Subscribe Us

ELIMU YA KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA KUTOLEWA MASHULENI.

 
Na Moreen Rojas
Dodoma.

Elimu ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya imeshauriwa kutolewa kunzia shuleni ili kulinusuru kundi la watoto wenye miaka kati ya kumi hadi kumi na mbili ambalo kwa siku za hivi karibuni limetajwa kuwa hatarini zaidi kwenye uraibu wa dawa za kulevya.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Kamishna wa kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo wakati akifunga mafunzo ya Programu ya TAKUKURU rafiki katika tatizo la dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Rushwa kwa maafisa waaohusika na uelimishaji umma na mawasilino.


"Tumieni mafunzo mliyoyapata kutoa elimu kwa jamii kwani tunaamini jamii ikielimika na kupata uelewa itakuwa ni rahisi kuweza kupambana na suala zima la udhibiti wa madawa ya kulevya hivyo tumeanza kwa wanafunzi ngazi za msingi,sekondari hadi vyuo vikuu hivyo kupitia klabu zao za kupambana na Rushwa watatumia pia klabu hizohizo kupambana na madawa ya kulevya ikiwa ni ajenda ya wananchi kukataa madawa ya kulevya ili kuokoa kizazi cha taifa hili" Amesisitiza Lymo.

Aidha ameongeza kuwa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) zimeamua kuungana kwani zinafanana katika utendaji kazi wake na kuamua kutokomeza kabisa madawa ya kulevya na Rushwa ambayo ni chanzo kikubwa cha kumaliza nguvu kazi ya taifa ambayo asilimia kubwa ni vijana,kuhakikisha wanatetea nchi kwani haki huinua taifa.

"Kupitia mafunzo haya naamini mmeweza kuona uhusiano mkubwa kati ya Rushwa na Dawa za kulevya  kwani kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameweza kutumia Rushwa kufanikisha uuzwaji na usambazaji wa dawa hizo na kuharibu kabisa rasilimali watu na kupunguza kasi ya uchumi kwani watumiaji hushindwa kufanya kazi ipasavyo na kuwa warahibu wa dawa hizo"

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye amesema kuwa mafunzo hayo yaliyofanyika siku tatu yamewasaidia maafisa hao namna ya mbinu za kuongeza katika utendaji kazi na hususani katika programu ya kushirikisha jamii katika mapambano  ya Rushwa programu mahususi ya TAKUKURU rafiki,ambapo ni matumaini yao kwamba mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kwa jamii ya kitanzania dhidi ya Rushwa na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

"Tunatarajia kuona kiwango cha ushiriki wa wananchi katika kushirikiana na taasisi hizi mbili kikiongezeka na kukuwa lakini pia ushiriki wa wadau ukiongezeka ikiwemo taasisi zisizo za kiserikali kuungana pamoja nasi katika kushiriki kuthibiti lakini pia kuzuia Rushwa na madawa ya kulevya" Ameongeza Bi.Neema












0 Comments:

Post a Comment