Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

MATUKIO YA PICHA ZA MAFUNZO YA USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI DODOMA.

 
Na. Kadala Komba Dodoma

Shirika binafsi lilosajiliwa na Serikali la R.B.A Initiative. Limetoa mafunzo ya Usugu wa vimelea vya Magonjwa kwa waandishi wa Habari Mkoani Dodoma, Lengo ni kutambua mchango wa Waandishi wa Habari katika kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii Mafunzo yamefanyika Tarehe 19/12/2023  katika Ukumbi wa Nala centrurion hotel.



















SERIKALI IPO MBIONI KUTENGENEZA MFUMO WA KITAIFA WA KIELETRONIKI.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma

Serikali  ipo mbioni kutengeneza mfumo wa kitaifa wa kieletroniki wa taarifa za soko la ajira utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 346.9 kwa ajili ya kuwezesha ukusanyaji wa taarifa kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Taifa.

Hatua hiyo imelenga kupunguza taarifa za upotoshaji wa nafasi za ajira ambazo mara nyingi zimekuwa zikisambazwa mitandaoni na kuleta taharuki kwa wahitaji wa ajira na kusababisha kutapeliwa na wakati mwingine kuingizwa kwenye majanga mbalimbali.

Hayo yameelezwa leo Desemba 14,2023 Jijini hapa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa baadhi ya shughili zinazotekelezwa kwenye Wizara hiyo.

Aidha amesema kwa upande wa huduma za watu wenye ulemavu Serikali
imetoa kiasi cha shilingi bilioni 3.46 za kitanzania kwa ajili ya ukarabati vyuo vya ufundi stadi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu vilivyopo Sabasaba-Singida,Yombo-Dar Es Salaam ,Mtapika- Masasi na Luanzari-Tabora na Mirongo -Mwanza .

Amesema Vyuo hivyo vina Vijana wenye ulemavu watapao 774 na kiasi cha shilingi milioni 568 kimetumika kuwezesha mafunzo husika.

"Serikali imeendelea kutoa mafunzo kupitia vyuo vipya vinne vya ufundi stadi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu vya Songwe,Mwanza ,Kigoma na Ruvuma na kiasi cha shilingi bilioni 3.4 kimetumika kwa kwaka wa fedha 2023/2024 kiasi cha shilingi bilioni 3 kimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi kwa vyuo husika,"amesema

Pamoja na hayo Naibu Waziri Katambi ameeleza kuwa katika kuwaenzi zaidi wenye ulemavu Serikali inazindua mfumo wa taarifa za watu wenye ulemavu (PD-MIS)utakaoweza kusaidia upatikanaji wa taarifa zao na kurahisisha utoaji huduma kwa kundi hili maalumu.

"Pamoja na mambo hayo yote Serikali pia imeendelea kusimamia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu kila ifikapo Desemba 3,2023,wiki ya viziwi ambayo huadhimishwa September 2023,na siku ya watu wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Oktober 25,lengo ni kuengeza uelewa wa haki na ustawi wa watu wenye ulemavu kwa jamii,"amesisitiza.

Mwisho.


TRA DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI KWA KUWAFIKIA MAKUNDI MAALUMU.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imeadhimisha siku ya mlipa kodi kwa kuwafikia makundi maalumu ambapo wameweza kutembelea hospitali ya taifa ya afya ya akili(mirembe) pamoja na nyumba ya matumaini iliyopo kata ya miyuji.

Wakiadhimisha siku hiyo Meneja TRA Mkoa wa Dodoma Castro John amesema wanawashukuru wateja wao kwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri na mamlaka hiyo na wanatambua mchango ambao wameutoa kwa serikali na mkoa kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kutambua mchango wa walipa kodi asubuhi walifanya matembezi ya shukrani na jioni  watakuwa na hafla ya kuwatunuku wafanyabiashara waliofanya vizuri zaidi ili iwe chachu kwa wanaofanya vizuri kufanya vizuri zaidi.

