Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

ZAIDI YA VIJANA 147 WAMEHITIMU MAFUNZO YA UANAGEZI

Na. Kadala Komba
DODOMA

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji  Ajira na Ujuzi  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki ameshauri Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Dodoma (SIDO) kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na vijana zinakuwa na ubora.

Msaki ameyasema hayo Aprili 25, 2023 SIDO Dodoma kwenye hafla ya kuhitimisha mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 147 na kukabidhi vifaa vilivyotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Ujerumani GIZ.

Amewataka vijana kutumia ujuzi walioupata kuzalisha bidhaa zenye ubora unaohitajika katika soko la kitaifa na kimataifa.

Msaki amesema kwa Mwaka  2022/23 serikali imetenga Sh.Bilioni tisa ili kuwezesha vijana kupata mafunzo ya ujuzi katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

"Jukumu la serikali ni kuhakikisha kunakuwepo sera na mipango ya kuwaongoza vijana ili wajiajiri, kuweka miundombinu sahihi ya kuwawezesha vijana kufanya shughuli za kiuchumi na kuhamasisha wadau kuhakikisha vijana wanafanya shughuli za kiuchumi,” amesema.

Naye, Meneja wa Mradi wa Jukwaa la Ushirikiano wa  Kimataifa (FIC), Erustus Ouko amesema lengo la mradi huo ni kushirikiana na serikali katika kusaidia kukuza ajira kwa vijana na wanawake.

Awali, Meneja wa Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ), Awadhi Milasi, amesema shirika hilo limechangia vifaa vyenye thamani ya Sh.Milioni 34 ili kufanikisha malengo ya SIDO Dodoma hususani kuwainua wajasiriamali wadogo.

Mkurugenzi wa SIDO Dodoma, Sempeho Manongi amesema vijana 147 kati ya 151 waliosajiliwa wamehitimu mafunzo yao huku baadhi wakishindwa kuhitimu kwa sababu mbalimbali.

Mmoja wa Wanufaika wa mafunzo hayo, Anthon Makasi amesema amepata  ujuzi ambao hakuwa nao awali na  kutoka kuwa mjasiriamali mdogo hadi kuwa  mkubwa na anatarajia kujiajiri baada ya mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji  Ajira na Ujuzi  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki

 Akikabidhi cheti kwa Muhitimu wa uanagezi 


Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji  Ajira na Ujuzi  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki Akikagua Bidhaa za wajasiriamali 





Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji  Ajira na Ujuzi  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki



WAKUU WA MIKOA DHIBITINI MAAMBUKIZI YA MALARIA-MAJALIWA



*Aitaja mikoa ya Tabora, Mtwara, Kagera, Shinyanga na Mara kuongoza kwa kiwango cha maambukizi

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa mikoa ambayo ina kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Malaria ianze kusimamia utekelezaji wa afua za ugonjwa huo ili kupunguza viwango hivyo.

 

Amesema kuwa lengo la Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutokomeza maambuzi ya ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030 “Upatikanaji wa afua za kinga kama vyandarua vyenye dawa na upatikanaji wa vitendanishi na dawa za malaria utasaidia sana kupungua kwa idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na Malaria hapa nchini”

 

Ametoa wito huo leo Jumanne (Aprili 25, 2023) wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Sukuhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2023 ambapo Kitaifa yamefanyika Jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Mkuu amesema takwimu zinaonesha mikoa inayoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria ni Tabora una asilimia 23, Mtwara asilimia 20, Kagera asilimia 18, Shinyanga asilimia 16 na Mkoa wa Mara una asilimia 15.

 

“Kwa upande mwingine, nimeelezwa kuwa mikoa 9 ina kiwango cha maambukizi chini ya asilimia moja nayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Songwe, Iringa, Dar es salaam na Mwanza. Kwa namna ya pekee kabisa ninaipongeza sana mikoa yote iliyofanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria”

 

Ameongeza kuwa takwimu zilizopo zinaonesha kuendelea kupungua kwa maambukizi ya Malaria mwaka hadi mwaka kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022. “nitoe wito kwa kuendelea kuongeza nguvu katika mapambano ya kutokomeza Malaria”

 

