Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA VANNILA WAZINDULIWA DODOMA

 
Na. Mwandishi wetu Dodoma 

 

Kampuni ya Vanilla international Limited imezindua Mradi wa kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma Vanilla village Dodoma katika Kitongoji cha Zamahero Kata ya Mayamaya Wilaya ya Bahi.

Uzinduzi huo umeambatana na utoaji Elimu kwa wananchi wa eneo hilo kuhusu kilimo cha Vanilla ambao umefanyika Julai 22 2023 katika shamba la kitalu (green House)kubwa ya kilimo hicho inayotumia njia za kisasa.

Mkurugenzi Mtendaji na muasisi wa makampuni ya Vanilla international Limited ,Simon Mkondya amesema shamba kitalu
 hilo lipo kilomita 40 kutoka katikati  ya JIJI la Dodoma barabara kuu ya kwenda Arusha lenye ukubwa wa hekta 125.

Mkondya amesema uwekezaji huo unakuja baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia kilimo hicho katika kisiwa cha Zanzibar.








HOSPITALI YA APOLLO INDIA KUWEKEZA TANZANIA


Uongozi wa Hospitali ya Apollo umeahidi kuja Tanzania na kuwekeza katika Sekta ya Afya kwa kufungua Hospitali itakayokuwa imejikita kwenye utoaji wa huduma za matibabu ya kibingw ana ubingwa bobezi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea Hospitali hiyo iliyopo Jijini New Delhi India na kufanya kikao na uongozi wa Hospitali hiyo Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Hosoitali Dkt. Prathap Chandra Raddy.

“Hospitali hii kubwa ya Apollo imekuwa na ushirikiano  na Tanzania kwa kipindi kirefu sasa hususani katika kuwahudumia wagonjwa  mbalimbali wanaopewa rufaa  za matibabu ya kibingwa na ubobezi  wa juu pamoja na magonjwa ambayo yanahitaji matibabu kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi pamoja na kuendelea na programu ya kuwaongezea ujuzi wataalamu wa Sekta ya Afya katika maeneo ya ubingwa na ubobezi” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema kuwa kupitia mazungumzo yake na uongozi wa Hospitali hiyo chini ya Dkt. Prathap Chandra Raddy amekubali ombi la kufanya uwekezaji wa  Hospitali kubwa itakayotoa huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

“Uwekezaji huu utakuwa umefanyika kwa wakati sahihi na utasidia sana katika kuwapunguzia gharama za matibabu wagonjwa wengi wanaohitaji matibabu ya kibingwa nje ya nchi. Kwa kuzingatia uhitaji huo, uwekezaji wa Taasisi ya Apollo utajikita katika Huduma za kibingwa ikiwemo upasuaji za kupandikiza Figo, Upandikizaji wa Ini, Upandikizaji wa Uloto, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, upasuaji mkubwa wa moyo na mishipa ya damu, ini, Figo, Saratani, Ubongo na Mishipa ya Fahamu” amesema Waziri Ummy.


HATUA KUU NANE UNAZO TAKIWA KUZICHUKUA KABLA YA KUOVATECK

  (1) hakikisha hakuna dereva nyuma yako aliye omba kuovateck kabra yako.2) hakikisha mazingira uliyopo yana kuruhusu kufanya hivyo.3) hakikisha kwamba aliyopo mbele yako yuko tayari kupitwa.4) hakikisha kwamba wewe mwenyewe upo tayari kuovateck.5) hakikisha kwamba mbele yako kuna usalama wa kutosha mahesabu yako yako sahihi kufanya hivyo.6) hakikisha kwamba umetoa ishara sahihi ya kuovateck na wengine wameiona ishara uliyo itoa.7) hakikisha kwamba gar yako ina uwezo wa speed kuliko gar la mbele yako.8) hakikisha kwamba mzunguko wa tair yako unaelewana na mzunguko wa kas ya Engen yako au Engen yako na tair vinaelewana pamoja.NB: nikwamba kama hauwezi kuchukua hatua hizo nane na kama gari yako haina uwezo au umadhubut acha usifanye hivyo please.KUMBUKA USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE ASANTE.


ZAMBIA YAVUTIWA NA MFUMO WA MASOKO YA MADINI NCHINI TANZANIA

 

Dodoma

 

Sekta ya Madini nchini Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingi za Afrika kwa namna ilivyoweza kurasimisha sekta ndogo ya uchimbaji madini na hivyo kupelekea wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao kupitia mfumo ulio rasmi ambapo Serikali inaweza kufuatilia shughuli zao mpaka hatua ya kuuza madini yao, kupitia katika masoko ya madini yaliyopo nchini.

 

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga Julai 24, 2023 jijini Dodoma alipokutana na ujumbe kutoka Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi ya Jamhuri ya Zambia katika ziara inayolenga kujifunza mifumo ya usimamizi wa Sekta ya Madini hususan kwenye shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo.

 

Dkt. Mwanga amesema kuwa, uwepo wa masoko ya madini umewezesha wachimbaji kupata soko la uhakika pamoja na kuongeza mapato kutoka Sekta ya Madini na mchango wa sekta kwenye Pato la Taifa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2022 umefikia asilimia 9.1 ikiwa lengo ni kufikia mchango wa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

 

Naye, Meneja wa Biashara kutoka Tume ya Madini George Kaseza, ameueleza ujumbe huo kuwa, hadi sasa kuna Masoko ya Madini 42 na Vituo vya ununuzi wa madini 94 katika maeneo mbalimbali yenye shughuli za uchimbaji madini.

