Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

MAAFISA ELIMU KATA, WALIMU WAKUU, WALIMU WA MAZINGIRA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA WAJENGEWA UWEZO JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI KATIKA MAZINGIRA YA SHULE BAHI

Na. Kadala Komba Bahi 
 
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson akifunga mafunzo hayo  kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji  wa Halmshauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Zaina Mlawa  ametoa maagizo kwa walimu wa mazingira na  wakuu wa shule za msingi kutunza mazingira ya shule na kupanda miti ya kutosha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya shule zao. Akitoa maagizo hayo ameeleza umuhimu  wa uwepo wa miti shuleni na ujenzi wa madarasa  unaozingatia vigezo vya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson
            akifunga semina ya mazingira  ya siku tatu
 
 
 
Hayo yamejiri wakati wa semina ya mazingira  ya siku tatu iliyohusu mafunzo kwa walimu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika shule zao. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi.

"Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Boniphace Wilson akifunga mafunzo hayo ametumia nafasi hiyo  kuishukuru serikali kupitia OR TAMISEMI kwa kuleta mafunzo hayo Bahi pia amewashukuru  wafadhili wa program hiyo ambao ni  Shule Bora kwa kutoa zaidi ya Milioni mia tatu,  kwajili kukamilisha maboma kumi na nane yaliyojengwa kwa kuzingatia vigezo vya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwezesha  mafunzo mbali mbali kwa walimu yakiwepo haya ya mazingira
 
 
picha ya pamoja meza kuu 

 








Kwa upande wa walimu wakiongea kwa niaba, walimu wenzao wa wilaya ya Bahi  mwalimu Kondo,  Mwashi Benedict Cheo na Mkuu wa shule  Bahi English medium bi Farida Aloyce  Wameishukuru serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuwaletea mradi wa mazingira chini ya program ya shule bora  ambao utaenda kubadilisha mazingira ya shule zetu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

.Naye Afisa maendeleo ya jamii kata ya Babayu wilaya ya Bahi Nasibu Saidi Amewashukuru wafadhili wa mradi wa mazingira Shule bora kwa kuwakumbuka kata ya Babayu.




RC SENYAMULE AIPA KONGOLE BAHI USIMAMIZI WA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI

 Ikiwa ni miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan kwenye kiti cha Urais na yamefanyika Maendeleo makubwa chanya
Kupitia shamlashamla hizo za miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amefanya ziara  Wilaya ya Bahi na kukagua Miundombinu ya hospitali ya Wilaya pamoja na miradi inayotekelezwa Katika Hospitali hiyo ikiwemo ukamilishaji wa mochuali ambao tayari lipo jokofu moja kwaajili ya kuhifadhia miili,pia amekagua jengo la kulazwa wanaume na jengo la kulazwa wanawake,

Kupitia ziara hiyo mkuu wa Mkoa ametembelea pia Zahanati ndogo iliyopo Nagulo kata ya Bahi ambayo ilizindiliwa siku za karibuni na kupitia ukaguzi wake ameridhishwa na huduma kwani Zahanati hiyo kwani imekua msaada mkubwa wa kuwahudumia Wananchi wa Nagulo Bahi waliokua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule ameipongeza sana Wilaya ya Bahi na uongozi wake kwa jitihada kubwa wanayoifanya ikiwemo usimamizi mzuri wa fedha za ujenzi wa miradi zinazotolewa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, na kupitia ziara hiyo amesisitiza kuwa dhana ya uwajibikaji bora iwe nguzo kuu kwa watumishi wote ili kuweza kuchochea maendeleo chanya ndani ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.


WAZIRI ULEGA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WA MIZANI KUPISHA UCHUNGUZI

 
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Balozi Aisha Amour, kuwasimamisha kazi wasimamizi wote wa Mizani waliokuwa zamu katika Mizani zilizopo katika barabara kuu ya T1 inayoanzia Dar es Salaam – Zambia kupitia mpaka wa Tunduma kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa malalamiko katika Mizani hizo.