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wizara ya Afya kufanya kampeni ya kutosha katika kuhamasisha matumizi ya vyandarua vya kisasa hadi maendeo ya vijijini “hakikisheni afua hii inaanza kutekelezwa katika Mikoa yenye kiwango cha maambukizi chini ya asilimia moja ili tuweze kuharakisha ufikiwaji wa malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria hapa nchini”

 

“Naipongeza Wizara ya Afya kwa dhamira ya dhati katika mapambano dhidi ya malaria nchini Tanzania. Hivi sasa, zaidi ya 98% ya kesi za malaria zinathibitiwa, kesi za malaria zilizothibitiwa kwa mwaka zinaonesha kati ya kila watu 1,000 zilipungua kutoka 106 mwaka 2020 hadi 76 mwaka 2021 na zaidi hadi 58 mwaka 2022”

 

Nape Nnauye Vyombo vya habari, Mitandao ya kijamii hakikisheni mnakuwa na  mpango endelevu wa kuifanya Tanzania inakuwa na 0 ‘Zero’ Malaria kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake.

 

Naye, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa Wizara hiyo kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria na kwa kushirikiana na Wadau pamoja na Ofisi ya Rais - TAMISEMI inatekeleza Mpango Mkakati wa Malaria wa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.

 

Amesema kuwa mpango Makati huo unalenga kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria nchini kutoka wastani wa asilimia 7.5 ya mwaka 2017 hadi kufikia wastani wa chini ya asilimia 3.5 ifikapo mwaka 2025.

 

“Mkakati wa udhibiti wa mbu waenezao malaria unatekelezwa kupitia afua kuu nne za ugawaji na matumizi ya vyandarua vyenye dawa, upuliziaji viuatilifu ukoko kwenye kuta ndani ya nyumba, utunzaji na udhibiti wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu pamoja na unyunyiziaji wa viuadudu vya Kibaiolojia kwenye mazalia ili kua viluwiluwi vya mbu”

 

Naye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa wito kwa Vyombo vya habari, Mitandao ya kijamii na makampuni ya simu kuhakikisha wanakuwa na mipango endelevu ya kuifanya Tanzania inakuwa na Ziro’ Malaria “kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake”

 

Akizungumza Kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt Wilson Mahela amesema kuwa Ili kufanikisha mapambano dhidi ya Malaria, TAMISEMI imeendelea kusimamia utekelezaji wa Afua kinga na Afua tiba zinazotekelezwa Nchini.

 

Amesema kuwa katika kutekeleza Afua kinga, OR-TAMISEMI inasimamia mazoezi ya ugawaji wa vyandarua katika vituo vya kutolea huduma,mashuleni,kwa makundi maalumu(wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na zaidi,watoto wenye umri chini ya miaka 5 waliolazwa na Malaria kali”

 

Naye, Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani nchini Dkt. Zabulon Yoti ameipongeza Tanzania kwa kuwa moja kati ya mataifa manne Afrika katika kupunguza vifo duniani vitikanavyo na malaria kwa asilimia 52 ikiungana na nchi za Nigeria, Niger na Congo huku Tanzania ikirekodi asilimia Nne tu ya vifo.




MASHINDANO YA RIADHA MEI MOSI MOROGORO, UTALII WAZIDI KUTANGAZIKA*

 


Wizara ya Maliasili na Utalii  imeibuka  mshindi namba moja kwenye mbio za mita 800 kwenye  mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea  mkoani Morogoro.

Akizungumza leo mkoani humo mara baada ya ushindi  Elibariki Buko ambaye ndio mshindi namba moja wa mbio za mita 800 kutoka Wizara hiyo,  amesema ushindi huo utasaidia kuimarisha michezo na kuutangaza utalii Ili kuunga mkono juhudi  Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya 'The Royal Tour' za kutangaza utalii.

" Ushindi huu ni muhimu sana kwetu, tunaushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuhamasisha michezo. Ushindi huu ni moja ya sehemu ya kusaidia juhudi za kutangaza utalii kupitia filamu ya The Royal Tour ya Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. SAMIA Suluhu Hassan." alisema Buko.

Naye,  Afisa Utalii Mkuu na mmoja kati ya Viongozi wa Timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii,  Martin Mrema amesema Wizara  itahakikisha inaendelea kupambana ili kushinda michezo iliyobakia.

" Tumefurahi tumeshinda riadha, lakini si riadha tu, tumekuja kupambana na tutahakikisha tunatangaza utalii kupitia michezo. alisema.

