Na.Mwandishi wetu Mbeya
Katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, ikiwemo Krismas na Mwaka mpya timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya City ikiongozwa na viongozi wake wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Kitengo cha Wazazi META kwaajili ya kutoa zawadi na kuwafariji wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kurudusha kwa jamii.
Akiongea kwa niaba ya Uongozi wa Timu ya Mbeya City, Paul Nonga mcheza wa timu hiyo amesema hii ni sehemu ya utaratibu wao kama timu lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii, hivyo wametembelea Hospitalini hapo kwa lengo la kuwafariji wagonjwa pamoja na kutoa zawadi zikiwemo Sabuni, Mashuka 50, Dawa za Meno, mafuta, pamoja na Mifuko maalumu kwaajili ya kubebea vitu.
“Timu ya Mbeya City pamoja na Mdhamini wetu (Peri March) tumeweza kukabidhi Mashuka 50, na hii ni moja ya vitu huwa tunavifanya kwaajili ya Kurudisha kwa jamii.” – Paul Nonga.
Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Wazazi Meta, Muuguzi wa Zamu Bi. Fatuma Saimoni ameushuru uongozi wa Timu hiyo na kuwasihi wandelee kuwa na moyo huo wa upendo wa jamii.
“Kwa hiyo tunashukuru kwa watu wa Mbeya City kwa kweli mna upendo, sisi kama wana META tunawashukuru sana Mungu aendelee kuwabariki kwa upendo huu.” - Fatuma Saimoni
MATUKIO YA PICHA TIMU YA MPIRA WA MIGUU MBEYA CITY WAKIWA NA VIONGOZI WAKITEMBELEA HOSPITAL YA RUFAA KANDA YA KATI KITENGO CHA WAZAZI
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
UONGOZI DOREFA WAAGIZWA KUFUTILIA MAENEO YALIYOTENGWA KWAJILI YA MICHEZO
Na Kadala Komba Dodoma
Wanamichezo nchini waaswa kupambania tasnia ya michezo ikiwa ni agenda ya kuhakikisha tasnia hiyo inapewa thamani na kipaumbele kama sekta zingine.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa michezo Nchini Ndg.Ally Mayai Tembele wakati akizungumza na wadau wa soka kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mpira wa miguu jijini Dodoma(DOREFA) uliofanyika ukumbi wa dear mama hotel.
Mayai amesema kuwa ili tasnia hii ya michezo iendelee kukua ni wajibu wa kila mwanamichezo kuwajibika kwa nafasi yake na hii itasaidia kukua kwa tasnia hii bila kusahau kuwa na nidhamu kwa kila mmoja kumuheshimu mwenzake bila kujali cheo.
Nawapongeza chama cha soka cha Mkoa wa dodoma kwa kuweza kufanya kazi bila kuwa na tofauti katika utendaji na hii itasaidia soka la Dodoma kuweza kukua kwa kasi kwani maendeleo bora huletwa na viongozi bora"Amesisitiza Ndg.Mayai
Aidha ameongeza kuwa anawapongeza Dodoma kwa kuwa na programu ya vijana chini ya miaka 20 kwani itawasaidia vijana kukua kisoka na kuweza kuvumbua vipaji wakiwa bado na umri mdogo.
"Milango ya serikali ipo wazi kwa yeyote mwenye nia njema na tasnia hii na tunawakaribisha wadau wote kuweza kujitokeza kusapoti vipaji vya watoto wetu kwani kila mtu anaelewa mpira ni ajira kwa ajili ya kukuza uchumi na kuondokana na umasikini na kila mtu ameshuhudia namna ambavyo familia nyingi zimejikwamua kiuchumi kupitia michezo"
Aidha ametoa rai kwa wadau wa mpira wa miguu kuingia mitaaani kwenda kusaka vipaji,kwani huko ndiko kwenye chimbuko la mpira wa miguu na hata historia ya watu wengi maarufu waliofanikiwa kwenye soka historia yao inaonyesha wametokea mitaani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu jijjni Dodoma (DOREFA) amesema kuwa anawashukuru wadau wa soka jijini hapa kwa kuendelea kutoa maoni na ushauri ili kuhakikisha wanaboresha sekta ya michezo haswa mpira wa miguu jijini Dodoma.
