Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

UCHAGUZI MWAKA 2024\2025 UMEWAKUTANISHA WADAU WA SIASA NA VIONGOZI WA DINI

Na. Kadala Komba Bahi 

Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi,kuanzia hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura. 

Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa kikao kazi cha  wadau wa vyama vya siasa na viongozi wa dini kikao  kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wilayani Bahi Septemba 26\09\2024 alisema kwa mujibu wa kanuni ya 27 GN. Na. 571 Kampeni za uchanguzi zitaanza tarehe 20 hadi tarehe 26 Novemba 2024 .

 Aidha Mkurugenzi  Mlawa amesema kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ni hatua muhimu inayompa kila mwananchi mwenye sifa haki ya kisheria kushiriki uchaguzi kama mpiga  kura au mgombea hivyo wananchi nawahimiza kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutumia haki yako ya kupiga kura au kugombea nafasi za uongozi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi amesema Ushiriki wa wananchi wengi katika kugombea nafasi za uongozi ni muhimu katika kukuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu .
 

 
Upande wa kulia ni
Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa kushoto kwake ni Michael Ziwa Afisa Uchaguzi Bahi.
 
 
 
Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa akipitia tangazo la uchanguzi.

 
 
 
Picha ni Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Bahi Paulina Deus Bupamba
 
 
Picha ni Shekh Ramadhani Utengule akizungumza namna alivyopokea tanagzo la uchanguzi kama kiongozi wa kiislamu


Kasisi wa kanisa la Anglikana parishi ya Bahi Nason Mjimbu,Akielezea namna ambavyo wamepokea Tangazo la uchanguzi 

Katibu Uvccm wilaya ya Bahi Hussein Muya akizungumza namna ambavyo chama mapinduzi kilivyo jipanga katika utekelezaji wa zoezi la kujiandikisha kupiga kura .



 
 
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la FPCT Bahi
Peter  Sponga  akijitambulisha katika mkutano
 



Katibu UWT wilaya ya Bahi Hilda Mdaki akijitambulisha wakati wa  mkutano wa kikao kazi cha  wadau wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.

JKT HATUTOI AJIRA TUNATOA MAFUNZO


Na. Kadala Komba Dodoma .

JESHI la kujenga Taifa nchini JKT limesema linatoa mafunzo kwa Vijana wa kitanzania kwajili ya kujiajiri lakini halitoi ajira.

Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai
ameyaeleza hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari  kuhusu kutoa wito kwa Vijana wa Kitanzania kujiunga na mafunzo ya kujitolea Kwa Mwaka 2024.


Aidha Kanali Mrai ametoa wito kwa  Wananchi kujihadhari na matapeli ambao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kudanganya watu kuwa Jeshi la JKT linatoa ajira na kuwatapeli wananchi.

Aidha Usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 01 oktoba,2024 kwa mikoa yote Tanzania bara na visiwani,Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya Jeshi kuanzia tarehe 01Novemba,2024 hadi 03 Novemba 2024.

"Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo,unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambako mwombaji anaishi"

Aidha Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa Jeshi la kujenga Taifa kuwa halitoi ajira,pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi,Vyombo vya Ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya kiserikali,bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la kujenga taifa.

" Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz"

Sanjari na hayo Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa hiyo kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo,Umoja wa kitaifa,Ukakamavu,Kufundishwa stadi za kazi,Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.



Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai

Baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza  Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai

INEC, VYAMA VYA SIASA KUANDAA KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI

 

Na Mwandishi wetu- Dodoma
 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amesema, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushauriana na vyama vyote vya siasa itaandaa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024.
 
Mhe. Nderiananga ameyasema hayo leo tarehe 02 Septemba, 2024 katika Mkutano wa 16 Kikao cha Tano, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Neema Lugangira ambapo alitaka kufahamu ni lini kanuni za maadili ya uchaguzi zitakuwa tayari baada ya makosa ya ukatili wa Kijinsia kuongezwa kwenye Sheria za Uchaguzi mwezi Februari, 2024.
 
“Kwa mujibu wa Kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 kinaeleza kuwa, Tume baada ya kushauriana na vyama vyote vya Siasa itaandaa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi; aidha, kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 1.2 ya Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za mwaka 2020, maadili ya Uchaguzi yatatumika katika Uchaguzi Mkuu na katika chaguzi ndogo,” alifafanua Mhe. Nderiananga.
 
Aidha, Naibu Waziri huyo alieleza kwamba, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushauriana na vyama vyote vya siasa itaandaa Kanuni hizo kwa kuwa maadili mpya ya uchaguzi huandaliwa katika kila mwaka wa uchaguzi Mkuu.
 
=MWISHO=




WALIOITWA KWENYE USAILI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA BAHI PART 1

 












Naibu Waziri Ummy, Apokea jedwali la uchambuzi la Sheria Ndogo

 

Na Mwandishi wetu- DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo za Mwaka 2024 katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimewasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.

Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma Leo tarehe 16/ 08/ 2024 ambapo amesema mafanikio ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yanatokana na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na Kamati ya Bunge ya Sheria ndogo.