Jumla ya michezo 10 imechezwa, kwa upande wa wanaume mbio za  za mita 1500 Elibariki Buko alishika nafasi ya  02 ,huku mbio za mita 3000 Kispani Saigoti akishika nafasi ya 02 huku Athumani Simbiri  akishika nafasi ya 03 katika mbio za mita 300 na 400.

Kwa Upande wa wanawake, mbio za mita 800 Jehovanesa Sarakikya alishika nafasi  03 na mbi


o za mita 1500  akishika nafasi ya 03.

MADAI YA KICHANGA KUGEUKA JIWE MARA, JE NINI MAONI YAKO:?

 Wakazi katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara leo Aprili 20 wameingiwa na taharuki baada ya mwili wa mtoto, AMIRI HAMIS mwenye umri wa mwezi mmoja na siku 12 kudaiwa kugeuka jiwe huku baadhi ya watu wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikiana.


#taharuki #kichanga #jiwe #ushirikina #tukio  #imani  #mara


 



WAKULIMA WA DODOMA WAMETAKIWA KULIMA MTAMA KWA WINGI

Na Kadala Komba Dodoma KATIBU Mtendaji wa Shirika la Dodoma Agriculture Seeds Production Association (DASPA) Aithan Chaula Álisema kuwa wanekuwa wakihamasisha wakulima kulima mtama kwani ni zao ambalo Lina sokola úhakika ikiwemo Shirika la Mpango wa Çhakula Duniani (WFP) kununua mtama kwa wakulima wa Mkoani Dodoma. " Mkulima anapotumia njia za kitaalam hupata mavuno kwa wingi hadi gunia 20 hadi 30 kwa ekari moja.. Àkizungumza na Shine News shambani kwake Kati Kijiji Cha Zinje nje kidogo ya Jiji la Dodoma alisema kilimo cha mtama kinalipa sana hii ni fursa kwa wakulima kufaidika na kilimo . Chaula ambaye anajishughulisha na uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali ikiwemo karanga na mtama alisema kuwa Mtama ni zao lenye uwezo mkubwa wa kustahimili ukame ukilinganisha na mazao mengine ya nafaka. ''Mtama unafursa kubwa ya kuzalishwa kwa wingi zaidi kama zao la chakula , hali ya hewa ya Dodoma inakubali sana zao.la mtama,mkoa wa Dodoma mtama unafanya vizuri.," ÁlisemaAlisema kuwa mtama ukilimwa kwa kutumia njia za kitaalam mkulima ana uwezo wa kuvuna gubia 20 hadi 30 kwa ekari moja. Álisema kuwa wanekuwa wakihamasisha wakulima kulima mtama kwani ni zao ambalo Lina sokola úhakika ikiwemo Shirika la Mpango wa Çhakula Duniani (WFP) kununua mtama kwa wakulima wa Mkoani Dodoma "Bado wakulima hawajaweza kutosheleza soko laWFP Ni vyema wakulima wakachangamkia fursa ya killimo Cha mtama , hapa tunazo mbegu Bora za mtama," Álisema Álisema kuwa mwaka Jana walipata mbegu ya mtama ainanya Kari 1 kutoka Shirika Utafiti wa Mazao Yanayomea Nyanda Kame (ICRISAT) lla nchini Malawi na mbegu hiyo imefanya vizuri shambani. Álisema kuwa sifa nyingine ya mbegu hiyo ni kuwa na Nani refu kwa juu ambalo huzuia ndege kutua na kula mtama. "Hii ni aina ya mtama ambayo ndegu haugusi, kwani hata akijaribu kutua Kuna Nani refuambalo huwa limamgongagonga huwa anajihisi hayuko salama" Álisema Pia alisema upepo mkali uliopita wiki iliyopita ulisababisha baadhi ya mtama kulala. "Mtama unapolala kutokama na upepo hupaswi kuuinua unapouinua unauvunja mtama Kama haujagusa ardhi utakuwa salama mpaka utakapovunwa" Álisema. kwa upande wake,Fabian Ngoloi ambaye ni mfanyakazi wa shamba la mbegu la DASPA alisema kuwa kilimo Cha mtama kina fursa kubwa katika mkoa wa Dodoma kwani unastawi vizuri. Álisema kuwa ni vyema vijana wakajikita mwenye shughuli za kilimo hicho kwani ardhi ya Dodoma inakubali vizuri zao hilo. mwisho
KATIBU Mtendaji wa Shirika la Dodoma Agriculture Seeds Production Association (DASPA) Aithan Chaula akiwa kwenye shamba lake la mtama Kati Kijiji Cha Zinje nje kidogo ya Jiji la Dodoma
Fabian Ngoloi ambaye ni mfanyakazi wa shamba la mbegu la DASPA akielezea fursa kwa vijana

