Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

HUDUMA ZA UGANI KUPITIA MATUMIZI YA TEHAMA IMEIMARISHWA VYEMA.

 
Na Sifa Lubasi,Dodoma


MRATIBU wa Programu ya Uhimilivu wa  Mifumo ya Chakula  Nchini, Timoth Semuguluka amesema kuwa wameimarisha huduma za ugani kupitia matumizi ya Tehama ili wakulima waitumie  kupata huduma za ugani pale walipo
.Alisema hayo jana Jijini hapa kwenye maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni,
Mratibu huyo alisema kuwa wameimarisha mifumo ya kidigitali iliyopo na kutengeneza mifumo rafiki ili wakulima waitumie ili kupata huduma za ugani
Alisema kuwa program ya ugani inalenga kuimarisha upatikanaji huduma ya ugani kwa mazao ya chakula na biashara,kwani ni daraja kati ya teknolojia kwenda vituo vya utafiti Kisha kwaa wakulima.
Alibainisha kuwa mahitaji ya maofisa ugani ni 20,000 lakini waliopo ni 7,000 tu, mapungufu yaliyopo ni zaidi ya asilimia 50“ a'lisema
"Tunachokifanya ni kutumia mifumo ya kidigitali iliyopo na kutengeneza mifumo rafiki ili wakulima waitumie ili kupata huduma za ugani, maofisa ugani wamesajiliwa kupitia mifumo hiyo kupitia simu zao na wamekuwa wakiulizwa maswali na wakulima wamekuwa wakipata masuluhisho mbalimbali,” alisema
Alitaja maeneo mengine ya utekelezaji ni pamoja na kufanya utafiti wa teknoloijia mbalimbali za mbegu za kilimo zinazohimili mabadiliko ya tabia nchi, kuimarisha mifumo ya upatikanaji na udhibiti wa mbegu bora, kuimarisha usimamizi na utumiaji wa miundombinu ya umwagiliaji, kuandaa mfumo mpya wa usimamizi wa uendeshaji wa ghala zote za umma, kupima afya ya udongo katika vijiji vyote vya Tanzania bara  na kuandaa ramani ya afya ya udongo.
Pia alisema lengo la program hiyo ni kuongeza ufanisi, kuleta matokeo chanya ya uwekezaji wa raslimali za umma na masuala ya kisera
,“Utekelezaji wa program hii utaongeza tija na mchango wa uwekezaji wa serikali unaolenga kupunguza athari zinazotokana na uhaba wa maji kwenye mifumo ya mwagiliaji iliyopo na kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna,” alisema
Alisema kuwa program hiyo inatekeleza vipaumbele vya mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo, sehemu ya mazao ikiwemo ununuzi wa vifaa vya kupimia udongo, ujenzi wa nyumba za maofisa ugani, ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji, ujenzi wa maabara ya kudhibiti wa ubora wa mbegu, uchimbaji wa visima kwa ajili ya umwagiliaji, ujenzi wa maabara ya tissure culture,Pia uzalishaji wa mbegu, ukarabati wa vituo vya maonesho ya nane nane.
mwisho


 


