Na Moreen Rojas,
Dodoma
Serikali imetia saini ya mkataba wa upembuzi yakinifu na ununuzi wa meli za uvuvi wa bahari kuu na ujenzi wa viwanda viwili vya kuchakata samaki(kilwa na fungurefu)kupitia programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi itakayogharimu jumla ya Dola za kimarekani 77.4 millioni.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa shughuli za Serikali wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Salimu Mwinjaka wakati wa utiaji saini wa hafla hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Ngome jijini Dodoma.
Aidha programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi (AFDP)ni programu ya miaka 6 kuanzia 2021/22 hadi 2027/28 na itagharimu jumla ya Dola za kimarekani 77.4 milioni,kati ya fedha hizo,Mkopo toka IFAD ni Dola za Marekani millioni 58.8,Serikali Dola za Marekani milioni 7.8,Sekta binafsi Dola za Marekani milioni 8.5 na Wananchi Dola za Marekani millioni 2.4.
"Lengo kuu la programu ni kuwa na uzalishaji endelevu wa kibiashara na wenye kuzingatia mazingira hususani uzalidhaji wa mbegu za mazao ya kilimo(Mahindi,Alizeti,Maharagwe na Mimea jamii ya mikunde),uvuvi na ufugaji wa viumbe maji,ukizingatia uwezeshaji wakinamama na ushiriki wa vijana,programu hii inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu(SBU) na kutekelezwa na Wizara ya mifugo na Uvuvi,Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi_Zanzibar kupitia Taasisi ambazo ziko chini ya Wizara hizo ikiwa ni pamoja na TAFICO,ZAFICO,Wakala wa mbegu _ASA,Taasisi ya utafiti wa kilimo,Tanzania TARI,na Taasisi ya udhibiti wa ubora wa mbegu_TOSCI"
Aidha ameongeza kuwa programu inatarajia kuwanufaisha watu takribani 1,300,000 ikiwemo kaya za wakulima wadogo 200,000 ambao watakuwa wanapata mbegu bora za mahindi,alizeti na maharage,wazalishaji wadogo na kati wa mbegu na wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo takribani 1,000 ambao watapata mbegu bora na mafunzo,wavuvi wadogo na wafanyabishara wa samaki takribani 48,000,na wafugaji wa samaki na viumbe maji pamoja na mwani 21,000 .
"Programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi inatekeleza sehemu ya Ilani ya chama cha mapinduzi ambapo imesema wazi kuwa Serikali inakusudia kununua meli name(8) kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu ikijumuisha meli 4 kwa ajili ya TAFICO na Meli nyingine 4 kwa ajili ya ZAFICO,meli hizi zinakusudia kutumia jumla ya Tsh 30,413,275,427.00 ambapo zitanunuliwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza kutakuwa na meli tatu(3) na meli tano(5) zilizobakia zitanunuliwa katika awamu ya pili,meli hizi zinakusudiwa kuendeshwa kwa njia ya PPP"
Aidha Serikali ya Muungano wa Tanzania(SMT) na mfuko wa kimataifa wa kilimo Duniani (IFAD) zimekubaliana maeneo muhimu ya msingi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa kina kabla ya ununuzi/ujenzi wa meli hizo,maeneo hayo ni pamoja na (i)Tathmini ya athari ya kimazingira na kijamii(ESIA)kwa meli ambazo zitavua katika Bahari kuu na (ii)upembuzi yakinifu wa meli za uvuvi na bahari kuu,kazi zote hizi mbili nilazima zikamilike ndipo ununuzi /ujenzi wa meli uweze kuanza.
