Na. Kadala Komba Bahi
Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa
Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa ametoa wito kwa wananchi wote
wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi,kuanzia
hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura.
Hayo
yamejiri wakati wa mkutano wa kikao kazi cha wadau wa vyama vya siasa
na viongozi wa dini kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wilayani Bahi Septemba 26\09\2024 alisema kwa mujibu wa kanuni ya 27 GN. Na. 571 Kampeni za uchanguzi zitaanza tarehe 20 hadi tarehe 26 Novemba 2024 .
Aidha
Mkurugenzi Mlawa amesema kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ni
hatua muhimu inayompa kila mwananchi mwenye sifa haki ya kisheria
kushiriki uchaguzi kama mpiga kura au mgombea hivyo wananchi nawahimiza
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutumia haki yako ya kupiga kura
au kugombea nafasi za uongozi.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi amesema Ushiriki wa wananchi wengi katika
kugombea nafasi za uongozi ni muhimu katika kukuza demokrasia na
kuhakikisha upatikanaji wa viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu .
Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa
Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa akipitia tangazo la uchanguzi. |
Picha ni Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Bahi Paulina Deus Bupamba
Picha ni Shekh Ramadhani Utengule akizungumza namna alivyopokea tanagzo la uchanguzi kama kiongozi wa kiislamu |
Katibu Uvccm wilaya ya Bahi Hussein Muya akizungumza namna ambavyo chama mapinduzi kilivyo jipanga katika utekelezaji wa zoezi la kujiandikisha kupiga kura . |
Katibu UWT wilaya ya Bahi Hilda Mdaki akijitambulisha wakati wa mkutano wa kikao kazi cha wadau wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.
0 Comments:
Post a Comment