Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWA

Na Kadala Komba- Dodoma JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWA Jamii imeaswa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya utumiaji dawa za binadamu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo usugu wa dawa hizo mwilini. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali (RBA-Initiative), Michael Mosha, Jijini Dodoma wakati wa mwendelezo wa kampeni ya kuongeza uelewa kuhusu Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa ambayo hufanyika Duniani kote kila ifikapo Novemba 18 hadi 24 Novemba kila mwaka. Amesema kama shirika limekuwa likifanya hivyo mara kwa mara kwa kuwashirikiana na Shule mbalimbali na watoa huduma za Afya, wakulima na wafugaji, akisema kuwa Vimelea vya magonjwa havina mipaka vinampata kila mtu bila kujali kabila wala rangi. “Tunatoa elimu hii kwa njia mbalimbali kama vipeperushi, usafiri wa Bajaji ambapo zimebandikwa vipeperushi vinavyozungumzia Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa lugha ya kiswahili na maeneo ya kimkakati kama stendi ya mabasi Nane Nane, Soko kuu la Machinga Complex Dodoma na maeneo mengine tukitoa elimu,”Amesema Mratibu huyo. Pia Mratibu huyo ametoa wito kwa wananchi na jamii kwa ujumla kufuata kanuni nzuri ya matumizi ya dawa kwa wakati sahihi na ulioshauriwa na daktari. Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Bakir Hussen ameeleza kuwa kampeni hii inafanyika Dunia nzima kwa kutoa elimu ya uelewa kuhusu usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, “Kupitia shirika hili tunatumia vyombo vya moto kama daladala, bajaji na kugawa vipeperushi maeneo sambamba na mashuleni kwa kuanzisha Club kwenye shule hizo kwa lengo moja kila mtu apate elimu hii,”Ameeleza Mfamasia huyo. Aidha Mwalimu mlezi wa RBA-Club kutoka Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege Bwa. Musa Sulemani amesema tangu kuanzishwa kwa Programu hiyo shuleni imesaidia kuleta mabadiliko kitabia kwa wanafunzi kuanzia wanafunzi wa shule za Msingi hadi Sekondari. Naye Mwalimu wa Shule ya Meriwa, Bw. Brighton Nashon amesema mwanzoni kulikuwa na mwitikio mdogo lakini baada ya kuendelea kuwapatia Elimu sasa wanafunzi wamekuwa na mwitikio mzuri uliyopelekea baadhi yao kutunga nyimbo zenye ujumbe juu ya matumizi sahihi ya Dawa Nao Madereva Bajiji Haule Mkwasa na Abusasani Bundala wamelipongeza shirika la RBA Kwa kuwathamini na kutambua mchango wao katika jamii kwa kuwapatia mafunzo kwa vitendo iliyoambatana na matembezi katika jiji la Dodoma. “Matembezi yamefanyika kuzunguka Dodoma na viunga vyake tukiendesha bajaji zetu zilizobandikwa mabango yaliyobeba ujumbe kwa lengo la kuigusa jamii moja kwa moja kuchukua tahadhari,” Wameeleza madereva hayo.
Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali (RBA-Initiative), Michael Mosha Akitoa Elimu kuhusu Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa
Mfamasia kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Bakir Hussen akieleza Madhara ambayo Binadamu anawedha kupata asipofuata ushauri wa daktari
Mwalimu mlezi wa RBA-Club kutoka Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege Bwa. Musa Suleman Akielezia faida ya Elimu hii mashuleni
Mwalimu wa Shule ya Meriwa, Bw. Brighton Nashon mwitikio mzuri kwa wanafunzi
Madereva Bajiji Haule Mkwasa na Abusasani Bundala Wakilipongeza shirika la RBA kwa kuwakumbuka Madereva Bajaji
PICHA YA PAMOJA VIONGOZI WA RBA NA MADEREVA BAJAJI KATIKA UKUMBI WA DEA MAMA JIJINI DODOMA
DAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WALIYOTUNUKIWA VYETI KWA KUTAMBUA MCHONGO WA VYOMBO VYA HABARI
WANANCHI WA DODOMA WAKIPATIWA VIPEPERUSHI KATIKA MAENENO TOFAUTI