“Naomba niwahakikishie kamati; nimepokea jedwali hili na tutawasilisha kwa Wizara zinazohusika ili zije zilete majibu, naomba tuendele kupata ushirikiano wakati wizara hizo zitakapokuja kuwasilisha,” alisema Naibu Waziri Ummy.







TUME WATANGAZA NAFASI ZA KAZI DAFTARI LA WAPIGA KURA

 




MHE. UMMY NDERIANANGA APONGEZWA KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU

 


Na Mwandishi wetu-Kilimanjaro

Baadhi ya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Kilimanjaro wamemshukuru Mbunge wa Viti Maalum kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga kwa moyo wake wa kujitoa kuwahudumia watu wenye ulemavu.

Wakizungumza  mara baada ya mkutano wa ndani uliofanyika katika Tarafa ya Vunjo Mashariki, Wilaya Moshi Vijijini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa huo  wamesema wamekuwa wakipokea misaada ya vifaa saidizi  vikiwemo viti mwendo na fimbo nyeupe kwa wasioona kutoka kwa Mbunge huyo vinavyowasaidia kufanya shughuli zao.

Akizungumza baada ya mkutano huo mkazi wa Njiapanda Himo mwenye ulemavu  Bi. Flora Ngowi aliipongeza Serikali kwa kuendelea kupaza sauti kukemea vitendo vya baadhi ya watu wanaowaficha watu wenye ulemavu ndani akisema vitendo hivyo huwanyima fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.

“Tunamshukuru Mhe. Ummy kwa kuendelea kutusaidia sisi  watu wa Kata ya Njiapanda  kwa kutuletea viti mwendo na amekuwa akipiga kelele sana kwa wazazi au walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu kwa sababu ukishafanya vile wanajikana wakati wana vitu vingi na uwezo wa kufanya mambo makubwa,”Alishukuru Bi. Flora.

Pia mkazi wa Tarafa ya Vunjo Mashariki mwenye mtoto mwenye ulemavu Bi. Sabina Mazengo aliishukuru Serikali kwa  kuweka  miundombinu rafiki inayoweza kutumiwa katika majengo na mahali penye huduma za kijamii kama hospitali, masoko, vituo vya Daladala na shule kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Tunaomba uzidi kutupigania kwa sababu watoto tulionao hapa ni  wenye mahitaji maalum kabisa hawasikii, hawaongei na hawatembei tunajua kuna shule zao hivyo  tunaomba utusaidie waweze kwenda shule kama watoto wengine wapate haki yao ya elimu,”Aliiomba Bi. Sabina

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kundi la watu wenye ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga aliwapongeza kwa kuendelea kuwatunza watoto hao akisema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa fedha za  ujenzi wa mabweni 80 Nchi nzima kwa ajili ya watoto wenye ulemavu waweze kusoma katiika mazingira rafiki na salama.

“Mhe. Rais Dkt. Samia anatupenda sana sisi watu wenye ulemavu mwaka 2022 aliahirisha sherehe za uhuru akatujengea mabweni 80 ya watoto wenye ulemavu ili  waende shule na kina mama mfanye kazi. Ninaamini hata kama hawa watoto hawawezi kwenda shule wana vipaji hivyo ninaomba mniamini nitashirikiana na viongozi wenzangu kuhakikisha tunapata namna ya kuwasaidia nawashukuru kwa heshima mlionipa,”Alieleza Mhe. Nderiananga.

Aidha Mhe. Nderiananga alikabidhi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa  Masjid Mussa uliopo katika Tarafa ya Hai Mashariki, Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro.

==MWISHO==






“WAGONJWA WANAHITAJI FARAJA KUTOKA KWA WAUGUZI” MHE. NDERIANANGA

 


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewataka Viongozi wa Kata na Wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana kuwatambua wagonjwa waliofichwa ndani na watu wenye ulemavu ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupata huduma ya afya hatimaye kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Mhe. Nderiananga alitoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii 170 yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Apotheker Health Access Initiative kwa kushirikiana na Taasisi ya Dkt. Godwin Mollel Mbunge wa Jimbo la siha na Naibu Waziri wa Afya ambapo alisema kila mwananchi ana haki ya kupata matibabu sahihi kwa mujibu wa sheria bila kujali hali yake ikiwa ni mwenye ulemavu au hana ulemavu huku akiwasisitiza kuwa sehemu ya faraja kwa wagonnjwa badala ya kuwanyanyapaa.

Aliwahimiza kufanya kazi kwa ushirikiano hatua itakayosaidia kuwafichuwa baadhi ya wagonjwa waliofichwa ndani na kukosa matibabu pamoja na kuisaidia jamii kwa kutoa elimu ya masuala ya afya kwa lengo la kuepukana na magonjwa mbalimbali hatimaye kuwa na jamii yenye afya bora.

“Viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii nyinyi mna jukumu kubwa sana la kuhakikisha mnavumbua wagonjwa waliofichwa, aidha wagonjwa au wenye ulemavu kwani na wao wana haki ya kupata huduma, tusiwaweke ndani watoeni ili wapate msaada kwa sababu kumfungia ndani kunahatarisha afya yake na utakuwa umemfanyia ukatili,” Alisema Mhe. Nderiananga.

