This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
*Waziri Nape Afanya Mazungumzo na Balozi wa Finland Tanzania*
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Theresa Zitting Ofisini kwake jijini Dar es Salaam aliyeambatana na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi huo, Bw. Juhana Lehtinen na Mkurugenzi wa Nokia nchini Tanzania Amouneu Lopy.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Machi 25, 2024 na yamehusisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika sekta ya TEHAMA hasa kwenye vipengele vya elimu ya TEHAMA, ubunifu na kukuza teknolojia na matumizi ya TEHAMA katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Waziri Nape amesema kuwa ushirikiano baina ya Finland na Tanzania umekuwa na mchango mkubwa katika kukuza Sekta ya TEHAMA nchini na kuzungumzia Mradi wa TANZICT (2011-2016) uliotekelezwa baina ya Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Finland ndio uliowezesha uandaaji wa Sera ya TEHAMA ya mwaka 2016.
Ameongeza kuwa sera hiyo ilikuwa msingi wa kutengeneza sheria nzuri zilizowezesha kuku
a kwa matumizi ya TEHAMA nchini. Hivyo, hatuwezi kuzungumzia mafanikio ya Sekta ya TEHAMA bila kuitaja Finland.
Viongozi hao walizungumzia pia masuala ya usalama mtandao, ulinzi wa taarifa binafsi, uchakataji wa taka za kielektroniki pamoja na kukuza matumizi ya vifaa janja vya kielektoniki kwa kuhakikisha vinapatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu ili matumizi ya TEHAMA yaende sambamba na uwekezaji unaofanyika
.
UKIMWI,KIFUA KIKUU NA MALARIA MBIONI KUTOKOMEZWA.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,DK.John Jingu amezindua mradi wa mzunguko wa saba wa Mfuko wa Dunia (Global Fund Circle7)ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia sasa kwaaijili ya kutokomeza Ukimwi,Kifua kikuu na Malaria nchini Tanzania ili kutokomeza Magonjwa hayo ifikapo Mwaka 2030.
DK.Jingu amezindua mradi huo,Machi 21 Jijini Dodoma, ambapo amewataka wanaotekeleza Mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza tija katika kutokomeza magonjwa hayo.
“Ni muhimu sana sisi ambao tunatekeleza Mradi huu kuhakikisha tunatumia fedha ambazo tumefadhiliwa na Mfuko huu wa Dunia kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuwa na huduma bora kwa Wananchi,”Amesema Dk. Jingu
Amefafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dk. Samia imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika Sekta ya afya kwa Lengo la kuboresha afya za Wananchi wake na Kuwataka watumishi hai kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa.
Kwa upande Wake,Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Dk.Tumaini Nagu amesema wapo kwaajili yakujipima na kuangalia walipotoka na walipo ili kufikia malengo ya Kidunia namba tatu kwa kutekeleza Strategic Plan ya afya namba tano.
“Serikali imeona umuhimu katika kutokomeza magonjwa haya ambayo ni Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria ili kuhakikisha inatokomeza magonjwa hayo ifikapo Mwaka 2030,”Amesema Profesa Nagu
Awali Mwakilishi wa Serikali ya Marekani ambao Pia wanatekeleza Mradi wa PEPFAR,GETRUDE TEMBA amesema wanatambua mchango wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Magonjwa hayo huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa umakini katika kuhakikisha rasilimali wanazopatiwa wanazitumia kwa usahihi.
MWISHO
UBORA WA HUDUMA ZA AFYA UNACHANGIWA NA WAKUNGA NA WAUGUZI.
Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema asilimia 60 ya watumishi katika sekta ya afya nchini wanatoka kada za uuguzi na ukunga hivyo kuchangia ubora wa huduma zinazotolewa katika Hospitali na Vituo vya kutolea huduma za afya.
Dkt. Mollel amebainisha hayo Machi 18, 2024 wakati wa kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa utendaji kazi wa utoaji wa huduma za uuguzi na Ukunga zoezi lililoenda sambamba na uzinduzi wa jarida la idara ya Uuguzi na Ukunga jijini Dodoma.
Dkt. Mollel amesema kada ya Uuguzi imekuwa muhimu katika kutoa huduma bora kwa sababu asilimia 80 ya kazi za afya zinatekelezwa na kada hiyo na kutoa rai kada hiyo kujumuishwa kwenye mfumo wa utoaji wa maamuzi.