PESA INAWEZA KUWA MBARAKA AU LAANA*

Pesa si laana yenyewe kama yenyewe; bali ni kitu chenye thamani kubwa kwa sababu ikitumiwa ipasavyo, inaweza kufanya mema katika kuleta wokovu wa roho za watu, katika kuwabariki wengine ambao ni maskini kuliko sisi wenyewe. Kwa matumizi ya kiholela au yasiyo ya busara .... pesa zinaweza kuwa mtego kwa mtumiaji. Anayetumia pesa kuridhisha kiburi na matamanio yake anaifanya kuwa laana badala ya baraka. Pesa ni jaribio la mara kwa mara katika kupima mielekeo ya moyo. Yeyote anayepata zaidi ya mahitaji yake halisi anapaswa kutafuta hekima na neema ya kuujua moyo wake na aweze kuulinda moyo wake kwa bidii, asije akawa na matamanio ya kufikirika na akawa wakili asiye mwaminifu, akitumia kwa upotevu mtaji wa Bwana wake aliokabidhiwa. Ukurasa: 372, Aya:1

SHULE YA VIPAJI NCHINI FOUNTIN GATE KUWATAMBULISHA WACHEZAJI KWA MSIMU WA 2022 \2023

Na. Kadala Komba Dodoma 

 Akizungumza na Waandishi wa Habari  Jijini Dodoma  Mtendaji Mkuu wa Shule ya vipaji ya Fountion Gate Thabiti Kandoro Amesema tupo kwenye maandalizi ya uzinduzi wa Mpango  wa   maendeleo ya msimu wa michezo ya Mwaka 2022/2023 siku za hivi karibuni  mnamo Novemba tarehe 27 Mwaka huu Jijini Dodoma uzinduzi huu utaambatana pamoja na kuwatambulisha wachezaji wa Timu ya Soka ya wanawake  Princess ya Fountain Gate Kwa msimu wa 2022/2023 ambapo  Timu ya Lady Dovu toka Uganda imethibitisha kushiriki katika uzinduzi.

 Kandoro amesema Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa ni KATIBU Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Dk.Hassan Abbasi ambaye atazindua Mpango  wa   maendeleo ya msimu wa michezo Amesema. 

 Aidha Kandoro amesema Fountin kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu ya wanawake [WPL] haya ni mafanikio makubwa tunayojivunia kutika kwa vijana wetu  katika shule hii.

Sambamba na hilo Kandoro amesema  Pamoja na mambo mengine  kituo hicho wamepokea watoto zaidi ya mia moja kutoka Mikoa mbalimbali Kwa ajili ya kuwapatia Elimu na kuwaendeleza vipaji vyao walivyonayo vya  mpira.

 

 


Mtendaji Mkuu wa Shule ya vipaji ya Fountion Gate Thabiti Kandoro

 


Akizungumza na Waandishi wa Habari  Jijini Dodoma  Mtendaji Mkuu wa Shule ya vipaji ya Fountion Gate Thabiti Kandoro

Baadhi ya Waandishi wa Habari  Jijini Dodoma  wakimsikiliza  Mtendaji Mkuu wa Shule ya vipaji ya Fountion Gate Thabiti Kandoro



 
 
 
 

“MBEYA INAENDA KUFANANA NA HADHI YA MAJIJI, TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA” DKT. TULIA*

Na. Mwandishi Wetu Mbeya Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi wa Mbeya Mjini kumshukuru na kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoliwezesha Jimbo hilo katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu. Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 14, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Zahanati ya Itezi iliyopo katika Kata ya Itezi Jijini humo iliyogharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 117.4 kwa ushirikiano wa Serikali kuu, Wananchi Pamoja na Taasisi ya Tulia Trust. Amesema kuwa ni rekodi kubwa imeweza kufanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia ndani ya kipindi kifupi kwa kuwaboreshea maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo barabara, elimu, afya n.k Katika sekta ya afya, Serikali imewezesha ujenzi wa kituo cha afya Iyela, Zahanati Ndanyela, Zahanati ya Iduda, Serikali imeipandisha hadhi kilichokuwa kituo cha afya Igawilo na kuwa hospitali ya Wilaya ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni mbili zimetolewa. Hospitali ya Meta zimewekwa zaidi ya bilioni 11 ili kuwasaidia wakinamama. Kuhusu changamoto za maji, Dkt. Tulia amesema “Mhe. Rais ametuletea zaidi ya Shilingi Bilioni tano ili tuanze ujenzi wa mradi wa mto Kiwira ambao utagharimu zaidi ya Bilioni 250 kwahiyo msiwe na wasiwasi kazi imeanza na ndani ya muda mfupi wananchi wote mtakuwa mnapata maji ya uhakika” “Kuhusu miundiombinu Mbeya Mjini tuliachwa nyuma sana lakini sasa kazi imeanza na ule mradi wa barabara ya njia nne unaanza hivi punde bilakusahau barabara za mitaa yetu itatandikwa rami ili Mbeya ifanane na hadhi ya Jiji ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge” amesisitiza Dkt. Tulia

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA AMETOA MAELEZO KUHUSU AJALI YA NDEGE

