Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WAITWA JKT

 Na. Mwandishi wetu 


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anatoa wito Kwa vijana waliohitimu elimu ya Sekondari Kidato Cha Sita kwa mwaka 2025,kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025.

Hayo yameelezwa na Kanali Juma Mrai Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT wakati akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 27 Mei 2025 Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma.

Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa Mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 28 Mei 2025 hadi tarehe 08 Juni 2025.

Aidha Vijana hao wamepangwa katika Kambi za JKT zifuatazo; JKT Rwamkoma - Mara,JKT Msenge- Tabora,JKT Ruvu na JKT Kibiti - Pwani,JKT Mpwapwa, JKT Makutupora - Dodoma,JKT Mafinga - Iringa,JKT Male - Ruvuma,JKT Mgambo na JKT Maramba - Tanga,JKT Makuyuni na JKT Orjolo - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila - Kigoma,JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa   - Rukwa pamoja na JKT Nachingwea - Lindi.

"Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana Kwa macho(Physical Disabilities) waripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo"


Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na Bukta ya Dark Bluu yenye mpira kiunoni(lastic)iliyo na mfuko mmoja nyuma,urefu unaoishia magotini,isiyo na zipu, T-shirt rangi ya kijani,Raba za Michezo zenye rangi ya kijani na Bluu,shuka mbili za kulalia zenye rangi ya Bluu bahari,soksi ndefu za rangi nyeusi,Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi,Track suit ya rangi ya kijani au Bluu,Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya juu,zikiwemo Cheti Cha kuzaliwa,vyeti vya kuhitimu kidato Cha Nne,nauli ya kwenda kuripoti makambini na kurudi nyumbani.

"Orodha kamili ya majina ya vijana hao,Makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo,inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz"

Aidha ili kufahamu Kambi kijana aliyopangiwa,atatakiwa kuingiza jina la Shule au namba ya Shule aliyohitimu elimu ya kidato Cha Sita,mbele ya jina lake la Shule ataona neno lililoandika waliochaguliwa,akichagua neno hilo ataona jina au majina ya waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa sheria kwa mwaka 2025,ikionesha kambi aliyopangiwa,Mkoa na wilaya ilipo kambi hiyo.

"Ili kuona majina yote ya vijana na Kambi waliopangiwa,mtumiaji atapakua JKT PDF 2025 iliyopo juu kulia katika ukurasa huo"

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha Vijana wote waliohitimu kidato Cha Sita mwaka 2025 kuungana na Vijana wenzao ili kujengewa uzalendo,Umoja wa Kitaifa,kufundishwa stadi za kazi,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao.





WANAOSIMAMIA MITANDAO YA SERIKALI WATAKIWA KUHAKIKISHA USALAMA WAKE

 




Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amewataka watumishi wanaosimamia akaunti za mitandao ya kijamii ya Serikali kuongeza umakini na kushirikisha  wataalam wa TEHAMA ili kupata elimu ya namna ya kuweka njia za kiusalama katika mitandao hiyo.

Msigwa amesema hayo leo, Mei 21, 2025 wakati akifungua mafunzo ya usalama wa mtandao (cyber security) yalioandaliwa na kitengo cha TEHAMA cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa watumishi wa Wizara hiyo.

Msigwa ameeleza kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya athari za matumizi mabaya ya mtandao zinatokana na uelewa mdogo wa juu ya utumiaji wa mitandao ambapo wengi hawajaweka tahadhari za kiusalama ikiwemo kutobadili taarifa za siri mara kwa mara.

Vilevile Msigwa amesema kuwa, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha usalama wa kimtandao Tanzania ikiwemo uwepo wa sheria ambazo zimetungwa ili kudhibiti matumizi holela ya kimtandao.

Ametaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 na sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao ya mwaka 2019 na kuandaa Sera na miongozo mbalimbali ya kusaidia kuhakikisha usalama wa taarifa za Serikali.