“Ukiona kituo cha afya kinatoa huduna bora ni kwa sababu ya uwepo wa wauguzi ambao ndio wamekuwa watendaji wakuu ambao wanakaa muda mwingi na wagonjwa hivyo ni muhimu wakawekwa kwenye mfumo wa uongozi na utoaji wa maamuzi na uundwaji wa sera”. Amesema Dkt. Mollel.
Dkt. Mollel Ameongeza kuwa wauguzi na wakunga wanapopata fursa ya kuingia ndani ya mfumo wa uongozi watasaidia kuhakikisha mambo yanaboreshwa kwenye sekta ya Afya lakini pia maslahi yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sella ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuajiri Wauguzi na Wakunga zaidi ya 40,000 kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa kada hiyo ina dhamana kubwa katika utoaji wa huduma hivyo wazingatie miongozo, kanuni na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya taifa.
“Tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri wauguzi na wakunga zaidi ya elfu arobaini hii inaonyesha umuhimu na dhamana ya kada hii kwa sababu hawa ndio hutumia muda mwingi kukaa na wagonjwa.
Kikao hicho kilichowakutanisha Viongozi wauguzi na Ukunga kote nchini kimebeba kauli Mbiu isemayo “Huduma Staha na Mawasiliano ni Wajibu wa Kila Mtoa Huduma za Afya”.
UNDP YAZINDUA WAZO LA KIBUNIFU LA MATUMIZI BORA YA NISHATI NCHINI.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Shirika la Maendeleo la Kimataifa UNDP limezindua wazo la kibunifu la matumizi bora ya Nishati nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi 15,2024 jijini Dodoma Mtaalamu mshauri wa Shirika hilo Robert Washaija amesema kuwa mradi huu ni wa kimkakati kuhusu matumizi bora ya Nishati na unafadhiliwa na umoja wa Ulaya na Ubalozi wa Ireland na wanafanya kazi pamoja na Wizara ya Nishati.
Washaija amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha kwamba Tanzania kama nchi inakuwa na matumizi bora ya Nishati kwa sababu nishati ni kitu bora katika maendeleo ya viwanda
"Mradi huu kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na wafadhili wetu umoja wa Ulaya tunafanya Kazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Viwanda, Tunafanya Kazi na Shirika la Viwango Tanzania TBS, Tunafanya Kazi na Takwimu NBS, Tunafanya Kazi na taasisi ya elimu DIT na ni mradi ambao ni mpana sana na unalenga maeneo makubwa Sana"Amesema Washaija
Aidha amesema kuwa moja ya matunda ya mradi huo ni Kujenga uwezo nchini na kuwa na wataalamu wa kisasa ambao wataweza kutoa huduma mbalimbali pale zinapohitajika kuhusu matumizi bora ya Nishati,na kuzijengea uwezo Taasisi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake.
" Tunatambua kwamba eneo hili ni geni kwani tukianzia majumbani ni wengi wanapoteza nishati kwa kushindwa kutumia nishati kwa usanifu na kuweza kutumia nishati kubwa na kuipoteza kwani tungekuwa tunafuata matumizi bora ya nishati tusingekuwa na mgao wa umeme kama tungekuwa na matumizi rasmi ya umeme"Amesisitiza Washaija
Kwa upande wake Afisa Mahusiano (habari) wa UNDP Jolson Masaki amesema kuwa kwenye shindano hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati nchini wanalenga zaidi vijana wakike na wakiume wenye mawazo ya kibunifu yanayoenda kutoa mchango mkubwa katika kupunguza matumizi ya Nishati
"Ninaposema kupunguza matumizi ya Nishati ina maana kwamba kuna Nishati ambayo tunaitumia vibaya,sasa kupitia mawazo hayo ya kibunifu tutaenda kupokea maoni kutoka kwa Watanzania"Amesema Masaki
Aidha amesema kuwa ili uweze kushiriki katika shindano hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati kitu cha Kwanza lazima uwe na wazo la kibunifu ambalo linahusiana na matumizi bora ya Nishati,Lazima uwe Mtanzania na washindi kumi watachaguliwa ambapo katika hao washindi watapata Milioni Ishirini na tano kwa kila mmoja.
Ameongeza kuwa katika mawazo hayo ya kibunifu wanatazamia kupokea mawazo ambayo yanaweza kupunguza matumizi ya Nishati na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa yakiathiri nchi zetu.
