Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Waziri wa Elimu Prof.Adolph Mkenda amepokea dola za Canada milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini.
Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi ya wizara jijini Dodoma ambapo asilimia 25 itatumika kwa ajili ya shule za wanafunzi wa kike na asilimia 25 zingine kutumika katika mafunzo ya amali kwa ajili ya kuwaandaa vijana kwa ajira.
"Tunafurahi mahusiaano yetu katika sekta ya elimu yanakuwa na kuimarika siku hadi siku na watanzania wengi wamesoma Canada kupitia serikali ya Canada pamoja na kuwa na elimu ya lazima ya miaka 10 badala ya miaka 7" Amesema Prof.Mkenda.
Kwa upande wake Mhe.Harjit S.Sajjan Waziri wa maendeleo ya kimataifa na waziri mwenye dhamana ya shirika la maendeleo ya uchumi la Pasifiki ya Canada amesema kuwa shule nyingi hazikidhi mahitaji ya wasichana walio katika kipindi cha balehe katika suala la usalama au upatikanaji wa maji au vyoo maalumu vya kujihifadhi wakati wa hedhi.
Aidha ameongeza kuwa uwekezaji katika elimu ya wasichana hubadilisha jamii huimarisha uchumi na kupunguza ukosefu wa usawa,inachangia jamii kuwa imara zaidi,jamii imara inayotoa fursa kwa watu wote ikiwa ni pamoja na wavulana na wanaume fursa ya kutumia uwezo wao.
"Tumeshirikiana kuboresha viwango vya elimu na upatikanaji wa elimu kwa shule zote za msingi na sekondari kwa wasichana na wavulana na niko hapa kuthibitisha Canada kwamba itaendelea kusaidia jitihada za elimu nchini Tanzania kama Mwalimu Julius Nyerere alivyosema " Elimu sio njia ya kukimbia umaskini,ni nyenzo ya kupambana nao"Amesema Mhe.Sajjan.
Aidha ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 14 iliyopita Canada imetoa zaidi ya dola milioni 250 za Canada kwenye mfumo wa elimu,kwa kushirikiana na Serikali Canada imewekeza katika mafunzo madhubuti kwa walimu wa baadae katika vyuo 35 vya ualimu.
"Sera yetu ya usaidizi wa kimataifa ya kijinsia inaweka msisitizo katika fursa sawa kwa wanawake na wasichana,kutumia mtazamo wa kijinsia kunamaanisha kuhoji ubaguzi nyumbani na duniani kote na kutambua mambo yanayosababisha ukosefu wa usawa,tumejifunza umuhimu wa kuwapa wasichana nafasi salama kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi"Amesisitiza Mhe.Sajjan.
Sanjari na hayo amesema kuwa wasichana wajawazito na mabinti waliojifungua wanastahuki kupata elimu,stadi za maisha,ujuzi wa malezi na mafunzo ya ujuzi,kisha wanaweza kuendelea na masomo yao,kupata fursa sawa ya ajira yenye staha na kuvunja mzunguko wa umasikini ambao kina mama wengi wadogo wanaangukia.
Canada imetangaza dola milioni 25 kwa mradi wa Binti Asome(Every Girl Learns_EAGL )Tanzania Bara na Zanzibar chini ya UNICEF ambapo maradi huu utawezesha elimu kwa mabinti katika ngazi ya msingi na sekondari,haswa katika masomo ya hisabati na sayansi.
Programu hii itachangia kuongeza viwango vya uhitimu kwa wasichana katika shule za sekondari na kuwasaidia mabinti wenye umri kuanzia kati ya 10 na 19 kujifunza na kuongeza ujuzi wao ili kuendana na mahitaji ya soko ya sasa na baadaye nchini Tanzania.
Home »
» CANADA YATOA SHILINGI DOLA MILIONI 50 KWA AJILI YA MAENDELEO YA ELIMU NCHINI.
0 Comments:
Post a Comment