Katika hatua nyingine, Msigwa amezitaka taasisi na mashirika ya Serikali kufanya mafunzo hayo ya usalama wa kimtandao mara kwa mara kwa watumishi ili kulinda mifumo na taarifa za Serikali.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA cha Wizara hiyo, Ndg. Kulwa Magingila amewataka watumishi hao kuweka nguvu za pamoja kuhakikisha mitandao ya Serikali inalindwa na kuhakikisha wanatoa taarifa za wanaofanya uhalifu huo kwani ni ajenda ya dunia na uhalifu hauna mipaka.

DC JOACHIM NYINGO ATAKA TUZO ZA ELIMU ZIPELEKWE KWA VIONGOZI WALIO MTANGULIA

 



Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo Akizungumza na Walimu,wazazi,viongozi wa dini katika hafla ya kuwapongeza Walimu wa Shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa. 

 

Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlaw akisoma  risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo

 
Katibu Tawala wa Bahi Bi.Mwanamvua Bakari akimkaribishaMkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo akitoa pongeza walimu wa Halmashauri ya Bahi


Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Bahi Stuwart Masima akisisitiza swala la elimu na umuhimu wa elimu kwa wazazi 


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) amewataka wakina mama,vikundi mbalimbali vya sanaa kuhamasisha maswala ya elimu kupitia karama zao 


Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe.Keneth Nollo ameelezea mikakati ya elimu katika wilaya ya Bahi tusilizike kufika namba mbili kitaifa bali tuongeze juhudi mwakani 2026 tuwe namba moja 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mh George O. Fuime akijitapa kuwapita halmashauri ya bahi kielimu.


Mwenyekiti wa Alet Mkoa White Zubari ameipongeza halmashauri yawilaya ya Bahi kwa kuweka utaratibu wa kupongezana kwa kutoa zawaidi hata sisi tumekuja kujifunza kwenu hii tutachukua na kuifanyia kazi.
Zawadi Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio
Zawadi Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio

Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlawa akipokea tuzo kwa kusimamia vyema maendeleo ya elimu katika Halmashauri ya Bahi
 


Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bahi Misheni Paschal Mchewa akipokea tuzo 
Afisa Elimu ya Awali na Msingi wa Wilaya ya Bahi, Bonaface William aliyeshika tuzo akifurahi na waalimu


 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.
Mhe. Diwani kata ya Ilindi Sangula akipokea bahasha ya fedha pamoja na walimu

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.


 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.


Walimu shule za msingi Halmashauri ya Bahi

Wanafunzi wa shule ya msingi Bahi Misheni 


 

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.Diwani kata ya Bahi Mhe.Ndonu na Diwani viti maalumu  Kurusumu sambamba na mwalimu



 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio mwalimu Asifiwe  Kiula .

 
 
 
 

 Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.
Mhe. Diwani kata ya Sosthenes Mpandu na mwalimu

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bahi Misheni Paschal Mchewa akiwa na wanafunzi


Wanafunzi wa Engli Medimu
Meza kuu

Kikundi cha ngoma Chonde wakiimba wimbo maalumu wa elimu

Na. Kadala Komba Bahi 

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo alisema mimi ni mgeni kwenye hii wilaya mambo makubwa yamefanyika, yametekelezeka na viongozi wenzangu waliyo nitangulia hata hizo sifa sistahili kupata  wala hizo pongezi kwa sababu ya ugeni wangu mimi ni mgeni najifunza tu, naomba katika kujifunza kwangu mnifundishe taratibu ili niweze kuelewa vizuri na kushika vinavyopasika kushika vizuri. Zaidi ili niweze kuwa mwanafunzi mzuri katika kutekeleza majukumu yangu , hivyo naelekeza sifa zote zilizotolewa na nyimbo zilizoimbwa na kila kilichoelezwa naomba kwanza kupelekwe kwa watangulizi wangu ambao natamani wangekuwepo siku hii ya leo tuwapongeze kwa kazi kubwa waliyofanya , pia natumia nafasi hii kumpongeza Rais Dkt.   Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na ndoto zake za kuamua kuiweka Bahi kwenye ramani ya Tanzania kwa kuleta fedha na kuhakikisha kuna miundo mbinu mizuri iliyosababisha elimu iweze kupatikana.

Hayo yamejiri  Viwanja vya shule ya msingi Bahi Misheni Tarehe 10 May,2025 katika hafla ya kuwapongeza Walimu wa Shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa. Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya ya Bahi  hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ni  wadau wa elimu ambao kila mtu kwa nafasi yake  amehakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio, Katika hafla hiyo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Joachim Thobias  Nyingo.

Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlawa amesoma risala kwa mgeni rasmi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ina shule themanini na sita za msingi (86) na shule ishirini nasaba (27) za Sekondari na shule moja binafsi ya  sekondari, idadi ya wanafunzi kwa sekondari ni helfu kumi na moja mia tisa stini na tisa kwa upande wa elimu ya msingi tunawanafunzi halfu hamsini na nane mia saba thelathini na saba Mheshimiwa mgeni rasmi Halmashauri ya Bahi imepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ikiwa katika awamu hii ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.   Samia Suluhu Hassan baadhi ya mafanikio hayo ni kutoka mwaka 2021 hadi 2025 tulikuwa tunaidadi ya shule za msingi 72 hadi sasa tunashule za msingi 86 ambapo tumepata ongezeko la shule 14 mpya kwa elimu sekondari tulikuwa na jumla ya shule 21 na vipi sasa tuna jumla ya shule 27 haya ni mafanikio makubwa chini ya Jemedari wetu   Rais Dkt. . Samia tumeweza kufanikiwa .

Aidha, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo amewapongeza walimu wa Halmashauri ya Bahi mumeiheshimisha Bahi lakini mumeuheshimisha mkoa wa Dodoma kazi mliyoifanya imeonekana,sisi waalimu tunakazi mbili tu ambazo tunapimwa na jamii kazi ya kwanza ni malezi ya mtoto tunayekabidhiwa wazazi na wadau wengine wanauliza mtoto mwenye tabia hizi ametoka shule gani ? Kwaiyo idadi ya wanafunzi wenye nidhamu,heshima na adabu na mambo yote mema yanaangalia mtoto amesoma shule gani walimu ambao walimfundisha uyo mtoto ni wa shule gani ,kwa hiyo ya kwanza ni malezi kazi ambayo walimu mumeifanya hongereni sana alisema .

Naye mwalimu wa shule ya msingi Bahi Misheni Paschal Mchewa amesema mafanikio kwanza yanatoka kwa wazazi wanafanikisha watoto wanapata chakula cha mchana lakini pia wanapata uji pamoja na ushirikiano wote ndani ya Halmashauri mbali na hayo walimu wa shule ya msingi Bahi Misheni ni walimu ambao wanawajibika bila kufuatiliwa lakini kitu kingine kinacho tusaidia motisha kwa walimu tumejitahidi kutoa motisha kila mwishoni mwa mwaka tunawaona wadau wa elimu mbalimbali tunaomba fedha ,tunaomba vitu basi walimu wanapata motisha kwa kupewa vitu na fedha pia wanaenda tua mbalimbali mfano mwaka juzi tumeenda Serengeti kwa mwaka jana tumeenda Dodoma mjini mwaka huu Mei mosi nimewapeleka Dodoma mjini kupata chakula cha mchana kwaiyo motisha inasaidia sana .

Viongozi wa dini

Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Bahi Ndugu.Dastan William Mpangala awaapisha Waandishi wasaidizi na Bvr Kit Operators


 Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Bahi Ndugu.Dastan William Mpangala awaapisha Waandishi wasaidizi na Bvr Kit Operators ambao watashiriki katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kidumu la Mpiga Kura awamu ya pili ambalo litaanza Rasmi Tarehe 16/05/2025 Jimbo la Bahi ambapo kata 22 za Jimbo la Bahi zitahusika.

Zoezi hili la awamu ya pili litahusisha wale ambao hawakujiandikisha katika zoezi lilopita kwasababu mbalimbali,waliopoteza viitambulisho vyao vya kupigia Kura,kuboresha taarifa zilizokosewa,kuhamishia taarifa lakini pia kufuta taarifa watu waliofariki.

mzunguko wa pili wa  uboreshaji wa Daftari awamu ya pili na uwekaji wazi wa Daftari la awali kwa muda wa siku Saba kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 22 Mei, 2025.

Mikoa ya mzunguko wa pili ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida,

Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo  vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.

