Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Waziri wa nchi,ofisi ya waziri mkuu,sera,bunge na uratibu Mhe.Jenista J.Mhagama ametioa wito kwa umma kutumia vizuri mvua za EL_NINO vizuri ili ziwe na manufaa kupitia shughuli za uzalishaji mali kama kilimo.
Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini Dodoma kueleza hatua za kuchukua kwa umma,kamati za usimamizi wa maafa na sekta kufuatia taarifa ya uwepo wa EL_NINO wakati wa mvua za msimu wa vuli,oktoba_disemba 2023.
Aidha amesema kuwa pamoja na madhara yanayoweza kujitokeza ni vizuri kuandaa mabwawa na malambo kwa ajili ya kuvuna maji,kupanda mazao yanayohitaji maji mengi kama vile mpunga,uzashaji wa samaki na kuandaa na kuhifadhi malisho ya mifugo.
"Madhara yanayoweza kutokea katika sekta kutokana na uwepo wa El_Nino utakaosababisha mvua kubwa ni mafuriko kuharibu miundombinu,madhara ya kiafya,kiuchumi,kijamii na upotevu wa mali,maporomoko ya ardhi kuathiri makazi,mazingira,mashamba,usafiri,na shughuli zingine hususani uchimbaji madini,magonjwa ya milipuko kwa binadamu na wanyama na wadudu waharibifu wa mazao na mimea" Amesisitiza Mhe.Mhagama.
Aidha ameongeza kuwa tarehe 24 agosti 2023,mamlaka ya hali ya hewa Tanzania(TMA) ilitoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu wa vuli kwa kipindi cha mwezi oktoba hadi disemba 2023,utabiri umeonesha uwepo wa El_Nino itakayosababisha vipindi vya mvua kubwa kwa mwezi oktoba mpka disemba 2023 na kuendelea mpka mwezi januari 2024.
Aidha msimu wa vuli ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili yavua kwa mwaka unahusisha maeneo ya mikoa ya Kagera,Geita,Mwanza,Shinyanga,Kusini mwa mkoa wa Simiyu,Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma,Dar es Salaam,Tanga,Pwani(ikiwemo visiwa vya Mafia) na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.
"Kwa kuzingatia sheria za usimamizi wa maafa namba 6 ya mwaka 2022 na kanuni zake,kamati za usimamizi wa maafa za mikoa,wilaya kata na vijiji au mitaa zinaelekezwa kuchukua hatua kwa lengo la kuzuia na kupunguza madhara ya majanga na kujiandaa kukabili na kurejesha hali endapo maafa yatatokea serikali inaelekeza kamati za usimamizi wa maafa na sekta kushirikiana na umma kutambua maeneo hatarishi na yenye viashiria vya kuathirika na maafa na kuandaa mipango ya kuzuia madadha na kukabiliana na maafa endapo yatatokea,kuanisha na kuandaa rasilimali za usimamizi wa maafa kwa kila sekta kushiriki kikamilifu katika eneo lake,kuandaa mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kwa binadamu,wanyama na mimea"
"Kuhifadhi mazingira na kulinda miundombinu ya barabara,maji,umeme,na mawasiliano ili kupatikana huduma wakati wote,kuelimisha wananchi juu ya hatua za kuchukua tahadhari ili kuokoa maisha na mali,kutoa taarifa kwa haraka kwa mamlaka husika kuhusu dalili za kutokea maafa na yanapotokea maafa pamoja na kuhama kwenye maeneo hatarishi na kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo salama"
Aidha madhara ya mvua kubwa yanaweza kujitokeza katika mikoa ambayo haihusiki na mvua hizi za vuli,hali hii inatokana na mazingira ya kijiografia ya nchi yetu kuwa na mabonde,mabwawa na mito mikubwa ambayo inapokea maji mengi kutoka kwenye mikoa iliyopo katika uwanda wa milimani,hivyo wananchi wote wanaoishi na kuendesha shughuli za kiuchumi maeneo ya uwanda wa chini na pembezoni mwa mabonde ya maji wanatahadharishwa kuchukua hatua ili kunusuru maisha na mali zao.
Ofisi za waziri Mkuu itaendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa maafa nchini kwa kuzingatia Sera ya taifa ya menejimenti ya maafa 2004,sheria ya usimamizi wa maafa na 6 ya mwaka 2022,pamoja na maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi 2020_2025 na mikakati,mipango na miongozo.
Waziri wa nchi,ofisi ya waziri mkuu,sera,bunge na uratibu Mhe.Jenista J.Mhagama akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini Dodoma
MATUKIO YA PICHA KATIKA MKUTANO WA WAZIRI MHAGAMA NA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DODOMA |