*YALIYOJIRI LEO NOVEMBA 14, 2022 WAKATI MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI - MAELEZO NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA AKITOA TAARIFA YA MAELEKEZO YA BARAZA LA MAWAZIRI KUHUSU AJALI YA NDEGE YA KAMPUNI YA PRECISION AIR ILIYOTOKEA NOVEMBA 6, 2022* #Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Novemba 14, 2022 jijini Dodoma kimepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyotokea mnamo Novemba 6, 2022 na hatua zilizochukuliwa baada ya ajali. #Baraza la Mawaziri limewaelekeza Wataalam wa ndani kushirikiana na Wataalam kutoka nje ya nchi katika kufanya uchunguzi kuhusiana na ajali hii ili kupata chanzo cha ajali na kutoa mapendekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa mara baada ya ajali kutokea. #Baraza la Mawaziri limetoa maelekezo haya kwa kuzingatia kwamba nchi yetu imesaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa ambayo inasimamia usafiri wa anga na hatua zinazopaswa kuchukuliwa mara baada ya ajali ya anga kutokea. #Baraza la Mawaziri pia limeelekeza vitengo vyote vinavyohusika na kukabiliana na majanga viimarishwe kwa namna mbalimbali ambazo zitatuwezesha sisi kama nchi kuongeza uwezo zaidi ya tulionao sasa katika kukabiliana na majanga pale yanapotokea. #Ajali za ndege zinapotokea, zipo hatua tatu zinazofuatwa katika uchunguzi ikianza na timu ya uchunguzi ya ajali ya ndege ambayo inafanya uchunguzi wake na kutoa maelezo ya awali ndani ya siku 14, inafuatiwa na ripoti ya awali ambayo inatolewa ndani ya siku 30 na tutamaliza na ripoti kamili ambayo inatolewa ndani ya miezi 12 baada ya ajali kutokea, hatua hizi zote tayari zimeshaanza. #Serikali inawaomba wananchi wote kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi huu unafanyika na baada ya uchunguzi kukamilika wananchi watajulishwa. #Baraza la Mawaziri linawashukuru na kuwapongeza Wananchi na wote waliohusika katika uokozi baada ya ajali hii kutokea. #Maeneo ya uchunguzi yote yanaainishwa na timu za wachunguzi, taratibu zote za kimataifa ambazo zinaelekeza juu ya maeneo yanayopaswa kufanyiwa uchunguzi zinazingatiwa. *IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO*

UCHIMBAJI MAKAA YA MAWE KULETA TIJA KWA WATANZANIA

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa amebainisha kuwa, biashara ya Makaa ya Mawe inatarajia kuleta tija kwa Watanzania kutokana na uhitaji mkubwa wa madini hayo ndani na nje ya nchi. Dkt. Kiruswa ameeleza hayo Novemba 12, 2022 wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma alipotembelea mgodi wa uchimbaji wa Makaa ya Mawe wa Ruvuma Coal Ltd ili kujionea shughuli za uchimbaji zinazoendelea katika mkoa huo. Ameeleza kuwa, Serikali imeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayovutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani kuja kuwekeza na kufanya biashara ya madini mbalimbali yakiwemo Makaa ya Mawe. Aidha ameongeza, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa Makaa ya Mawe kutoka kwenye migodi hususan barabara ya kuelekea mkoani Mtwara ili kusafirisha Makaa ya Mawe hayo katika bandari. "Katika mikoa yote yanapochimbwa Makaa ya Mawe mnakaribishwa katika mkutano maalum utakaowasaidia kupata uelewa sahihi wa makaa ya mawe na madini mengine yanayopatikana katika mkoa huo na maeneo jirani," amesema Dkt. Kiruswa. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo amesema, kutokana na uwepo wa migodi imesaidia wilaya hiyo kupata faida nyingi katika kutekeleza shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa shule na vituo vya afya. Amesisitiza wadau wa Makaa ya Mawe katika wilaya hiyo kushiriki mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Madini ili kujifunza uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR) katika siku zilizopangwa ili kupata uelewa zaidi. Naye, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Benaya Kapinga amesema Makaa ya Mawe yanahitajika kwa wingi duniani kwa sasa. Amesema Serikali itumie fursa hiyo kuhakikisha wilaya inapata faida ya uwepo wa migodi kwa kutoa ajira na kuleta maendeleo kwa jamii zinazozunguka mgodi hiyo. Naye, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Makaa ya Mawe Ruvuma, Benedicto mshingwe amesema, hadi sasa mgodi huo umetoa ajira zaidi ya 700 kwa Watanzania hususan wanaozunguka mgodi. Pia, amesema mgodi umeendelea kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa na zahanati ili kujenga mahusiano mazuri. Awali, Dkt. Kiruswa amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas na wadau mbalimbali wa sekta ya Madini na kuzungumzia shughuli za uchimbaji madini zinazofanyika katika mkoa huo na changamoto wanazopitia.

