Home »
» VIONGOZI WANACHAMA SOMENI KATIBA TUJIBIZANE KWA HOJA
VIONGOZI WANACHAMA SOMENI KATIBA TUJIBIZANE KWA HOJA
Na. Kadala Komba Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM) Kenneth Nollo amewataka wanachama na Viongozi wa chama cha mapinduzi ccm Wilayani humo kusoma na kuielewa vyema katiba,kanuni na tarabitu za chama Ili kufanya majukumu yao vyema pasipo kuyumbishwa na mtu.
Nollo ametoa kauli hiyo wakatai wa kikao cha Halmashauri kuu ya Ccm Wilaya ya Bahi kilichofanyika Wilayani humo.
Nollo amefafanua kuwa ,hivi Sasa kumekuwa na baadhi ya watu wanajivika vyeo sio vyao na kuwakalipia wengine hivyo ni Vyema wakajibizana kwa hoja.
"Napenda nisisitize kuwa Kila Mwanachama akisoma vyema katiba atatambua wajibu wako kama Kiongozi na Kazi za chama wapi unatakiwa,amesema
"Mimi kama mbunge nimeendelea kutekeleza Kazi zangu za jimbo na sasa tunaona jimbo hili lina Sura tofauti,tunakamilisha shughuli mbalimbali za miundo mbinu Kazi iliyopo mbele ni kujiimarisha zaidi kwa kiasi kikubwa,"amesema Nollo.
Licha ya hayo amesema kuwa Kazi za maendeleo zinafanyika tumeona Barabara, Zahanati, Shule madaraja na hivyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Donald Mejeti amesema Kazi waliyonayo wanachama ni kuhakikisha huduma zilizo kusudiwa zinasimamiwa na zinatekelezwa.
Mejeti amebainisha kuwa katika Halmashauri hiyo kimejekwa kituo cha Afya Kazi yetu Viongozi wa chama ni kuhakikisha wataalamu wa Afya wanatoa huduma bora hivyo ni Vyema wakasimama imara kuwatetea Wananchi wetu.
Naye Katibu wa Ccm (wanawake) Bahi Pauline Lupamba amewapongeza Viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWISHO
MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM) Kenneth Nollo Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Ccm Wilaya ya Bahi kilichofanyika Wilayani ukumbi wa Halmashauri Bahi
Mwenyekiti wa Halmashauri na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Donald Mejeti
Athman Masasi Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Bahi
Katibu wa Ccm (wanawake) Bahi Pauline Lupamba akisalimiana na wajumbe wa chama wakati wa Ufunguzi wa Kikao
mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe Godwin Gondwe Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa miradi
Stewart Masima Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bahi Akiwapongeza Viongozi wanachama kwa kusimamia vyema miradi ya wilaya
0 Comments:
Post a Comment