"TRA tunajivunia kuwahudumia walipa kodi na wafanyabiashara kwani ni sehemu ya mchakato hivyo tunawaomba walipa kodi wetu kutumia machine ya EFDs kwani matumizi ya EFDs yanasaidia kuweka kumbukumbu na kupata makadirio ya kodi sahihi kwani wengine wanakuwa wanasema kodi ni kubwa na wakati hawana kumbukumbu hivyo niwasihi walipa kodi kuhakikisha wanatumia mashine hiyo" Amesisitiza Castro

Naye Faraja Mazengo Afisa Ustawi wa jamii Hospitali ya Taifa  afya ya akili  (Mirembe)  amesema wamefarijika kuona TRA inawafikia walengwa na wanaishukuru serikali kwa mwaka wa fedha suala la Afya limepewa kipaumbele na TRA nao wanaendelea kuonyesha kwa vitendo na wanaamini vifaa walivyoletewa vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa ambapo pamoja na hayo changamoto kubwa waliyonayo ni kuwahudumia wateja wengi ambao hawana ndugu na wengine wametelekezwa na ndugu zao.

"Kwa kuzingatia maadhimisho ya siku ya mlipa kodi tumeona siyo vibaya kuhakikisha tunawafikia ndugu zetu ili na wao waone ni sehemu ya jamii na tumewaletea zawadi mbalimbali" Amesisitiza Meneja Mkoa TRA Dodoma Castro John.

"Tunawashukuru kwa kutufariji na kutukumbuka Mungu awabariki sana na muendelee kufanya hivi kwa wahitaji wengine kwani tumejiona na sisi ni wenye thamani kwenye jamii na tungeomba taasisi zingine zifanye kama mlivyo fanya nyinyi na liwe ni zoezi endelevu" Amesema mmoja wa wagonjwa wa Afya ya akili.

Kwa upande wake Sister Maria Peter ambaye ni mwalimu na mlezi nyumba ya matumaini amesema anaishukuru mamlaka ya mapato Dodoma kwa kuwakumbuka kwa kuwaletea mahitaji mbalimbali ambapo watoto hao  wanawakusanya kupitia maafisa ustawi wa jamii kwani wanaushirikiano mzuri na wanahakikisha wanawalea watoto hao vizuri kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na elimu kwa kuhakikisha wanapata elimu bora kuanzia awali hadi kidato cha sita na kuendelea mpaka chuo kikuu ndipo wanaweza kumruhusu kuweza kujitegemea.

Sanjari na hayo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema anaipongeza TRA kwa kuendelea kushirikiana vizuri na walipa kodi lakini ni muhimu kuhamasishana watu wote kulipa kodi kwa manufaa ya taifa letu na kuhakikisha kila mtu anatii sheria bila shuruti.

"Miongoni mwa sababu ya wafanyabiashara wengine kuanguka  kibiashara ni pamoja na kufanya mambo kienyeji kukataa kulipa kodi kujiona wajajanja kulipa kodi kesho unataka mkopo benki wanashindwa kukupa kwa sababu watataka taarifa ya mapato na matumizi yako kwa sababu ya ujanja ujanja hutapata mkopo unao stahili hivyo nawasihi  wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati" Ameongeza Shekimweri

Naye Joseph Chowa mwakilishi wa wafanyabiashara amesema anampongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kusimamia vizuri mamlaka hiyo kwa kufanya mazingira rafiki kwa walipa kodi lakini anawaomba wafanyabiashara wenzake kulipa kodi pamoja na matumizi sahihi ya mazuri ya utendeji kazi kama mashine kwani itawasaidia kuweka rekodi zao vizuri na kwa upande wa TRA wamekuwa na vijana wengi sana na wafanyabiashara wengi ni watu wa makamo wanaomba waende nao taratibu.




WASTANI WA MATUMIZI KWA SIKU KWA MTU NI SHILINGI 1,419.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.


Matokeo yameonesha kuwa katika kaya za Walengwa, wastani wa matumizi kwa siku kwa mtu ni TZS 1,419 (sawa na US$0.6 kwa siku) kwa mwaka 2022, ambapo kiwango hicho kipo chini ya mstari wa umaskini wa Tanzania Bara wa TZS 1,859 (US$0.80) kwa mwaka 2022.

