Na. Kadala Komba Dodoma
Naibu Waziri Katambi pamoja na Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule wakikabidhi mashine kwa wakulima.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,
vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhe Patrobas Katambi Amelipongeza shirika la
Dodoma Agriculture Seeds Production Association (DASPA) kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika jitihada
zake za kuleta maendeleo sekta ya kilimo.
Naibu Waziri Katambi ameyasema hayo wakati wa kilele cha maonesho na sherehe za wakulima nanenane yaliyofanyika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma wakati alipotembelea banda la wakulima Halmashauri ya Singida.
“ DASPA imemuelewa Rais ambaye anataka wakulima kulima kilimo cha biashara ili kujikwamua kiuchumi,DASPA mumeliona hili kwa kutoa somo la kilimo na kuwasaidia wakulima kwa kuwapatia zana za Kisasa za kupandia mbegu ambazo zitamsaidia mkulima kuondokana na zana duni( Jembe la mkono ) nawapongeza kwa kuwapatia wakulima zana bora za kilimo zitakazoraisisha shuguli za kilimo pia kulima kilimo bora chenye tija ”
Alisema amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha na kuweka fedha nyingi na kuweka pembejeo katika swala la kilimo kwa lengo likiwa ni kuwawezesha wakulima kiuchumi hivyo basi wakulima changamkieni fursa hizi .
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Shirika la Dodoma Agriculture Seeds Production Association (DASPA) Janeth Nyayahasi alisema shirika la DASPA ni shirika linalojihusisha na uzalishaji mbegu za karanga na mtama lisilo la kiserikali lakini, pia amesema teknolojia inakua na imepelekea kuondokana na kilimo cha mazoea na kutumia kilimo cha teknolojia na wao kama shirika la DASPA wameona watoe mashine za kupandia zenye thamani ya shilingi la 700,000 (laki saba) kwa vikundi viwili kutoka Singida kwa namna walivyojieleza wanavyopambana kutengeneza Mnyororo wa thamani, lakini bila kuwa na vifaa ama teknolojia za kupandia Kwenda kwa mfumo sahihi na kutumia mbegu sahihi itakuwa kazi bure hivyo tumeona vyema kuwapa mashine mbili kwaajili ya kupandia Tunaomba kwa heshima yako Kuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule na Naibu Waziri Mhe. Katambi kuwakabidhi vifaa hivi kwa wanavikundi.
Aidha Vailet Sikunyingi ambaye ni Mkulima kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kijiji cha laikala ameishukuru Serikali Pamoja na DASPA Kwa kuona umuhimu wa vikundi na kuvisaidi kwa kutupatia zana za kilimo tunashukuru sana.
MATUKIO YA PICHA VIONGOZI WAKIKABIDHI MASHINE KWA WAKULIMA
PICHA ZOTE NA KADALA KOMBA
0 Comments:
Post a Comment