Subscribe Us

MASHINDANO YA RIADHA MEI MOSI MOROGORO, UTALII WAZIDI KUTANGAZIKA*

 


Wizara ya Maliasili na Utalii  imeibuka  mshindi namba moja kwenye mbio za mita 800 kwenye  mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea  mkoani Morogoro.

Akizungumza leo mkoani humo mara baada ya ushindi  Elibariki Buko ambaye ndio mshindi namba moja wa mbio za mita 800 kutoka Wizara hiyo,  amesema ushindi huo utasaidia kuimarisha michezo na kuutangaza utalii Ili kuunga mkono juhudi  Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya 'The Royal Tour' za kutangaza utalii.

" Ushindi huu ni muhimu sana kwetu, tunaushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuhamasisha michezo. Ushindi huu ni moja ya sehemu ya kusaidia juhudi za kutangaza utalii kupitia filamu ya The Royal Tour ya Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. SAMIA Suluhu Hassan." alisema Buko.

Naye,  Afisa Utalii Mkuu na mmoja kati ya Viongozi wa Timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii,  Martin Mrema amesema Wizara  itahakikisha inaendelea kupambana ili kushinda michezo iliyobakia.

" Tumefurahi tumeshinda riadha, lakini si riadha tu, tumekuja kupambana na tutahakikisha tunatangaza utalii kupitia michezo. alisema.

Jumla ya michezo 10 imechezwa, kwa upande wa wanaume mbio za  za mita 1500 Elibariki Buko alishika nafasi ya  02 ,huku mbio za mita 3000 Kispani Saigoti akishika nafasi ya 02 huku Athumani Simbiri  akishika nafasi ya 03 katika mbio za mita 300 na 400.

Kwa Upande wa wanawake, mbio za mita 800 Jehovanesa Sarakikya alishika nafasi  03 na mbi


o za mita 1500  akishika nafasi ya 03.

0 Comments:

Post a Comment