Naye mwakilishi wa wanamichezo jijini Dodoma amesema sekta ya michezo iko vizuri ila wanaiomba serikali chini ya Waziri wa michezo Mohamed Ncheregwa kutatuliwa changamoto inayojitokeza mara kwa mara ya uwanja wa jamuhuri kufungiwa mara kadhaa kutokana na matumizi mengine ambayo ni tofauti na michezo hivyo kufanya wapenzi wa soko jijini hapa kukosa burudani ya mpira wa miguu na kutumia viwanja vingine vilivyopo nje ya Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa michezo Nchini Ndg.Ally Mayai Tembele wakati akizungumza na wadau wa soka kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mpira wa miguu jijini Dodoma(DOREFA) uliofanyika ukumbi wa dear mama hotel.
mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu jijjni Dodoma (DOREFA)Mohamed All Akiwashukuru wadau wa soka kwa kuendelea kutoa maoni na ushauri
MATUKIO YA PICHA ZA WAJUMBE MKUTANO MKUU NA WAALIKWA
PICHA YA PAMOJA MGENI RASMI NA WAJUMBE WA SOKA
MKUU WA MKOA DODOMA MHE. ROSEMARY SENYAMULE AMEPOKEA HATI YA PONGEZI KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea hati ya pongezi kutoka kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita kwa kutambua mchango wake na kuleta mageuzi katika kipindi ambacho amekua Mkuu wa Mkoa huo.
Hati hiyo imewasilishwa leo tarehe 19/12/2022 na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko akiambatana na Katibu wake Bw. Novatus Lyaruu.
Bw. Masuguliko amesema kwa takribani mwaka mmoja ambao Mhe. Mkuu wa Mkoa Bi. Senyamule amekuwa mkoani Geita, amefanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta zote na kumpongeza kwa kusimamia kwa vitendo kaulimbiu aliyoianzisha ya “Geita ya dhahabu, Utajiri wa heshima”
“Mkuu wetu wa Mkoa Mhe. Senyamule alivyokuja na hii kaulimbiu mwanzoni hatukumuelewa, lakini kwa kipindi kifupi amefanya mengi katika sekta ya elimu, afya, miundombinu, maji, uchumi na uzalishaji, hivyo watu wa Dodoma mna bahati ya kupata kiongozi mahiri” Amesisitiza Bw. Masuguliko.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amekishukuru Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita kwa kumpa tuzo ya heshima kwa kutambua mchango alioutoa akiwa Geita.
Amepongeza uongozi wa Chama hicho kwa kuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi kwa weledi na maarifa na kusisitiza kuwa kazi hiyo iwe endelevu ili jamii iweze kunufaika na kufahamu mambo ambayo Serikali imekuwa ikitekeleza katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Bw. Mussa Yusuph na Katibu wake Bw. Ben Bago ambao pia waliambatana na ugeni huo kutoka Geita, wamesema jitahada zinaendelea ili Makao Makuu ya Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania yahamie katika Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipokea hati ya pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko kwa kutambua mchango wake na kuleta mageuzi kwa kipindi ambacho alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Hati hiyo ya pongezi amekabidhiwa leo tarehe 19/12/2022 Ofisini kwake Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kupokea hati ya pongezi ya kutambua mchango wake na kuleta mageuzi kwa kipindi ambacho alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma Bw. Mussa Yusuph, Bw. Novatus Lyaruu Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita na Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma Ben Bago.