VIONGOZI WANACHAMA SOMENI KATIBA TUJIBIZANE KWA HOJA

Na. Kadala Komba Dodoma MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM) Kenneth Nollo amewataka wanachama na Viongozi wa chama cha mapinduzi ccm Wilayani humo kusoma na kuielewa vyema katiba,kanuni na tarabitu za chama Ili kufanya majukumu yao vyema pasipo kuyumbishwa na mtu. Nollo ametoa kauli hiyo wakatai wa kikao cha Halmashauri kuu ya Ccm Wilaya ya Bahi kilichofanyika Wilayani humo. Nollo amefafanua kuwa ,hivi Sasa kumekuwa na baadhi ya watu wanajivika vyeo sio vyao na kuwakalipia wengine hivyo ni Vyema wakajibizana kwa hoja. "Napenda nisisitize kuwa Kila Mwanachama akisoma vyema katiba atatambua wajibu wako kama Kiongozi na Kazi za chama wapi unatakiwa,amesema "Mimi kama mbunge nimeendelea kutekeleza Kazi zangu za jimbo na sasa tunaona jimbo hili lina Sura tofauti,tunakamilisha shughuli mbalimbali za miundo mbinu Kazi iliyopo mbele ni kujiimarisha zaidi kwa kiasi kikubwa,"amesema Nollo. Licha ya hayo amesema kuwa Kazi za maendeleo zinafanyika tumeona Barabara, Zahanati, Shule madaraja na hivyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Donald Mejeti amesema Kazi waliyonayo wanachama ni kuhakikisha huduma zilizo kusudiwa zinasimamiwa na zinatekelezwa. Mejeti amebainisha kuwa katika Halmashauri hiyo kimejekwa kituo cha Afya Kazi yetu Viongozi wa chama ni kuhakikisha wataalamu wa Afya wanatoa huduma bora hivyo ni Vyema wakasimama imara kuwatetea Wananchi wetu. Naye Katibu wa Ccm (wanawake) Bahi Pauline Lupamba amewapongeza Viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. MWISHO
MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM) Kenneth Nollo Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Ccm Wilaya ya Bahi kilichofanyika Wilayani ukumbi wa Halmashauri Bahi
Mwenyekiti wa Halmashauri na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Donald Mejeti
Athman Masasi Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Bahi
Katibu wa Ccm (wanawake) Bahi Pauline Lupamba akisalimiana na wajumbe wa chama wakati wa Ufunguzi wa Kikao
mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe Godwin Gondwe Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa miradi
Stewart Masima Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bahi Akiwapongeza Viongozi wanachama kwa kusimamia vyema miradi ya wilaya

WAFUNGWA KUNUFAIKA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE


Na WAF, Bungeni Dodoma.


NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa kundi la wafungwa ni moja kati ya makundi maalumu ambayo Serikali imeliweka kwenye wanufaika wa mpango wa Bima ya Afya kwa wote, huku akiweka wazi kuwa, kwasasa Serikali imeweka utaratibu maalum wa kutoa huduma za matibabu kwa wafungwa katika magereza mbalimbali nchini kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya vya serikali bila malipo.

 Dkt. Mollel amesema hayo, leo Aprili 19, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Asia Halamga katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha kumi.

"Katika kuhakikisha kuwa wafungwa wanapata haki yao ya msingi ya kupata huduma za afya, Serikali imeweka utaratibu maalum wa kutoa huduma za matibabu kwa wafungwa katika magereza mbalimbali nchini kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya vya serikali bila malipo yoyote." Amesema

"Serikali inakamilisha Muswada wa bima ya Afya kwa wote ambapo utakapokamilika utakuwa suluhisho ya upatikanaji wa huduma za afya kwa makundi yote ya kijamii wakiwemo wafungwa." Amesisitiza Dkt. Mollel.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, katika vituo vya kutolea huduma za afya vyote kuna Wataalamu wa ustawi wa jamii ambao kazi yao kubwa ni kuhakikisha watu wenye uhitaji wakiweni wenye ulemavu wanapata huduma za matibabu kulingana na vigezo.

