Benki ya NMB kilichofanyika katika Makao Makuu ya ofisi za e-GA jijini Dodoma, kwa lengo la kujadili namna taasisi hizo zinavyoweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya teknolojia.

Maeneo hayo ni pamoja na utafiti, matumizi ya teknolojia za kisasa, kuvumbua vipaji na kuviendelea kwa wavijana wabunifu wa Kitanzania, pamoja na kutoa fursa kwa vijana wavumbuzi na wabunifu ikiwa ni sehemu ya kuendeleza Sekta ya TEHAMA nchini.

Ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza na kukuza fursa za ajira kwa vijana sambamba na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Serikali na sekta binafsi kwenye eneo la TEHAMA, alisema Ndomba .  

“e-GA imekuwa ikishirikiana na Vyuo Vikuu mbalimbali nchini  katika kuwapata vijana wenye ujuzi, hivyo makubaliano hayo kati ya e-GA na NMB ni muendelezo wa ushirikiano mazuri uliopo kati ya e-GA na wadau mbalimbali wa TEHAMA”, alifafanua Ndomba.

Aliongeza kuwa, katika kikao hicho taasisi hizo zimekubaliana kushirikiana na kuandaa mkataba wa makubaliano (MOU) ambapo baada ya kukamilika kwa mkataba huo, pande zote mbili zitakutana na kujadiliana namna ya utekelezaji wa makubaliano hayo.

“e-GA imekuwa ikiwatengeneza vijana wanaoshiriki programu maalum ya mafunzo kwa vitendo pamoja na utaratibu wa kujitolewa (interns and volunteering) kupitia kituo chetu cha utafiti na ubunifu, kwa kuwajengea uwezo zaidi ili kwenda sambamba na soko la ajira pamoja na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoibuka kila siku”, alisema Ndomba.

Aidha, Ndomba aliishukuru Benki ya NMB kwa kuona umuhimu wa kutengeneza wataalamu wazawa wa TEHAMA   kupitia programu hiyo na kuwa,  e-GA ipo tayari kushirikiana na benki nyingine zenye dhamira ya kuijenga Tanzania ya kidijitali katika sekta zote za serikali na binafsi.

Naye Meneja eGovRIDC Dkt. Jaha Mvulla alisema, e-GA ipo tayari kushirikiana na Benki ya NMB katika maeneo mbalimbali yanayolenga kukuza matumizi ya TEHAMA nchini ikiwemo eneo la rasilimali za miundombinu na vifaa vya TEHAMA vya kufanyia mazoezi na majaribio, ubunifu hasa maeneo ya teknolojia mpya, kujenga uwezo na uzoefu kwa vijana, mafunzo kwa vitendo, utafiti na machapisho, maonesho, mashindano mbalimbali ya kidigitali kwa ajili ya kuvumbua vipaji, na maeneo mengine yanayohusiana na jitihada za Serikali Mtandao na teknolojia za kifedha.

“e-GA ipo tayari kufanya kazi na NMB kupitia programu maalumu ya mafunzo kwa vitendo inayoendeshwa na eGovRIDC, ili kuchochea ubunifu katika matumizi ya teknolojia mpya zinazoibuka duniani ikiwemo Akili Bandia (AI), Machine Learning,  Blockchain na matumizi yake kama vile kujenga ulewa wa teknolojia kama za Digital Currency na FinTech, Utengenezaji wa mifumo (System Development) kwa ajili ya kutatua changamoto zetu nchini na usalama mtandaoni (Cyber Security)”, alisema Dkt.Jaha.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu- Kituo cha Taaluma NMB Bi. Joanitha Rwegasira alisema kuwa, Benki ya NMB imeandaa programu hiyo ili kuongeza idadi ya vijana wabobezi kwenye masuala ya TEHAMA watakaofanya kazi katika sekta za umma na binafsi kwa lengo la kukuza taifa la kidijitali.