Pia Masaki amesema kuwa wazo hili la kibunifu la matumizi bora ya Nishati ambalo limezinduliwa leo litakuwa ni la mda wa mwezi mmoja kuanzia leo Siku ya Uzinduzi hadi mwishoni mwa mwezi wa nne.
Kuhusu mwendelezo wa hili shindano la kibunifu la matumizi bora ya Nishati Masaki amesema kuwa huu mradi ni wa muda wa miaka mitatu.
Naye Mhandisi Collins Lwanga Kutoka Wizara ya Nishati amewaomba watanzania wote kuchangamkia fursa hii ya wazo la kibunifu la matumizi bora ya Nishati.
"Tumekuja kushuhudia uzinduzi wa shindano la wazo la kibunifu kuhusu matumizi bora ya nishati nchini ningependa kuwaalika watanzania wote kuweza kushiriki na kuendelea kubuni bunifu zenye tija kwani kila mmoja anatambua umuhimu wa sekta hii ya nishati"Ameongeza Lwanga
TUENDELEE KUUNGANA KUKABILIANA NA MAAFA NCHINI” MKURUGENZI MSAIDIZI JANE
NA. MWANDISHI WETU
Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Jane Kikunya amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimnali katika masuala ya uratibu wa maafa nchini ili kuendelea kuwa na stahimilivu na maafa.
Ameyasema hayo wakati akifungua Warsha ya siku moja iliyowakutanisha wadau kutoka Serikalini, Makampuni ya simu, Taasisi zinazotoa Misaada ya kibinadamu kwa lengo la kujadili fursa na kutoa maoni kuhusu njia sahihi ya ujumuishaji wa teknolojia ya simu katika mifumo ya kutoa tahadhari ya Awali (Early Warning System – EWS) iliyofanyika tarehe 14 Machi, 2024 Jijini Dodoma.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maji, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi ikiwemo TCRA, TMA, REDCROSS, makampuni ya simu pamoja na Airtel, Vodacom, Tigo/Zanztel.
Aidha alitumia fursa hiyo kueleza majukumu ya msingi ya Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ni kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini huku akiwaasa kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika mzingo wa menejimenti ya maafa ikiwemo wa kuzuia, kujiandaa, kukabili pamoja kurejesha hali pindi maafa yanatokea.
“Tumienie warsha hii kwa matokeo chanya yaliyokusudiwa kwa kuongeza ujuzi na kushirikishana uzoefu katika masuala yanayohusu fursa mbalimbali kuhusu njia sahihi za kutumia teknolojia ya simu katika mifumo na kutoa taarifa za tahadhari za awali ili kuendelea kuwa na utayari katika kukabili maafa,” alieleza Bi. Jane
Aliongezea kuwa nchi ya Tanzania imekuwa ikikumbwa na maafa ya asili na yale yasiyo ya asili ikiwemo ya mafuriko, matetemeko ya ardhi, moto, maporomoko ya tope na mawe, ukame, upepo mkali, magonjwa ya milipuko kwa binadamu na wanyama hivyo warsha hiyo ni muhimu kwa kuzingatia umuhimu wa taarifa za tahadhari za awali ili kuendelea kujiandaa kisha kukabili kwa wakati na kupunguza madhara yanayoweza kutokea wakati wa maafa hayo.
Alifafanua kuwa, taarifa za awali zinaipa jamii uelewa wa hatua za awali za kuchukua kabla ya madhara ya maafa kuwa makubwa hivyo upo umuhimu wa kuendelea kuzijengea uwezo jamii juu ya matumizi sahihi ya taarifa hizo.
Awali aliwakumbusha kuendelea kupiga namba 190 endapo kunatokea majanga, maafa au dharura ili kupata msaada zaidi kupitia Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.
=MWISHO=
Mkurugenzi wa Mashirikiano ya Kimkakati kutoka Taasisi ya GSMA Bw. Dulip Tillekeratne akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyolenga kujadili fursa na kutoa maoni kuhusu njia sahihi za ujumuishaji wa teknolojia ya simu katika mifumo ya kutoa Tahadhari ya Awali (Early Warning System – EWS) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Best Western City Dodoma. Baadhi ya washiriki wakifuatilia warsha iliyolenga kujadili fursa na kutoa maoni kuhusu njia sahihi za ujumuishaji wa teknolojia ya simu katika mifumo ya kutoa Tahadhari ya Awali (Early Warning System – EWS) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Best Western City Dodoma.