Sanjari na hayo upembuzi yakinifu wa awali tayari umefanyika na kubainisha kuwa meli hizi za uvuvi zitaleta tija kwenye uchumi,litaongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa,kuboresha lishe na kipato kwa wananchi mmoja mmoja hususani wale ambao wapo katika eneo la mradi,upembuzi yakinifu wa awali pia umependekeza meli hizo ziwe na urefu mita 26,hata hivyo ili kujiridhisha na matokeo haya ya awali kumekuwepo na haja kubwa na upembuzi yakinifu kamili ambapo kandadasi yake Leo ndio inategemewa kuingia mkataba na mkandarasi DMG Ltd.
"Katika eneo la upembuzi yakinifu linalenga zaidi kuangalia faida na hasara za uwekezaji tunaokusudia kwani tayari urefu wa meli Serikali imeamua uwe ni kuanzia mita 25 kwa kuangalia urefu wa meli ambazo zinavua katika EEZ yetu kutokana na Takwimu za DSFA,hivyo feasibility study itajikita zaidi kwenye kuangalia hasara na faida financial modeling kama PPP Act inavyoelekeza,hata hivyo SMT na IFAD zinekubaliana kuwa urefu wa meli maamuzi yanafanyika kupitia feasibility study ambapo pia itapendekeza msawazo wa meli pamoja na kutoa Hadidu za rejea zitakazotumika kutafuta mshiriki katika kuendesha meli hizo kwa njia ya PPP"
Kwa upande Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na UratibuDkt.Jim Yonazi programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ni ya kimkakati katika kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi, hivyo, katika zoezi hili la upembuzi yakinifu walatalisimamia kwa karibu ili kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi unaotakiwa ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zote zitakazojitokeza.
" Mkataba huu tunaoingia leo utatekelezwa kwa muda za siku zisizozidi 45 kwa gharama ya Shilingi milioni 348, ni mategemeo yangu kuwa mtafanya kazi hii kwa weledi mkubwa na kumaliza kwa wakati"Amesisitizi Dkt.Yonazi
"Ninawasihi kuwa, wakati wa utekelezaji wa zoezi hili la Upembuzi Yakinifu, mara mtakapopata changamoto yoyote, tafadhali msisite kuwasiliana na ofisi yangu kwa utatuzi wa haraka ili tuweze kukamilisha zoezi ndani ya muda tuliokubaliana, kukamilika kwa upembumbuzi yakinifu kwa wakati kutawezesha Serikali kuanza taratibu za ujenzi wa meli za uvuvi katika bahari kuu pamoja na viwanda vya kuchakata samaki,ni matarajio yetu kuwa hamtachelewesha utaratibu huo kuanza kwa wakati"Ameongeza Dkt.Yonazi
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
SERIKALI IMETIA SAINI YA MKATABA WA UPEMBUZI YAKINIFU
TENGENEZENI HISTORIA NZURI YA CHUO CHA VETA BAHI-RC SENYAMULE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka uongozi wa Wilaya na Chuo cha Ufundi stadi VETA Bahi kuhakikisha wanatengeneza historia nzuri ya chuo hicho ili kilete matokeo chanya na kiwanufaishe watu mbalimbali hususani wakazi wa wilaya hiyo na watu/ wanafunzi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Hayo yamesemwa mapema hii leo Februari 20/2024 na Mhe. Senyamule wakati alipofanya uzinduzi/ ufunguzi wa mafunzo ya ufundi stadi yaliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Chakula la Chuo hicho wakati akizungumza na wanafunzi, Walimu na wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi wa mafunzo hayo.
“Ufundi ni Ubunifu na kusoma bila vitendo bado hujawa fundi mahili sasa ili kufikia malengo ni lazima kuwa wabunifu na msome kwa vitendo ili muwe bora Zaidi na tengenezeni Misingi mizuri ya chuo chenu ili kiwe mfano wa kuigwa kwa wilaya yenu, Mkoa na Taifa kwa Ujumla na kupitia misingi mtakayoitengeneza mtakua mmeifaharisha Dodoma“,amesema Senyamule.
