Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewaasa wananchi na wakazi wa Dodoma kuacha kudanganya maeneo ya makazi ili kuepusha migogoro ya ardhi.
Mhe.Senyamule ameyasema hayo wakati akizindua mpango mkakati kwa ajili ya kushughulikia na kutatua migogoro ya ardhi kwa jiji la Dodoma.
Aidha amesema kuwa jiji la Dodoma limekuwa na ongezeko la wananchi hivyo kufuatia ongezeko hilo limepelekea matumizi ya ardhi kuwa ni mengi na mengine kuwa ya kiholela bila mpangilio ambapo kwa kutatua changamoto hii mkoa wa Dodoma kupitia Mkuu wa mkoa wa Dodoma imeandaa timu kwa ajili ya kutatua na kumaliza migogoro.
"Kuna changamoto mbalimbali zinazochangia migogoro hii kushindwa kuisha kutokana na uchache wa vifaa vya tehama, ukosefu wa huduma bora kwa wananchi,eneo la jiji kuwa dogo, lugha mbaya kwa wananchi zinazotolewa na watumishi wa jiji,kipandikizi yaani kupandikiza zaidi ya kiwanja kimoja kupewa watu tofauti pamoja na wananchi kupuuza jumbe za simu" Amesisitiza Senyamule.
Aidha ameongeza kuwa jambo hili litafanyika ndani ya miezi 6 yaani Julai hadi Disemba ambapo kutafanyika uhakiki wa maeneo ambayo yanamalalamiko ambapo wahusika wanavamia maeneo ambayo sio ya kwao pamoja na kurekebisha mifumo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais tamisemi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri amesema kuwa mpango huo utaweza kuwasaidia kutambua mapungufu gani ya ndani na madhaifu gani ya nje ili ili kuishi matarajio ya kiongozi wa kitaifa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha jiji la Dodoma linapagwa vizuri ili kuendana na hadhi ya makao makuu ya nchi.
Aidha amesema kuwa ni matumaini yake kwamba elimu ya kutosha itatolewa kwa kamati ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa huku akisisitiza maeneo ya wazi kupewa watu sahihi ili kuhakikisha wanajenga vitu vyenye manufaa kwa wananchi.
"Mifugo kuzurura mjini nilipata nafasi ya kuongea na wafugaji tulikuwa na kikao kizuri hivyo ni rai yangu tuliyokuwa tukiyaongelea yatakuwa yamezingatiwa,wakati mmoja tulikamata mifugo ya kiongozi mmoja,akanipigia simu nikamwambia lazima ulipe fidia haijalishi wewe ni nani huwezi acha mifugo kiholela" Amesema Shekimweri.
Aidha ametoa rai kwa watumishi wa ardhi kuhudumia wateja vizuri kwa kutoa kauli nzuri kwa wateja pamoja na kuheshimu watu.
Home »
» WANANCHI WAASWA KUACHA KUDANGANYA MAENEO YA MAKAZI.
0 Comments:
Post a Comment