Kwa upande mwingine, Dkt. Mollel ameeleza katika kudhibiti matumizi holela ya dawa za binadamu, Serikali imekuwa ikitoa elimu kupitia vyombo vya habari, kusimamia mwongozo unaobainisha matibabu kwa kila ugonjwa ikiwemo dawa zinazohitajika kutibu magonjwa hayo na kusimamia ueledi wa watoa dawa katika maeneo yote yanayohusika na utoaji wa dawa kama vile maduka ya dawa na vituo vya kutolea huduma za afya.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Wizara kwa kushirikiana na OR TAMISEMI itaendelea kutafuta vibali vya ajira kwaajili ya kuajiri wafamasia ili kutatua changamoto ya uhaba wa wafamasia nchini utaosaidia kupunguza changamoto ya matumizi holela ya dawa.

Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amesema, Serikali itaendelea kusimamia vizuri na kuhakikisha utaratibu unafuatwa na wafanyabiashara ili kuzilinda afya za wananchi.

Mwisho.

 

HUAWEI CALLS FOR A ‘NON-STOP’ DIGITAL FUTURE FOR AFRICA’S BANKING INDUSTRY


Cape Town, ] Huawei today announced its ‘Non Stop Banking’ initiative. Unveiled at the Huawei Intelligent Finance Summit for Africa 2023, the initiative calls for hand-in-hand collaboration between the ICT and banking industries and facilitate a digital future of ‘non-stop’ services, ‘non-stop’ development, and ‘non-stop’ innovation.





In a keynote speech announcing the initiative, Leo Chen, president of Huawei Sub-Saharan Africa Region spoke about why going digital has become such a major imperative for the banking industry. Not only does it make it easier for banks to broaden their customer base, he said, it also saves operational costs, allows them to develop new products, and deepen the customer relationship, thus generating revenues for banks. 




In Africa, he added, there’s an even greater imperative for banks to embrace digitization, as it allows for greater financial inclusion. While Chen lauded the innovative work done by many African banks in embracing digitization, he pointed out that all players in the industry need to go further if they’re to embrace the ‘non-stop’ approach that will characterise the future of banking.




Huawei has already served more than 2500 financial customers in over 60 countries and regions, including 50 of the world's top 100 banks. Numerous Huawei technologies, Chen said, are helpful on this front. Over the years, it has provided the foundation and backbone for the digitalization of the banking industry in Africa by supporting the construction of the continent’s ICT infrastructure and digital connectivity in rural areas. Its extensive focus on research and development (R&D), meanwhile, means that it’s well-poised to help the industry shape its future too.




From a technical perspective, he pointed to Huawei's strength in storage, fibre optic networks, IP networks and data communication, which enable ‘multi-domain collaboration’ solutions for banks. For example, its ‘storage and optical connection coordination (SOCC)’ solutions can reduce system switchover time from two minutes to two seconds after a network breakdown, ensuring zero transaction interruptions. The multilayer ransomware protection (MRP) technology, meanwhile, can provide 6-layer protections, from storage, to network, to applications and other layers. It enables a reliable and secure ‘end-to-end’ protection to the whole system. Finally, Huawei’s intelligent network O&M solutions enable faults to be detected in one minute, diagnosed in three minutes, and rectified in five minutes.




Huawei Cloud, the world's fastest-growing major cloud service provider, can additionally support the hybrid multi-cloud service required by banks. Huawei’s digital energy solutions, meanwhile, can help to provide an uninterrupted and green power supply for the banking sector. This effectively addresses power deficit issues and supports ‘non-stop’ banking.




That kind of technological innovation will be important because, as Jason Cao, CEO of Huawei Global Digital Finance pointed out, financial services are becoming mobile and intelligent at a blistering pace.




“The financial industry should pay acute attention to users and their demands, embracing changes,” he said. “Huawei is dedicated to helping its African financial customers address challenges and accelerate changes across six fields: shifting from transaction to digital engagement, cloud-native and agile businesses, data democratization, secure and reliable infrastructure, hybrid multi-cloud and Lego-style modular services, and automated and predictable operation.”




