Na Mwandishi wetu- DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo za Mwaka 2024 katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimewasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.
Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma Leo tarehe 16/ 08/ 2024 ambapo amesema mafanikio ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yanatokana na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na Kamati ya Bunge ya Sheria ndogo.
“Naomba niwahakikishie kamati; nimepokea jedwali hili na tutawasilisha kwa Wizara zinazohusika ili zije zilete majibu, naomba tuendele kupata ushirikiano wakati wizara hizo zitakapokuja kuwasilisha,” alisema Naibu Waziri Ummy.
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
Naibu Waziri Ummy, Apokea jedwali la uchambuzi la Sheria Ndogo
MHE. UMMY NDERIANANGA APONGEZWA KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU
Baadhi ya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Kilimanjaro wamemshukuru Mbunge wa Viti Maalum kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga kwa moyo wake wa kujitoa kuwahudumia watu wenye ulemavu.
Wakizungumza mara baada ya mkutano wa ndani uliofanyika katika Tarafa ya Vunjo Mashariki, Wilaya Moshi Vijijini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa huo wamesema wamekuwa wakipokea misaada ya vifaa saidizi vikiwemo viti mwendo na fimbo nyeupe kwa wasioona kutoka kwa Mbunge huyo vinavyowasaidia kufanya shughuli zao.
Akizungumza baada ya mkutano huo mkazi wa Njiapanda Himo mwenye ulemavu Bi. Flora Ngowi aliipongeza Serikali kwa kuendelea kupaza sauti kukemea vitendo vya baadhi ya watu wanaowaficha watu wenye ulemavu ndani akisema vitendo hivyo huwanyima fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.
“Tunamshukuru Mhe. Ummy kwa kuendelea kutusaidia sisi watu wa Kata ya Njiapanda kwa kutuletea viti mwendo na amekuwa akipiga kelele sana kwa wazazi au walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu kwa sababu ukishafanya vile wanajikana wakati wana vitu vingi na uwezo wa kufanya mambo makubwa,”Alishukuru Bi. Flora.
Pia mkazi wa Tarafa ya Vunjo Mashariki mwenye mtoto mwenye ulemavu Bi. Sabina Mazengo aliishukuru Serikali kwa kuweka miundombinu rafiki inayoweza kutumiwa katika majengo na mahali penye huduma za kijamii kama hospitali, masoko, vituo vya Daladala na shule kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
“Tunaomba uzidi kutupigania kwa sababu watoto tulionao hapa ni wenye mahitaji maalum kabisa hawasikii, hawaongei na hawatembei tunajua kuna shule zao hivyo tunaomba utusaidie waweze kwenda shule kama watoto wengine wapate haki yao ya elimu,”Aliiomba Bi. Sabina
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kundi la watu wenye ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga aliwapongeza kwa kuendelea kuwatunza watoto hao akisema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa fedha za ujenzi wa mabweni 80 Nchi nzima kwa ajili ya watoto wenye ulemavu waweze kusoma katiika mazingira rafiki na salama.
“Mhe. Rais Dkt. Samia anatupenda sana sisi watu wenye ulemavu mwaka 2022 aliahirisha sherehe za uhuru akatujengea mabweni 80 ya watoto wenye ulemavu ili waende shule na kina mama mfanye kazi. Ninaamini hata kama hawa watoto hawawezi kwenda shule wana vipaji hivyo ninaomba mniamini nitashirikiana na viongozi wenzangu kuhakikisha tunapata namna ya kuwasaidia nawashukuru kwa heshima mlionipa,”Alieleza Mhe. Nderiananga.
Aidha Mhe. Nderiananga alikabidhi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Masjid Mussa uliopo katika Tarafa ya Hai Mashariki, Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro.
==MWISHO==
“WAGONJWA WANAHITAJI FARAJA KUTOKA KWA WAUGUZI” MHE. NDERIANANGA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewataka Viongozi wa Kata na Wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana kuwatambua wagonjwa waliofichwa ndani na watu wenye ulemavu ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupata huduma ya afya hatimaye kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Mhe. Nderiananga alitoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii 170 yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Apotheker Health Access Initiative kwa kushirikiana na Taasisi ya Dkt. Godwin Mollel Mbunge wa Jimbo la siha na Naibu Waziri wa Afya ambapo alisema kila mwananchi ana haki ya kupata matibabu sahihi kwa mujibu wa sheria bila kujali hali yake ikiwa ni mwenye ulemavu au hana ulemavu huku akiwasisitiza kuwa sehemu ya faraja kwa wagonnjwa badala ya kuwanyanyapaa.
