Subscribe Us

JKT HATUTOI AJIRA TUNATOA MAFUNZO


Na. Kadala Komba Dodoma .

JESHI la kujenga Taifa nchini JKT limesema linatoa mafunzo kwa Vijana wa kitanzania kwajili ya kujiajiri lakini halitoi ajira.

Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai
ameyaeleza hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari  kuhusu kutoa wito kwa Vijana wa Kitanzania kujiunga na mafunzo ya kujitolea Kwa Mwaka 2024.


Aidha Kanali Mrai ametoa wito kwa  Wananchi kujihadhari na matapeli ambao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kudanganya watu kuwa Jeshi la JKT linatoa ajira na kuwatapeli wananchi.

Aidha Usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 01 oktoba,2024 kwa mikoa yote Tanzania bara na visiwani,Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya Jeshi kuanzia tarehe 01Novemba,2024 hadi 03 Novemba 2024.

"Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo,unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambako mwombaji anaishi"

Aidha Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa Jeshi la kujenga Taifa kuwa halitoi ajira,pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi,Vyombo vya Ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya kiserikali,bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la kujenga taifa.

" Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz"

Sanjari na hayo Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa hiyo kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo,Umoja wa kitaifa,Ukakamavu,Kufundishwa stadi za kazi,Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.



Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai

Baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza  Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai

0 Comments:

Post a Comment