Akizungumza
katika kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho inayoendelea kwenye
hospitali ya Wilaya Mbarali Bw. Antony Ndwenywa(83) kutoka kitongoji cha
Mkanyageni-Rujewa ambaye alifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho macho
yake mawili mwezi Disemba 2022, amesema tangu amefanyiwa upasuaji
anaendelea vizuri na hivi sasa anasoma hata magazeti
"Mimi
nilifanyiwa macho yote mawili yalikuwa na mtoto wa jicho na hadi sasa
naendelea vizuri.Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia huduma sisi watu wa
chini ,huduma hizi ni bila malipo ninashukuru sana.
Naye, Bi.
Vailet Mbelewele mkazi wa Mabadaga ambaye alikua na mtoto wa jicho kwa
muda wa mwaka mmoja amewashukuru watoa huduma wakiwemo madaktari na
wauguzi kwa huduma nzuri walizompatia na kuongeza kuwa ametolewa bandeji
na sasa anaona.
Amesema mara baada ya kupata tatizo hilo alikua
akinunua dawa kwenye maduka bila ushauri wa madaktari "nawashauri
wananchi wasijinunulie dawa mje moja kwa moja kwani madaktari wapo na
huduma ni nzuri".
Vilevile Mzee Ahmed Abdallah Mkazi wa Igurusi
ambaye alishakwisha fanyiwa upasuaji wa jicho moja miaka miwili
iliyopita na kwa kambi hii amefanyiwa upasuaji jicho la pili
amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wake wa
chini kwa jitihada zake kwa kuwasaidia watu wa chini.
"Tunamshukuru
Mama kwa kutusaidia mambo mengi kama barabara,ametuletea mbolea,natoa
sifa kwa Dkt. Samia anatuhudumia sisi watu wa hali hii kwani habagui na
hachagui.
Kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho wilayani Mbarali
imeanza tarehe 11 Aprili,2023 na inatarajiwa kumalizika tarehe 20
Aprili,2023.Inaratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la
Hellen Keler International la hapa nchini.
Home »
» WAKAZI WA MBARALI WAIPONGEZA SERIKALI KWA MATIBABU YA MACHO*
WAKAZI WA MBARALI WAIPONGEZA SERIKALI KWA MATIBABU YA MACHO*
Wakazi wa Mbarali wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau
wa huduma za macho kwa kuwapatia matibabu ya macho bila malipo.
0 Comments:
Post a Comment