“In this way, Huawei will facilitate financial digitalization and innovatively improve productivity in Africa. Revolving around stability, agility, and intelligence, Huawei aims to build ‘non-stop’ financial services, and achieve ‘non-stop’ development alongside ’non-stop’ innovation,” he added.




Beyond technology, Huawei issued a call for all parties in the industry to come together and build more robust ICT infrastructure, facilitate more measures and policies to encourage digital finance innovation, cultivate a sound innovative ecosystem, and train more digital talent for the industry.




Huawei is particularly active on the last two points. Huawei Cloud’s Spark programme, for example, has pledged to assist 1 000 SMEs over the next three years. And having already trained more than 80 000 digital talents in Africa, it has launched the ‘LEAP’ digital talent training programme in Sub-Saharan Africa region, aiming to train another 100 000 people in the next three years.




The Huawei Intelligent Finance Summit for Africa 2023 brought together more than 200 attendees, including key industry opinion leaders, as well as executives from major banks across Africa.

STEADY OPERATIONS,SUSTAINABLE SURVIVAL AND DEVELOPMENT


Eric Xu speaking at the press conference


[Shenzhen, China] Huawei released its 2022 Annual Report today. The company reports steady operations throughout 2022, having generated CNY642.3 billion in revenue and CNY35.6 billion in net profits. Huawei continues to strengthen investment in R&D, with an annual expenditure of CNY161.5 billion in 2022, representing 25.1% of the company's annual revenue and bringing its total R&D expenditure over the past 10 years to more than CNY977.3 billion.




"In 2022, a challenging external environment and non-market factors continued to take a toll on Huawei's operations", said Eric Xu, Huawei's Rotating Chairman, at the company's annual report press conference. "In the midst of this storm, we kept racing ahead, doing everything in our power to maintain business continuity and serve our customers. We also went to great lengths to grow the harvest – generating a steady stream of revenue to sustain our survival and lay the groundwork for future development."




Also present at the event was Sabrina Meng, Huawei's CFO. She noted, "Despite substantial pressure in 2022, our overall business results were in line with forecast. At the end of 2022, our liability ratio was 58.9% and our net cash balance was CNY176.3 billion. In addition, our balance of total assets reached one trillion yuan, largely composed of current assets such as cash, short-term investments, and operating assets. Our financial position remains solid, with strong resilience and flexibility. In 2022, our total R&D spend was CNY161.5 billion, representing 25.1% of our total revenue – among the highest in Huawei's history. In times of pressure, we press on – with confidence."




In 2022, revenue from Huawei's carrier, enterprise, and consumer businesses was CNY284 billion, CNY133.2 billion, and CNY214.5 billion, respectively.




Huawei is a strong proponent of growing together with its ecosystem partners, and believes that openness and collaboration lead to shared success. The company has continued to open up its platform capabilities across its HarmonyOS, Kunpeng, Ascend, and cloud portfolio, focusing on improving developer experience as well as enabling and supporting its ecosystem partners on all fronts. Huawei currently works with more than nine million developers and over 40,000 ecosystem partners to fuel ecosystem-based innovation and create greater value for its customers.




"2023 will be crucial to Huawei's sustainable survival and development," Xu noted. "Plum blossoms tend to grow sweeter from a harsh winter's freeze. Today, Huawei is like a plum blossom. While it's true that we have considerable pressure ahead of us, we have what it takes to come out the other end – with opportunities to grow, a resilient business portfolio, a unique competitive edge, the enduring trust of our customers and partners, and the courage to invest heavily in R&D. We are confident in our ability to rise above any challenge that comes our way, laying a solid foundation for sustainable survival and development."




All financial statements in the 2022 Annual Report were independently audited by KPMG, an international Big Four accounting firm. To download the 2022 Annual Report, please visit https://www.huawei.com/en/annual-report/2022




Note: The 2022 closing exchange rate is US$1.00 = CNY6.9533

WAKAZI WA MBARALI WAIPONGEZA SERIKALI KWA MATIBABU YA MACHO*

Wakazi wa Mbarali wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau wa huduma za macho kwa kuwapatia matibabu ya macho bila malipo.


