Na. Mwandishi wetu Morogoro.
Chama Cha Biblia Cha Tanzania kwa kushirikiana na makanisa mkoani Morogoro kimefanya sherehe za uzinduzi wa Biblia ya Chikagulu, zilizofanyika katika Kanisa la Anglicana Mt Adrea Gairo, Jumapili tarehe 8
Sherehe hii iliudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, taasisi za kidini, viongozi wa dini (maaskofu , wachungaji) waumini na wanajamii (wakaguru) kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.
Katika tukio hili Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mh. Prof. Paramagamba Kabudi) aliongoza uzinduzi huo kwa kukipongeza Chama Cha Biblia kwa kuweza kuiheshimisha lugha ya Chikagulu kwa uiweka kwenye maandishi pia alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi lugha za asili za Kitanzania ambazo baadhi yake zimeanza kupotea.
Pia baadhi ya wageni waalikwa waliweza kutoa ujumbe na kuelezea furaha yao ya kupata Biblia kwa lugha ya Chikagulu. Kupitia Biblia hii, tutakuwa na Kanisa, jamii, familia na nchi yenye amani, upendo kwa sababu watu watakuwa wakimsikiliza Mungu kupitia Biblia yao; Mungu anazungumza na watu wake kwa lugha yao.
Huu ni mwanzo mpya kwa Wakagulu kuanza kumsikia Mungu kwa lugha yao ya mama!
Home »
» RASMI UZINDUZI WA BIBLIA YA CHIKAGULU WAFANYIKA MOROGORO
0 Comments:
Post a Comment