Ulega amefanya maamuzi hayo mara baada ya kadhia iliyojitokeza hivi karibuni kwa msafirishaji Bi. Pamela James Bukumbi mwenye gari ya mizigo namba T 137 DLQ likiwa na tela T 567 CUR iliyotokea katika kituo cha Mizani ya Vigwaza akilalamika kuhusu kutozwa faini ya kuzidisha uzito katika Mizani hiyo wakati mizani nyingine alizopita gari yake haikuwa imezidisha uzito.

Ulega ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma leo tarehe 20 Machi, 2025 mara baada ya kupata taarifa hiyo na kusikiliza pande zote mbili kutoka kwa mlalamikaji na mlalamikiwa ambaye ni Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kubaini kuwa lipo tatizo la wazi ambalo limesababisha kadhia hiyo na kutoa maelekezo makuu matano.

“Baada ya kugundua liko tatizo, Nimeamua kuchukua hatua zifuatazo moja ni kuwasimamisha wale wasimamizi wetu wa Mizani wa hii T1 barabara nzima kuanzia Tunduma mpaka inafika pale Vigwaza waliokuwa kwenye zamu kwa siku ile wakati tukio linatokea”, amesema Ulega.

Ulega ameeleza kuwa amewasimamisha wasimamizi hao kwa lengo la kufanya uchunguzi ambapo tayari timu ya wataalam ya kuchunguza tukio hilo imeundwa ili kufuatilia safari nzima ya gari hilo ili kupata hali halisi na kuwasilisha mapendekezo mengine ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi ya wale wote ambao watabainika na vitendo visivyoridhisha.

Aidha, Waziri Ulega ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuanza hatua za kubadilisha mifumo ya uendeshaji wa Mizani 78 zote nchini haraka iwezekanavyo kwa kutangaza kwa watoa huduma wenye nia kuja na teknolojia ambazo ni ‘automated’ ili kupunguza muingiliano baina ya watu na watu na hivyo kumuwezesha dereva kujihudumia kwa kutumia mifumo jambo ambalo ni mkakati wa Wizara wa muda mrefu.

Aidha Ulega ameielekeza TANROADS kuhakikisha mifumo ya Mizani zote inasomana kutoka Mizani moja hadi nyingine ambapo jambo hilo limekuwa likisemwa na kusisitizwa mara kwa mara na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu mifumo katika Serikali kusomana na kuagiza utekelekezaji huo ufanyike haraka iwezekanavyo.

Ulega amewalekeza Mameneja wote wa TANROADS nchini kuwa nambari moja katika usimamizi wa Mizani zilizopo katika mikoa yao na sio kuwaachia wasimamizi peke yake na Mizani zitakazolalamikiwa na Mameneja husika pia watachukuliwa hatua.

“Kwa muda mrefu Mameneja wamekuwa wakijiweka kando sana katika usimamizi wa Mizani lakini hapo mbele tutaanza mara moja mizani zitakazokuwa zikilalamikiwa tutaanza kuwachukulia hatua na Mameneja na sio wasimamizi tu”, amesisitiza Ulega.

Vilevile, Ulega ameeleza kuwa Serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ambayo kwa ujenzi wa kilometa moja unaigharimu Bilioni moja hadi mbili kutegemea mazingira ya eneo husika ambazo zinahusisha fedha za umma na hivyo kutoa rai kwa wananchi kuona umuhimu wa kuilinda rasilimali hiyo kwa kutokana na uwekezaji wake pamoja na usalama wa watumiaji wa miundombinu hiyo.



MBUNGE WA JIMBO LA BAHI MHE. KENNETH NOLLO AMSHUKURU MHE.RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO BAHI

 
Na. Kadala Komba Bahi

Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo  kwa wananchi wa wilaya ya Bahi.

Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma Mhe. Rosemary  Senyamule  akikagua  miradi ya maendeleo  katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi katika hospitali ya wilaya Bahi,  tar 19/03/2025  alisema Hospitali hii nikama ndoto kwa wana Bahi ni ukombozi mkubwa sana sisi watu wa Bahi yunasababu zote kumshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan rais wetu kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea katika Halmashauri ya Bahi.