RWANDA KUBADILI MUDA WA MASOMO SHULE ZOTE IFIKAPO MWAKA 2023
Rwanda wamebadili muda wa kuanza na kumaliza masomo na saa za kazi. Kuanzia Januari 01 2023, Shule zote zitaanza masomo saa 2:30 asubuhi na kumaliza saa 11 jioni.
Saa za kazi ni kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni. Hii kuwaongezea muda wa kulala watoto kwani wanaamshwa alfajiri sana na wanasinzia shuleni. Na pia ni kuwawezesha wazazi waweze kuwaona watoto wao na kunywa nao chai kabla ya kwenda shule/kazini.
WACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASA
WACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASA.
Wachakataji wa mazao ya uvuvi nchini wametakiwa kutumia fursa ya teknolojia katika shughuli zao ili kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi na kukabiliana na upotevu wa mazao hayo katika Ziwa Tanganyika.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji, wavuvi na wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kupitia miradi yake ya FISH4ACP na Flexible Multi-partner Mechanism (FMM) mafunzo ambayo yamefanyika mkoani Kigoma.
Afisa huyo amesema mradi wa FISH4ACP unatekelezwa katika nchi 12 za Africa, Caribbean na Pacific ambapo nchini Tanzania unafanyika katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ukilenga kukabiliana na changamoto za upotevu wa mazao ya samaki kabla na baada ya shughuli za uvuvi, wakati wa uchakataji wa samaki na wakati wa kusafirishwa kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
“Mafunzo haya yamefanyika kwa njia ya filamu zilizonakiliwa kutoka Kenya, Uganda na Ghana lengo ni kuwawezesha wachakataji kujifunza njia bora za kuchakata mazao yao kama tulivyoona kwa wenzetu wanatumia majiko banifu, chanja rafiki na salama za kuanikia dagaa,”Amesema Afisa huyo.
Pia ameongeza kuwa kupitia miradi hiyo wanatarajia kujenga miundo mbinu ya kuchakatia dagaa na samaki itakayoendana na mabadiliko ya tabia Nchi ambapo kwa sasa hatua zilizochukuliwa ni ufuatiliaji wa maeneo sahihi ya kuchakatia.
“Kama mradi tutatengeneza majiko ya kubanikia samaki tupate bidhaa nzuri kutoka Ziwa Tanganyika na tutaendelea na ufuatiliaji kuona kama mafunzo haya yanatafanya kazi kama tulivyokusudia na yatasaidia changamoto iliyopo sasa ya mabadiliko ya tabianchi ,”Ameeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala la Udhibiti Ubora wa Mazao ya Uvuvi na Masoko, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bw. Steven Lukanga amebainsiha kuwa sekta ya uvuvi inachangia karibu asilimia 1.8 ya pato la Taifa wakati ulaji ukichangia asilimi 30 ya virutubishi vitokanavyo na wanyama.
“Ulaji wetu unaonekana tunakula wastani wa kilo 8. 5 badala ya kilo 20.5 kwa mwaka hivyo mafunzo haya yamekuja wakati muafaka yatasaidia kuboresha shughuli zetu tunazofanya hasa unapovua samaki wako au dagaa uhakikishe unawahifadhi sehemu salama na hata ukaushaji wetu uwe wenye manufaa kimasoko,”Amefafanua.
Naye Afisa Uvuvi anayesimamia Wilaya ya Uvinza Bw. Venance Msongambele amesema elimu hiyo itawasaidia wadau wa uvuvi na wachakataji kuepuka kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake watakausha samaki kwa kutumia mkaa hatua inayoongeza thamani ya mazao hayo na kuvutia wateja.
“Kuna maboresho ambayo yakifanyika yatatusaidia sana kama kupata barafu kuhifadhi samaki na dagaa, majiko ya mkaa kwa sababu kuni siyo salama kwa afya kutokana na moshi na kupitia mafunzo haya tumejifunza kufanya uchakataji kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira,”Ameeleza Afisa huyo.