WAKULIMA WA ALIZETI KANDA YA KATI KUNUFAIKA NA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MAINLAND

 
Na Sifa Lubasi,Dodoma


MKUU wa Wilaya ya Singida Mjini, Godwin Gondwe amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na kiwanda cha mafuta ya alizeti cha kampuni ya Mainland utaleta uhakika wa masoko ya alizeti ya wakulima wa mikoa ya Singida na Dodoma.
Akizungumza wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kwenye maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma,Gondwe alisema kuwa  ujio wa kiwanda hicho Ni suluhisho la mazao ya wakulima wa alizeti.
"Hili litakuwa suluhisho kubwa la soko la wakulima wa kanda ya kati, kwani watakuwa na soko la uhakika"alisema 
Kwa upande wake Ofisa mauzo wa kiwanda hicho, Castro William alisema kuwa kiwanda hicho kipo eneo la Veyula jijini Dodoma ambapo uwekezaji huo kufikia takribani dola milioni 30 unaochukua eneo la mita za mraba 162,000.
A'lisema kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho cha kuzalisha mafuta ya alizeti Dodoma kutasaidia ukuaji wa kampuni katika bara la Afrika na kuchangia uzalishaji na biashara ya bidhaa za mazao ya kilimo Afrika Mashariki.
Alisema uwekezaji huo mkubwa unalenga kuzalisha mafuta safi ya kupikia,salama na yenye afya.
"Kampuni  itazalisha aina mbili za mafuta iliwemo Merrin Farm ambapo mafuta hayo yamesafishwa na yenye ubora wa hali ya juu ,hutengenezwa kwa mbegu za alizeti safi kwa asilimia 100,"alisema 
Alisema kuwa aina nyingine ni Sunland ambayo ni mafuta ya alizeti yaliyosafishwa hutengenezwa kwa mbegu za alizeti safi, asili  kwa asilimia 100 yenye wingi wa mafuta yatokanayo na mimea na vitamin E yanasaidia lishe bora,kwa afya ya moyo.
Mwisho


 


SIDO IMETOA MIKOPO YENYE THAMANI YA MILIONI 200 KWA WAJASIRIAMALI.

 
  
Na Sifa Lubasi,Dodoma 


MENEJA wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Dodoma Twaha Swedi amesema wametoa mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa kipindi cha mwaka moja kwa wajasiriamali wadogo na wachakataji wa mazao ya kilimo.
Akizungumza jana wakati wa mahojiano kwenye  maonesho ya wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini hapa,a'lisema kuwa kati ya waliopata mikopo hiyo wamo wazalishaji wa mvinyo na mafuta ya alizeti.
"SIDO hutoa mikopo kwa wajasiamali wadogo na  wa kati (SME's) kwa ajili ya kukuza mitaji ya miradi mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwenye sekta za biashara,uzalishaji pamoja na uwekezaji kwenye miundombinu ya biashara,zana na vifaa vya uzalishaji,"alisema.
Alisema kuwa mwaka huu zaidi ya wakulima 100 wa zabibu na alizeti wamewezeshwa mikopo,  elimu na matumizi ya teknolojia rahisi za Kilimo na usindikaji.
"Wakulima wa zabibu, alizeti na mazao mengine ya kimkakati wamenufaika na fursa mbalimbali kwenye mikopo kupata masoko ya ndani na kimataifa,"alisema 
Alisema kuwa SIDO mkoa wa Dodoma imetoa mikopo yenye zaidi ya Sh milioni 200 katika maeneo tofauti kwa wachakataji na wafanyabiashara wadogo wadogo 
Pia alisema  katika kutekeleza dira ya Maendeleo ya mwaka 2025-2050 Shirika hilo limejipanga katika kusaidia wakulima wa zao la zabibu na mazao mengine ya kimkakati kwenye matumizi ya teknolojia rahisi, kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi.
" Shirika  limejipanga kutekeleza dira ya 2025-2050 kwa kusaidia wakulima wa zabibu, alizeti na mazao mengine ya kimkakati kwenye mnyororo wa thamani,"alisema
Aidha alisema wakulima na wasindikaji wamekuwa waliopata elimu ya kutambua jinsi matumizi ya teknolojia rahisi zinavyoweza kusaidia katika kuchakata mazao ya kilimo.
Pia alisema wamejipanga kuwa na ofisi kila wilaya katika mkoa wa Dodoma na wameanza na wilaya ya Kondoa .
Alisema kuwa mikakati nyingine ni kuinua vikundi cikinsu iya vijana na kimamama kwani nguvu kubwa ya uzalishaji iko kwenye maeneo hayo.
Mwisho


 


EMMANUEL SALLY KAFULYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KATA YA BAHI

 Baadhi ya viongozi nchini Tanzania wameanza kuchukua fomu za kugombea Udiwani katika kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

