Baadhi ya viongozi nchini Tanzania wameanza kuchukua fomu za kugombea Udiwani katika kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Miongoni mwa waliotangaza nia hiyo ni EMMANUEL SALLY KAFULYA* , ambaye leo Jumamosi, Juni 28, 2025, amechukua fomu ya kugombea Udiwani kata ya Bahi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Kata ya Bahi , Kafulya amesema:"Nikiwa kama mwanachama wa CCM, nimekuja kutekeleza haki yangu ya kikatiba ya kuchaguliwa. Nimechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Udiwani kuwakilisha Kata ya Bahi
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
EMMANUEL SALLY KAFULYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KATA YA BAHI
MATHIAS LYAMUNDA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA BAHI KUPERERUSHA BENDERA YA CCM.
Na. Kadala Komba Bahi
![]() |
Haya yamejiri leo tarehe 28/06/2025 ofisi za Chama cha Mapinduzi Ccm kata ya Bahi wakati
Mathias Lyamunda Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali Foundation for Environmental Management and Campaign Against Poverty-FEMAPO, na Rais wa Rotary Club of Bahi, ambaye pia ni mbobevu wa maswala ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi, amesema Leo nimechukua fomu kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kupitia Jimbo la Bahi, Dodoma.
Aidha nikiongea na baadhi ya wananchi wa Bahi wanao mfahamu wamesema Mathias Lyamunda ni mwanasiasa maarufu na anayetajwa sana katika Jimbo la Bahi, na iwapo Chama kitampatia ridhaa atakiletea ushindi wa Kishindo.
Sambamba na hilo Mathias Lyamunda amesema kitaalama yeye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam katika fani ya Sayansi ya Siasa, Utawala wa Umma na Mazingira.
"Hivyo naamini ninayo nafasi kubwa ya kutumia uzoefu wangu wa shughuli za kimaendeleo Kitaifa na Kimataifa katika kutatua changamoto za kimaendeleo zinazo likabili Jimbo la Bahi kwasasa.
![]() |
*MKUTANO WA KIMATAIFA WA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA MWILI (ORGAN TRANSPLANTS) KUFANYIKA MWAKANI NCHINI TANZANIA CHINI YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA DODOMA*
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa Kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma wanatarajia kufanya Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya huduma za Afya za upandikizaji wa viungo vya mwili (Organ Tranplants).
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Prof. Abel Makubi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ugonjwa wa Selimundu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali hiyo ambayo kwa sasa ndio pekee nchini Tanzania inayotoa huduma ya kutibu ugonjwa wa Selimundu kwa njia ya kupandikiza Uloto kwa watoto wenye ugonjwa huo.
Mkutano huo tunatarajia utafanyika mwakani, utahusisha Wataalamu wa Kitaifa na Kimataifa ili kusaidia kukuza na kubadilishana Uzoefu, ujuzi na utaalamu na kutoa fursa ya kutangaza uwekezaji na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali katika sekta ya Afya" alifafanua Prof. Makubi.
RASMI UZINDUZI WA BIBLIA YA CHIKAGULU WAFANYIKA MOROGORO
Na. Mwandishi wetu Morogoro.
Chama Cha Biblia Cha Tanzania kwa kushirikiana na makanisa mkoani Morogoro kimefanya sherehe za uzinduzi wa Biblia ya Chikagulu, zilizofanyika katika Kanisa la Anglicana Mt Adrea Gairo, Jumapili tarehe 8
Sherehe hii iliudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, taasisi za kidini, viongozi wa dini (maaskofu , wachungaji) waumini na wanajamii (wakaguru) kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.
Katika tukio hili Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mh. Prof. Paramagamba Kabudi) aliongoza uzinduzi huo kwa kukipongeza Chama Cha Biblia kwa kuweza kuiheshimisha lugha ya Chikagulu kwa uiweka kwenye maandishi pia alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi lugha za asili za Kitanzania ambazo baadhi yake zimeanza kupotea.
Pia baadhi ya wageni waalikwa waliweza kutoa ujumbe na kuelezea furaha yao ya kupata Biblia kwa lugha ya Chikagulu. Kupitia Biblia hii, tutakuwa na Kanisa, jamii, familia na nchi yenye amani, upendo kwa sababu watu watakuwa wakimsikiliza Mungu kupitia Biblia yao; Mungu anazungumza na watu wake kwa lugha yao.
Huu ni mwanzo mpya kwa Wakagulu kuanza kumsikia Mungu kwa lugha yao ya mama!