 

“Uwepo wa masoko ya madini umeongeza mapato kutoka shilingi bilioni 8.30 Mwaka wa Fedha 2018/19 hadi kufikia shilingi bilioni 157.43 Mwaka wa Fedha 2022/23,” amesema Kaseza.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Madini Zambia Samson Phiri amesema mafunzo hayo nchini yamelenga kuwawezesha wataalam wa Sekta ya Madini nchini Zambia kujifunza mifumo ya usimamizi wa Sekta hiyo hususan kwenye shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo.

 

Ujumbe huo unatarajia kutembela Soko la Madini Mkoa wa Shinyanga, Soko la Dhahabu mkoa wa Geita ili kujifunza namna biasharaya madini inavyofanyika katika masoko hayo.

 

Ziara ya Zambia nchini inakuja ikiwa zimepita siku chache tangu ujumbe kutoka nchi ya Kenya ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Uchumi wa Bluu wa nchi hiyo Elijah Mwangi  kufika nchini kujifunza kuhusu namna bora ya usimamizi wa Sekta ya Madini.


Zifuatazo ni picha za Matukio mbalimbali wakati Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga alipokutana na ujumbe kutoka Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi ya Jamhuri ya Zambia katika ziara inayolenga kujifunza mifumo ya usimamizi wa Sekta ya Madini hususan kwenye shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo jijini Dodoma



 

 

 



SERIKALI YA KANADA IMETOA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 240 KUBORESHA SEKTA YA AFYA TANZANIA.

 Na Moreen Rojas,
Dodoma

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameishukuru Serikalia ya Kanada kupitia Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan wake kwa kusaidia  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia kiasi cha shilingi Bilioni 240 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya.

Waziri Ummy amebainisha hay leo Jijini Dodoma wakati wamkutano na vyombo vya habari baada ya Waziri wa Maendeleo ya jamii Kanada kuzungumza na vyombo vya habari pia

Waziri Ummy ameeleza kuwa kati ya kiasi kiasi hicho shilingi 140 zinaingia serikalini kwa ajili ya kuchangia mfuko wa afya wa pamoja ambapo mpaka sasa Serikali ishapokea kias cha shilingi Bilioni 94 ambazo zimeelekezwa kwenye akaunti za ngazi ya msingi ambazo ni zahanati na vituo vya afya nchini.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Vituo vya afya na zahati watapanga  vipaumbele vyao kwajili ya kulipia maji, umeme, kununua dawa, kwajili ya uzazi salama na wanatumia kufanya ukarabati mdogo pamoja na kununua vifaa tiba.

“Kwa ujumla mchango wa Serikali ya Kanada kwa Tanzania umeleta matokeo mazuri kwa Huduma za afya Tanzania leo tunaongea wanawake karibu asilimia 90 wajawajito wanajifungulia katika vituo vya kutoa Huduma za afya kwa sababu ya mchango wa Kanada”, aweka wazi Waziri Ummy.

Lakini pia ameongeza kuwa wamepunguza vifo vya watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano kutoka vifo 67 katika kila vizazi hai 1000 hadi vifo 43.

Vile vile amesema wamefanikiwa kuongeza idadi ya wanawake wanao tumia njia za kisasa za uazazi wa mpango kutoka asilimia 32 hadi asilimia 38 .

“Lakini pia tumeweza kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi asilimia 22 , tumepunguza udumavu kutoka asilimia 38 na sasa tunazungumzia asilimia 31 na kwa watoto wetu wanapata chanjo”, Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan amesema kuwa wametangaza miradi mitano mipya ya afya yenye thamani ya dola za Canada milioni 128.5 ambapo dola za Canada milioni 75 kwa mfuko wa ruzuku wa shughuli za Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Sector Busket Fund, HSBF)  kwa serikali ya Tanzania na nyongeza ya dola za Canada 500,000  kwa UNICEF kwa usaidizi wa kitaalam.

"Leo nina furaha pia kutangaza dola za Canada milioni 23 katika ufadhili wa shirika la CanGIVE kwa miradi miwili mipya kwa ushirikiano na UNICEF Tanzania na shirika la Afya Duniani,Tanzania miradi hii ya CanGive itasaidia juhudi za watanzania kuchanja makundi yaliyopewa kipaumbele kwa njia ambayo itaimarisha huduma za afya kwa mapana zaidi”,  Amesema Mhe.Sajjan

Ameongeza kuwa miradi hiyo  itasaidia wafanyakazi wa afya kushirikisha jamii na kukabiliana vyema na vizuizi vya kijimii kwa kutoa chanjo  na huduma za afya

Aidha ametangaza mradi wa dola za Canada 15 chini ya Shirika la Kimataifa  Plan International Canada kwa ajili ya mradi wa afya na haki za wasichana, vijana, mradi uliopo Mkaoni Katavi pamoja na nyongeza ya dola za Canada 15 kwa ajili ya mradi wa kukuza matumaini na maendeleo kwa vijana nchini Tanzania huu utatekelezwa na shirika la la Kimataifa  World Vision Canada katika maeneo Mikoa ya Dar es salaam na Dodoma.
MWISHO


CANADA YATOA SHILINGI DOLA MILIONI 50 KWA AJILI YA MAENDELEO YA ELIMU NCHINI.

 Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Waziri wa Elimu Prof.Adolph Mkenda amepokea dola za Canada milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini.

Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi ya wizara jijini Dodoma ambapo asilimia 25 itatumika kwa ajili ya shule za wanafunzi wa kike na asilimia 25 zingine kutumika katika mafunzo ya amali kwa ajili ya kuwaandaa vijana kwa ajira.

"Tunafurahi mahusiaano yetu katika sekta ya elimu yanakuwa na kuimarika siku hadi siku na watanzania wengi wamesoma Canada kupitia serikali ya Canada pamoja na kuwa na elimu ya lazima ya miaka 10 badala ya miaka 7" Amesema Prof.Mkenda.

Kwa upande wake Mhe.Harjit S.Sajjan Waziri wa maendeleo ya kimataifa na waziri mwenye dhamana ya shirika la maendeleo ya uchumi la Pasifiki ya Canada amesema kuwa shule nyingi hazikidhi mahitaji ya wasichana walio katika kipindi cha balehe katika suala la usalama au upatikanaji wa maji au vyoo maalumu vya kujihifadhi wakati wa hedhi.

Aidha ameongeza kuwa uwekezaji katika elimu ya wasichana hubadilisha jamii huimarisha uchumi na kupunguza ukosefu wa usawa,inachangia jamii kuwa imara zaidi,jamii imara inayotoa fursa kwa watu wote ikiwa ni pamoja na wavulana na wanaume fursa ya kutumia uwezo wao.

"Tumeshirikiana kuboresha viwango vya elimu na upatikanaji wa elimu kwa shule zote za msingi na sekondari kwa wasichana na wavulana na niko hapa kuthibitisha Canada kwamba itaendelea kusaidia jitihada za elimu nchini Tanzania kama Mwalimu Julius Nyerere alivyosema " Elimu sio njia ya kukimbia umaskini,ni nyenzo ya kupambana nao"Amesema Mhe.Sajjan.


Aidha ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 14 iliyopita Canada imetoa zaidi ya dola milioni 250 za Canada kwenye mfumo wa elimu,kwa kushirikiana na Serikali Canada imewekeza katika mafunzo madhubuti kwa walimu wa baadae katika vyuo 35 vya ualimu.

"Sera yetu ya usaidizi wa kimataifa ya kijinsia inaweka msisitizo katika fursa sawa kwa wanawake na wasichana,kutumia mtazamo wa kijinsia kunamaanisha kuhoji ubaguzi nyumbani na duniani kote na kutambua mambo yanayosababisha ukosefu wa usawa,tumejifunza umuhimu wa kuwapa wasichana nafasi salama kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi"Amesisitiza Mhe.Sajjan.

Sanjari na hayo amesema kuwa wasichana wajawazito na mabinti waliojifungua wanastahuki kupata elimu,stadi za maisha,ujuzi wa malezi na mafunzo ya ujuzi,kisha wanaweza kuendelea na masomo yao,kupata fursa sawa ya ajira yenye staha na kuvunja mzunguko wa umasikini ambao kina mama wengi wadogo wanaangukia.

Canada imetangaza dola milioni 25 kwa mradi wa Binti Asome(Every Girl Learns_EAGL )Tanzania Bara na Zanzibar chini ya UNICEF ambapo maradi huu utawezesha elimu kwa mabinti katika ngazi ya msingi na sekondari,haswa katika masomo ya hisabati na sayansi.

Programu hii itachangia kuongeza viwango vya uhitimu kwa wasichana katika shule za sekondari na kuwasaidia mabinti wenye umri kuanzia kati ya 10 na 19 kujifunza na kuongeza ujuzi wao ili kuendana na mahitaji ya soko ya sasa na baadaye nchini Tanzania.


WANANCHI WAASWA KUACHA KUDANGANYA MAENEO YA MAKAZI.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewaasa wananchi na wakazi wa Dodoma kuacha kudanganya maeneo ya makazi ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Mhe.Senyamule ameyasema hayo wakati akizindua mpango mkakati kwa ajili ya kushughulikia na kutatua migogoro ya ardhi kwa jiji la Dodoma.

Aidha amesema kuwa jiji la Dodoma limekuwa na ongezeko la wananchi hivyo kufuatia ongezeko hilo limepelekea matumizi ya ardhi kuwa ni mengi na mengine kuwa ya kiholela bila mpangilio ambapo kwa kutatua changamoto hii mkoa wa Dodoma kupitia Mkuu wa mkoa wa Dodoma imeandaa timu kwa ajili ya kutatua na kumaliza migogoro.

"Kuna changamoto mbalimbali zinazochangia migogoro hii kushindwa kuisha kutokana na uchache wa vifaa vya tehama, ukosefu wa huduma bora kwa wananchi,eneo la jiji kuwa dogo, lugha mbaya kwa wananchi zinazotolewa na watumishi wa jiji,kipandikizi yaani kupandikiza zaidi ya kiwanja kimoja kupewa watu tofauti pamoja na wananchi kupuuza jumbe za simu" Amesisitiza Senyamule.

