Subscribe Us

TRA DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI KWA KUWAFIKIA MAKUNDI MAALUMU.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imeadhimisha siku ya mlipa kodi kwa kuwafikia makundi maalumu ambapo wameweza kutembelea hospitali ya taifa ya afya ya akili(mirembe) pamoja na nyumba ya matumaini iliyopo kata ya miyuji.

Wakiadhimisha siku hiyo Meneja TRA Mkoa wa Dodoma Castro John amesema wanawashukuru wateja wao kwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri na mamlaka hiyo na wanatambua mchango ambao wameutoa kwa serikali na mkoa kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kutambua mchango wa walipa kodi asubuhi walifanya matembezi ya shukrani na jioni  watakuwa na hafla ya kuwatunuku wafanyabiashara waliofanya vizuri zaidi ili iwe chachu kwa wanaofanya vizuri kufanya vizuri zaidi.

"TRA tunajivunia kuwahudumia walipa kodi na wafanyabiashara kwani ni sehemu ya mchakato hivyo tunawaomba walipa kodi wetu kutumia machine ya EFDs kwani matumizi ya EFDs yanasaidia kuweka kumbukumbu na kupata makadirio ya kodi sahihi kwani wengine wanakuwa wanasema kodi ni kubwa na wakati hawana kumbukumbu hivyo niwasihi walipa kodi kuhakikisha wanatumia mashine hiyo" Amesisitiza Castro

Naye Faraja Mazengo Afisa Ustawi wa jamii Hospitali ya Taifa  afya ya akili  (Mirembe)  amesema wamefarijika kuona TRA inawafikia walengwa na wanaishukuru serikali kwa mwaka wa fedha suala la Afya limepewa kipaumbele na TRA nao wanaendelea kuonyesha kwa vitendo na wanaamini vifaa walivyoletewa vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa ambapo pamoja na hayo changamoto kubwa waliyonayo ni kuwahudumia wateja wengi ambao hawana ndugu na wengine wametelekezwa na ndugu zao.

"Kwa kuzingatia maadhimisho ya siku ya mlipa kodi tumeona siyo vibaya kuhakikisha tunawafikia ndugu zetu ili na wao waone ni sehemu ya jamii na tumewaletea zawadi mbalimbali" Amesisitiza Meneja Mkoa TRA Dodoma Castro John.

"Tunawashukuru kwa kutufariji na kutukumbuka Mungu awabariki sana na muendelee kufanya hivi kwa wahitaji wengine kwani tumejiona na sisi ni wenye thamani kwenye jamii na tungeomba taasisi zingine zifanye kama mlivyo fanya nyinyi na liwe ni zoezi endelevu" Amesema mmoja wa wagonjwa wa Afya ya akili.

Kwa upande wake Sister Maria Peter ambaye ni mwalimu na mlezi nyumba ya matumaini amesema anaishukuru mamlaka ya mapato Dodoma kwa kuwakumbuka kwa kuwaletea mahitaji mbalimbali ambapo watoto hao  wanawakusanya kupitia maafisa ustawi wa jamii kwani wanaushirikiano mzuri na wanahakikisha wanawalea watoto hao vizuri kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na elimu kwa kuhakikisha wanapata elimu bora kuanzia awali hadi kidato cha sita na kuendelea mpaka chuo kikuu ndipo wanaweza kumruhusu kuweza kujitegemea.

Sanjari na hayo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema anaipongeza TRA kwa kuendelea kushirikiana vizuri na walipa kodi lakini ni muhimu kuhamasishana watu wote kulipa kodi kwa manufaa ya taifa letu na kuhakikisha kila mtu anatii sheria bila shuruti.

"Miongoni mwa sababu ya wafanyabiashara wengine kuanguka  kibiashara ni pamoja na kufanya mambo kienyeji kukataa kulipa kodi kujiona wajajanja kulipa kodi kesho unataka mkopo benki wanashindwa kukupa kwa sababu watataka taarifa ya mapato na matumizi yako kwa sababu ya ujanja ujanja hutapata mkopo unao stahili hivyo nawasihi  wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati" Ameongeza Shekimweri

Naye Joseph Chowa mwakilishi wa wafanyabiashara amesema anampongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kusimamia vizuri mamlaka hiyo kwa kufanya mazingira rafiki kwa walipa kodi lakini anawaomba wafanyabiashara wenzake kulipa kodi pamoja na matumizi sahihi ya mazuri ya utendeji kazi kama mashine kwani itawasaidia kuweka rekodi zao vizuri na kwa upande wa TRA wamekuwa na vijana wengi sana na wafanyabiashara wengi ni watu wa makamo wanaomba waende nao taratibu.




0 Comments:

Post a Comment