Naye Kaimu Msajili wa Chuo hicho Bw.Daudi J. Lyanga ameweka bayana ukubwa wa chuo hicho kuwa kina takribani hekari 52 ambazo zilitolewa na wananchi kupitia Halmashauri ya Wilaya hiyo na hadi sasa kimekamilika Katika hatua ya ujenzi na tayari kimeanza kutoa mafunzo.
Miongoni Mwa kozi zinazotolewa katika chuo hicho ni Ufundi ujenzi, uchomeleaji vyuma, Ushonaji, Uhazili na kompyuta,ufundi umeme wa majumbani na ufundi magari ambapo mpaka sasa jumla ya wanafunzi 66 wamepokelewa chuoni hapo.
Awali katika kuendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuhakikisha Dodoma inakua ya kijani Mhe. Senyamule akifuatana na viongozi wa ngazi mbalimbali wamepata fursa ya kupanda miti katika maeneo yanayozunguka chuo hicho.
MATUKIO YA PICHA Mhe. Senyamule WAKATI ALIPOFANYA UZINDUZI /UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UFUNDI STADI
ELIMU YA KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA KUTOLEWA MASHULENI.
Na Moreen Rojas
Dodoma.
Elimu ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya imeshauriwa kutolewa kunzia shuleni ili kulinusuru kundi la watoto wenye miaka kati ya kumi hadi kumi na mbili ambalo kwa siku za hivi karibuni limetajwa kuwa hatarini zaidi kwenye uraibu wa dawa za kulevya.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Kamishna wa kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo wakati akifunga mafunzo ya Programu ya TAKUKURU rafiki katika tatizo la dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Rushwa kwa maafisa waaohusika na uelimishaji umma na mawasilino.
"Tumieni mafunzo mliyoyapata kutoa elimu kwa jamii kwani tunaamini jamii ikielimika na kupata uelewa itakuwa ni rahisi kuweza kupambana na suala zima la udhibiti wa madawa ya kulevya hivyo tumeanza kwa wanafunzi ngazi za msingi,sekondari hadi vyuo vikuu hivyo kupitia klabu zao za kupambana na Rushwa watatumia pia klabu hizohizo kupambana na madawa ya kulevya ikiwa ni ajenda ya wananchi kukataa madawa ya kulevya ili kuokoa kizazi cha taifa hili" Amesisitiza Lymo.
Aidha ameongeza kuwa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) zimeamua kuungana kwani zinafanana katika utendaji kazi wake na kuamua kutokomeza kabisa madawa ya kulevya na Rushwa ambayo ni chanzo kikubwa cha kumaliza nguvu kazi ya taifa ambayo asilimia kubwa ni vijana,kuhakikisha wanatetea nchi kwani haki huinua taifa.
"Kupitia mafunzo haya naamini mmeweza kuona uhusiano mkubwa kati ya Rushwa na Dawa za kulevya kwani kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameweza kutumia Rushwa kufanikisha uuzwaji na usambazaji wa dawa hizo na kuharibu kabisa rasilimali watu na kupunguza kasi ya uchumi kwani watumiaji hushindwa kufanya kazi ipasavyo na kuwa warahibu wa dawa hizo"
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye amesema kuwa mafunzo hayo yaliyofanyika siku tatu yamewasaidia maafisa hao namna ya mbinu za kuongeza katika utendaji kazi na hususani katika programu ya kushirikisha jamii katika mapambano ya Rushwa programu mahususi ya TAKUKURU rafiki,ambapo ni matumaini yao kwamba mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kwa jamii ya kitanzania dhidi ya Rushwa na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
"Tunatarajia kuona kiwango cha ushiriki wa wananchi katika kushirikiana na taasisi hizi mbili kikiongezeka na kukuwa lakini pia ushiriki wa wadau ukiongezeka ikiwemo taasisi zisizo za kiserikali kuungana pamoja nasi katika kushiriki kuthibiti lakini pia kuzuia Rushwa na madawa ya kulevya" Ameongeza Bi.Neema