Tukio Hilo limefanyika katika Ukumbi wa Side view Wilayani Bahi
                    https://www.instagram.com/p/DJofBlWMFf_/?igsh=N2R5eTViazhkMjd6





*NAIBU WAZIRI UMMY AZINDUA MIRADI YA KIUCHUMI YA WENYE ULEMAVU*


Na Mwandishi wetu- Dar es salaam 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amezindua miradi ya kiuchumi ambayo iko chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Strategic Alternative Learning Technique (SALT), inayohudumiwa na vijana wenye changamoto za ufahamu.


Mhe. Nderiananga alifanya uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam kwa miradi ambayo ni pamoja na Salt Special Supermarket, Mgahawa na Bakery itakayohudumiwa na vijana wenye ulemavu wa ufahamu huku akisema jumla ya vijana na Watoto 83 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutoa huduma kwa wananchi hatua itakayowasaidia kujipatia kipato chao na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Aidha, Mhe. Nderiananga aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu, kujiwezesha kiuchumi na kusaidia mashirika yanayoshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu.


“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya Awamu ya Sita imeendelea kutoa fedha kwa watu wenye ulemavu ili wafanye kazi zao vizuri. Nimefurahi kuona Shirika hili la SALT linafanya kazi zake kwa ubunifu kwa kuwafundisha stadi za kazi na ubunifu wa mavazi,” alisema Mhe. Nderiananga.


Vilevile, alifafanua kwamba ikiwa kila mmoja atafanya kwa nafasi yake katika kuwawezesha watu wenye ulemavu itaongeza chachu kwao kujituma kufanya kazi kwani vipaji na uwezo wao utatambulika na kuungwa mkono hali itakayoongeza uzalishaji katika Nchi.


“Nitoe wito tuendelee kuliunga mkono Shirika hili na mengine yanayowasaidia watu wenye ulemavu wa aina zote kwani yanafanya kazi kubwa hivyo viongozi wetu wa Serikali za Mitaa tuyapokee mashirika haya na kuwapa ushirikiano kwa manufaa ya Taifa letu.

Aidha alibainisha kwamba watu wenye ulemavu wanahitaji fursa bila kunyanyapaliwa huku akiwataka wazazi na walezi kutosikiliza maneno ya kukatisha tamaa na badala yake wawaamini watoto wao kuwa wana uwezo wa kipekee.

Aliwahimiza wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kutumia fursa za mafunzo yanayotolewa katika taasisi mbalimbali ili kuwajengea Watoto kujiamini kuwa wanaweza na wanamchango katika jamii.


“Baadhi ya mafunzo yanayotolewa na SALT ni pamoja na uokaji, mapishi, mitindo ya mavazi na wahudumu katika migahawa hatua inayowajengea ujuzi wa kujipatia kipato ili kuendesha maisha hayo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Strategic Alternative Learning Technique (SALT), Bi. Rebeca Lebi alieleza kuwa Shirika hilo lilianza mwaka 2019 kwa lengo la kuwasaidia watoto na vijana wenye changamoto za ufahamu ambazo ni Usonji (Autistic Spectrum Disoder), Down syndrome, Mtindio wa ubongo (Cerebral Palsy ), Ulemavu wa akili (Intellectual Impairment) , Kifafa kikali (Severe epilepsy) na changamoto zote zinazohusiana na ulemavu wa ubongo na ufahamu.


Awali akisoma risala Meneja wa Operesheni kutoka Shirika la SALT, Bi. Jasmine Omary Iddy alisema SALT, ilianzisha chuo cha ufundi na uzalishaji (Vocational training and production) ikiwa na malengo ya kumuandaa kijana mwenye changamoto za ulemavu wa ufahamu kuweza kuwa mzalishaji kupitia mpango wa Viwanda 10 ambavyo vitazalisha bidhaa tofauti, kama vile sabuni za kuogea, shampoo, mafuta ya kupaka, vitambaa vya batiki, mikate na ufugaji wa samaki, kuku pamoja na bustani za mbogamboga.

“Kituo hiki kilianzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana wenye changamoto za kiakili na ufahamu kupata stadi za kazi, stadi za maisha na mazingira salama ya kujifunza na kushiriki katika shughuli za kiuchumi. Lengo letu kuu ni kuwapatia fursa ya kujitegemea, kuongeza thamani katika maisha yao na kupunguza utegemezi kwa familia au jamii,” alieleza Meneja huyo.

