Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Waziri wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)Mhe.Innocent Bashungwa amewaalika wananchi wa mkoa wa Dodoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo yatakayofanyika tarehe 10 julai siku ya jumatatu katika uwanja wa jamuhuri jijini Dodoma.
Waziri Bashungwa ameyasema hayo hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo lengo likiwa ni kutoa muongozo na taratibu kufuatia siku hiyo ya miaka 60 ya JKT.
Aidha amesema kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa ni Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha maadhimisho ya miaka 60 ya JKT yalitanguliwa na shughuli mbalimbali ambapo June 25 kulikuwa na tukio la JKT marathon ikiwa ni tukio la kwanza tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi wa tukio hilo alikuwa Rais mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Aidha ameongeza kuwa JKT inajivunia kuwa moja ya taasisi inayotambua na kuvumbua vipaji ikiwemo michezo na sanaa.
"Jeshini vipaji vyote vipo tunavilea tunavijengea ustawi na tunaangalia namna ya kutambua vipaji hivi na kuviendeleza mfano mzuri ukisikiliza bendi ya JKT au waimbaji wetu wa taarabu utaona ni kwa namna gani tunakuza na kuendeleza vipaji" Amesisitiza Waziri Bashungwa.
Sanjari na hayo miaka 60 ya JKT itapambwa na maonyesho ya vifaa mbalimbali kutoka JKT na wasanii mbalimbali bila kusahau gwaride huku wakiwaalika marafiki kupitia chaneli za kidiplomasia ikiwemo Izrael.
Jeshi la kujenga Taifa (JKT)lilianzishwa mwaka 1963 chini ya muasisi wa Taifa Rais Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Home »
» WANANCHI WAALIKWA MIAKA 60 YA JKT
0 Comments:
Post a Comment