‎Miongoni mwa waliotangaza nia hiyo ni EMMANUEL SALLY KAFULYA* , ambaye leo Jumamosi, Juni 28, 2025, amechukua fomu ya kugombea Udiwani kata ya Bahi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

‎Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Kata ya Bahi , Kafulya  amesema:"Nikiwa kama mwanachama wa CCM, nimekuja kutekeleza haki yangu ya kikatiba ya kuchaguliwa. Nimechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Udiwani kuwakilisha Kata ya Bahi

Katibu wa Ccm Kata ya Bahi Rajabu Mboge akikabidhi fomu ya ugombea Udiwani Emmanuel Kafulya kwenye Ofisi za Chama 






 

MATHIAS LYAMUNDA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA BAHI KUPERERUSHA BENDERA YA CCM.

 
‎Na. Kadala Komba Bahi 


 

leo tarehe 28/06/2025 ofisi za Chama cha Mapinduzi Ccm kata ya Bahi wakati Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Bahi Ndugu Paulina Bupamba  akikabidhi fomu ya ugombea Ubunge ndugu Mathias Lyamunda


‎Haya yamejiri leo tarehe 28/06/2025 ofisi za Chama cha Mapinduzi Ccm kata ya Bahi wakati 

‎Mathias Lyamunda  Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali Foundation for Environmental Management and Campaign Against Poverty-FEMAPO, na Rais wa Rotary Club of Bahi, ambaye pia ni mbobevu wa maswala ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi, amesema  Leo nimechukua fomu kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kupitia Jimbo la Bahi, Dodoma. 

‎Aidha nikiongea na baadhi ya wananchi wa Bahi wanao mfahamu wamesema Mathias Lyamunda ni mwanasiasa maarufu na anayetajwa sana katika Jimbo la Bahi, na iwapo Chama kitampatia ridhaa atakiletea ushindi wa Kishindo. 

‎Sambamba na hilo Mathias Lyamunda amesema kitaalama yeye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam katika fani ya Sayansi ya Siasa, Utawala wa Umma na Mazingira. 
‎"Hivyo  naamini ninayo nafasi kubwa ya kutumia uzoefu wangu  wa shughuli za kimaendeleo Kitaifa na Kimataifa katika kutatua changamoto za kimaendeleo zinazo likabili Jimbo la Bahi kwasasa.





 

*MKUTANO WA KIMATAIFA WA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA MWILI (ORGAN TRANSPLANTS) KUFANYIKA MWAKANI NCHINI TANZANIA CHINI YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA DODOMA*

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa Kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma wanatarajia kufanya Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya huduma za Afya za upandikizaji wa viungo  vya mwili (Organ Tranplants).

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Prof. Abel Makubi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ugonjwa wa Selimundu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali hiyo ambayo kwa sasa ndio  pekee nchini Tanzania inayotoa huduma ya kutibu ugonjwa wa Selimundu kwa njia ya kupandikiza Uloto kwa watoto wenye ugonjwa huo.

Mkutano huo tunatarajia utafanyika mwakani, utahusisha Wataalamu wa Kitaifa na Kimataifa ili kusaidia kukuza na kubadilishana Uzoefu, ujuzi na utaalamu na kutoa fursa ya kutangaza uwekezaji na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali  katika sekta ya Afya" alifafanua Prof. Makubi.


RASMI UZINDUZI WA BIBLIA YA CHIKAGULU WAFANYIKA MOROGORO

 Na. Mwandishi wetu Morogoro.

Chama Cha Biblia Cha Tanzania kwa kushirikiana na makanisa mkoani Morogoro  kimefanya sherehe za uzinduzi wa Biblia ya Chikagulu, zilizofanyika katika Kanisa la Anglicana Mt Adrea Gairo, Jumapili tarehe 8
Sherehe hii iliudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, taasisi za kidini, viongozi wa dini (maaskofu , wachungaji) waumini na wanajamii (wakaguru) kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.

Katika tukio hili Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mh. Prof. Paramagamba Kabudi) aliongoza uzinduzi huo kwa kukipongeza Chama Cha Biblia kwa kuweza kuiheshimisha lugha ya Chikagulu kwa uiweka kwenye maandishi pia alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi lugha za asili za Kitanzania ambazo baadhi yake zimeanza kupotea.