Programu hiyo itasaidia kufanya majaribio ya teknolojia mpya  zinazoibuka ikiwemo Sarafu ya mtandaoni na kutoa suluhu kwenye maeneo mbalimbali yenye changamoto katika utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo matishio ya usalama mtandaoni, ubunifu wa mifumo n.k, alisema Rwegasira

Aidha, aliishukuru Mamlaka kwa kuonyesha utayari wa kushirikiana na NMB na kwamba watatumia fursa hiyo katika kuhakikisha wanaboresha huduma za kibenki hususani huduma zinazotolewa kidijitali.


KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU

Na Mwandishi wetu- Shinyanga Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa mafanikio makubwa katika kutekeleza afua za VVU na UKIMWI nchini. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo wakati kamati ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua Mpango wa Dreams kupitia Mradi wa Epidemic Control (EPIC) unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI360) kwa wasichana balehe na wanawake vijana (AGYW) katika katika Mkoa wa Shinyanga. Akizungumza mara baada ya kukagua vikundi vya vijana vikiwemo Sitetereki kilichopo Kata ya Old Shinyanga, Jahazi, Kata ya Ibadakuli na Tunaweza katika Kata ya Kolandoto Mhe. Nyongo amesema lengo la ziara ni kujionea maendeleo ya mradi huo na kuishauri Serikali maeneo ya kuboresha ili kuendeleza jitihada za kuwa na vijana wenye afya nzuri wanaoshiriki katika shughuli za uzalishaji na kujiletea maendeleo yao. “Tunapongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa maelekezo ya kumlinda mtoto wa kike hasa katika gonjwa kubwa la UKIMWI, namna ya kumkomboa mtoto wa kike, kujifunza kazi za ujasiliamali ili kujikwamua katika maisha pamoja kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia hivyo sisi kama wabunge tumeridhishwa na kazi inayofanywa na Serikali,”Amesema Mwenyekiti huyo. Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewaomba vijana wa kike kuendelea kujiamini na kufanya kazi vizuri kwani Serrikali ya Awamu ya Sita inawajali vijana na kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa. Akizungumzia ziara hiyo Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Hassan Mtenga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kukamilisha na kujengwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo huku akiipongeza TACAIDS na wadau wa maendeleo kuwa na mwamko wa kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi. “Tumejifunza kitu kwasababu tunao watu wako tayari kupiga vita janga kuu la UKIMWI na niishukuru TACAIDS, Mawaziri wenye dhamana na hawa wadada ambao wameamua kutoka kwenye sughuli za kuuza bar na kuanzisha biashara zao sasa uwe mfano wa kuigwa kwa maeneo mengine,”Amepongeza Mhe. Mtenga. Vilevile Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Christina Mnzava amesema wazazi na walezi wana wajibu wa kusimamia malezi sahihi ya watoto ili kuwakomboa katika tabia hatarishi huku akiupongeza Mpango wa Dream kwa kuamua kuwafikia mabinti katika maeneo yao akishauri mradi huo kuongeza wigo na kuwafikia vijana wengine waliopo Vijijini . “Sisi kama wazazi na walezi tunaweza kuwakomboa watoto wetu katika tabia hatarishi ambazo wanazipata mtaani kuna wengine walikuwa wanauza miili yao, lakini kutokana na mradi huu wamejikwamua wamefundishwa ujasiriamali, kuwekeza tumeona wasichana wamejitambua wanatengeneza sabuni, batiki, vyungu katika vikundi vya Kata za Old Shinyanga, Ibadakuli na Kolandoto kwa kweli wamefanya vizuri,”Ameeleza Mjumbe huyo. Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Christina Mndeme amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuondoa unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU ambao upo juu, kuwajengea vijana uwezo wa kiuchumi ili muda mwingi wautumie kwenye uzalishaji na sio kwenye mambo yanayoweza kuwasababishai maambukizi ya VVU,kuelimisha jamii kuacha mila potofu ambazo zinasababisha ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mshauri Mwandamizi wa Mpango wa Dreams kupitia Mradi wa Epidemic Control (EPIC) unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI360) Bi. Agnes Junga amefafanua kuwa lengo la Mpango huo ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa wasichana kuanzia umri wa miaka Tisa hadi 24. “Mpango huu ulizinduliwa 2014 ukilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa Nchi 13 za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambapo tulianza na Halmashauri Sita na hadi sasa tumefikia Halmashauri 12. Shirika la (FHI360) kwenye mradi wa EPIC tunatekeleza Dreams katika Mikoa miwili ya Shinyanga ndani ya Halmashauri Tano na Iringa katika Halmashauri mbili na tunawafikia wasichana kuanzia miaka 15 hadi 25 walio nje ya shule pamoja na wazazi au walezi na jamii kwa ujumla tuhakikishe msichana anafikia ndoto zake. Aidha akizungumza kwa niaba ya wanakikundi kutoka Vikundi vya Mabinti Balehe na Wanawake Vijana vya Sitetereki, Tunaweza na Jahazi mwanakikundi Sungi Leonard amesema uanzishwaji wa vikundi hivyo vimewasaidia kama mabinti kujitambua, kufahamu elimu ya afya, kuwajengea uwezo wa kukabiliana na vitendo vya kikatili pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kuwawezesha kiuchumi . “Nilikutana na mwezeshaji kiuchumi na mwelimishaji rika nikapata elimu ya ukatili wa kijinsia, umuhimu wa upimaji wa afya, matumizi sahihi ya kinga, magonjwa ya ngono na VVU ambayo imenisaidia kujitambua kama binti. Pia nilifanikiwa kujiunga katika kikundi cha Sitetereki nikajifunza kutengeneza batiki kazi ambayo inanipatia kipato na ninamudu mahitaji yangu tofauti na ilivyokuwa awali,”Ameshukuru Mwanakikundi huyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya Mabinti balehe na wanawake vijana wakati za ziara ya Kamati hiyo mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kulia) akiangalia vyungu vinavyotengenezwa na Mabinti balehe na wanawake vijana kupitia kikundi cha Tunaweza kilichopo Kata ya Kolandoto, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakati za ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakikundi wa kikundi cha Sitetereki Kata ya Old Shinyanga wanaojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali wakati za ziara ya Kamati hiyo mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Mabinti balehe na wanawake vijana kupitia kikundi cha Tunaweza kilichopo Kata ya Kolandoto Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakionesha namna vyungu vinavyotengenezwa wakati za ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Mabinti balehe na wanawake vijana kupitia kikundi cha Tunaweza na Sitetereki wakifuatilia ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Mabinti Balehe na Wanawake Vijana kupitia kikundi cha Jahazi Kata ya Ibadakuli, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakionesha namna ya utengenezaji wa Sabuni za vipande mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ilipofanya ziara ya kutembelea vikundi mkoani Shinyanga. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