Akitoa shukrani zake Mchakataji kutoka Mwalo wa Katonga mkoani Kigoma Selestina Silvester ameipongeza FAO kwa kuandaa semina hiyo kwani itawasaidia katika uhifadhi wa rasilimali za Ziwa Tanganyika kwa manufaa yao na Nchi kwa ujumla.
“Tunaishukuru sana FAO kwa kutoa na elimu hii inatusogeza kutoka hapa tulipo hadi sehemu nyingine kwa sasa uchakataji tunafanya kienyeji sasa unakuta samaki au dagaa wanaharibika haraka kabla ya kufika sokoni na wanapungua ubora,”Amesema Selestina. Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin
Aidha Mwenyekiti wa Vyama vya Wavuvi Mkoa wa Kigoma Bwa. Francis John amewahimiza wadau hao kutumia ujio wa mradi huo kama fursa muhimu kwao kuongeza thamani ya bidhaa zao ili kuendana na hali ya soko la sasa.
MWISHO
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala la Udhibiti Ubora wa Mazao ya Uvuvi na Masoko, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bw. Steven Lukanga akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji wa mazao ya uvuvi Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma (kulia ) ni Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin .
Picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo.
Baadhi ya wadau wa sekta ya uvuvi wakiafuatilia mafunzo hayo kutoka kwa wawezeshaji(hawapo pichani).
Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji wa mazao ya uvuvi mkoani Kigoma.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mwalo wa Kibirizi mkoani Kigoma wakiendelea na biashara zao.
JAMII YAHIMIZWA KUPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI.
Na mwandishi wetu- Dodoma
JAMII YAHIMIZWA KUPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ameitaka jamii, wadau na kila mmoja kwa nafasi yake kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Dkt. Jingu ameyasema hayo Jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kuhusu mafunzo ya Usawa wa Kijinsia na Tathimini ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), Jijini Dodoma.
Amesema licha ya mafanikio yaliyopo kufuatia juhudi zinazofanywa kukabiliana na vitendo hivyo lakini bado ukatili umeendelea kufanywa hivyo ipo haja ya kuwa na afua mbalimbali za kuwatetea manusura wa vitendo hivyo.
“MTAKUWWA lengo lake ni kutokomeza ukatili wa aina zote unaofanywa katika jamii zetu sasa ukatili bado upo hivyo tumekubaliana kila mmoja wetu awe kinara wa mabadiliko chanya kuhakikisha tunakuwa na malezi bora, afua za kuyalinda makundi yote,”Amesema Dkt. Jingu.
Vilevile ametoa wito kila kundi kwa nafasi yake Wizara za Kisekta, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Kimataifa, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Viongozi wa Dini, Wazee wa Kimila na Vyombo vya Habari yana sehemu ya kufanya kwa kuongeza juhudi za kuimarisha usawa wa jinsia na kutokomeza ukatili .
“Nitoe rai tuendelee kushirikiana ili tuweze kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii na kufikia malengo na mikakati tuliyojiwekea na nishukuru wadau wote kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kuhakikisha makundi yote yanalindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia ,”Amefafanua.
Amebainisha kwamba miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuwepo kwa Mpango maalumu wa malezi ya vijana balehe ili waweze kukua katika maadili, kujitambua na kufahamu nafasi yao kwa jamii.
Sambamba na hayo Dkt. Jingu ameeleza kuwa uzingatiaji wa bajeti kwa mtizamo wa kijinsia katika Sera, Mipango na Bajeti za Wizara na Sekta utasaidia kuleta maendeleo endelevu katika nyanja zote za Kijamii.
“Uandaaji wa bajeti na mipango kwa mtizamo wa kijinsia una manufaa makubwa sana katika jamii yetu kama kushughulikia upungufu wa kijinsia hususan ule unaotokana na uwepo wa mahitaji tofauti baina ya wanawake na wanaume katika jamii au sehemu zetu za kazi,” Amesema.