Aliwahimiza kufanya kazi kwa ushirikiano hatua itakayosaidia kuwafichuwa baadhi ya wagonjwa waliofichwa ndani na kukosa matibabu pamoja na kuisaidia jamii kwa kutoa elimu ya masuala ya afya kwa lengo la kuepukana na magonjwa mbalimbali hatimaye kuwa na jamii yenye afya bora.
“Viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii nyinyi mna jukumu kubwa sana la kuhakikisha mnavumbua wagonjwa waliofichwa, aidha wagonjwa au wenye ulemavu kwani na wao wana haki ya kupata huduma, tusiwaweke ndani watoeni ili wapate msaada kwa sababu kumfungia ndani kunahatarisha afya yake na utakuwa umemfanyia ukatili,” Alisema Mhe. Nderiananga.
Naye Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alieleza kwamba ni muhimu kwa viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana katika kuhakikisha usalama wa afya za wananchi katika maeneo yao zinaimarika kwani wao ni watu wa karibu zaidi na jamii husika.
“Nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa akitoa fedha nyingi za kutekeleza miradi mikubwa ya huduma muhimu ya afya kama ujenzi wa Vituo vya Afya, hospitali za Wilaya, Mkoa na Rufaa pamoja na kutoa fedha za kununua vifaa tiba kuhakikisha wananchi wanatibiwa vizuri na kupunguza gharama ya kuwasafirisha kwenda nje ya Nchi,” Alipongeza Mhe. Dkt. Mollel.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Operesheni na Programu kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Apotheker Dkt. Angel Dillip amesema kuwa ni muda wa kuwaunganisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viongozi wa kata kwani wote wanafanya kazi eneo moja hivyo kurahisisha shughuli ya kuimarisha hali ya huduma za afya kwa wananchi endapo watakua pamoja.
Aidha Mkurugenzi wa Mipango, Maendeleo ya Biashara na Sera kutoka Apotheker Dkt. Suleiman Kimatta amewaasa viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kukabiliana na udumavu.
“Vijana balehe ni kuanzia miaka 10-19 kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa sana hususani katika kupunguza kasi ya maambukizi ya UKIMWI, Kupunguza mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia, afya ya akili na lishe kwa watoto. Viongozi mna wajibu wa kutumia mikutano yenu kuzungumzia masuala ya afya kuijengea jamii uelewa ili kuepukana na magonjwa mbalimbali,” Alieleza Dkt. Kimatta.
==MWISHO==
RAIS SAMIA APONGEZWA MIRADI YA MAENDELEO KILIMANJARO
Na Mwandishi wetu -Kilimanjaro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa juhudi kubwa anazozionesha za kuruhusu kuendelea ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati kwa kutoa shilingi Bilioni 51 kutekeleza miradi katika Wilaya ya Mwanga.
Pongezi hizo zilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati akiendelea na ziara yake katika Tarafa ya Mwanga, Lembeni na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Jipe-Ndea, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri huyo alieleza kwamba Mhe. Dkt. Samia ameendelea kujali wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu kwa kujenga mabweni 80 Nchi nzima kwa huku akimpongeza kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mwanga na mradi mkubwa wa maji katika Wilaya mbalimbali za Mkoa huo.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametujali sana watu wa Kilimanjaro na hapa Mwanga , kuna wakati alisema sherehe za uhuru zisifanyike na kuelekeza fedha hizo kutumika kujenga mabweni 80 Nchi nzima kwa lengo la kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye ulemavu,”Alipongeza Mhe. Nderiananga.
Vile vile aliwahimiza wazazi na walezi wenye Watoto wenye ulemavu kuendelea kuwathamini na kuwapeleka shule ili waweze kusoma na kutimiza ndoto zao akisema wakipewa nafasi wana uwezo wa kufanya mambo makubwa katika jamii.
Mhe. Nderiananga aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpigakura na Kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi na wao kuchaguliwa huku akisihi wanawake kujitokeza kugombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji ili nao washiriki katika nafasi za naamuzi.
Katika hatua nyingine alizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki kufuatia uwepo wa changamoto ya Wanyama hasa tembo ambao wamekuwa wakiwajeruhi wananchi wa Kata ya Kwakoa na kuharibu mazao yao ambapo Mhe. Kairuki aliwataka kuwa makini kwa kufuata utaratibu ambao wamekuwa wakipewa wakati serikali ikifanyia kazi changamoto hiyo.
Kwa upande wake Afisa Tarafa-Mwanga Bi. Zawadi Mirambo alieleza kwamba wananchi wanabudi kujivunia kutokana na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao akisema Wilaya imepokea shilingi Bilioni tatu kujenga hospitali ya Wilaya ya Mwanga, ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA).