RC SENYAMULE TUMEJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema azima ya Serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto za wananchi na kuleta maendeleo kwa watu wake.

Mhe.Senyamule ameyasema hayo alipotembelea Kijiji cha Mpwayungu kilichopo katika Wilaya ya Chamwino ikiwa ni katika utaratibu aliojiwekea wa kusikiliza kero za wananchi wa Dodoma ambapo amebaini changamoto mbalimbali za Wananchi hao ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme, na Barabara. Mhe. Senyamule amezipokea kero hizo na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kuja hapa leo ni kuhakikisha matamanio ya Rais wetu yanatimia kwa kusikiliza changamoto mlizonazo na kuzipatia ufumbuzi na zinazo muhusu yeye  kuziwasilisha kwake kwa ajili ya utekelezaji " amesema Mhe. Senyamule

Katika Hatua nyingine, akiwa katika mradi wa mashamba ya pamoja ya  'Bulding a Better Tomorrow '(BBT), ametoa shime kwa  wasimamizi wa mradi huo kuchukua hatua kwa Changamoto zinazojitokeza zinazopelekea  mradi huo kutokwenda kwa kasi iliyokusudiwa.

"Hakikisheni tarehe ambayo imepangwa kwa  kazi hii kuwa tayari inatimia ,hivyo basi fanyeni utaratibu wa kuweka mashine za  kufyatulia matofali sehemu ya mradi ifikapo Jumatano, mashine ziwe sehemu ya kazi ,pia ongezeni nguvu kazi ili kusadia mradi ukamilike kwa wakati "Amesisitiza Mhe. Senyamule

Kwa Upande Wake, Mkuu wa Wilaya ya chamwino Mhe. Gift Msuya, amemshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kufanya mambo ya maendeleo katika Tarafa ya Mpwayungu pamoja na mradi wa Kilimo cha pamoja, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Nkhambako na mengine.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambapo ziara hiyo ametembelea mradi wa Mashamba ya Kilimo cha pamoja, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Nkhambako na kusikiliza changamoto za wananchi wa tarafa ya Mpwayungu na kuzipatia ufumbuzi.


Waziri Mhagama, Azindua Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Manyara.

Na; Mwandishi Wetu - Manyara

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa watendaji wa Serikali; kujipanga na kuhakikisha Muongozo wa uwekezaji kwa Mkoa Manyara unawafikia wananchi wote ili kufanya kazi kwa tija.

Kauli hiyo ameitoa Mkoani Manyara wakati wa Ufunguzi wa wiki ya Kitaifa ya Vijana tukio alilolifanya kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa jana tarehe 10/10/2023.

“Tunataka Muongozo huu uweze kutoa fursa nyingi kwa vijana ili uweze kujenga kizazi ambacho kitatatumia Muongozo huu kwa muda mrefu” alieleza.

Aliendelea kusema kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu italeta timu ya baraza la uwezeshaji kiuchumi, timu ambayo itasaidia kujenga uwezo kwenye dhana kutengeneza vitu asilia (Local content) ili kuongeza tija na kuweka mazingira wezeshi yatakayochochea wanawekezaji.

“Makapuni yaliyowekeza katika Mkoa wa Manyara yaone namna ya kutumia fedha zile zinazorudi kwa jamii, kwa kuwekeza katika vikundi vya vijana wabunifu ili kupitia muongozo wa uwekezaji usaidie kuleta tija kwa vijana na maendeleo ya Mkoa,” alihimiza

Akizungumza kuhusu madhimisho ya wiki ya vijana, Mhe. Waziri Mhagama amesema ubunifu aliyouona wakati alipotembelea Mabanda, hasa uliofanywa na kijana Said Mussa wa kubuni namna ya kutengeneza taa za magari zilozoharibika na kurudisha katika muonekano mpya ni ubunifu mzuri.

“Kijana Huyu wa Kitanzania akifanikiwa kuhuisha teknolojia hiyo basi tutakuwa uwezo huko mbele kujenga viwanda vidogo vidogo vingi vya kuzalisha taa za magari nakusaidia kuongeza pato la kigeni na Kubrand Tanzania ya Mhe. Samia Kupitia Ubunifu wa Vijana,” alisema.

Namshukuru sana Mhe. Mhe. Prof. Joyce L. Ndalichako na Katibu Mkuu Mhandisi Cyprian John Luhemeja kwa kuridhia kumpatia Mkopo kijana huyu ili kuhakikisha anafanya vizuri katika ugunduzi alioufanya.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi vijana ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Joyce Ndalichako amesema wiki ya vijana inalenga kutambua Mchango wa Waasisi wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Shekh Abeid Amani Karume.

 

Ameongeza kusema Maadhimisho ya wiki ya vijana Kitaifa ya Mwaka 2023 yanayofanyika Mkoani Manyara, kauli mbiu yake ni,” Vijana na Ujuzi Rafiki kwa Mazingira na Maendeleo Endelevu”. Maadhimisho ya vijana yanakutanisha vijana na wananchi wa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ambapo vijana wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu. Ni fursa kwa Serikali na Wadau kutambua mchango mzuri wa vijana kwa maendeleo ya nchi yetu.

 “Natoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuthamini vijana wa Tanzania kwa matendo kwa kuhakikisha vijana wanapatiwa mitaji ya kuendeleza biashara zao au kwa kuanzisha shughuli za maendeleo,” alibainisha

Awali Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bi, Queen Sendiga alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuchagua Manyara kuwa Mwenyeji wa Kilele cha Madhimisho ya Siku ya vijana kitaifa, Mwenyeji wa Misa Maalumu ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa, na Mwenyeji wa Killele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.