Aidha ameongeza kuwa jambo hili litafanyika ndani ya miezi 6 yaani Julai hadi Disemba ambapo kutafanyika uhakiki wa maeneo ambayo yanamalalamiko ambapo wahusika wanavamia maeneo ambayo sio ya kwao pamoja na kurekebisha mifumo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais tamisemi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri amesema kuwa mpango huo utaweza kuwasaidia kutambua mapungufu gani ya ndani na madhaifu gani ya nje ili ili kuishi matarajio ya kiongozi wa kitaifa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha jiji la Dodoma linapagwa vizuri ili kuendana na hadhi ya makao makuu ya nchi.

Aidha amesema kuwa ni matumaini yake kwamba elimu ya kutosha itatolewa kwa kamati ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa huku akisisitiza maeneo ya wazi kupewa watu sahihi ili kuhakikisha wanajenga vitu vyenye manufaa kwa wananchi.

"Mifugo kuzurura mjini nilipata nafasi ya kuongea na wafugaji tulikuwa na kikao kizuri hivyo ni rai yangu tuliyokuwa tukiyaongelea yatakuwa yamezingatiwa,wakati mmoja tulikamata mifugo ya kiongozi mmoja,akanipigia simu nikamwambia lazima ulipe fidia haijalishi wewe ni nani huwezi acha mifugo kiholela" Amesema Shekimweri.

Aidha ametoa rai kwa watumishi wa ardhi kuhudumia wateja vizuri kwa kutoa kauli nzuri kwa wateja pamoja na kuheshimu watu.


*AWESO AMUONDOA MKANDARASI MRADI WA MAJI

KAZURAMIMBA-UVINZA-KIGOMA

Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amekasirishwa na kitendo cha Mradi wa Maji Kazuramimba kuchukua muda mrefu bila kukamilika wakati wananchi wakiendelea kuteseka na ukosefu wa huduma hii muhimu.
Awali changamoto ya Mradi wa Maji Kazuramimba ilikua ni kuchelewa kwa Tanki la Maji ambapo mwaka jana Waziri Aweso alifika na kuhakikisha Tenki linatoka na kufika Uvinza Kigoma.

Waziri Aweso amefanya maamuzi ya kumuondoa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Kazuramimba unaotekelezwa kwa Ufadhili wa Enabel na Mkandarasi akiitwa Nangai Engineering Company Limited baada ya kutembezwa umbali mrefu bila kuona vituo vya Maji akiongozana na wananchi wenye hasira kali.

Wakati wa ziara hiyo Mheshimwa Waziri hakuridhishwa na kasi ya Mkandarasi katika utekelezaji wa mradi huo ambao umeanza toka Novemba, 2020 na alitakiwa kukamilisha kazi katika kipindi cha miezi tisa na badala yake sasa ni mwaka wa tatu.

Kutokana na hali hiyo Mheshimiwa Waziriamemundoa kufanya kazi hiyo, ameivunja kamati ya Maji ya Mradi huo na kuitaka RUWASA kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuusimamia.


AFISA KILIMO GAIRO AMEWATAKA WAKULIMA NCHINI KUACHA KUFANYA KILIMO CHA MAZOEA

Na. Kadala Komba Gairo

 

Wakulima mkoani Morogoro wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea ili kuweza kuepuka hasara zinazojitokeza mara kwa mara badala yake wafuate ushauri unaotolewa na wa taalamu wa kilimo.

Hayo yamebainishwa na afisa  Kilimo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro  Philemon Isack Akizungumza  katika Kijiji cha Msingizi wakati wa kutambulisha aina mpya za mbegu  za karanga na mtama kwenye mkutano ulioandaliwa na Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA),

Mbegu zilizotambulishwa ni NARI nut 2015, Naliendele 2016 na Nachi 2015 ambazo ni za karanga. Mbegu za mtama ni TARI SORI 2 na Macia.

Isack alisema kuwa wakati huu ambao serikali inawekeza fedha nyingi kwenye kilimo kuna haja ya wakulima kubadili mitazamo na kuendesha kilimo chenye tija na kuachana na kilimo cha mazoea cha kutupia mbegu.

“Bado baadhi ya wakulima wamekuwa wakiendesha kilimo cha mazoea ,wakati trekta linalima wanapita nyuma kumwaga mbegu, wakati mwingine mbegu zinamwagika nyingi na hivyo kupelekea mazao kuota kwa kubanana na hivyo kushindwa kukua vizuri,” alisema.

Alisema kuwa kama wakulima watafuata kilimo cha kitaalam mbegu zitatumikachache na mazao yataota kwa utaratibu mzuri na hivyo kupelekea mavuno kuwa makubwa.

“Tumejiwekea malengo ili kuongeza uzalishaji kutoka gunia tatu kwa ekari hadi kufikia gunia 10 na 15 kwa ekari,” alisema

 

Kwa upande wao, wakulima wa Kijiji cha Msingisi wameiomba Serikali kuendelea kusambaza mbegu bora ili ziwafikie kwa wakati hali itakayochangia kuongeza uzalishaji.

 

Grace Petro ambaye ni mkulima wa mtama alisema kuwa juhudi zao kwenye kilimo zitafanikiwa iwapo serikali itasaidia upatikanaji wa mbegu bora.