Pia baadhi ya wageni waalikwa waliweza kutoa ujumbe na kuelezea furaha yao ya kupata Biblia kwa lugha ya Chikagulu.  Kupitia Biblia hii, tutakuwa na Kanisa, jamii, familia na nchi yenye amani, upendo kwa sababu watu watakuwa wakimsikiliza Mungu kupitia Biblia yao; Mungu anazungumza na watu wake kwa lugha yao.

Huu ni mwanzo mpya kwa Wakagulu kuanza kumsikia Mungu kwa lugha yao ya mama!





WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WAITWA JKT

 Na. Mwandishi wetu 


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anatoa wito Kwa vijana waliohitimu elimu ya Sekondari Kidato Cha Sita kwa mwaka 2025,kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025.

Hayo yameelezwa na Kanali Juma Mrai Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT wakati akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 27 Mei 2025 Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma.

Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa Mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 28 Mei 2025 hadi tarehe 08 Juni 2025.

Aidha Vijana hao wamepangwa katika Kambi za JKT zifuatazo; JKT Rwamkoma - Mara,JKT Msenge- Tabora,JKT Ruvu na JKT Kibiti - Pwani,JKT Mpwapwa, JKT Makutupora - Dodoma,JKT Mafinga - Iringa,JKT Male - Ruvuma,JKT Mgambo na JKT Maramba - Tanga,JKT Makuyuni na JKT Orjolo - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila - Kigoma,JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa   - Rukwa pamoja na JKT Nachingwea - Lindi.

"Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana Kwa macho(Physical Disabilities) waripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo"


Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na Bukta ya Dark Bluu yenye mpira kiunoni(lastic)iliyo na mfuko mmoja nyuma,urefu unaoishia magotini,isiyo na zipu, T-shirt rangi ya kijani,Raba za Michezo zenye rangi ya kijani na Bluu,shuka mbili za kulalia zenye rangi ya Bluu bahari,soksi ndefu za rangi nyeusi,Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi,Track suit ya rangi ya kijani au Bluu,Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya juu,zikiwemo Cheti Cha kuzaliwa,vyeti vya kuhitimu kidato Cha Nne,nauli ya kwenda kuripoti makambini na kurudi nyumbani.

"Orodha kamili ya majina ya vijana hao,Makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo,inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz"

Aidha ili kufahamu Kambi kijana aliyopangiwa,atatakiwa kuingiza jina la Shule au namba ya Shule aliyohitimu elimu ya kidato Cha Sita,mbele ya jina lake la Shule ataona neno lililoandika waliochaguliwa,akichagua neno hilo ataona jina au majina ya waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa sheria kwa mwaka 2025,ikionesha kambi aliyopangiwa,Mkoa na wilaya ilipo kambi hiyo.

"Ili kuona majina yote ya vijana na Kambi waliopangiwa,mtumiaji atapakua JKT PDF 2025 iliyopo juu kulia katika ukurasa huo"

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha Vijana wote waliohitimu kidato Cha Sita mwaka 2025 kuungana na Vijana wenzao ili kujengewa uzalendo,Umoja wa Kitaifa,kufundishwa stadi za kazi,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao.





WANAOSIMAMIA MITANDAO YA SERIKALI WATAKIWA KUHAKIKISHA USALAMA WAKE

 




Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amewataka watumishi wanaosimamia akaunti za mitandao ya kijamii ya Serikali kuongeza umakini na kushirikisha  wataalam wa TEHAMA ili kupata elimu ya namna ya kuweka njia za kiusalama katika mitandao hiyo.

Msigwa amesema hayo leo, Mei 21, 2025 wakati akifungua mafunzo ya usalama wa mtandao (cyber security) yalioandaliwa na kitengo cha TEHAMA cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa watumishi wa Wizara hiyo.