Aidha aliwashukuru Wadau wa Maendeleo, Taasisi za serikali na binafsi, viongozi wa dini, kimila na mtu mmoja mmoja kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha usawa wa jinsia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewataka maafisa maendeleo kupitia ngazi ya Vijiji, Kata hadi Wilaya kutimiza wajibu wao kuhakikisha maendeleo yanapatikana, wananchi wanakuza uchumi wao na kushiriki katika maendeleo kwa kulipa kodi.
“Kupitia mafunzo haya tumeongea mambo mengi yakiwemo mpango wa Kitaifa wa malezi kwa makundi ya vijana balehe ambao una malengo mengi kama kuzuia UKIMWI, mimba za utotoni, ajira na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kumuandaa mtoto kuwa kiongozi bora kuanzia ndani ya familia,”Ambainisha Dkt. Zainab.
Aidha Mratibu wa MTAKUWWA, Bw. Joel Mangi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ameeleza kuwa tangu kuanza kwa mpango huo mwaka 2017/18 na 2021/2022 ambao umekamilika na kufanyika kwa tathmini ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwemo kuongezeka kwa uelewa ndani ya jamii, uanzishwaji wa vituo 21 vya huduma kwa manusura wa ukatili ambapo vinafanya kazi nchi nzima.
“Mwelekeo katika awamu ijayo tumependekeza kuanzishwa kwa kampeni jumuishi ya Kitaifa itakayoleta sekta zote pamoja kupaza sauti , tuimbe kupinga ukatili huu jamii ijue vitendo hivi havifai kwa sababau vinazorotesha ustawi hasa kwa watoto ,”Amesema Mratibu huyo.
MWISHO
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kuhusu mafunzo ya Usawa wa Kijinsia na Tathimini ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
“UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU
“UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU
NA MWANDISHI WETU - DODOMA
Watafiti wa masuala ya kilimo nchini wametakiwa kutumia matokeo ya utafiti wao wanaofanya katika kuboresha mbegu bora za mazao zinazoendana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwa na tija katika sekta .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu wakati akifungua warsha ya kuelimisha wadau kuhusu Kazi za Muunganiko wa Taasisi za Kimataifa za Utafiti wa Kilimo (CGIAR) Jijini Dodoma.
Dk. Jingu amesema lengo kuu la warsha hiyo ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kwa kuboresha uratibu wa miradi ya OneCGIAR kwa kuzingatia utafiti utakaongeza uzalishaji.
“Kupitia Mkakati wa Utafiti na Ubunifu wa Mwaka 2030 CGIAR imeanzisha mkakati unaojulikana kama OneCGIAR ambao unalenga kufanya utafiti na maendeleo sasa ili tukuze sekta zetu za kilimo, mifugo na uvuvi lazima tuwekeze katika utafiti na maendeleo hivyo mkakati huu utasaidia katika uzalishaji na tija,” Amesema Katibu Mkuu huyo.
Pia alihimiza kwamba utafiti wa mbegu unaofanyika usaidie kuleta tija na faida katika shughuli za wakulima, wavuvi na wafugaji pamoja na kuendeleza ugunduzi wa mbegu mpya hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa.
“Hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo utafiti tunaoufanya uendane na hali ya hewa ya kipindi husika ukizingatia sasa hivi misimu ya mvua imebadilika kwahiyo tunahitaji mbegu zinazoendana na mazingira na namna ya kukabiliana na wadudu waharibifu,”Alieleza .
Katika hatua nyingine alisisitiza ushirikishwaji wa vijana katika sekta ya kilimo akisema licha ya uwepo wa sekta zingine kilimo kitaweza kustawi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi endapo vijana watawezeshwa kikamilifu.
“Vijana ili washiriki vizuri kilimo wanahitaji elimu , mafunzo kwa vitendo na namna ya kutumia fursa ya ukuaji wa teknolojia katika shughuli zao za uzalishaji wenye matokeo chanya na wafanye kwa tija itasaidia vijana kujikwamua kiuchumi wao wenyewe na kushiriki katika pato la Taifa,”Alisisistza Dk. Jingu.