TUNAIOMBA SERIKALI ITUSAIDIE KUFUNGIA MAKAMPUNI BUBU(UKUTA).
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Umoja wa makampuni binafsi ya ulinzi Tanzania (UKUTA) wameiomba serikali kufungia makampuni bubu kwani wanafungua kampuni hizo bila kufuata sheria jambo ambalo ni sawasawa na kuhujumu uchumi kwa kushindwa kuwa wazalendo.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndg.Abel Dendwa wakati wa mkutano Mkuu wa tatu wa taasisi ya makampuni binafsi ya ulinzi Tanzania(UKUTA) uliofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel jijini hapo.
Aidha ameongeza kuwa wanatoa mwezi mmoja kwa makampuni hayo wawe wamejitathimini kuweza kujiunga na na umoja huo ili waweze kutambulika na sio kufanya kazi kinyume na matakwa ya umoja huo.
"Nitumie fursa hii kuiomba serikali kilio chetu kwa wakurugenzi tuwe na sheria inayo tuongoza kwa maana sheria itatuamulia huyo mwenye kampuni bubu tunaweza kukabiliana nae vipi kufungiwa ili wafuate sheria kwani tunaendelea kuhubiri umoja tunakataa kutengana" Amesisitiza Katibu Abel
Naye John Joseph Muwakilishi wa mkurugenzi Mkuu Takukuru amesema wao kama taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa ni jukumu lao kuelimisha jamii kwani Rushwa ni dhambi na madhara ya Rushwa ni makubwa.
"Niwaombe tujikite katika kusimamia sheria na taratibu,sisi sote ni serikali,lakini kama taasisi kuelimisha umma ni jukumu letu,msingi na wajibu wetu ni kuwafuata wananchi walipo kuwapa elimu ya Rushwa na tumeanzisha klabu za kupinga Rushwa shule za msingi,sekondari na vyuo vikuu hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya madhara ya Rushwa na imani yangu ni kwamba kama kila mtu anatimiza wajibu wake basi ni rahisi kufuata sheria na taratibu zake bila kushurutishwa" Ameongeza Joseph
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo (UKUTA) Amani Mbijima ambaye pia ni Mkurugenzi wa Patmercy Security Co LTD amesema makampuni ya ulinzi binafsi yamekuwa wakikumbana na Changamoto hasa kwenye utaratibu wa ufatiliaji wa malipo kwenye tasisi kwani wamekuwa wakilazimila kupeleka risti kabla ya malipo hali aliyoisema ni shida kwao.
Amesema kwa Upande wao wanavyolazimishwa kutoa risti ya EFDs kabla ya malipo imekuwa ni shida kwao kwani wanavyotoa risti wanaonekana wamelipwa na wao kutakiwa kulipa kodi kulingana na sheria ya mlipa kodi.
Changamoto nyingine ni pamoja malipo wanayolipwa yapo chini ambapo kima cha chini wanachotakiwa kulipwa Shilingi 148000 tofauti na viwango wanavyotakiwa kulipwa na hiyo yote ni kutokana na kukithili kwa makampuni bubu.
" Kumezuka makampuni bubu hali inayopelekea kutukwisha sisi makampuni ya ulinzi binafsi tuliosajaliwa na kutambuliwa kwani makampuni hayo bubu ndio yamevunja bei na kutupelekea na sisi kukosa soko wamekuwa wakifanya kazi kiholela bila makubalinao na hata wakikubalina wanakubaliana kwa bei ya chini na kusababaisha na sisi kushindwa kuwalipa walinzi, " Amesema
Na kuongeza" Sasa tuna kwenda kushirikina na mamlaka husika ili makampuni hayo kuondolewa Mara Moja katika jamii kwani ndio yamekuwa yakileta Shinda na kupeleka kuharibu sifa yetu, "Amesema
REA YATOA ELIMU YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Viongozi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu, Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Hassan Saidy pamoja na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala na Jadidifu, Mhandisi, Advera Mwijage leo, Tarehe 9 Machi, 2024 wameshiriki kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia ambalo limekwenda sambamba na kuhitimisha Maadhimiho ya Siku ya Wanawake Duniani (2024) katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo ni Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliambata na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ambapo walipotembelea banda la REA ujumbe mkubwa ulikuwa ni kuendelea kutoa hamasa na elimu ya matumizi ya tekonojia rahisi na nafuu kwa Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na kurahisisha katika upatikanaji wake.