Msigwa ameeleza kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya athari za matumizi mabaya ya mtandao zinatokana na uelewa mdogo wa juu ya utumiaji wa mitandao ambapo wengi hawajaweka tahadhari za kiusalama ikiwemo kutobadili taarifa za siri mara kwa mara.

Vilevile Msigwa amesema kuwa, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha usalama wa kimtandao Tanzania ikiwemo uwepo wa sheria ambazo zimetungwa ili kudhibiti matumizi holela ya kimtandao.

Ametaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 na sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao ya mwaka 2019 na kuandaa Sera na miongozo mbalimbali ya kusaidia kuhakikisha usalama wa taarifa za Serikali.

Katika hatua nyingine, Msigwa amezitaka taasisi na mashirika ya Serikali kufanya mafunzo hayo ya usalama wa kimtandao mara kwa mara kwa watumishi ili kulinda mifumo na taarifa za Serikali.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA cha Wizara hiyo, Ndg. Kulwa Magingila amewataka watumishi hao kuweka nguvu za pamoja kuhakikisha mitandao ya Serikali inalindwa na kuhakikisha wanatoa taarifa za wanaofanya uhalifu huo kwani ni ajenda ya dunia na uhalifu hauna mipaka.

DC JOACHIM NYINGO ATAKA TUZO ZA ELIMU ZIPELEKWE KWA VIONGOZI WALIO MTANGULIA

 



Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo Akizungumza na Walimu,wazazi,viongozi wa dini katika hafla ya kuwapongeza Walimu wa Shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa. 

 

Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlaw akisoma  risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo

 
Katibu Tawala wa Bahi Bi.Mwanamvua Bakari akimkaribishaMkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo akitoa pongeza walimu wa Halmashauri ya Bahi


Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Bahi Stuwart Masima akisisitiza swala la elimu na umuhimu wa elimu kwa wazazi 


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) amewataka wakina mama,vikundi mbalimbali vya sanaa kuhamasisha maswala ya elimu kupitia karama zao 


Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe.Keneth Nollo ameelezea mikakati ya elimu katika wilaya ya Bahi tusilizike kufika namba mbili kitaifa bali tuongeze juhudi mwakani 2026 tuwe namba moja 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mh George O. Fuime akijitapa kuwapita halmashauri ya bahi kielimu.


Mwenyekiti wa Alet Mkoa White Zubari ameipongeza halmashauri yawilaya ya Bahi kwa kuweka utaratibu wa kupongezana kwa kutoa zawaidi hata sisi tumekuja kujifunza kwenu hii tutachukua na kuifanyia kazi.
Zawadi Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio
Zawadi Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio

Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlawa akipokea tuzo kwa kusimamia vyema maendeleo ya elimu katika Halmashauri ya Bahi
 


Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bahi Misheni Paschal Mchewa akipokea tuzo 
Afisa Elimu ya Awali na Msingi wa Wilaya ya Bahi, Bonaface William aliyeshika tuzo akifurahi na waalimu


 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.
Mhe. Diwani kata ya Ilindi Sangula akipokea bahasha ya fedha pamoja na walimu

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.


 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.


Walimu shule za msingi Halmashauri ya Bahi

Wanafunzi wa shule ya msingi Bahi Misheni 


 

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.Diwani kata ya Bahi Mhe.Ndonu na Diwani viti maalumu  Kurusumu sambamba na mwalimu



 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio mwalimu Asifiwe  Kiula .

 
 
 
 

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.
Mhe. Diwani kata ya Sosthenes Mpandu na mwalimu

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bahi Misheni Paschal Mchewa akiwa na wanafunzi


