Home »
» “MBEYA INAENDA KUFANANA NA HADHI YA MAJIJI, TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA” DKT. TULIA*
“MBEYA INAENDA KUFANANA NA HADHI YA MAJIJI, TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA” DKT. TULIA*
Na. Mwandishi Wetu Mbeya
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi wa Mbeya Mjini kumshukuru na kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoliwezesha Jimbo hilo katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 14, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Zahanati ya Itezi iliyopo katika Kata ya Itezi Jijini humo iliyogharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 117.4 kwa ushirikiano wa Serikali kuu, Wananchi Pamoja na Taasisi ya Tulia Trust.
Amesema kuwa ni rekodi kubwa imeweza kufanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia ndani ya kipindi kifupi kwa kuwaboreshea maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo barabara, elimu, afya n.k
Katika sekta ya afya, Serikali imewezesha ujenzi wa kituo cha afya Iyela, Zahanati Ndanyela, Zahanati ya Iduda, Serikali imeipandisha hadhi kilichokuwa kituo cha afya Igawilo na kuwa hospitali ya Wilaya ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni mbili zimetolewa. Hospitali ya Meta zimewekwa zaidi ya bilioni 11 ili kuwasaidia wakinamama.
Kuhusu changamoto za maji, Dkt. Tulia amesema “Mhe. Rais ametuletea zaidi ya Shilingi Bilioni tano ili tuanze ujenzi wa mradi wa mto Kiwira ambao utagharimu zaidi ya Bilioni 250 kwahiyo msiwe na wasiwasi kazi imeanza na ndani ya muda mfupi wananchi wote mtakuwa mnapata maji ya uhakika”
“Kuhusu miundiombinu Mbeya Mjini tuliachwa nyuma sana lakini sasa kazi imeanza na ule mradi wa barabara ya njia nne unaanza hivi punde bilakusahau barabara za mitaa yetu itatandikwa rami ili Mbeya ifanane na hadhi ya Jiji ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge” amesisitiza Dkt. Tulia
0 Comments:
Post a Comment