Na. Kadala Komba Dodoma
Katibu wa Ccm Mkoa wa Dodoma Mh Pili Mbaga ameomba viongozi wa dini na waumini kuendelea kuwapuuza wapotoshaji wanaopinga uwekezaji wa Bandari kwani vita ya kiuchumi na wengine ni wanasiasa wanaotaka kuchafua sura ya nchi yetu.
Hayo yamejili wakati Katibu Mbaga Akizungumza na Viongozi wa Dini na Wananchi Mkoani Dodoma kwenye Ibada ya kuwaweka wakfu Maaskofu REV. Con Saimon Maloda na REV. Leonald Matia iliyofanyika katika kanisa la Kiinjili Utatu Tanzania (CATHEDRAL) IHUMWA.
Alisema kumekuwepo na majadala unahusu swala ya bandari ya Dar Es Salaam mimi kama kiongozi wa chama cha mapinduzi ambaye nasimamia serikali ni kweli kwamba mpango huo wa uwekezaji unatokana na jitihada za serikali ya awamu ya sita ya kuendelea kupanua vyanzo vingi vya mapato na kuboresha .
“Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi kama ambavyo serikali na viongozi wa chama na wataalamu walivyoendelea kufafanua uwekezaji huo utakua na tija kubwa na utaongeza ufanishi wa Bandari ikiwa ni Pamoja na kuvutia Nchi nyingine kupitia Bandari yetu kupanua mnyololo wa ajira lakini pia kuongeza mapato ya kodi kutoka Tillion 7 inayokusanywa sasa hadi Tillion 27 kwa mwaka. Pia alisema hatua hii inaweza kuwa chachu ya kupanda pato la Taifa kutoka Bilion 79 mwaka 2023 hadi Dolla Bilion 126 ifikapo 2025”
Katibu Mbaga aliendelea kuwasisitiza viongozi wa dini na waumini kuwahakikishia kuwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan anania njema na Taifa letu ya kuwa kumekuwepo na minong’ono mingi ya kwamba mkataba huu utakua hauna ukomo na wengine wakasema kwamba ardhi hii wamepewa milele na wengine wakasema kwamba wafanyakazi wa bandari watapoteza hajira zao anapoingia mwekezaji hayo maneno sio ya kweli muyapuuze hayo yote yanapotoshwa na watu wasioitakia mema nchi yetu na sio sahihi kabisa na kusema ukomo wa uwekezaji huo utaainishwa kwenye mkataba wa biashara ikiwa kati TBA na mwekezaji na kwasasa serikali ipo kwenye mazungumzo na mwekezaji lakini upande wa wafanyakazi ibala ya 13 ya makubaliano iyo iliyokuwa imeandaliwa imeweka wazi kuwa mikataba itakayokuwa imesainiwa ya utekelezaji wa milady ni lazima iainishe mpango wa ushilikishwaji wa wazawa wa utekelezaji wa mladi husika kuakikisha kampuni itakayofanya uwekezaji itatekeleza huduma za kijamii na kulinda kazi, ajira ya Tanzania Alisema.
Kwaupande Askofu Julias Manyika wa Kanisa la Kiinjili la Utatu Tanzania Amewataka Maaskofu waliyowekwa Wakfu Kwenda kuchunga Kondoo watakao pewa na Mungu kwa Uaminifu hili wasipotee hata mmoja hiyo ndiyo kazi waliyoitiwa kwani kazi ya Askofu ni mwangalizi Biblia imeandika hii ni kazi njema kama ni kazi njema ni hipi? Sisi ni walinzi wa watu wa Mungu wawe Salama Haleluyah Alisema.
Aidha Askofu Saimon Maloda wa Kanisa la Kiinjili la Utatu Tanzania ambaye aliwekwa Wakfu siku hiyo Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa Dini katika ujenzi wa nchi pia amewashukuru viongozi mbalimbali na wananchi waliyojitokeza kwenye Ibada iyo.
Katibu Mbaga Akizungumza na Viongozi wa Dini na Wananchi Mkoani Dodoma kwenye Ibada ya kuwaweka wakfu Maaskofu.
Askofu Julias Manyika wa Kanisa la Kiinjili la Utatu Tanzania |
Baada ya kuwekwa wakfu Maaskofu REV. Con Saimon Maloda na REV. Leonald Matia iliyofanyika katika kanisa la Kiinjili Utatu Tanzania |
0 Comments:
Post a Comment