Akizungumza katika kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho inayoendelea kwenye hospitali ya Wilaya Mbarali Bw. Antony Ndwenywa(83) kutoka kitongoji cha Mkanyageni-Rujewa ambaye alifanyiwa upasuaji wa mtoto wa  jicho macho yake mawili mwezi Disemba 2022, amesema tangu amefanyiwa upasuaji anaendelea vizuri na hivi sasa anasoma hata magazeti

"Mimi nilifanyiwa macho yote mawili yalikuwa na mtoto wa jicho na hadi sasa naendelea vizuri.Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia huduma sisi watu wa chini ,huduma hizi ni bila malipo ninashukuru sana.

Naye, Bi. Vailet Mbelewele mkazi wa Mabadaga ambaye alikua na mtoto wa jicho kwa muda wa mwaka mmoja amewashukuru watoa huduma wakiwemo madaktari na wauguzi kwa huduma nzuri walizompatia na kuongeza kuwa ametolewa bandeji na sasa anaona.

Amesema mara baada ya kupata tatizo hilo alikua akinunua dawa kwenye maduka bila ushauri wa madaktari "nawashauri wananchi wasijinunulie dawa mje moja kwa moja kwani madaktari wapo na huduma ni nzuri".

Vilevile Mzee Ahmed Abdallah Mkazi wa Igurusi ambaye alishakwisha fanyiwa upasuaji wa jicho moja miaka miwili iliyopita na kwa kambi hii amefanyiwa  upasuaji jicho la pili amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wake wa chini kwa jitihada zake kwa kuwasaidia watu wa chini.

"Tunamshukuru Mama kwa kutusaidia mambo mengi kama barabara,ametuletea mbolea,natoa sifa kwa Dkt. Samia anatuhudumia sisi watu wa hali hii kwani habagui na hachagui.

Kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho wilayani Mbarali imeanza tarehe 11 Aprili,2023 na inatarajiwa kumalizika tarehe 20 Aprili,2023.Inaratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Hellen Keler International la hapa nchini.


FOUNTAIN GATE WAPONGEZWAKWA KUIHESHIMISHA TANZANIA NA DODOMA

atibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu  ameshiriki katika mapokezi ya Mabingwa wa Shule za Sekondari Afrika (CAF) Fountain Gate walioiwakilisha Tanzania na Ukanda wa Afrika mashariki (CECAFA) katika mashindano ya mpira wa Miguu kwa wasichana ngazi ya Shule za Sekondari yaliyofanyika Durban, Afrika Kusini.

 
Mapokezi hayo yamefanyika katika viwanja vya  Chinangali Park jijini Dodoma ambapo shule mbalimbali zilikusanyika na viongozi wa Serikali kwa ajili ya mapokezi ya Mabingwa hao.
 
"Sisi wenzenu wa Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma tuna furaha sana na tunawashukuru wenzetu wa Fountain Gate kwa kutuheshimisha na kutupa furaha hii na pengine ni kama vile sisi tulijua dhamira yenu na kazi kubwa  ambayo mmewekeza katika kuwajenga vijana hawa wa wakiume na kike katika kushiriki mashindano siyo tu ya Mkoa bali ngazi ya Kitaifa na Mataifa
 
"Nakumbuka kabla ya kwenda kwenye mashindano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilipata fursa ya kuwakaribisha pale Mkoani tulikutana na tulifurahi tukapata chakula cha pamoja na sisi kama watumishi wa Mkoa huu tumeona baraka wa lile  ambalo Mkuu wa Mkoa alilifanya kwasababu baada ya kuwaaga vizuri kwa kuwapa tuzo na hamasa ambayo Mkoa ulifanya tunawashukuru sana kwa kubeba dhima ile na kuenda kuifanyia kazi leo hii mmekuja kutufurahisha kwa kweli tunawashukuru sana na kuwapongeza kwa dhati. " Amesema Gugu
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fountain Gates Bw. Japhet Makau amewashukuru wana Dodoma kwa mapokezi mazuri kwani ni nje ya matarajio yao na kuelezea namna walivyoibuka washindi.
 