“Moja ya mambo makubwa yatakayoachwa katika Mkoa wa Manyara, kutokana na kuwa Mwenyeji wa kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru ni pamoja na Ujenzi wa uwanja Mkubwa wa kisasa wa Mpira wa Miguu ambao Umejengwa kwa hadhi,” alisema

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama katika picha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akizindua Muongozo wa uwekezaji kwa Mkoa Manyara.


 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama katika picha akipata maelezo kuhusu ubunifu wa kutengeneza taa za magari Kutoka kwa Kijana Said Mussa katika banda la Maonesho.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama katika picha akiwa na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Rashidi katika Banda la kumbukumbu ya Shekh Abeid Amani Karume wakati wa Ufunguzi wa wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama katika picha na Mhe. Tabia Maulid Mwita Waziri wa Vijana, Sanaa na Michezo Zanzibar, wakati akiangalia maandalizi kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru (2023) katika uwanja Tanzanite.


 

MADEREVA WA MALORI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI MAAMBUKIZI YA VVU

 

Na Mwandishi wetu- Singida

Madereva wa magari yaendayo masafa    marefu ndani ya ndani na nje  Nchi wamehimizwa  kuchukua tahadhari dhdi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI wakati wote wanaofanya shughuli zao za usafirishaji pamoja na kujenga utamaduni wa kupima afya zao ili kuanza matumizi ya dawa  mapema pindi watakapogundulika kuwa na maambukizi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga  wakati akizungumza na madereva wa malori  wanaoegesha malori hayo katika Kijiji cha Majengo, pamoja na kukagua Kituo cha Maarifa ya UKIMWI Halimashauri ya Wilaya ya Manyoni  mkoani Singida akiwa ameambatana  na  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI .

Mhe. Ummy amesema lengo la  kufika  katika kituo hicho ni kuzungumza na madereva hao akisema wako katika hatari  kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Kutokana na shughuli zao za masafa marefu pamoja na kukagua huduma za kiafya zinazotolewa kituoni hapo.

“Nipende kuwakumbusha na kuwasisitiza mjitokeze mpime afya zenu ili mjue mko katika hali gani, tunatambua kulingana na kazi zenu mnatembea umbali mrefu na mnaenda  maeneo mengi kama mikoani na nje ya Nchi kwahiyo mko hatarini  kupata maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na niwaombe mtumie kituo hiki cha Maarifa kupata elimu ya UKIMWI na magonjwa mengine ili muwe salama,” Amesema Mhe. Ummy.

Aidha Naibu Waziri huyo amewakumbusha kuendelea na matumizi ya dawa kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIWMI ili kuimarisha kinga ya mwili , kujiepusha na magonjwa nyemelezi ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi wakiwa imara kiafya huku akiissisitiza  jamii kutowanyanyapaa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na badala yake kuwaonyesha upendo, kuwajali  na kuwashirikisha katika maendeleo.

Aidha akisoma taarifa ya Kituo hicho mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI Mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Dkt. Ainea Mlewa  amebainisha kuwa hali ya upimaji kuanzia  mwezi Julai 2022 hadi Septemba 2023 jumla ya  madereva wa malori waliojitokeza kupima  maambukizi ya VVU ni 684 waliogundulika na maambukizi  wakiwa ni 19 kati yao 15 ni wanawake  wakati wanaume wakiwa ni wanne ambapo waliunganishwa katika Kliniki ya tiba na mafunzo.

 “Malengo ya mradi ni kuhamasisha wananchi kupima bila uoga, kutoa ushauri, kuhamasisha upimaji wa VVU kwa  hiari, kuhamasisha upimaji kwa kutumia ushawishi wa mtoa wa huduma, kutoa elimu ya UKIMWI pamoja na matibabu ya magonjwa ya zinaa, kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kugawa kinga na elimu ya matumizi  yake, elimu kwa vikundi vya WAVIU na elimu sahihi ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU,” Amefafanua Dkt. Mlewa.

=MWISHO=

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akisalimiana na baadhi ya wataalam wa afya katika Kituo cha Maarifa ya UKIMWI kilichopo Kijiji ch majengo, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida alipowasili kituoni hapo akiwa na   Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI tarehe 10 Oktoba, 2023.   