“Upatikanaji wa mbegu bora utasaidia sana wakulima hasa wa vijijini wakipata mbegu bora za wakatiitasaidia kuongeza uzalishaji,” alisema

Glads Ngalawa alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya ndege kushambulia mazao ni vyema wakulima wakapewa mbinu za kuzuia mazao kushambuliwa na ndege ikiwemo mtama.

Mtendaji Mkuu wa DASPA, Aithan Chaula aliwataka wakulima kulima mazao ya mtama na karanga kutkana na kuwa na soko la uhakika.

Alisema kuwa kupitia mradi huo wakulima watapewa mafunzo kwa ajili ya uzalishaji mbegu na watakaofanya vizuri watapewa vyeti naTaasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu nchini (TOSCHI) na watakuwa wauzaji wa mbegu kwenye maeneo wanayotoka.

 

“Tunataka tukija wakati mwingine tukute maduka ya wazalishaji wa mbegu ili kuuzia wakulima wengine,” alisema,

Alisema kuwa mtama una fursa kubwa ya kuzalishwa kwa wingi zaidi kama zao la chakula kuziba nafasi ya mazao mengine ambayo yameathiriwa na ukame kutokana na na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwenyekiti wa DASPA, Janeth Wilson aliwataka wakulima kulima mtama kwa wingi kwani una soko la uhakika.

Mwisho

 



 afisa  Kilimo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro  Philemon Isack Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msingizi



Mwenyekiti wa Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA), Janeth Wilson akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msingisi Wilaya ya Gairo Mkoani Dodoma wakati wa kutambulishwa kwa mbegu za mtama na karanga (Picha na Kadala Komba)



Mtendaji Mkuu wa DASPA, Aithan Chaula Akiwahakikishia wakulima aliwataka wakulima kulima mazao ya mtama na karanga kutkana na kuwa na soko la uhakika.
 


George Katoto:Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Gairo Akizungumza na viongozi wa shirika la DASPA ofisini kwake

Bi.Msifwahi Haule ,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo Akizungumza na uongozi shirika la DASPA  ofisini kwake walipofika kuripoti mkoani hapo.






MATUKIO YA PICHA

wakulima wa Vijiji vya  Msingisi na  Kibeya waliyopatiwa mafunzo ya utambuzi wa mbegu mpya za karanga na mtama  kutoka shirika la  DASPA



Peter Paulo Mratibu CCT Wilaya ya Gairo na Bwana shamba wakampuni ya Hans Agriculture machinery &DASPA

*MASHINE YA MRI IMEANZA KUFANYA KAZI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA*



Na Mwandishi wetu Mbeya.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe Julai 12, 2023 imeanza rasmi kutoa huduma ya vipimo kwa kutumia mashine ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa MRI (Magnetic Resonace Imaging)

Akiongea baada ya kumaliza ziara yake hospitalini hapo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mashine hiyo ambapo ambayo imekua ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya na kutoa upatikanaji bora wa vipimo vya kisasa kwa wananchi.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya kufanya uwekezaji huu katika katika Mkoa wa Mbeya ambapo kufanya kazi kwa mashine ya MRI italeta mabadiliko makubwa katika huduma za afya na kuimarisha uwezo wa Hospitali yetu na wataalamu wetu kutoa huduma bora kwa jamii na kupunguza gharama za kusafiri kwenda Dar es salaam kuifuata huduma hii” ameshukuru Mhe. Homera

Aidha Mhe. Homera ameishukuru Wizara ya Afya chini ya Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa jitihada kubwa zilizofanyika hadi kufanikisha shughuli za usimikaji wa mashine hiyo ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia takribani wakazi wa mikoa 7 ya Nyanda za Juu Kusini.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji amesema uwepo wa mashine hiyo utawezesha shuguli za huduma hospitalini hapo kufanyika  kwa ubora zaidi kwa kuwa hapo awali wataalamu walikuwa wakilazimika kutoa rufaa kwa wagonjwa kwenda Dar es salaam kufuata kipimo cha MRI.

“Tunaweza kupima wagonjwa ambao wana matatizo ya Saratani au vimbe za aina tofauti tofauti kwenye mwili, pia tunaweza kupima mabadiliko yanayoendana na umri.”

Akizungumza mara baada ya kupata huduma za uchunguzi kupitia mashine ya MRI, Bi. Reinfrida Kayombo mkazi wa Jijini Mbeya, ameishukuru Serikali kwa kwa kuwaletea huduma hiyo karibu na kuwasaidia kwa wakazi wa Nyanda za juu kusini ambao hapo awali walilazimika kutumia garama kubwa kuifuata huduma hiyo mbali.

“Tunamshukuru sana Mama Samia kwa kutuletea huduma hii maana hapo awali tulikuwa tunapata gharama kubwa kusafiri lakini kwa sasa tumeletewa huduma hapahapa.” Amesema Bi. Kayombo.