“REA kwa kushirikiana na STAMICO imefadhili ununuzi wa mashine kubwa tatu kwa ajili ya kuzalisha makaa ya mawe. Mradi huo, umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 5 na sisi kama Wakala tuna hamasisha matumizi ya mkaa mbadala (Mkaa salama) kama chanzo cha nishati safi ya kupikia”. Amesisitiza Mhandisi, Advera.
Mhandisi, Advera amemwambia, Mgeni Rasmi, Dkt. Philip Mpango kuwa REA inatekeleza jukumu la kuhakikisha nishati za aina zote zinapatikana vijijini na kwa Watu wote na kuongeza kuwa imekuwa mstali wa mbele kuwasaidia Waendelezaji wa teknolojia za nishati safi pamoja na Miradi inayolenga kwenye kuongeza upatikanaji wa bidhaa za nishati safi ya kupikia.
Mhandisi, Advera ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha wa 2023/2024, Wakala imetoa zaidi ya mitungi ya gesi ya kupikia 158,100 kwa Wananchi wa vijijini kama sehemu ya hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa mitungi zaidi ya laki 4 itatolewa kupitia utaratibu huo.
Mhandisi, Advera ameongeza kuwa mbali ugawaji wa mitungi ya gesi, REA imeanza kutekeleza program ya kusambaza gesi asili kwa Wananchi wa vijijini wa mkoa wa Pwani na Lindi, Mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 6.8 ambapo kwa kuanzia kaya zaidi 980 zitaunganishwa kwenye mtandao wa gesi asilia kwenye nyumba zao.
Ameutaja Mradi mwengine ni wa kuwaunganisha Wananchi wa vijijini katika mkoa wa Pwani na Mtwara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 13.5 ambapo kwa kuanzia kaya zaidi ya 1,400 zitanufaika.
Mhandisi, Advera amesema REA pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza, ambapo Tanzania kuna magereza zaidi ya 129 ambapo imeelezwa kuwa matumizi ya kuni pekee yake ni zaidi ya asilimi 93,mradi huo umeanza kutekelezwa na utagharimu shilingi bilioni 40.
Miradi mingine unaofanana na huo ni ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo kambi 26 zitanufaika na mradi huo uliotengewa zaidi ya bilioni 3.5 ambapo utaanza kutekelezwa hivi karibu.
Mradi wa Mwisho ambao REA imepanga kuutekeleza ni wa kujenga miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye shule kongarobaini za sekondari hapa nchi, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 2.6 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
HATUKUBALIANI NA SHERIA YA WENZA WA VIONGOZI KULIPWA MAFAO "CHADEMA".
Na Moreen Rojas,
Dodoma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepinga kitendo cha Bunge kupitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao huku kikishauri kufanyiwa kwa marejeo ya sheria ya Kikokotoo ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na watumishi.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Catherine Ruge, alibainisha hayo jana jijini hapa, alipokuwa akitoa hutuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Ruge, alisema inasikitisha kuona Wabunge ambao wamechaguliwa na wananchi kwenda kuwatetea wananchi wanao kabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo umasking wanakuwa time ya kusifu na kuabudu.
"Wananchi wengi bado wanakabiliwa na shida nyingi sana ikiwemo afya,huduma za maji, miundombinu na kupanda kwa gharama za maisha lakini leo bunge linapitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao.
"Wapo watumishi wa umma kwa mfano muuguzi wa ngazi ya cheti analipwa mafao ambayo hayaeleweki lakini leo hii Bunge linapisha sheria ya wenza wa viongozi kilipwa mafao"alisema Ruge
Alisema BAWACHA inashauri Bunge kufanya marejeo ya sheria ya kikokotoo ambayo yatawezesha kufanyika kwa maboresho ambayo yataleta ahuweni kwa watanzania wa hali ya chini.
"Bunge lipo kwa ajili ya kutetea wananchi wanyonge siyo watu watatu ambao ni wenza wa viongozi wanaotaka leo waume zao walipwe na wao walipwe pia"alisema
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu 2025 utakuwa wa kufa na kupona kwakuwa wataweka wagombe kila nafasi itakayo tangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Alisema kwa kufanya hivyo hakuna mgombe yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye atapita bila kupigwa kama ambavyo imekuwa katika miaka iliyopita.
Mbowe, alisema katika uchaguzi huo CHADEMA wamepanga kuwe mgombe kila nafasi itakayo tangazwa na NEC, katika ngazi zote kuanzia kitongoji hadi taifa.