"Tumetoka Durban, Afrika Kusini ambapo mabinti zetu timu ya Sekondari ya Wasichana ya Mpira wa miguu Fountain Gate wamekuwa mabingwa wa soka wa Afrika kwa shule za Sekondari, mashindano haya yalianza ngazi ya shule ambapo katika Tanzania shule za Mkoa wa Dar-es-Salaam na Tanga zilishirikishwa lakini sisi tuliomba kushiriki kwasababu muda ulikuwa ni mfupi na sisi tukaibuka kuwa washindi  
 
"Tulienda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya CECAFA ambapo tulijinyakulia Millioni Mia Mbili za Kitanzania kama washindi wa michuano hiyo sambamba na kombe baada ya hapo tukakakiwa kwenda Afrika Kusini ambapo kulikuwa na zaidi ya Mataifa 11 lakini katika timu za wasichana zilikuwa timu sita katika mashindano ambapo mechi ya kwanza tulipangwa kucheza na wenyeji Afrika Kusini na Fountain Gate ilishinda goli 7 kwa moja, mechi ya pili Gambia na Fountain Gate, nusu fainali goli nne kwa sifuri tukapata tiketi ya kucheza fainali na Morocco  ambapo alipata kichapo cha goli tatu kwa sifuri  kwa hiyo timu ya Fountain Gate kutoka Dodoma  wakawa Mabingwa kutoka Tanzania sambamba na  ubingwa tuliweza kupata mchezaji bora, mfungaji bora na goal keeper bora "Amesema Bw. Makau
Katika mashindano hayo timu ya Fountain Gate imejinyakulia kitita cha Dola za Marekani  300,000 pamoja na kombe.



SABABU ZA MAKATO YA BIMA YA AFYA KWA VITUO HIZI HAPA,



Na WAF, Bungeni, Jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amebainisha sababu zinazopelekea upotevu wa fedha katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka kwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini.

Dkt. Mollel amesema, Baadhi ya watoa huduma za afya wamekuwa wakiwasilisha madai yenye udanganyifu katika utoaji wa huduma kwa lengo la kujiongezea kipato kwa njia isiyo halali jambo ambalo limekuwa likisababisha kufa kwa mfuko huo.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 13, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Jesca Jonathan Msambatavangu katika Mkutano wa 11 kikao cha sita.

Ameendelea kusema, baadhi ya watoa huduma kutozingatia kwa miongozo ya tiba nchini (STG) inayotolewa na Wizara ya Afya, kama makubaliano baina ya pande zote yanavyoelekeza.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Sababu nyingine ni, kutozingatiwa kwa bei zilizoainishwa katika Mkataba wa Huduma baina ya Mfuko (NHIF) na Watoa Huduma.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Rais Samia amehakikisha mikoa yote nchini inahuduma za CT-SCAN, huku zikiwepo nyingine za ziada tayari kwa kuendelea kuwahudumia wananchi katika Mikoa yote nchini.

Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amemwelekeza Mkurugenzi wa Bima ya Afya kuhakikisha ndani ya saa 24 watu wote wenye vigezo vya kupata huduma waanze kupata huduma hizo za CT-SCAN.




Kwa upande mwingine  Dkt. Mollel amesema, Serikali itaendelea kuhakikisha huduma za chanjo zinaendelea kuboreka na tayari imetenga baadhi ya magari yatayotumika katika kuhakikisha huduma za chanjo zinapatikana katika maeneo yote nchini.

Mwisho

MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMEWAAMBIA WAKRISTO "MIMI SIYO YESU

Mwigizaji Robert Powell, mtu aliyeigiza uhusika wa"Yesu" katika filamu maarufu ya Yesu wa Nazareti amewasihi wanaoabudu Picha yake wakiamini kuwa yeye ndiye Yesu waache.


 anasema “ACHENI KUNIABUDU MIMI SIYO YESU”

 Tangu Robert alipoigiza uhusika wa Yesu katika filamu ya mwaka 1977, Jesus of Nazareth, picha za Robert Powell zimetundikwa makanisani, majumbani, kwenye magari, mashuleni, maofisini na kwenye majumba mengi matakatifu duniani kote wakiamini kuwa yeye ndiye Yesu wa Nazareth.

 Hata hivyo, Powell amepiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye si Yesu na watu waache kumwabudu.  Badala yake, wanapaswa kumstahi Yesu wa kweli na kumwabudu Mungu.

 Kwa maneno yake aliandika: “Siachi kusema na ninarudia kwa ulimwengu


tangu 1977. Mimi sio Yesu Kristo, mimi ni mwigizaji wa kawaida tu kutoka Uingereza.  Nimechoka kuona picha zangu zikiwa katika sehemu za ibada"

" Ninatengeneza filamu ili kujipatia riziki.  Choma picha yangu na kumwabudu Mungu pekee katika ukweli!  Mimi ni mwigizaji tu ... Yesu ni Bwana!