Mashine ya MRI ni teknolojia ya hali ya juu ambayo inatumika kuchunguza na kutoa picha za mwili wa binadamu kwa kutumia mawimbi ya umeme na magneto.  Mashine hiyo inatoa maelezo ya kina na inaweza kuchunguza hali mbalimbali za kiafya, kama vile matatizo ya ubongo, saratani, magonjwa ya moyo, na matatizo ya mfumo wa musculoskeletali. Uwepo wa mashine hiyo utasaidia wakazi Mikoa saba ya Nyanda za Kusini ikiwemo Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Njombe na Iringa pamoja na nchi za jirani kupata huduma za kibingwa za uchunguzi na tiba kwa haraka Jirani na maeneo waliyopo.


WAPIGA KURA 74,642 KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI KESHO

 
Na Mwandishi maalum - NEC
Wapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara kesho Julai 13,2023.

Jumla ya wapiga kura 74,642 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu mdogo na jumla ya vituo 205 vya kupigia kura vitatumika.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele katika Risala ya Uchaguzi huo mdogo unaofanyika kujaza nafasi wazi za udiwani.

Jaji wa Rufaa Mwambelegele  amewataka wasimamizi wa uchaguzi, vyama vya siasa na wagombea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi wakati wa Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara.

Uchaguzi huo mdogo utashirikisha, Kata ya Ngoywa katika  Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Kata ya Kalola katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora  na za  Sindeni katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,  Potwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,  Kwashemshi katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na Bosha katika Halmashauri ya  Wilaya ya Mkinga zote za Mkoa wa Tanga.

Kata nyingine ni  Mahege katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani, Kata ya Bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mkoa wa Simiyu, Kata ya Njoro na Kalemawe zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kata ya Kinyika katika Halmashauri ya Wilaya ya  Makete mkoa wa Njombe , Kata ya Magubike katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro na Kata ya Mbede katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.

Aidha, amevitaka vyama vya siasa, wagombea na wadau wa uchaguzi kuepuka kujihusisha na matukio yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwani jukumu la kulinda amani ni la kila mmoja, hivyo wahakikishe wanalinda amani iliyopo  nchini.

“Jukumu la kulinda amani ya nchi yetu ni la kila mmoja wetu wakiwemo wananchi, vyama vya siasa, wagombea na wadau wengine wa uchaguzi,”alisema Jaji wa Rufaa Mwambegele.

Aliongeza kuwa  Sheria na Kanuni za Uchaguzi zimeweka mamlaka na taratibu zinazotakiwa kufuatwa iwapo kutakuwepo na malalamiko yoyote wakati wa uchaguzi, hivyo amevitaka vyama vya siasa na wagombea kufuata taratibu hizo ili  uchaguzi huo ufanyike kwa uhuru na haki.

Mweyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amewataka wapiga kura wote waliojiandikisha katika Kata 13 za Tanzania Bara kujitokeza kupiga kura ili waweze kuwachagua madiwani wanaowataka.

Amevitaka vyama vya siasa wagombea na wafuasi wao kuzingatia kuwa kampeni za uchaguzi zinakamilika leo Julai 12,2023 saa 12:00 jioni hivyo hawaruhusiwi kufanya mikutano ya kampeni kuanzia muda huo na hawaruhusiwi kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi.

 Aidha Jaji Rufaa Mwambegele amevikumbusha vyama vya Siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo, kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya kupigia, kuhesabu na kujumlishia kura.

“Upigaji kura utafanyika katika vituo vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. Iwapo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao walifika kabla ya saa 10:00 jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura, mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa 10:00 jioni”alisema Jaji Rufaa Mwambegele.

Aliongeza   “Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 62(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292, imeruhusu wapiga kura ambao wamepoteza kadi zao au kadi kuharibika kutumia vitambulisho mbadala”.

Amevitaja vitambulisho mbadala kuwa ni Passi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Mpiga kura aliyepoteza kadi au kadi yake kuharibika ataruhusiwa kutumia kitambulisho mbadala iwapo tu atakuwa ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na jina lake lipo kwenye orodha ya wapiga kura kwenye kituo anachopigia  kura.

Mwambegele amekumbusha kuwa katika vituo vya kupigia kura kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokuwa na watoto vituoni na kutakuwa na majalada ya nukta nundu katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona ili weweze kupiga kura wenyewe. Alifafanua kuwa kwa wapiga kura wenye ulemavu wa kuona ambao hawawezi kutumia majalada hayo wanaruhusiwa kwenda vituoni na watu watakaowachagua wenyewe kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Jumla ya vyama vya siasa 17 vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo mdogo ambapo Tume imevipongeza vyama hivyo na wagombea wao kwa kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Udiwani.

MWISHO


WANANCHI WAALIKWA MIAKA 60 YA JKT

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Waziri wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)Mhe.Innocent Bashungwa amewaalika wananchi wa mkoa wa Dodoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo yatakayofanyika tarehe 10 julai siku ya jumatatu katika uwanja wa jamuhuri jijini Dodoma.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo lengo likiwa ni kutoa muongozo na taratibu kufuatia siku hiyo ya miaka 60 ya JKT.

Aidha amesema kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa ni Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Aidha maadhimisho ya miaka 60 ya JKT yalitanguliwa na shughuli mbalimbali ambapo June 25 kulikuwa na tukio la JKT marathon ikiwa ni tukio la kwanza tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi wa tukio hilo alikuwa Rais mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Aidha ameongeza kuwa JKT inajivunia kuwa moja ya taasisi inayotambua na  kuvumbua  vipaji ikiwemo michezo na sanaa.