 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na baadhi ya Madereva wa  Malori  wanaoegesha Malori yao katika Kijiji cha Majengo , Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida akiwa pamoja na   Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI tarehe 10 Oktoba 2023.


Mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Dkt. Ainea  Mlewa akitoa taarifa ya  Kituo cha Maarifa ya UKIMWI kilichopo Kijiji cha Majengo , Halmashuri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida  mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI ambaye pia ni Mbunge Viti Maalumu  Mhe. Juliana Shonza (wa pili kulia) akiuliza swali wakati wa ziara ya Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Maarifa ya UKUMWI kilichopo KIjiji cha Mjengo, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida tarehe 10 Oktoba, 2023.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


 

IDADI YA WATALII KUTOKA NJE YA NCHI IMEONGEZEKA.

 
Na Moreen Rojas
Dodoma.



OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa  idadi ya Watalii kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Agosti Mwaka 2023 imeongezeka na kufikia 1,131,286 ikilinganishwa na Watalii 900,182 walioingia kwa kipindi kama hicho Mwaka Jana  sawa na ongezeko la  asilimia 25.7

Mkurugenzi wa Takwimu za uchumi kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)DANIEL MASOLWA ameyaelwza hayo  Oktoba 9 Jijini  Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari  ambapo amesema  ongezeko hilo limechagizwa na filamu ya Royal tour alayoifanya Mhe Rasi Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN.

 

Aidha amebainisha kuwa  kati ya Watalii wote waluoingia nchini katika kipindi hicho,Watalii236047 waliingia nchini kupitia Zanzibar ambao ni sawa na asilimia 31.1 ya Watalii wote.



"Watalii walioingia Nchini Mwezi Agosti Mwaka 2013 p3kee wqliongez3ka  hadi 186,030ikilinganishwa na Watalii158,049walioingia nchini MwwziAgosti2022 sawa na ongezeko la asilimia 17.7,"Amesema Masolwa



Pamoja na hayo,Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa Wataluu 336203kati ya Watalii wote walioingia Nchini Mwezi Agosti Mwaka 2023 waliingia kupitia Zanzibar sawa na asilimia 29.7ya idadi  ya  Watalii wote.




Akielezea Watalii walioingia Nchini kwa mchanganuo wa Utaifa,Januari hadi Agosti kutoka nje ya Bara la Afrika Januari hadi Agosti walitoka Marekani ikiwa ni watalii84541.



"Nchi nyingine zilizokuwq na idadi kubwa ya Watalii ni Ufaransa72,009,Ujerumani watalii57798,Uingereza Watali51,505 na Italia walikuwa Watalii 51056,"Amesema



Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo amesema kuwq katika kipindi cha Januari hadi Agosti2023 Tanzania ilipokea Watalii kutoka katika Bara la Afrika  ambapo idadi kubwa ya Watalii walitokw Kenya128,753,Burundi walikuwa 12319,Zambia 6,649,Rwanda5,124 na Uganda 4,052





MWISHO


*MAADHIMISHO YA SIKU YA MWALIMU BUKOMBE 2023*


Leo Oktoba 6, 2023 Sherehe ya Siku ya Mwalimu Duniani inaadhimishwa katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambayo itahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa pamoja na Walimu kutoka wilayani Bukombe.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda.

Viongozi wengine wanaoshiriki  sherehe hiyo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella.

Kaulimbiu ya Siku hii ni "Asante Mwalimu, Wewe ni Taa Yetu"

*Taarifa rasmi itawasilishwa*


*RAIS SAMIA AMEIBEBA KWA DHATI AJENDA YA MATUMIZI NISHATI MBADALA – NAIBU WAZIRI KAPINGA*


 *Lilian Lundo, Veronica Simba na Zuena Msuya - Songea*

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameibeba kwa dhati ajenda ya matumizi ya nishati mbadala kutokana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Mhe. Kapinga amesema hayo leo Oktoba 5, 2023 wakati wa Baraza Maalum la Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Ruvuma, sanjari na ugawaji wa majiko/mitungi ya gesi yaliyotolewa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“Ninyi nyote mnafahamu ajenda ya Mhe. Rais kuhusiana na umuhimu wa nishati mbadala, tunafahamu changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na changamoto za mazingira kwa ujumla. Hii ni ajenda ambayo Mhe. Rais ameibeba kwa dhati kabisa kuhakikisha tunaanza mchakato wa kuelimisha Watanzania ili kuondokana na nishati ambazo sio rafiki kwa mazingira, na kutumia zilizo rafiki kwa mazingira,” amesema Mhe. Kapinga.