MWISHO
 

 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga Akizungumza na Wananchi wa Jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amezindua miradi ya kiuchumi




*Uchaguzi Mkuu 2025: Majimbo mapya nane yaanzishwa, 12 yabadilishwa majina*



Na. Mwandishi Wetu, Dodoma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024.

Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Kivule amabalo limegawanywa kutoka Jimbo la Ukonga na  Jimbo la Uchaguzi la Chamanzi  ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala yote ya mkoani Dar es Salaam.

“Mkoani Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba na Mkoani Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Mbeya Mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Uyole,” amesema.

Ameongeza kuwa Mkoani Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la uchaguzi la Bariadi Mjini.

Jaji Mwambegele amesema Mkoani Geita yameanzishwa majimbo mawili ambapo Jimbo la Uchaguzi la Busanda limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Katoro na Jimbo la Uchaguzi la Chato limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Chato Kusini.

“Mkoani Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Itwangi,” amesema.

Akizungumza kuhusu majimbo kumi na mbili (12) ya uchaguzi yaliyobadilishwa majina, Jaji Mwambegele ameyataja majimbo hayo kuwa ni pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Chato ambalo limebadilishwa jina kuwa Jimbo la Uchaguzi la Chato Kaskazini.

“Jimbo la Uchaguzi la Nkenge limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Missenyi, Jimbo la Uchaguzi la Mpanda Vijijini limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Tanganyika na Jimbo la Uchaguzi la Buyungu limebadilishwa jina sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Kakonko,” amesema.

Ameongeza kuwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi Vijijini, Jimbo la Uchaguzi la Manyoni Mashariki limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Manyoni na Jimbo la Uchaguzi la Singida Kaskazini limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Ilongero.

Majimbo mengine ni Jimbo la Manyoni Magharibi kuwa Jimbo la Itigi, Jimbo la Singida Mashariki kuwa Jimbo la Ikungi Mashariki, Jimbo la Singida Magharibi kuwa Jimbo la Ikungi Magharibi, Jimbo la Tabora Kaskazini kuwa Jimbo la Uyui na Jimbo la Handeni Vijijini kuwa Jimbo la Handeni.

“Kutokana na ongezeko hilo la majimbo nane, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano.  Kati ya majimbo hayo 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa  kutakuwa na kata 3,960 zitakazofanya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mwisho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele

DC JOACHIM NYINGO AKABIDHI VIFAA VYA SHULE VYA MILIONI 5.3

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Joachim Nyingo tarehe 06 Mei 2025 amekabidhi  vifaa vya Shule, Vitambaa , madaftari ,mashati

Kushoto ni DC JOACHIM NYINGO Aliyesimama ni Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Zaina Mlawa kulia ni Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara
 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) akizungumza na Mkutano
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Joachim Nying akizungumza na Mkutano


Na. Kadala Komba Bahi

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Joachim Nyingo tarehe 06 Mei 2025 amekabidhi  vifaa vya Shure, Vitambaa , madaftari ,mashati ya shule zenye  thamani ya shilingi
Milioni tano laki tatu ishirini na nne na mia nane.(50,324,800)  Katika shule ya Bahi Sekondari Kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni.

Nyingo amekabidhi vifaa hivyo wakati akipokea  taarifa ya Mfumo wa Elimu  kwa Mwaka 2025,  shuleni hapo iliyosomwa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara

DC Nyingo amempongeza Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) kwa kuendelea kusisitiza na kusimamia swala la Elimu, unahaki ya kupongezwa sana  kwenye Halmashauri yako imeweka utaratibu mzuri wa kutokumwacha mtoto  asiende shule mtoto ni tunu mpe elimu bora, naipongeza Halmashauri kwa kutekeleza ndoto ya Rais  Dkt.   Samia Suluhu Hassan ambaye ataki mwanafunzi aachwe nyuma kwa sababu elimu ni ufunguo wa maisha ,mshike sana elimu,mpende sana elimu ,mtumikie sana elimu ,mkumbatie sana elimu. Nawapongeza sana waalimu kwa ujumla wenu kwa kazi  nzuri na kubwa ambayo mnaifanya yakuendelea kuibeba elimu si tu kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Bahi bali Mkoa wetu wa Dodoma na Jamuhuri ya Muungano kwa ujumla, fedha zinazowekwa na serikali zinazoletwa na Dkt. Samia kwajili ya swala la elimu wenye dhamana ya kusimamia ni Halmashauri ikiongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya na Mkurugenzi lakini watekelezaji wa ile ndoto ya Mhe. Rais Samia ni waalimu ninawapongeza sana alisema  DC Nyingo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri hiyo Zaina Mlawa amewapongeza wanafunzi wa Bahi Sekondari kwa usafi wa mazingira na sale za shule alisema uko mbele tunakondelea tutadumisha usafi wetu hata nyumbani, kipekee niwapongeze wazazi pamoja na waalimu kwa kuitikia wito wa kufika kwenye afla hiyo nyinyi tunawategemea sana ili tuweze kuibadilisha Bahi yetu kwa videndo kwamba Serikali imedhamiria, Halmashauri imedhamiria na viongozi wamedhamiria Bahi kuipeleka mbele Bahi ki elimu .


Sambamba na hilo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Donald Mejiti ( MNEC) alisema kipaji akijui kama mzazi ana uwezo tukasema hivi vipaji vya watoto tusiviache vikapotea mtoto alizaliwa na kipaji amefaulu vizuri sisi kama Halmashauri tumsaidie mzazi wake ambaye bahati mbaya mazingira ya kiuchumi siyo mazuri nyinyi watu wa Bahi naendelea kusema wananchi wa Bahi watoto wetu wanaakili sana uwenda wewe ukujua hapo nyuma ulichukulia tu kawaida lakini watoto wetu wanaakili mwaka jana wilaya yetu ya Bahi kwenye Halmashauri 184 nchi nzima Halmashauri yetu ya Wilaya ya Bahi ilishika nafasi ya pili Tanzania nzima hili siyo jambo dogo wazazi wa Bahi alisema .

Naye Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara akitoa taarifa ya Mfumo wa Elimu  kwa Mwaka 2025, Amesema kutokana na hali duni ya kiuchumi katika familia, baadhi ya wanafunzi huacha shule kwa sababu ya kukosa mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na sare ,vifaa vya shule kama vile madaftari,kalamu pamoja na magodoro kwa wale waliochaguliwa kwenda shule za bweni.

"Divisheni ya Elimu Sekondari Bahi Annette Nara amesema Baraza la Madiwani liliona changamoto hii na kukubaliana kuanzisha mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu Bahi kwa Lengo la kunusuru wanafunzi hawa kwa mstakabali wa maisha bora kwa wananchi wetu, Mfuko huu wa kusaidia na kuboresha Elimu ulianzishwa rasmi Oktoba 2014  kwa lengo la mfuko ni kusaidia wanafunzi watokao kwenye familia duni watasomeshwa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Aidha,  Mfuko wa Elimu kwa Mwaka 2025 umefanikiwa kusaidia wanafunzi 982 (Wavulana 403 na Wasichana 579) kuendelea na masomo katika shule mbalimbali za Sekondari. Baraza la madiwani limeendelea kufanya Shule ya Sekondari ya Mudemu kuwa shule Maalumu ya Sayansi kwa kuchagua wanafunzi wenye ufaulu mkubwa waliopata daraja A waliokosa nafasi za kwenda shule za bweni za Serikali, kwa kuzingatia ufaulu huo Baraza la Madiwani liliweka utaratibu wa kuchagua wanafunzi 120 (wavulana 60 na wasichana 60) kutoka Kata zote za Wilaya ya Bahi ili kujiunga na Shule ya Sekondari Mudemu.  Pia Halmashauri imekuwa ikipeleka kiasi cha Tsh1,500,000 kila mwezi ikiwa ruzuku ya chakula kwa Wanafunzi hao .






Wanafunzi wa Shule ya Bahi Sekondari walimsikiliza Mkuu wa Wilaya Joachim Nyingo

Wazazi wa wanafunzi waliyopatiwa vifaa vya shule wakipunga mikono.