Home »
» ZAO LA MTAMA LA MACIA LILIMWE KWA WINGI ILI KUONDOKANA NA BAA LA NJAA
Na.Kadala Komba Dodoma
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma (JUWACHA) na
Shirika la Uzalishaji Mbegu DASPA Janeth Nyamayahasi amesema kuwa
tukililima vizuri zao la mtama la macia kwa wananchi wa Dodoma tutaweza
kuondokana na baa la njaa kwa sababu zao hilo linastahili ukame.
Nyamayahasi
amesema hayo wakati alipotembelewa na Mwenyekiti baraza la madiwani
Halmasahuri ya wilaya ya Chamwino Mhe.Edison Mdonondo kwenye maonesho ya
nane nane yanayoendelea katika viwanja vya nane nane Nzuguni jijini
Dodoma.
Amesema kuwa tukililima vizuri zao hili wilayani
chamwino na mkoa wa Dodoma tutakuwa tumeondokana na baa la njaa na hii
italeta matumaini kwenye jamii lakini na Taifa kwa ujumla
Aidha
amesema tukiliongezea thamani zao hili la macia lina lishe kubwa kwa
hiyo tukililima zao hili na kulichakata vizuri tukapata unga itakuwa
imesaidia kuondoa utapiamlo na kuwatia nguvu kina mama wajawazito.
Pia
Nyamayahasi amezungumzia mbegu ya karanga ya nariendele ambayo
ilifanyiwa utafiti katika kituo cha utafiti Mtwara amesema kuwa ni
karanga nzuri ambayo inavumilia ukame na inazalisha mazao ya mbegu
kuanzia moja hadi mia Hamsini na ukitaka izalishe kwa wingi ni kutumia
zile kanuni za kilimo ambazo shimo hadi shimo unapanda mbegu moja kwa cm
10 lakini mstari kwa mstari unapanda cm 50.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa baraza la madiwani Halmshauri ya wilaya ya Chamwino
Mhe.Edison Mdonondo amemhakikishia mwenyekiti wa jukwaa hilo na shirika
la DASPA Janeth Nyamayahasi kuwa ataenda kuzipanda na kuzimwagili ilia
one kama zitamletea matunda kama alivyomwambia.
Aidha
amesema kama Halmashauri wataona ni jinsi gani watawawezesha mikopo ya
10% ili kuweza kuwasidia katika kazi zao na kufikia malengo wanayotaka
kuyafikia.
Mwenyekiti wa baraza la madiwani Halmshauri ya wilaya ya Chamwino
Mhe.Edison Mdonondo akiwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo na shirika
la DASPA Janeth Nyamayahasi kwenye maonyesho ya nane nane Banda la DASPA Dodoma.
Mwenyekiti wa baraza la madiwani Halmshauri ya wilaya ya Chamwino
Mhe.Edison Mdonondo akiwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo na shirika
la DASPA Janeth Nyamayahasi kwenye maonyesho ya nane nane Banda la DASPA Dodoma.
Baadhi ya wananchi wakipatiwa elimu namna ya kuzalisha mbegu Bora kwa kipato Zaidi.
0 Comments:
Post a Comment