Hayo yameelezwa na Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nchi,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati akizindua ripoti ya awali ya kutathimini kipindi cha pili cha mpango wa kunusuru kaya maskini Tanzania 2022 uliofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Aidha ameongeza kuwa matokeo yanaonesha pia kuwa, wastani wa matumizi ya kaya moja ya Mlengwa kwa mwezi ni TZS 152,621 (US$65.50), ambapo matumizi ya chakula yanachukuwa nafasi kubwa kwa TZS 113,256 (US$48.6), sawa na asilimia 74.2 ya matumizi yote ya kaya.  Kiwango hiki cha matumizi ya kaya za Walengwa kwa mwezi kipo chini ukilinganisha na wastani wa matumizi ya Kaya moja kwa mwezi Nchini Tanzania.


"Kwa msingi wa matokeo haya ni dhahiri kuwa Walengwa katika Mpango wa TASAF matumizi yao yanatumika zaidi kwenye huduma za chakula badala ya kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji ili kuongeza mtaji na kutoka katika hali ya umaskini iliyopo kwa sasa, kwa msingi huo, Serikali itaelekeza nguvu zaidi katika kaya hizi na kuhamasisha Walengwa kuwekeza zaidi kwenye uzalishaji kwa lengo la kujiongezea kipato na hatimae kutoka katika Umaskini uliokithiri" Amesema Simbachawene


Aidha ameongeza kuwa kama tunavyofahamu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ilianzisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) ili kupunguza umaskini uliokithiri (Extreme Poverty) na kuondoa mwendelezo wa umaskini kwa vizazi vijavyo.

"Mpango huu unalenga kuimarisha hali za maisha ya Kaya za Walengwa kiuchumi na kijamii kwa kuziwezesha kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji ya msingi,ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa, Mpango wa TASAF unatoa ruzuku kwa Kaya za Walengwa zinazopaswa kutimiza masharti yaliyoainishwa katika maeneo ya huduma za jamii, kiuchumi na mazingira wanayoishi"


"Napenda nizungumzie kuhusu shughuli za kiuchumi za Kaya za Walengwa wa Mpango, matokeo yanaonesha kuwa, katika shughuli za uzalishaji, asilimia 50 ya Kaya za walengwa zinajishughulisha na kazi za shamba la familia, asilimia 22 zinafanya kazi za malipo, na asilimia 15 wamejiajiri wenyewe,takriban asilimia 57 ya chakula katika Kaya za Walengwa huzalishwa na kaya zenyewe kwa matumizi yao wenyewe au kupewa zawadi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki na asilimia 43 iliyobaki ya chakula hununuliwa, kwa matokeo haya napenda kuhamasisha Walengwa wa Mpango wa TASAF kuhakikisha wanazalisha chakula kwa kutumia fursa zinazotolewa na Serikali au wadau wengine katika maeneo wanayoishi, kwa sasa mvua zinazoendelea kunyesha Nchi nzima sote tutumie fursa ya kuotesha mazao ya muda mfupi kama mboga za majani, mahindi na mazao mengine kwa lengo la kujiongezea kipato"Amesisitiza Mhe.Simbachawene


Aidha mwaka 2024 TASAF itafanyika tathmini ya pili kwa lengo la kufuatilia na kutathimini malengo yalibainishwa katika Mpango unawahusisha Walengwa 5,146,720.


"Tathmini hii ya awali imekusanya taarifa za kaya na wanakaya zinazohusu hali ya elimu; afya; uwezeshaji wa wanawake; matumizi na usalama wa chakula; namna ya kukabiliana na majanga katika kaya; makazi na rasilimali za kaya; shughuli za kaya zisizokuwa za kilimo; akiba na mikopo; ajira na matumizi ya muda; shughuli za kilimo na mifugo; na unyanyasaji wa kijinsia,taarifa hizi zote ni za msingi katika kutoa viashiria vya hali ya umaskini katika kaya" Ameongeza Mhe.Simbachawene


Kwa upande wa Hali ya Makazi, matokeo yanaonesha kuwa, Kaya za Walengwa zinaishi katika mazingira yasiyoridhisha,asilimia 38 ya Kaya za Walengwa kuta za nyumba zimejengwa kwa udongo.