Aidha alishauri uwepo wa ushirikiano kati ya Wizara za kisekta na wadau wa maendeleo kwa kuanzisha miradi mikubwa itakayoleta matokeo chanya katika sekta hizo muhimu kupitia mkakati huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Dk. Geoffrey Mkamilo alibainisha kwamba kufanyika kwa utafiti wa mbegu kunasaidia kubaini hali ya mbegu, changamoto na namna ya kuboresha uzalishaji wake utakaoendana na kipindi husika.
“Warsha hii inatuweka pamoja kama wataalamu na wizara za kisekta kubalishana uzoefu na namna ya kufanya utafiti wenye manufaa katika sekta zote za kilimo. Mifugo na uvuvi kubaini mbegu bora na wakati husika wa kuzifanyia kazi ziweze kuzalisha mazao bora kwa jili ya kuimarisha lishe na kipato,”alieleza Mkurugenzi.
Naye Mtaalamu kutoka OneCGIAR Dk. Regina Kapinga alifafanua kwamba licha ya kufanya utafiti unaowezesha mazao kuhimili mabadiliko ya tabia nchi pia unazingatia uboreshaji wa virutubishi katika mazao ya uvuvi, mifugo na mimea.
MWISHO
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya kuelimisha wadau kuhusu Kazi za Muunganiko wa Taasisi za Kimataifa za Utafiti wa Kilimo (CGIAR) iliyofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akitembelea mabanda baada ya kufungua warsha hiyo
ASKOFU DKT CHANDE AMETOA MSAADA KWA YATIMA NA WAJANE
DODOMA
Askofu Dkt Evance Chande wa Kanisa la Karmeli Assemblis Of God la jijini Dodoma Leo ni siku muhimu Kwa watoto yatima,wajane na waishio katika mazingira magumu kupatiwa misaada mbalimbali kutoka. ujumbe Dini iliyo nzuri ni kuwajali yatima na wajane
MKURUGENZI WA MASHTAKA MWAKITALU AMETEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA DODOMA
Na. Mwandishi wetu Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ametembelea Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Maafisa wa Magereza katika kuwatunza wafungwa pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili mahabusu.
Akizungumza baada ya kutembelea Gereza Kuu la Isanga Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa lengo la kutembelea wafungwa na mahabusu ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa misingi ya sheria na kanuni zake.
'’kufanya haya yote ni kuona haki jinai inasimamiwa ipasavyo lakini tukipata hizi changamoto na kuzisikiliza tunaenda kuzifanyia kazi na kuzishughulikia. Changamoto tulizozipokea ambazo hazipo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka tunazichukua na kuzipeleka ofisi ambazo zinahusika lengo ikiwa ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo.Amesema DPP Mwakitalu
Hata hivyo,Mwakitalu amezitaja changamoto ambazo amezipokea katika ziara yake ambapo mahabusu wamezieleza ikiwa ni sula zima la ucheleweshwaji wa kesi na kuchelewa kwa upelelezi ambapo ameeleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kuzishughulikia changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa wameshasajili Hati za Mashtaka Mahakama Kuu ambazo hivi sasa zipo katika mchakato wa kusikilizwa.
'’Mahabusu wengi ambao nimewasikiliza wamesema kesi zao zimechelewa upelelezi ,lakini hali halisi ni kwamba kesi zao hazijachelewa upelelezi kwa kuwa tayari zimekamilika na kinachosubiriwa ni utaratibu wa kisheria ambao utawezesha kesi hizo kusikilizwa na Mahakama Kuu Amesema DPP Mwakitalu.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini imeanza mwendelezo wa ziara zake katika Magereza mbalimbali nchini kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa wa Magereza, wafungwa pamoja na mahabusu ili kuhakikisha Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Mwisho.