Home »
» PESA INAWEZA KUWA MBARAKA AU LAANA*
PESA INAWEZA KUWA MBARAKA AU LAANA*
Pesa si laana yenyewe kama yenyewe; bali ni kitu chenye thamani kubwa kwa sababu ikitumiwa ipasavyo, inaweza kufanya mema katika kuleta wokovu wa roho za watu, katika kuwabariki wengine ambao ni maskini kuliko sisi wenyewe. Kwa matumizi ya kiholela au yasiyo ya busara .... pesa zinaweza kuwa mtego kwa mtumiaji. Anayetumia pesa kuridhisha kiburi na matamanio yake anaifanya kuwa laana badala ya baraka.
Pesa ni jaribio la mara kwa mara katika kupima mielekeo ya moyo. Yeyote anayepata zaidi ya mahitaji yake halisi anapaswa kutafuta hekima na neema ya kuujua moyo wake na aweze kuulinda moyo wake kwa bidii, asije akawa na matamanio ya kufikirika na akawa wakili asiye mwaminifu, akitumia kwa upotevu mtaji wa Bwana wake aliokabidhiwa.
Ukurasa: 372, Aya:1
0 Comments:
Post a Comment