WAZIRI SIMBACHAWENE, AMPONGEZA MAMA TUNU PINDA

Na Mwandishi wetu Kuimba kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuewa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Mtakatifu Theresia, Mtoto wa Yesu inayoitwa Mungu asiye shindwa iliyofanyika katika Parokia ya Nzinje Mjini Dodoma. “Kwaya hii ya Mtakatifu Theresia, Mtoto yesu ndio anayoimbia Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda, amechagua jambo zuri sana la kufanya baada ya Kustaafu”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Theresia, Mtoto yesu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akimkabidhi kanda ya nyimbo (CD)Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda.
Mama Mbonimpaye Mpango Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza jambo wakati wa Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Theresia, Mtoto wa Yesu.
Mama Tunu Pinda (kulia) ambaye ni miongoni mwa Wanakwaya wa Matakatifu Theresia Mtoto yesu wakiimba mbele ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu.

WALIMU WA SHULE BINAFSI NA SERIKALI WAMEUNGANA KWA PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO MASHULENI

Na. Kadala Komba Dodoma
Mwenyekiti wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Ester Manyanda Akizungumza na Waandishi wa Habari lengo la kukutana pamoja Walimu wa Shule Binafsi
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma,Josephine Mwaipopo akizungumza Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Wamiliki wa Shule wakipokea vyeti kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo
Picha ya Pamoja kwa washiriki na Wadau wadhamini wakiwa na Mgeni Rasmi
WALIMU wa Shule binafsi za Awali na Msingi toka Mikoa mbalimbali Nchini wakiwemo wamiliki wa Shule hizo wamekutana Jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza malezi na makuzi ya watoto ili kuwalinda na vitendo viovu dhidi ya ukatili na maadui kwa mustakabali wa maisha yao ya Sasa na baadae. Hatua hiyo imekuja kufuatia kuongezeka kwa wimbi la vitendo vya ukatili katika Jamii dhidi ya Watoto ambavyo vinazidi kuongezeka kila siku. Mwenyekiti wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Ester Manyanda Akizungumza kwa niaba ya Walimu na Wamiliki wa shule binafsi katika Tamasha hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza Jijini Dodoma alisema tunaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana kupambambana na vitendo vya ukatili vinavyotokea kwenye Jamii inayotuzunguka kwakufanya hivyo ni mwanzo mzuri ili kuwa na Taifa lenye malezi bora. Aidha Mkuu wa shule ya Kimataifa ya Almes, Reuben Kiloy ametumia nafasi hiyo kuwaomba Wadau mbalimbali wakiwemo Elimu na Jamii kuwaunga mkono. Kiloy alisema kuwa malengo ya kukutana ni kuwaleta pamoja na kuwaunganisha walimu wa shule binafsi ili kuwapa walimu fursa ya kujifunza malezi na makuzi ya watoto ili kuwalea na kuwafundisha vema ikiwa ni pamoja na kuwalinda watoto dhidi ya maadui na vitendo viovu n hatarishi kwa maendeleo ya watoto. "Lengo lingine la kukutanisha walimu hapa ni kutoa mchango madhubuti katika kuhamasisha jamii kuelimisha watoto wetu katika mazingira yasiyokinzana na utamaduni,mila na desturi za kitanzania,"alisema. Kwaupande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma,Josephine Mwaipopo akizungumza Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,alisema kuwa kama Serikali wamekuwa wakifanya jitihada kubwa katika kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo kutoa Elimu kwa Jamii kwa vitendo . "Serikali imekua ikitoa miongozo mbalimbali kwajili ya uanzishaji shule za watoto kuanzia miaka 0 hivyo miongozo hiyo ikifuatwa watoto watalindwa na watakua katika makuzi sahihi,"alisema. Alisema kuwa masuala ya ukatili wa kijinsia na ukatili wa watoto umekua mkubwa kwasasa hivyo ni vizuri kutoa elimu zaidi kwa jamii na wazazi ilikukomesha vitendo hivyo. "Mamlaka za Serikali za mtaa zimewekewa sheria za kuhakikisha watoto wanalindwa katika maeneo yao,"alisema. Pamoja na hayo afisa ustawi huyo aliwataka watanzania kujenga tabia ya kuasili watoto kwani watoto waliopoteza wazazi ni wengi na wanakosa malezi sahihi kwakukosa walezi. Aidha Katibu wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Rehema Andrew Amesema sisi kama walimu wa shule binafis tutaendelea kutoa mchango madhubuti katika jamii kuhamasisha watoto wetu wanakuwa katika mazingira yasiyokinzana na utamaduni mila na desturi za kitanzania. Mwisho