Katika sekta ya afya katika mwaka 2021hadi sasa mwaka 2025 vijiji kumi na saba vimepata  vituo vya Afya (Zahanati) ambapo awali vijiji kumi na tisa vilikuwa havina kituo cha afya  (Zahanati)


MSAKO MKALI WALIOGUSHI VYETI VYA JKT

 
Na. Angel Haule Dodoma

Jeshi la kujenga taifa JKT kimetoa onyo kwa watu wanaogushi vyeti vya Jeshi Hilo vinavyoonesha wamepitia mafunzo ya JKT na kutumia kama sifa ya kuombea kazi sehemu mbalimba Nchini, wakati watu hao hawajawahi Kupitia mafunzo yoyote ndani ya jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari  katika Makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Jijini Dodoma Kaimu mkuu wa tawi la utawala JKT KANALI JUMA MRAI amesema,

Hivi karibuni JKT imebaini uwepo wa vyeti vya kugushi vilivyotumika na baadhi ya vijana ambao sio waaminifu ili kujipatia ajira katika taasisi na makampuni yanayohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya JKT.

Kaimu  Mkuu huyo wa tawi la utawala JKT ameongeza kuwa JKT inapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa, wale wote waliobainika na watakaobainika kugushi cheti Cha JKT kwa matumizi yoyote yale na hatua Kali za kisheria zitachukukiwa dhidi yao

Aidhi KANALI JUMA MRAI amesisitiza kuwa Jeshi la JKT lipo teyale kutoa ushirikiano kwa taasisi na makampuni yote yanayohitaji uhakiki wa vyeti vya JKT kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya jeshi hilo.

Katika hatua nyingine Jeshi la kujenga Taifa JKT Kupitia Kaimu huyo wa tawi la utawala JKT JUMA MRAI limesema jeshi hilo kinaendelea nafasi za kujiunga na mfunzo ya JKT zinatolewa Kila mwaka kwa vijana wa kitanzania wenye sifa , ili wamalizapo mafunzo ya JKT waweze kupata cheti Cha kuhitimu mafunzo hayo kihalali.


Akizungumza na waandishi wa Habari  katika Makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Jijini Dodoma Kaimu mkuu wa tawi la utawala JKT KANALI JUMA MRAI 


 


Baadhi ya waandishi wa Habari  katika Mkutano makuu na  KANALI JUMA MRAI Jijini Dodoma

WANACHAMA WAPYA 20 WA CUF WAKABIDHIWA KADI

 


Na Mwandishi Wetu, Kondoa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara)  Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua  wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho ili wakazuie bajeti zinazowakandamiza Watanzania.

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani Dunga aliwataka wananchi kuchagua wabunge na madiwani ili wakazuie bajeti zinaxowakabili wananchi.
Alisema kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.

Alisema kuwa kwa sasa asilimia 99 ya wabunge wanatatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Alisema kuwa iwapo wananchi watakichagua chama hicho, watauza mazao yao vizuri,tofauti na sasa wananchi wanalazimishwa kuuza mazso kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wamekuwa wakiuza kwa mkopo.


"Hospitali nyingi zimejengwa lakini  hakuna huduma,hakuna dawa  lakini CUF itahakikisha huduma zinaboreshwa hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa wakipata adha kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, "alisema

Alisema kuwa umaskini wa wananchi sio laana ya Mungu , CUF  ikishika dola itafanikisha mambo mengi ikiwemo wazee watapata posho ya kujikimu kila mwezi, "alisema.

Alisema kuwa elimu bure haijaleta matokeo mazuri kwa wananchi kutokana na shule nyingi kuwa na michango mingi inayozidi hata ada zilizoondolewa.


Katika mkutano huo zaidi ya wanachama wapya 20 walikabidhiwa kadi.
Mkazi wa Kondoa, Hamidu Mkopi alitaka wananchi kuziishi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwisho




ALIYENG'OA BENDERA YA CUF ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

 
Na Mwandishi Wetu,, Kondoa

MTU mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa  bendera na mabango ya Chama cha Wananchi (CUF)   wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa (Bara)  Othman Dunga).