"Hapa niagize TASAF na viongozi wengine katika ngazi ya kata, Kijiji na kitongoji kufuatilia kwa karibu mazingira wanayoishi hawa ndugu zetu na kuweza kutoa ushauri wa kutosha wa namna ya kujenga kwa gharama nafuu na kutumia vyombo vingine vya Serikali kama Shirika la Nyumba la Taifa,nchi nyingine katika Bara la Afrika na duniani kote kundi hili hupewa kipaumbele katika makazi wanayoishi,serikali italifanyia kazi katika mpango mwingine unaofuata ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuwaweka hawa walengwa katika mazingira mazuri zaidi"Amesisitiza Mhe.Simbachawene


 

WAZAZI KUWAJIBIKA KWENYE MALEZI YA MTOTO Ndg , KINGWANDE

 Na. Kadala Komba Dodoma


Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Mary Chatanda  Novemba 24,2023  umeendelea na ziara yake  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.

Uongozi huo ukiwa katika ziara yake umegawanyika katika timu mbalimbali ambapo  Naibu Katibu Mkuu Ndg , Riziki Kingwande amefanikiwa  kutembelea Kata ya
Ibugule kijiji cha  Mapanga
Kata Chibelela
Kijiji Isangha
Kata ya Mtitaa na Kukagua mradi ya  madarasa matano (5) ya shule ya msingi Isangha Kukagua nyumba ya mtumishi two ni One Kukagua matundu 10 ya choo Yenye Gharama za Tsh.  233,800,000/= Pamoja na kusikiliza kero za wananchi .

Akizungumza na wananchi wa Kata ya  Mtitaa    amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwalinda  kwani maadili yameporomoka hivyo amewasihii kundokana na desturi ya  kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .

"Wazazi naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani ndio viongozi wa leo na kesho yao hatuwezi kukaa kimya na kulifumbia macho hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa kukatishwa ndoto zao tumechoka kusikia mara mtoto amelaitiwa mara kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande .

Sambamba na hilo, Ndg  .Kingwande Amewahimiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutekeleza majukumu yao kwa nafasi zao kuanzia ngazi ya shina , matawi kata kwa lengo la kuwaaminisha wananchi waone kazi vinazofanywa na viongozi wa chama cha Mapinduzi, hivyo viongozi wenzangu tujitume katika kazi ya kuwasaidia wananchi tufanye ziara pamoja na mafunzo kwa viongozi hili kuwajengea uwezo.

Naibu Katibu Mkuu Ndg , Riziki Kingwande Akizungumza na Wananchi wa kata ya Mtitaa
 



 MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA












Na Mwandishi wetu.

Imeelezwa kwamba uwekezaji wa hoteli kubwa na za kisasa unasaidia katika kuchochea shughuli za utali na kuongeza thamani ya Mji wa Mbinga, kwa sababu ya upekee wa vivutio vyake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Hotel ya One Pacific yenye hadhi ya nyota tatu katika wilaya ya Mbinga.

Waziri Mhagama amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwa kuwa balozi kinara wa sekta ya utalii na uwekezaji kwa ujumla katika sekta ya utalii.

“Mkakati wa Taifa wa ROYAL TOUR na kuifungua nchi yetu Tanzania katika sekta ya utalii ni mkakati mkubwa sana, na uliotukuka na tunaungana na wawekezaji katika kutafsiri ROYAL TOUR ndani ya wilaya yetu ya Mbinga,” Alifafanua

Akieleza kuhusu vivutio vinavyopatikana, Waziri amesema, wilaya ya Mbinga inavivutio vya kutosha; kama safu za milima zilizojipanga kwa kuvutia, zenye maporomoko ya maji, uoto wa asili, unaopendezesha madhari ya milima hiyo.

Aidha hapa ndio mahali ambapo kuna mapango ya kale katika eneo la Litembo, na inaaminika wazee wetu wa zamani waliishi katika mapango hayo.

“Hii historia kama itawekezwa vizuri, ni kivutio na utalii wa kutosha sana katika eneo letu,” Alibainisha.