"Jeshini vipaji vyote vipo tunavilea tunavijengea ustawi na tunaangalia namna ya kutambua vipaji hivi na kuviendeleza mfano mzuri ukisikiliza bendi ya JKT au waimbaji wetu wa taarabu utaona ni kwa namna gani tunakuza na kuendeleza vipaji" Amesisitiza Waziri Bashungwa.

Sanjari na hayo miaka 60 ya JKT itapambwa na maonyesho ya vifaa mbalimbali kutoka JKT na wasanii mbalimbali bila kusahau gwaride huku wakiwaalika marafiki kupitia chaneli za kidiplomasia ikiwemo Izrael.

Jeshi la kujenga Taifa (JKT)lilianzishwa mwaka 1963 chini ya muasisi wa Taifa Rais Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)Mhe.Innocent Bashungwa
Kaimu Mkurugenzi Idara ya habari maelezo Ndugu Rodney akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wakati wa maswali na majibu
Wakuu wa wilaya Mhe.Godwin Gondwe mkuu wa wilaya ya Bahi ambaye amekuja kwa niaba ya mkuu wa mkoa
Wakuu wa jeshi pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia kwa ukaribu taarifa ya Mhe.Innocent Bashungwa kuhusu maadhimisho ya miaka 60 ya JKT


SERIKALI HAIPO TAYARI KUMPOTEZA MTU

 
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Serikali haipo tayari kuona Mwananchi yeyote anapoteza uhai wake  kwa sababu za ama ujambazi au udereva mbovu barabarani au migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Sagini ameyasema hayo wakati akihitimisha bonanza la michezo lililoandaliwa na Umoja wa Maafisa Usafirishaji (Bodaboda ) Wilaya ya  Butiama kwa lengo la kupinga matukio ya mauaji na ukatili katika jamii.

"Nataka niwaambie Serikali ya awamu ya sita chini ya  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitaki kumpoteza kijana hata mmoja au Mwananchi yoyote yule kwa sababu ama za ujambazi au udereva mbovu barabarani au migogoro baina ya wakulima na wafugaji. Ni aibu kuwa na matukio ya uhalifu tutawakamata wahalifu wote. Niwaombe vijana tuache kutumia njia za mkato kujipatia fedha."Alisema Sagini

Sagini amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo imara na linawataalamu wenye ujuzi wa kutosha kuwabaini watu mbalimbali wanaojihusisha na matukio ya kihalifu na hivyo amewaasa wale wote wanaotamani kushiriki kufanya uhalifu kuacha mara moja.

Sagini amesema kuwa Serikali inaunga mkono jitihada za bodaboda hao katika kukemea na kupinga matukio ya kikatili na mauaji ni jambo jema na Serikali haitamani kusikia kuendelea kwa matukio hayo.

Katika hatua nyingine Sagini amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo imara na linawataalamu wenye ujuzi wa kutosha kuwabaini watu mbalimbali wanaojihusisha na matukio ya kihalifu na hivyo amewaasa wale wote wanaotamani kushiriki kufanya uhalifu kuacha mara moja.

Sagini amesema kuwa Serikali inaunga mkono jitihada za bodaboda hao katika kukemea na kupinga matukio ya kikatili na mauaji ni jambo jema na Serikali haitamani kusikia kuendelea kwa matukio hayo.

Awali akitoa taarifa za lengo la bonanza hilo Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Samson Samwel Atoo amesema kuwa lengo la Bonanza hilo ni kuwaunganisha kwa pamoja, kupiga vita na kukemea matukio ya kihalifu yakiwemo mauaji yaliyotokea mwezi uliopita ambapo waendesha bodaboda 03 walipoteza maisha kwa kushambuliwa na kuuawa kinyama.

Tamasha hilo lilihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbiza kuku,


HUAWEI AT MWC SHANGHAI 2023:BOOSTING 5G EVOLUTION TOWARDS 5.5G REVITALIZE THE DIGITAL ECONOMY

Huawei has shown up in full force for MWC Shanghai 2023, with their activities all falling under their theme of "GUIDE to the Intelligent World". This year, the company's activities include an experiential tour that takes audiences to multiple cities to learn about their technology and business, as well as the launch of its newest innovative products and solutions for 5GigaGreen, 5G intelligent core networks, Intelligent OptiX Networks, private line + X products, and other intelligent digital transformation solutions.


At these activities, Huawei will also host numerous roundtables and dialogues with global operators, industry partners, and opinion leaders, to explore a variety of topics which include speeding up 5G prosperity, advancing intelligent digital transformation, and striding towards the 5.5G era to realize business, industry, and social value. The company says its goal is to create new value for customers and revitalize the digital economy through sustained innovation.

