Na. Kadala Komba Bahi
![]() |
Haya yamejiri leo tarehe 28/06/2025 ofisi za Chama cha Mapinduzi Ccm kata ya Bahi wakati
Mathias Lyamunda Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali Foundation for Environmental Management and Campaign Against Poverty-FEMAPO, na Rais wa Rotary Club of Bahi, ambaye pia ni mbobevu wa maswala ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi, amesema Leo nimechukua fomu kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kupitia Jimbo la Bahi, Dodoma.
Aidha nikiongea na baadhi ya wananchi wa Bahi wanao mfahamu wamesema Mathias Lyamunda ni mwanasiasa maarufu na anayetajwa sana katika Jimbo la Bahi, na iwapo Chama kitampatia ridhaa atakiletea ushindi wa Kishindo.
Sambamba na hilo Mathias Lyamunda amesema kitaalama yeye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam katika fani ya Sayansi ya Siasa, Utawala wa Umma na Mazingira.
"Hivyo naamini ninayo nafasi kubwa ya kutumia uzoefu wangu wa shughuli za kimaendeleo Kitaifa na Kimataifa katika kutatua changamoto za kimaendeleo zinazo likabili Jimbo la Bahi kwasasa.
![]() |
0 Comments:
Post a Comment