Na Moreen Rojas,
Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameishukuru Serikalia ya Kanada kupitia Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan wake kwa kusaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia kiasi cha shilingi Bilioni 240 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya.
Waziri Ummy amebainisha hay leo Jijini Dodoma wakati wamkutano na vyombo vya habari baada ya Waziri wa Maendeleo ya jamii Kanada kuzungumza na vyombo vya habari pia
Waziri Ummy ameeleza kuwa kati ya kiasi kiasi hicho shilingi 140 zinaingia serikalini kwa ajili ya kuchangia mfuko wa afya wa pamoja ambapo mpaka sasa Serikali ishapokea kias cha shilingi Bilioni 94 ambazo zimeelekezwa kwenye akaunti za ngazi ya msingi ambazo ni zahanati na vituo vya afya nchini.
Waziri Ummy ameongeza kuwa Vituo vya afya na zahati watapanga vipaumbele vyao kwajili ya kulipia maji, umeme, kununua dawa, kwajili ya uzazi salama na wanatumia kufanya ukarabati mdogo pamoja na kununua vifaa tiba.
“Kwa ujumla mchango wa Serikali ya Kanada kwa Tanzania umeleta matokeo mazuri kwa Huduma za afya Tanzania leo tunaongea wanawake karibu asilimia 90 wajawajito wanajifungulia katika vituo vya kutoa Huduma za afya kwa sababu ya mchango wa Kanada”, aweka wazi Waziri Ummy.
Lakini pia ameongeza kuwa wamepunguza vifo vya watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano kutoka vifo 67 katika kila vizazi hai 1000 hadi vifo 43.
Vile vile amesema wamefanikiwa kuongeza idadi ya wanawake wanao tumia njia za kisasa za uazazi wa mpango kutoka asilimia 32 hadi asilimia 38 .
“Lakini pia tumeweza kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi asilimia 22 , tumepunguza udumavu kutoka asilimia 38 na sasa tunazungumzia asilimia 31 na kwa watoto wetu wanapata chanjo”, Amesema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan amesema kuwa wametangaza miradi mitano mipya ya afya yenye thamani ya dola za Canada milioni 128.5 ambapo dola za Canada milioni 75 kwa mfuko wa ruzuku wa shughuli za Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Sector Busket Fund, HSBF) kwa serikali ya Tanzania na nyongeza ya dola za Canada 500,000 kwa UNICEF kwa usaidizi wa kitaalam.
"Leo nina furaha pia kutangaza dola za Canada milioni 23 katika ufadhili wa shirika la CanGIVE kwa miradi miwili mipya kwa ushirikiano na UNICEF Tanzania na shirika la Afya Duniani,Tanzania miradi hii ya CanGive itasaidia juhudi za watanzania kuchanja makundi yaliyopewa kipaumbele kwa njia ambayo itaimarisha huduma za afya kwa mapana zaidi”, Amesema Mhe.Sajjan
Ameongeza kuwa miradi hiyo itasaidia wafanyakazi wa afya kushirikisha jamii na kukabiliana vyema na vizuizi vya kijimii kwa kutoa chanjo na huduma za afya
Aidha ametangaza mradi wa dola za Canada 15 chini ya Shirika la Kimataifa Plan International Canada kwa ajili ya mradi wa afya na haki za wasichana, vijana, mradi uliopo Mkaoni Katavi pamoja na nyongeza ya dola za Canada 15 kwa ajili ya mradi wa kukuza matumaini na maendeleo kwa vijana nchini Tanzania huu utatekelezwa na shirika la la Kimataifa World Vision Canada katika maeneo Mikoa ya Dar es salaam na Dodoma.
MWISHO
Home »
» SERIKALI YA KANADA IMETOA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 240 KUBORESHA SEKTA YA AFYA TANZANIA.
0 Comments:
Post a Comment