Kwa upande wake Dkt. Erasmo Nyika akizungumza kwa niaba ya bodi ya wawekezaji wa mradi wa Hotel hiyo amesema wamesukumwa kuja kuwekeza Mbinga kutokana na Msukumo wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga mazingira rafiki ya uwekezaji.

“Tumuwekeza miradi miwili ndani ya wilaya ya Mbinga yenye thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 4, na tumeona fursa zipo na tunashukuru Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbinga kwa kutushawishi kuwekeza Mbinga, mradi umelenga kuzalisha ajira nyingi kwa wazawa,” Alisema

Awali, Mhandisi Selemani Kinyaka katika taarifa yake amesema Ujenzi wa Majengo ya mraadi wa One Pacific Hotel; unavyumba vya kawaida 14, vyumba vya daraja la juu 23 vyumba vya hadhi ya kiutawala 3, Ukumbi mdogo wa mikutano, Migahawa 2, sehemu ya mazoezi, eneo la kuogelea na eneo la kufulia nguo.

 

Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi tumetoa ajira zaidi ya 250 ambapo 30 zilikuwa ajira za kudumu, na nyingine ni ajira zilizojitokeza kila siku.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kulshoto akizindua) Mradi wa Hotel ya One Pacific katika ziara yake ya Kikazi wilayani Mbinga.
 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo wakitembelea baadhi ya maeneo ya mradi wa Hotel One Pacific kabla ya uzinduzi rasmi kufanyika.

 

WANAFUNZI CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUTUMIA TAFITI ZAO KWA MANUFAA YA JAMII.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Wanafunzi Chuo cha Mipango ya  Maendeleo Vijijini wametakiwa kutumia tafiti zao kwa manufaa ya jamii ili kuleta tija na matokeo chanya ya tafiti zao.

Hayo yamesemwa na Bwana. Moses Dulle   Mkurugenzi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye amemwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo Mgeni rasmi katika kongamano la kitaaluma ambapo wanafunzi wamepewa tuzo mbalimbali kutokana na tafiti zao ili kuwapa motisha na wengine kuendelea kufanya tafiti hizo ambapo tukio hilo limefanyika ukumbi wa  miyuji North jijini Dodoma.


Aidha ameongeza kuwa tafiti nyingi hazitangazwi kutokana na udhaifu kutoka kwa wahitaji na wazalishaji kwa kawaida jamii inabidi iwe na uhitaji wa tafiti fulani kwa ajili ya ubunifu na wakati mwingine inawezekana jamii yenyewe hawana uhitaji hivyo kuwapa ugumu watafiti kutumia tafiti zao lakini jamii inapaswa kuwa na muamko wa kufanya uwekezaji kwenye tafiti hizo.

"Maendeleo ni hatua na hayawezi kuja ghafla ni jukumu la wanafunzi na walimu kuweza kutangaza tafiti zao pamoja na waandishi wa habari kuuliza taasisi zinazofanya tafiti kujua namna wanavyofanya tafiti zao na kuzitangaza kwa wananchi lakini pia ni jukumu la jamii yote kwa ujumla wake kuhamasisha namna watu wanaweza kupata taarifa za utafiti" Amesisitiza Bwana Dulle

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof.Hozen Mayaya amesema chuo kinakuwa na wamewapongeza watu wao mbalimbali na kuwafikishikia umma kwamba wanajenga uwanja wa watu wao,hivyo pamoja na kwamba wanawaleta wanafunzi na kwa sasa hivi wanataaluma 79 ambao wanasoma katika maeneo mbalimbali kati yao 45 walikuwa wanasoma vyeo vya PHD ambao ni vyeo vya juu zaidi.

"Hii maana yake ni kwamba miaka michache ijayo chuo hiki kitakuwa kinatoa wasomi wenye elimu ya juu lakini kwa upande wa kuwapa tuzo wanafunzi ni kuwajengea hamu ambao wanaendelea kusoma ili kufanya vizuri zaidi na kuwa bora kwenye masomo yao na kujifunza kutoka kwa wingine" Amesisitiza Prof.Mayaya

Naye Dorcas Samson ambaye ni mhitimu wa chuo hicho amesema anashukuru kuwa miongoni mwa wahitimu kwani kupitia chuo hicho ameweza kuwa mjasiriamali na hivi sasa anajishughulisha na uongezaji wa thamani kwenye bidhaa za chakula anatengeneza unga wa lishe pamoja na soya ambapo ndoto yake kubwa ni kuwa mjasiriamali mkubwa kutokana na ujuzi alionao na kuajiri wengine.