Naye Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alieleza kwamba ni muhimu kwa viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana katika kuhakikisha usalama wa afya za wananchi katika maeneo yao zinaimarika kwani wao ni watu wa karibu zaidi na jamii husika.

“Nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa akitoa fedha nyingi za kutekeleza miradi mikubwa ya huduma muhimu ya afya kama ujenzi wa Vituo vya Afya, hospitali za Wilaya, Mkoa na Rufaa pamoja na kutoa fedha za kununua vifaa tiba kuhakikisha wananchi wanatibiwa vizuri na kupunguza gharama ya kuwasafirisha kwenda nje ya Nchi,” Alipongeza Mhe. Dkt. Mollel.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Operesheni na Programu kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Apotheker Dkt. Angel Dillip amesema kuwa ni muda wa kuwaunganisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viongozi wa kata kwani wote wanafanya kazi eneo moja hivyo kurahisisha shughuli ya kuimarisha hali ya huduma za afya kwa wananchi endapo watakua pamoja.

Aidha Mkurugenzi wa Mipango, Maendeleo ya Biashara na Sera kutoka Apotheker Dkt. Suleiman Kimatta amewaasa viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kukabiliana na udumavu.

“Vijana balehe ni kuanzia miaka 10-19 kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa sana hususani katika kupunguza kasi ya maambukizi ya UKIMWI, Kupunguza mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia, afya ya akili na lishe kwa watoto. Viongozi mna wajibu wa kutumia mikutano yenu kuzungumzia masuala ya afya kuijengea jamii uelewa ili kuepukana na magonjwa mbalimbali,” Alieleza Dkt. Kimatta.

==MWISHO==





RAIS SAMIA APONGEZWA MIRADI YA MAENDELEO KILIMANJARO

 


Na Mwandishi wetu -Kilimanjaro

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa juhudi kubwa anazozionesha za kuruhusu kuendelea ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati kwa kutoa shilingi Bilioni 51 kutekeleza miradi katika Wilaya ya Mwanga.

Pongezi hizo zilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu  Mhe. Ummy Nderiananga wakati akiendelea na ziara yake katika Tarafa ya Mwanga, Lembeni na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Jipe-Ndea, Wilaya ya Mwanga  mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri huyo alieleza kwamba Mhe. Dkt. Samia ameendelea kujali wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu kwa kujenga mabweni 80 Nchi nzima kwa  huku akimpongeza kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mwanga na mradi mkubwa wa maji katika Wilaya mbalimbali za Mkoa huo.

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametujali sana watu wa Kilimanjaro na hapa Mwanga , kuna wakati alisema sherehe za uhuru zisifanyike na kuelekeza fedha hizo kutumika kujenga mabweni 80 Nchi nzima  kwa lengo la kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye ulemavu,”Alipongeza Mhe. Nderiananga.

Vile vile aliwahimiza wazazi na walezi wenye Watoto wenye ulemavu kuendelea kuwathamini na kuwapeleka shule ili waweze kusoma na kutimiza ndoto zao akisema wakipewa nafasi wana uwezo wa kufanya mambo makubwa katika jamii.

Mhe. Nderiananga aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpigakura na Kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi na wao  kuchaguliwa  huku akisihi wanawake kujitokeza kugombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji ili  nao washiriki katika nafasi za naamuzi.

Katika hatua nyingine  alizungumza  kwa njia ya simu na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki kufuatia uwepo wa changamoto ya Wanyama hasa tembo ambao wamekuwa wakiwajeruhi wananchi  wa Kata ya Kwakoa na kuharibu mazao yao ambapo Mhe. Kairuki aliwataka kuwa makini  kwa kufuata utaratibu ambao wamekuwa wakipewa wakati serikali ikifanyia kazi changamoto hiyo.

Kwa upande wake Afisa Tarafa-Mwanga Bi. Zawadi Mirambo alieleza kwamba wananchi wanabudi kujivunia kutokana na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao akisema Wilaya imepokea shilingi Bilioni tatu kujenga hospitali ya Wilaya ya Mwanga, ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA).

“Hospitali imeanza huduma ya (OPD) na tunaendelea kupokea vifaa ili kutoa huduma zote za kiafaya, kam ahaistoshi tuna mradi wa  Veta ambapo tuimepokea Bilioni 3 ili Watoto wetu weweze kusoma fani mbalimbali na tunamshukuru pia kwa mradi wa maji Wilaya ya Same, Mwanga na Korogwe pamoja na ujenzi wa  shule ya Sekondari Toroha,” Alifafanua Afisa Tarafa huyo.

Naye Diwani wa Kata ya Kwakoa  Bwa. Kiende Mvungi alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi Milioni  43  mwaka 2023 ili kujenga madarasa ya kupokea wanafunzi kidato cha kwanza, shilingi Milioni  77 kwa jili ya ujenzi wa madarasa shikizi.

==MWISHO==