Wanafunzi wa Engli Medimu
Meza kuu

Kikundi cha ngoma Chonde wakiimba wimbo maalumu wa elimu

Na. Kadala Komba Bahi 

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo alisema mimi ni mgeni kwenye hii wilaya mambo makubwa yamefanyika, yametekelezeka na viongozi wenzangu waliyo nitangulia hata hizo sifa sistahili kupata  wala hizo pongezi kwa sababu ya ugeni wangu mimi ni mgeni najifunza tu, naomba katika kujifunza kwangu mnifundishe taratibu ili niweze kuelewa vizuri na kushika vinavyopasika kushika vizuri. Zaidi ili niweze kuwa mwanafunzi mzuri katika kutekeleza majukumu yangu , hivyo naelekeza sifa zote zilizotolewa na nyimbo zilizoimbwa na kila kilichoelezwa naomba kwanza kupelekwe kwa watangulizi wangu ambao natamani wangekuwepo siku hii ya leo tuwapongeze kwa kazi kubwa waliyofanya , pia natumia nafasi hii kumpongeza Rais Dkt.   Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na ndoto zake za kuamua kuiweka Bahi kwenye ramani ya Tanzania kwa kuleta fedha na kuhakikisha kuna miundo mbinu mizuri iliyosababisha elimu iweze kupatikana.

Hayo yamejiri  Viwanja vya shule ya msingi Bahi Misheni Tarehe 10 May,2025 katika hafla ya kuwapongeza Walimu wa Shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa. Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya ya Bahi  hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ni  wadau wa elimu ambao kila mtu kwa nafasi yake  amehakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio, Katika hafla hiyo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Joachim Thobias  Nyingo.

Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlawa amesoma risala kwa mgeni rasmi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ina shule themanini na sita za msingi (86) na shule ishirini nasaba (27) za Sekondari na shule moja binafsi ya  sekondari, idadi ya wanafunzi kwa sekondari ni helfu kumi na moja mia tisa stini na tisa kwa upande wa elimu ya msingi tunawanafunzi halfu hamsini na nane mia saba thelathini na saba Mheshimiwa mgeni rasmi Halmashauri ya Bahi imepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ikiwa katika awamu hii ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.   Samia Suluhu Hassan baadhi ya mafanikio hayo ni kutoka mwaka 2021 hadi 2025 tulikuwa tunaidadi ya shule za msingi 72 hadi sasa tunashule za msingi 86 ambapo tumepata ongezeko la shule 14 mpya kwa elimu sekondari tulikuwa na jumla ya shule 21 na vipi sasa tuna jumla ya shule 27 haya ni mafanikio makubwa chini ya Jemedari wetu   Rais Dkt. . Samia tumeweza kufanikiwa .

Aidha, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo amewapongeza walimu wa Halmashauri ya Bahi mumeiheshimisha Bahi lakini mumeuheshimisha mkoa wa Dodoma kazi mliyoifanya imeonekana,sisi waalimu tunakazi mbili tu ambazo tunapimwa na jamii kazi ya kwanza ni malezi ya mtoto tunayekabidhiwa wazazi na wadau wengine wanauliza mtoto mwenye tabia hizi ametoka shule gani ? Kwaiyo idadi ya wanafunzi wenye nidhamu,heshima na adabu na mambo yote mema yanaangalia mtoto amesoma shule gani walimu ambao walimfundisha uyo mtoto ni wa shule gani ,kwa hiyo ya kwanza ni malezi kazi ambayo walimu mumeifanya hongereni sana alisema .

Naye mwalimu wa shule ya msingi Bahi Misheni Paschal Mchewa amesema mafanikio kwanza yanatoka kwa wazazi wanafanikisha watoto wanapata chakula cha mchana lakini pia wanapata uji pamoja na ushirikiano wote ndani ya Halmashauri mbali na hayo walimu wa shule ya msingi Bahi Misheni ni walimu ambao wanawajibika bila kufuatiliwa lakini kitu kingine kinacho tusaidia motisha kwa walimu tumejitahidi kutoa motisha kila mwishoni mwa mwaka tunawaona wadau wa elimu mbalimbali tunaomba fedha ,tunaomba vitu basi walimu wanapata motisha kwa kupewa vitu na fedha pia wanaenda tua mbalimbali mfano mwaka juzi tumeenda Serengeti kwa mwaka jana tumeenda Dodoma mjini mwaka huu Mei mosi nimewapeleka Dodoma mjini kupata chakula cha mchana kwaiyo motisha inasaidia sana .

Viongozi wa dini