"Uchaguzi ujao utakuwa wa kufa na kupona CHADEMA tutahakikisha tunaweka wagombea kila nafasi itakayo tangazwa lazima kila mgombe atakaye jitokeza CHADEMA tuwepo pale kumpinga hakuna kupita bila kupingwa"alisema Moore
Alisema kutokana hali hiyo anamwagiza katibu mkuu wa Chama hicho pamoja na mfumo mzima wa chama kuhakikisha kuwa kila eneo anapatikana kipngozi bora na siyo bora kiongozi.
"Lazima mhakikishe kila eneo anapatikana mtu wa kwenda kugombea na awe na uwezo wa kushinda siyo kushiriki na kwa kiongozi yoyote ambaye atashindwa kuweka mgombea chama hatutamchekea katika hilo tutachekea kwa mambo mengine siyo hilo lazima tuwe na uchungu sisi ndiyo tutaweza kuondoa huu msiba wa CCM"alisisitiza Mbowe
Alisema CHADEMA ndiyo Chama pekee ambacho kitakwenda kumaliza malalamiko ya wananchi ambak hivi sasa wanalalamikia ugumu wa maisha.
Aidha, alisema wanachoomba ni Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya kwani ndiyo itasaidia kumaliza tabia ya kuingia madarakani kwa viongozi ambao hawana kibali cha watu na Mungu.
"Asilimia 90 ya viongozi waliopo madarakani hivi sasa wengi wao wamengia katika nafasi hizo kwa njia zisizo za haki kutokana na uwepo wa tume hii ya uchaguzi hali ambayo imesababisha uwepo wa ufisadi,uminyaji haki na uvunjifu wa demokrasia nchini"alisema
Alisema hivi sasa wanachi wanalalamika gharama za maisha kupanda lakini wabunge ambao wamechaguliwa kuwawakilisha wananchi wanajiongozea mishahara.
"Mfumuko wa bei umepanda mara tatu lakini wabunge mwaka jana wamejipandishia mishahara hadi milioni 18 kwa mwezi"alisema Mbowe
Mwenyeki wa BAWACHA Taifa Sharifa Sulaiman, alisema wanawake wengi wameonyesha nia ya kugombe nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao ikiwemo nafasi ya Urais.
"Wanawake wengi wameonyesha ni ya kugombe nafasi mbalimbali ikiwemo urais katika uchaguzi mkuu ujao wanachosubiria ni Richard ya Chama tuu na tutaendelea kuwahamasha ili wengi wajitokeze katika nafasi mbalimbali"alisema
SERIKALI IMEOMBWA KUPUNGUZA BEI YA NISHATI YA GESI YA KUPIKIA.
Na Moreen Rojas,
Dodoma
Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda ameiomba Serikali kupunguza bei ya Nishati ya gesi ili wanawake Waweze kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa kwenye shughuli za mapishi.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo leo Machi 9 , 2024 kwenye kongamano la wanawake la ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia jijini Dodoma,ambapo amesema sasa wanawake wanakwenda kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa hali itakayopelekea utunzaji wa mazingira katika jamii.
Amesema Bei ya Nishati safi ya Gesi ya kupikia ikipungua tofauti na ilivyo kwa sasa basi wananchi wengi wakiwemo wanawake wataweza kununua majiko na kuachana na Matumizi hatarishi ya kuni.
"Bei ya gesi ikipunguzwa madukani wanawake watakuwa na uwezo wa kununua kila yanapoisha na yatakuwa yanatumika nasio kuwa mapambo majumbani kwetu kama ilivyo sasa," Amesema
Na kuongeza " Ninaimani baada ya kongamano hili wanawake wote tuna kwenda kuwa mabarozi wazuri juu ya Matumizi ya mishati safi ya kupikia na sio kuni na mkaa, " Amesema Komredi Chatanda
Aidha amewapongeza waandaaji wa kongamano hilo ambao ni wizara ya Nishati kwa kuwaalika wanawake zaidi ya 10,000 kutoka mikoa tofauti tofauti na kuwapatia elimu na vitendea kazi vya nishati.