Sabrina Meng, Huawei's Rotating Chairwoman and CFO, gave a keynote titled "Embracing 5G transformation". She said, "The digital infrastructure of the future intelligent world will be deeply integrated into every aspect of our lives, industry, and society. It won't be based on advancements in individual technologies, but rather on incredibly massive, complex systems – the convergence of multiple elements. It's going to require systems-level thinking and design. When watching a chess game, you can see the big picture. But when you're playing chess, you focus on the details. Likewise, systematic capabilities to integrate technology and transform management are critical for the future success of 5G. First, let's talk about integrating different technologies. We can achieve greater synergy across cloud, networks, edge, and devices through systematic design and innovation across domains. When coupled with optimization across software, hardware, chips, and algorithms, we can address the challenges associated with developing complex solutions for vastly different industrial scenarios. Next, management transformation. Digital and intelligent transformation is not just about technology itself. It's more about transforming your approach to management. Going digital requires redefining the relationships between people, events, things, and theory, and adopting a more open, forward-looking management approach to address future challenges."

There are currently over 1.2 billion 5G users worldwide, and operators who moved quickly to develop 5G are already enjoying the first wave of benefits. This is thanks to the increasing network requirements being set by new applications in various markets. In the consumer market, new services like New Calling, cloud phones, and glasses-free 3D require faster data rates and lower latency, while in the industrial market, the RedCap ecosystem has matured, the passive IoT market is expanding, and the Internet of Vehicles (IoV) requires higher uplink speeds. These all-scenario applications are expected to result in 100 billion connections. These new service models are also expected to drive industry upgrade that will create a second wave of benefits.

Commercial 5G services hit the market four years ago, and has since been introduced to more than 17,000 private-network projects around the world. Both revenue from 5G private networks and the number of industrial connections have tripled. In addition, many operators have leveraged the CNY10 billion in revenue earned from 5GtoB private networks to drive a CNY100 billion increase in DICT revenue from cloud, data storage, and platform services. While many 5GtoB services were piloted in China, they have since expanded to other parts of the world, and have been commercially replicated in Asia Pacific, Europe, the Middle East, and Africa. These services allow industry customers to reduce costs and improve efficiency, while enabling intelligent digital transformation in industries like manufacturing, ports, mines, oil fields, and healthcare.

5.5G is also rapidly approaching for the communications industry. 5.5G technologies are expected to improve network capabilities 10-fold and create 100 times more business opportunities for operators. At this year's MWC Shanghai, Huawei is showcasing four of the major features of 5.5G – 10 Gbit/s downlink, 1 Gbit/s uplink, 100 billion connections, and native AI. It is also exploring the five connectivity areas expected to go mainstream with 5.5G – connectivity for people, for things, for vehicles, for industries, and for homes. Huawei has already started helping a number of operators around the world begin commercial verification of 5.5G. The 5.5G industry will continue growing quickly as the first release of 5.5G standards is expected to be frozen in the first half of 2024 and related technologies have already been extensively verified.




MWC Shanghai 2023 runs from June 28 to June 30 in Shanghai, China. Huawei will showcase its products and solutions at stands E10 and E50 in Hall N1 of Shanghai New International Expo Centre (SNIEC). Together with global operators, industry professionals, and opinion leaders, we dive into topics such as speeding up 5G prosperity, striding towards the 5.5G era, and intelligent digital transformation. 5.5G creates new business value in areas like connecting people, Internet of Things (IoT), and Internet of Vehicles (IoV), supporting countless industries as they move towards an intelligent world


BAHI KINARA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA BOOST

 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe madarasa 51, Vyoo 63 na nyumba 1 ya waalimu ikiwa ni sawa na shule 7 zilizokamilika katika Wilaya ya Bahi.
 
Akipokea shule na miundombinu yake Senyamule amepongeza uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa kukamilisha mradi huo tarehe 28 Juni 2023 ikiwa ni siku mbili kabla ya tarehe iliyopangwa na Mkoa yaani tarehe 30 Juni 2023.
 
“Bahi mnajipambanua sana katika suala la elimu, awali tu tulikuwa tunaziambia Halmashauri zingine zije zijifunze kwenu kuhusu kufaulu, leo tutawatuma kujifunza kuhusu mnavyojipanga kukamilisha miradi ya ujenzi kwa wakati na viwango vya hali ya juu” Senyamule amesisitiza.
 
Amesema Mkoa wa Dodoma umepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya 16 zenye miundombinu ya kisasa ikiwa ni pamoja na michezo ya watoto na uzio kwa ajili ya madarasa ya awali.
 
Akikabidhi madarasa hayo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe amesema Wilaya yake imekamilisha ujenzi huo wa Shule na madarasa kwa muda ulioelekezwa kwa ubora na viwango elekezi, huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa ya kufanikisha ujenzi huo.
 
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa naomba upokee Shule hii na madarasa ambayo yamekamilika kwa viwango vya ubora wa hali ya juu kwa niaba ya wana Bahi naomba utufikishie shukrani zetu kwa Mhe Rais” Amefafanua Mhe. Gondwe
 
Kwa upande wake Afisa Elimu Wilaya ya Bahi Mwl. Boniphace Wilson amesema kukamilika kwa madarasa hayo ni suluhu ya msongamano wa wanafunzi katika madarasa ya awali ambapo Wilaya hiyo ilipokea fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya mbili zenye jumla ya vyumba 28, madarasa manne ya awali, majengo mawili ya utawala na vichomea taka.
 
Wilaya ya Bahi imekuwa Wilaya ya kwanza katika Mkoa wa Dodoma kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya mradi wa Boost ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa shule mpya za msingi, vyumba vya madarasa, madarasa ya mfano ya elimu ya awali, matundu ya vyoo na nyumba za walimu.