Wakizungumzia tukio hilo,  Mjumbe wa kamati tendaji CUF wilaya ya Kondoa, Ayubu Hamisi alisema kuwa asubuhi ya Machi 7 mwaka huu, wakati wakiwa katika maandalizi ya kumpokea Makamu Mwenyekiti Othuman Dunga kulitokea  jambo la kusikitisha ambapo  vijana wanaosadikiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  waliingia mitaani na kung'oa bendera 13 na mabango 25 .

Alisema kuwa baada ya kufanya msako waliweza kumkamata kijana mmoja ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliofanya uhalifu huo na sasa anashikiliwa na Jeshi la polisi.

Mwanachama wa Chama hicho, Hadija Selemani alisema kuwa kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimewasikitisha sana. "Tulikuwa tumejiandaa vizuri wanachama wamefika wakiwa wamevalia sare zao vizuri kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao lakini kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimetusikitisha sana," alisema na kuongeza.

"Jambo hili limetusikitisha sana kwani kwa mara ya kwanza Kondoa inapata kiongozi  mwenye wadhifa mkubwa, lakini wasiotutakia mema ,wameshusha bendera, waking'oa mabango  ,kinachofanyiika ni mbinu za kuua siasa za upinzani jambo ambalo  limeleta taharuki,"alisema

Mwanachama mwingine wa chama hicho Nassoro  Junguke  alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitaka kuendeshwa kwa siasa za kistaarabu lakini baadhii ya watu wamekuwa wakifanya vitendo vinavyohatarisha amani iliyopo.

"Wakishusha tena bendera za CUF sisi hatutaenda polisi wataenda wao ,Jambo kama hili halikubaliki katika demokrasia yetu, "alisema.
Pia alisema walifanya msako na kufika hadi nyumba inayoficha wahalifu, walibaini wahalifu waliofanya tukio hilo ambao wamekuwa wakitembea na kapu la kukusanyia bendera wanazong'oa.

Pia alisema Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kondoa amewafuata na kuwataka waondoe bendera kwenye nguzo.
Alisema kuwa jambo hilo limewatafakarisha   sana kwani nguzo nyingi hata mahali panye nyaya bendera za CCM zinapepea lakini bendera za CUF hazitakiwi.
"Watendaji wa serikali wasiingizwe kwenye mitego ya siasa wafanye kazi za kutoa huduma kwa wananchi,"alisema
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kupokelewa wilayani Kondoa Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga,, alisema hiyo ni mara ya pili bendera za chama hicho zinang'olewa wakati chama hicho kikiwa na mikutano.
Alisema kuwa tukio  kama hilo lilitokea Julai mwaka jana wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipofika Kondoa ambapo bendera zaidi ya 60 ziling'olewa siku moja kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano.
"Huo ni uoga tushindane kwa hoja na sio kung'oa mabango na kuleta taharuki, "Alisema
Dunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kondoa alisema kuwa bendera ni alama ya chama tu .
"Wakati wengine wakihangaika kushusha bendera sisi  tunahangaika kutafuta wanachama wapya wajiunge na chama.
Nyie ng'oeni bendera  sisi tutaiba nyoyo za watu ili wajiunge kwa wingi na CUF, "alisema.
Dunga alichaguiliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania bara Desemba mwaka jana.

Alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, George Katabazi alisema kuwa taarifa kamili hazijamfikia anafuatilia suala hilo na atatoa taarifa ..Kaption




1.Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Wananchi (CUF) Taifa IBara)  Othuman Dunga akizungumza na wanachama na wananchi wa wilaya ya Kondoa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa kwa ajili ya kumpogeza kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ,mnkutano huo ulifanyika katika uwanja wa stendi ya zamani jana.,


2Makamu Mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi (CUF) Taiifa (Bara) Othuman Dunga akiwasalimia wanachama wa CUF wa wilaya ya Kondoa waliokuja kumpokea kwa ajili ya kufanya mkutano wa kumpongeza  kwa kucahaguliwa kwake kushika wadhifa huo.


3.Wanawake wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kondoa  wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga (hayupo pichani) baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa kwa ajili ya kupongeza uliofanyika jana