"Kwa wanafunzi ambao hawajajiunga na chuo cha mipango nawashauri wajiunge na chuo hiki kwani mbali na masomo watafundishwa elimu ya ujasiriamali na kuweza kujiajiri wenyewe na kupunguza wimbi kubwa la kutegemea kuajiriwa na serikali ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati na nchi yetu kupunguziwa lawama kutoka kwa vijana lakini kwa upande wa serikali tunaomba ihakikishe inawasapoti wajasiriamali wadogo na wanaochipukia hasa hasa vijana" Ameongeza Tabitha Yusuph ambaye ni mhitimu na mjasiriamali.



MWENYEKITI UWT TAIFA ATEMBELEA HOSPITALI YA MJI KONDOA

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa UWT na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mhe. Marry Chatanda, leo tarehe 22 Novemba 2023 ametembelea Hospitali ya Mji Kondoa ikiwa ni ziara yake kwa Halmashauri hiyo kujionea Miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita.

Akiwa Hospitalini, hapo Mhe. Chatanda amewajulia hali wagonjwa waliokuwepo kwenye jengo la dharura ambalo limejengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 300 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu chini ya Mpango wa UVIKO.

Aidha, Mhe. Chatanda ametembelea jengo jipya la Mama na Mtoto ambalo lipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake baada ya kupata fedha kiasi cha Shilingi Milioni 900 za ukarabati wa Hospitali ya Mji ambapo majengo matatu yamejengwa ikiwemo jengo la upasuaji, mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia Maiti (Mochwari).

Hata hivyo, ameagiza kufanyiwa marekebisho yaliyoonekana katika majengo hayo ikiwemo kumalizia jengo la mama na mtoto ili wananchi waanze kupata huduma katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na wahandisi kusaidia kutoa utaalam ili kujenga majengo yaliyo bora.










DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA.

 
Wananchi wa kijiji cha Hurui kata ya Kikore Wilayani Kondoa  Mkoani Dodoma wamesema ujenzi wa daraja la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 linalotarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba 2023 litatatua  kero ya muda  ya mrefu ya kutumia daraja la kamba kuvuka mto na  kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii  hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watoto kutofika shule Pia   wakazi wa Kijiji hicho kushindwa kuuza mazao yao kutokana na kukosekana kwa miundombinu hiyo.

Hayo yamebainishwa Leo Novemba 22,2023 baada ya Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Timu iloyoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Joketi Mwegelo na Wataalamu wengine wa Mkoa na Wilaya hiyo kufika katika daraja hilo  kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

Aidha Ndg. Mwegelo wakati akitembelea mradi wa Maji katika Kata ya Kisese amemtaka mkandarasi anaye tekeleza mradi huo kuanza ujenzi wa tanki ndani ya  siku saba awe ameshaanza utekelezaji wa mradi huo ili kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi wa Kisese.Wito huo umetolewa baada ya kupita siku ishirini na moja ambazo mkandarasi alitakiwa awe eneo la mradi akiendelea na Ujenzi wa Mradi.

Hata hivyo Ndg. Mwegelo amesema licha ya Viongozi mbalimbali kuwachukulia hatua baadhi ya Viongozi ambao walikuwa wakitekeleza mradi huo lakini bado inaonekana kuendelea kusuasua jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa ukamilishaji wa Mradi huo.

Pia, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Kikore na Kisese kupeleka watoto shule na kuachana na tabia ya kugeuza watoto kufanya kazi za ndani .

Mkoa wa Dodoma umekuwa wa 17 kufikiwa na  ziara ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Mary Chatanda na Viongozi wengine ambapo wanatarajia kupita katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ikiwa tayari wamesha kamilisha ziara yao Wilaya ya Kondoa kwa  kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) na maendeleo ya miundombinu mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa huo.