Naibu Waziri Kapinga ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma amewataka vijana kushirikiana na wanawake, wazee na makundi mengine katika kuhakikisha wanapunguza changamoto za kimazingira kwa matumizi ya nishati mbadala.

“Wengi wanadhani ajenda hii ya nishati mbadala ni kwa ajili ya akina mama tu, lakini wote tunafahamu nguvu na mchango wa vijana kwenye masuala ya mabadiliko chanya. Kwa hiyo ajenda hii ni lazima twende nayo pamoja wanawake, vijana, wazee na kila kundi kwenye jamii. Ndiyo maana nikaona busara kushirikisha Baraza la Mkoa kwa sababu ninyi ndio viongozi kwenye Wilaya zenu,” amesema Mhe. Kapinga.

Akifafanua, amesema kuwa ajenda ya matumizi ya nishati mbadala ni ya Serikali ya Awamu ya Sita  na inatakiwa kuungwa mkono na wananchi wote ili kuweza kuboresha mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea hivi sasa duniani kote.

Kapinga amesema ni wakati wa vijana kusaidia katika anjenda mbalimbali zenye manufaa ya taifa na kwamba ajenda ya nishati mbadala ikibebwa na vijana inaweza kwenda kwa kasi katika  kusaidia kupunguza changamoto za uharibifu wa mazingira unaofanywa na jamii.

Aidha, ameongeza kuwa wakati huu ambapo REA wanaendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati mbadala, Mhe. Rais ametoa mitungi ya gesi kwa Wabunge wote ili iende kwenye maeneo yote, na majimbo yote ili kuhamasisha umuhimu wa nishati mbadala.

Awali, akiwasilisha Mada kuhusu nishati safi ya kupikia, Mhandisi Kelvin Tarimo kutoka REA amesema Wakala hiyo inaendeshwa kwa Mipango Mikuu mitatu ambayo ni Mpango wa Sera ya Taifa wa Upelekaji Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan), Mpango wa usambazaji wa huduma ya umeme vijijini (Rural Electrification Master Plan) pamoja na Mpango wa Nishati safi za kupikia.

Kuhusu Mpango wa nishati safi ya kupikia, Mhandisi Tarimo amesema umelenga kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo salama kwa mtumiaji na kwa mazingira, ubora, upatikanaji wake, gharama nafuu, rafiki kwa mazingira na iliyo endelevu.

Akizungumzia aina za nishati za kupikia na kiwango cha matumizi yake kwa hapa nchini, Mhandisi Tarimo amebainisha kuwa kuni inaongoza kwa asilimia 63. 5 ikifuatiwa na mkaa asilimia 26.2, gesi oevu asilimia 5.1, umeme asilimia 3 na asilimia 2.2 vyanzo vinginevyo.

Amesema, kutokana na matumizi makubwa ya mkaa na kuni, imechangia uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na ukataji miti. Pia, amesema athari nyingine ni za kiafya kwa watumiaji wa nishati hizo ambapo vifo zaidi ya 33,000 hutokea kwa mwaka kutokana na kuvuta hewa ya ukaa. Vilevile, kiuchumi amesema matumizi ya nishati zisizo salama yanachelewesha maendeleo ya shughuli za kiuchumi.

Kufuatia hali hiyo, amesema Serikali imeweka mikakati ya makusudi katika kuelimisha na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala hivyo akatoa wito kwa wananchi wanaopata elimu hiyo kuifikisha kwa wengine.