"Tunashukuru kwa elimu,mitaji na vitendea kazi kwani tupo kwenye maadhimisho ya wiki ya wanawake tunashukuru kwa kutukumbuka wanawake, "Amesema Chatanda
Na kuongeza "Na sisi tunaahidi Kwenye ziara zetu za Kata kwa Kata tunakwenda kuhamasisha matumizi sahihi ya gesi safi ya kupikia na wanawake wote kuachana na kuni ili kutunza mazingira kwani kunamsemo usemao mwanamke ni mazingira CCM hoyeeee, "Amesema
Amesema serikali imeongeza bajeti mwaka wa fedha 2023/24 ambapo fedha hizo za ruzuku ziliweza kusaidia makampuni ya usambazaji wa gesi kusambaza Nishati hiyo kwa Baraka na wepesi hadi pembezoni.
Hata hivyo kufuatia fedha hizo aliyataka makampuni hayo kwenda kusimamia makubaliano waliokubaliana na serikali kwa kuhakikisha Nishati hiyo inamfikia kila mtu Hali itakayosaidia kumtua mzigo wa kuni mama kichwani.
Mwisho
PROGRAMU YA AFDP YALETA MATOKEO CHANYA SEKTA YA KILIMO UVUVI.
Na. MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inalengo la uzalishaji endelevu wa kibiashara na wenye kuzingatia mazingira hususan uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji wa viumbe maji kwa kuzingatia uwezeshaji kinamama na ushiriki wa vijana.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara Mkoani Pwani ya kutembelea na kuona eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki na kuona utayari wa Halmashari na Jamii katika kupokea Mradi huo.
Aidha Waziri Ummy amesema Programu hiyo inatekelezwa katika Halmashauri 44 zilizo kwenye Mikoa 11 ya Tanzania Bara pamoja na Unguja na Pemba ambapo inatarajiwa kunufaisha watu takribani Milioni moja na laki 3 ikiwemo kaya za wakulima wadogo, wazalishaji wadogo na kati wa mbegu wafanyabishara wa pembejeo za kilimo, wavuvi wadogo, wafanyabiashara wa samaki na wafugaji wa samaki pamoja na viumbe maji (mwani).
"Lengo la kutembelea ni kukagua na kuangalia yale maagizo mahususi yakuendeleza kilimo tuliambiwa tuwe na ghala la chakula lakini nia ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ni maono yake kuwa Tanzania tuwe mstari wa mbele kwenye kilimo, uvuvi, uvuvi wa Bahari Kuu, uvuvi wa kisasa kwa vijana wetu ili kuendelea kutoa ajira lakini tunawaona waheshimiwa mawaziri na Manaibu na viongozi wote wa Wizara hizi mbili jinsi wanavyopambana kuhakikisha dhamira ya Mheshimiwa Rais inakamilika"."Alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Mussa Kunenge amesema katika Mkoa wake shughuli za uvuvi zinafanyika zaidi katika halmashauri za wilaya zilizopakana na bahari pia uwepo wa mabwawa ya asili unafanya Mkoa kuwa na Fursa kubwa ya Uvuvi.
"Katika Mkoa wa Pwani mazao makuu yatokanayo na Bahari, Mito na Mabwawa ni samaki, mwani na Dagaa, pia tunaanzisha ufugaji wa Jongoo bahari ekari nane katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na kwa mwaka 2022/2023 jumla ya kilo 612 zilivunwa na lengo la mkoa ni kuongeza uzalishaji hadi 1,200 kwa Mwaka hivyo tunawashauri watu wetu waacha mazoea na watafute biashara zilizo na tija kwao ." Alisema Mhe. Kunenge.
=MWISHO=
CAPTIONS
P1.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akiwa katika ziara yake Mkoani Pwani ya kutembelea na kuona eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki na kuona utayari wa Halmashari na Jamii katika kupokea Mradi huo unaotarajiwa kujengwa Bagamoyo Mkoani Pwani.
P 2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa ziara yake Mkoani Pwani ya kutembelea na kuona eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki na kuona utayari wa Halmashari na Jamii katika kupokea Mradi huo unaotarajiwa kujengwa Bagamoyo Mkoani Pwani.
P 3
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Mussa Kunenge akieleza namna Mkoa wake ulivyojipanga katika kukuza na kuendeleza mradi wa AFDP wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani).
P 4
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda wakati akiwasilisha Taarifa ya Mradi wa eneo la ujenzi wa Vichanja vya samaki linalotarajiwa kujengwa katika halamashauri hiyo.
P 5
Eneo ambapo ujenzi wa Vichanja vya samaki vitakapo jengwa katika halamashauri hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)