Subscribe Us

AFISA KILIMO GAIRO AMEWATAKA WAKULIMA NCHINI KUACHA KUFANYA KILIMO CHA MAZOEA

Na. Kadala Komba Gairo

 

Wakulima mkoani Morogoro wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea ili kuweza kuepuka hasara zinazojitokeza mara kwa mara badala yake wafuate ushauri unaotolewa na wa taalamu wa kilimo.

Hayo yamebainishwa na afisa  Kilimo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro  Philemon Isack Akizungumza  katika Kijiji cha Msingizi wakati wa kutambulisha aina mpya za mbegu  za karanga na mtama kwenye mkutano ulioandaliwa na Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA),

Mbegu zilizotambulishwa ni NARI nut 2015, Naliendele 2016 na Nachi 2015 ambazo ni za karanga. Mbegu za mtama ni TARI SORI 2 na Macia.

Isack alisema kuwa wakati huu ambao serikali inawekeza fedha nyingi kwenye kilimo kuna haja ya wakulima kubadili mitazamo na kuendesha kilimo chenye tija na kuachana na kilimo cha mazoea cha kutupia mbegu.

“Bado baadhi ya wakulima wamekuwa wakiendesha kilimo cha mazoea ,wakati trekta linalima wanapita nyuma kumwaga mbegu, wakati mwingine mbegu zinamwagika nyingi na hivyo kupelekea mazao kuota kwa kubanana na hivyo kushindwa kukua vizuri,” alisema.

Alisema kuwa kama wakulima watafuata kilimo cha kitaalam mbegu zitatumikachache na mazao yataota kwa utaratibu mzuri na hivyo kupelekea mavuno kuwa makubwa.

“Tumejiwekea malengo ili kuongeza uzalishaji kutoka gunia tatu kwa ekari hadi kufikia gunia 10 na 15 kwa ekari,” alisema

 

Kwa upande wao, wakulima wa Kijiji cha Msingisi wameiomba Serikali kuendelea kusambaza mbegu bora ili ziwafikie kwa wakati hali itakayochangia kuongeza uzalishaji.

 

Grace Petro ambaye ni mkulima wa mtama alisema kuwa juhudi zao kwenye kilimo zitafanikiwa iwapo serikali itasaidia upatikanaji wa mbegu bora.

“Upatikanaji wa mbegu bora utasaidia sana wakulima hasa wa vijijini wakipata mbegu bora za wakatiitasaidia kuongeza uzalishaji,” alisema

Glads Ngalawa alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya ndege kushambulia mazao ni vyema wakulima wakapewa mbinu za kuzuia mazao kushambuliwa na ndege ikiwemo mtama.

Mtendaji Mkuu wa DASPA, Aithan Chaula aliwataka wakulima kulima mazao ya mtama na karanga kutkana na kuwa na soko la uhakika.

Alisema kuwa kupitia mradi huo wakulima watapewa mafunzo kwa ajili ya uzalishaji mbegu na watakaofanya vizuri watapewa vyeti naTaasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu nchini (TOSCHI) na watakuwa wauzaji wa mbegu kwenye maeneo wanayotoka.

 

“Tunataka tukija wakati mwingine tukute maduka ya wazalishaji wa mbegu ili kuuzia wakulima wengine,” alisema,

Alisema kuwa mtama una fursa kubwa ya kuzalishwa kwa wingi zaidi kama zao la chakula kuziba nafasi ya mazao mengine ambayo yameathiriwa na ukame kutokana na na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwenyekiti wa DASPA, Janeth Wilson aliwataka wakulima kulima mtama kwa wingi kwani una soko la uhakika.

Mwisho

 



 afisa  Kilimo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro  Philemon Isack Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msingizi



Mwenyekiti wa Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA), Janeth Wilson akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msingisi Wilaya ya Gairo Mkoani Dodoma wakati wa kutambulishwa kwa mbegu za mtama na karanga (Picha na Kadala Komba)



Mtendaji Mkuu wa DASPA, Aithan Chaula Akiwahakikishia wakulima aliwataka wakulima kulima mazao ya mtama na karanga kutkana na kuwa na soko la uhakika.
 


George Katoto:Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Gairo Akizungumza na viongozi wa shirika la DASPA ofisini kwake

Bi.Msifwahi Haule ,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo Akizungumza na uongozi shirika la DASPA  ofisini kwake walipofika kuripoti mkoani hapo.






MATUKIO YA PICHA

wakulima wa Vijiji vya  Msingisi na  Kibeya waliyopatiwa mafunzo ya utambuzi wa mbegu mpya za karanga na mtama  kutoka shirika la  DASPA



Peter Paulo Mratibu CCT Wilaya ya Gairo na Bwana shamba wakampuni ya Hans Agriculture machinery &DASPA

0 Comments:

Post a Comment