Amewasihi wananchi kubadili mitazamo hasi dhidi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo imani kwa baadhi ya watu kwamba chakula huwa kitamu zaidi kikipikwa kwa kutumia mkaa au kuni kuliko kikipikwa katika jiko la gesi au umeme.

Mhandisi Tarimo ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono kampeni ya Mheshimiwa Rais kuhusu matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

Naibu Waziri Kapinga yuko katika ziara ya kazi mkoani Ruvuma kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati pamoja na kuzungumza na wananchi.


UTPC KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA WANACHAMA NA WADAU.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Rais wa UTPC Deogratius  Nshokolo amesema katika kipindi cha 2023_2025 UTPC inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya wanachama na wadau wengine wa habari nchini.

Rais wa UTPC ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi na mpango mkakati wa UTPC kwa mwaka 2023_25 jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania Ms.Charlotta Ozak .

Aidha amesema kuwa wadau wa habari nchini ni pamoja na vyombo vya habari,taasisi za habari,asasi za kiraia na serikali,ili kufanya kazi pamoja kufanikisha malengo kwa ufanisi zaidi.

"Ni vyema nikatumia nafasi hii kutoa wito kwa wanachama wa UTPC(Press Clubs) kote nchini kuunga mkono mpango mkakati na kuchukua jukumu kubwa la kufanya kazi kwa Juhudi ili kuleta mabadiliko ambayo UTPC imejiwekea,kwa pamoja tuna nafasi ya kipekee ya kujenga tasnia ya habari iliyoimarika zaidi na kuwa chombo  nguvu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu" Amesisitiza Ndg.Deogratius

"Tunapojikita katika uzinduzi wa ofisi hii mpango mkakati wa UTPC leo pia tunasherekea miaka 60 ya ushirikiano wa kimaendelea baina ya nchi ya Sweden na Tanzania,ushirikiano huu umekuwa wa thamani kubwa katika kusaidia maendeleo ya nchi yetu na tasnia ya habari,tunatoa shukrani zetu za dhati kwa serikali ya Sweden kwa mchango wao kujenga na kuimarisha sekta mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania ikiwemo sekta ya habari ambapo UTPC na klabu zake ni wanufaika"

Aidha ameongeza kuwa mpango mkakati wa UTPC unazingatia malengo makuu matano ambayo ni kukuza uwezo wa kitaaluma wa waandishi wa habari,Kukuza Uhuru wa kupata taarifa na Uhuru wa habari,kuhakikisha klabu za waandishi wa habari zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kuweka mifumo mizuri na thabiti ya usimamizi wa klabu,kuhakikisha ulinzi na usalama wa waandishi wa habari na maslahi yao unazingatiwa pamoja na kuhakikisha UTPC inakuwa na mifumo mizuri inayochangia utekelezaji wa shughuli za UTPC kwa ubora zaidi.

"Tunafahamu jukumu letu kama waandishi wa habari ni kuleta mabadiliko chanya kwa jamii yetu,hasa kwa kuwa sekta ya habari ina jukumu kubwa katika kutoa habari za ukweli na kujenga jamii yenye taarifa na maarifa ili iweze kufanya maamuzi sahihi"

UTPC kwa kushirikiana na wadau wadau wa habari,ikiwemo serikali,wadau wa maendeleo kama vile ubalozi wa Sweden,Uswis na Marekani na wadau wengine ndani ya nchi,itaendelea kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanaendelea kupiga hatua katika kufanya kazi zao kwa Uhuru zaidi bila vitisho wala kuingiliwa.

Naye Zamaradi Kawawa ambaye ni afisa wa Serikali akizungumza kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa serikali na mkurugenzi idara ya habari Maelezo amesema kuwa wanaishukuru UTPC kwa kuwa na ofisi zake makao makuu ya nchi kwani itawasaidia waandishi wa Dodoma kuweza kutatua changamato mbalimbali kwani wataweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo viovu na kuhakikisha kunakuwa na usawa huku waandishi wakifanya kazi yao kwa uadilifu bila kuingiliwa na mamlaka yeyote hivyo uwepo wa UTPC utasaidia kulinda maadili ya sekta ya habari kwa makao makuu ya nchi.