Subscribe Us

MIAKA 4 YA RAIS DKT. SAMIA HEKTA LAKI 7 ZATENGWA KWAJILI YA MALISHO YA MIFUGO.



Na. Anselima Komba DODOMA.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kipindi cha maika minne ya Dkt Samia Serikali imetenga hekata 7000,799.96 kwaajili ya upatikanaji wa maeneo ya malisho ya mifugo lakini kuepusha migogoro baina ya wafugaji wa watumiaji wengine wa ardhi.

Dkt Kijaji ameeleza hayo leo hii Mei 6,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akielezea mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Na kuongeza kuwa idadi hiyo ya maeneo ya malisho ineongezeka kutoka hekta 2,788,901.17 mwaka 2020/21 hadi hekta 3,489,701.13 mwaka 2024/25.

"Katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita,Serikali imeendelea kutenga maeneo ya malisho kwaajili ya kuongeza upatikanaji wa malisho ya mifugo,kuweka miundombinu stahiki ya shughuli za ufagaji na kupunguza migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.Katika kipindi hiki jumla ya hekta 700,788.96 zimetengwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali".

"Idadi hiyo imeongeza maeneo ya malisho kutoa hekta 2,788,901.17 mwaka 2020/21 hadi hekta 3,489,701,13 mwaka 2024/25".

Aidha Dkt Kijaji amesema kuwa katika kuendelea kuimarisha afya ya mifugo nchini,Serikali inatarajia kuzindua kampeni ya chanjo ya mifugo Kitaifa kati ya mwezi Mei hadi Juni 2025 ambapo jumla ya dozi 19,099,100 ,za chanjo ya homa ya mapafu ya ng'ombe zimenunuliwa na zinatarajia kuchanja jumla ya ng'ombe 19,099,100 na jumla ya dozi 17,224,200 za chanjo ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo, kwaajili ya kuchanja Mbuzi na Kondoo 17,224,200,na dozi 40,000,000 za chanjo ya ugonjwa wa kideli/mdondo,ndui na mafua ya Kuku,kwaajili ya kuchanja kuku wa asili 40,000,000.

Ambapo uchanjaji huu utaiwezesha Tanzania kukidhi masharti ya biashara ya mifugo na mazao yake kukingana na matakwa ya Shirika la afya ya Wanyama Duniani(WOAH)

Dira ya Wizara hii ni kuwa Sekta ya mifugo na Uvuvi shindani yenye kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali na kuchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi,kijamii na kimazingira ifikapo mwaka 2030.


Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiuliza maswali kuhusu serikali kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima



0 Comments:

Post a Comment