“Hospitali imeanza huduma ya (OPD) na tunaendelea kupokea vifaa ili kutoa huduma zote za kiafaya, kam ahaistoshi tuna mradi wa Veta ambapo tuimepokea Bilioni 3 ili Watoto wetu weweze kusoma fani mbalimbali na tunamshukuru pia kwa mradi wa maji Wilaya ya Same, Mwanga na Korogwe pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Toroha,” Alifafanua Afisa Tarafa huyo.
Naye Diwani wa Kata ya Kwakoa Bwa. Kiende Mvungi alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi Milioni 43 mwaka 2023 ili kujenga madarasa ya kupokea wanafunzi kidato cha kwanza, shilingi Milioni 77 kwa jili ya ujenzi wa madarasa shikizi.
==MWISHO==
MBEGU BORA YA MTAMA TARISOR1 LIMA KIDOGO PATA ZAIDI
WAKULIMA wa zao la mtama wameshauriwa kutumia mbegu ya mtama aina ya TARISOR1 kwa kuwa mtama huo hauliwi na ndege kama ilivyo kwa mtama mwingine.
Mbegu ya mtama TARISOR1 ukomaa kwa siku 120. Nafasi za kupanda sm 75-90 x sm 30 panda mbegu 2, kisha ikiota ing'olei ibaki moja.
*WANANCHI WAJIONEA UTEKELEZAJI MIRADI YA GESI ASILIA NANENANE DODOMA*
📌 *Teknolojia ya Uhalisia Pepe yawa kivutio*
📌 *Elimu Matumizi ya Nishati Safi Kupikia yatolewa*
Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yamekuwa ni sehemu ya wananchi kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwemo miradi ya Gesi Asilia na Mafuta
Katika Banda la Wizara ya Nishati wananchi wameonesha kuvutiwa na teknolojia ya Uhalisia
Pepe (Virtual reality) ambayo inawawezesha wananchi kuona moja kwa moja miradi ya uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa gesi asilia iliyopo mkoani Mtwara na Lindi.
Kupitia teknolojia hiyo wananchi wameweza kuona namna gesi inavyozalishwa kutoka kwenye visima na kuingiwa kwenye mitambo ya uchakataji kisha kusafirishwa kwa bomba kwenda kwenye matumizi mbalimbali ya viwandani, kuzalisha umeme, kwenye magari, taasisi pamoja na matumizi ya majumbani.
Aidha, Wizara ya Nishati inaendelea kutoa elimu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).
WAZIRI MAVUNDE, WAZIRI MCHENGERWA KUKUTANA KUSHUGHULIKIA TOZO ZA HALMASHAURI KWENYE MADINI
Ni Kufuatia Changamoto za tozo za Halmashauri zilizowasilishwa na wachimbaji Morogoro
Waziri Mavunde awapongeza Morogoro kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli
Serikali kuongeza nguvu ya Utafiti Morogoro
Wachimbaji wamshukuru Rais Samia kwa mashine za uchorongaji
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Wizara ya Madini imekubaliana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kukutana na kutatua changamoto ya tozo zinazowekwa na Halmashauri kwa wachimbaji wa madini nchini.
Aliyasema hayo Agosti 5, 2024 Mkoani Morogoro wakati wa kikao na Wachimbaji wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji mkoani hapa.
“Nimesikiliza kwa umakini mkubwa kilio hiki cha tozo za Halmashauri na tozo nyinginezo kwa wachimbaji wadogo,kero hizi sio hapa tu zipo maeneo yote nchini," alisema Mavunde.
Aliongeza kwamba maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kuzitaka Wizara hizo mbili kukutana ili kushughulikia suala hilo.
"Nataka niwahakikishe mimi na Mwenzangu Mhe. Mohamed Mchengerwa tumekubaliana kwamba mara baada ya ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu mkoani Morogoro tutaitisha kikao cha pamoja ili kushughulikia suala hili,".
Pia, Waziri Mavunde alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wachimbaji wa Morogoro kuhusu dhamira ya Rais Dkt. Hassan kuongeza nguvu kwenye eneo la utafiti wa madini ikiwemo Mkoa Morogoro kunufaika.
Mhe. Mavunde aliipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Morogoro kwa kuvuka lengo la ukusanyaji maduhuli kufikia shilingi bilioni 4.9 zaidi ya lengo lililowekwa la shilingi bilioni 4.2bn.
Akisoma risala kwa niaba ya wachimbaji, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Morogoro(MOREMA) Dkt. Omar Mzeru, alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mashine za uchorongaji kwa wachimbaji wadogo na kutumia fursa hiyo kumuomba Waziri wa Madini kushughulikia changamoto kubwa inayotokana na uwepo wa tozo nyingi zinatozwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kwakuwa zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimapato wachimbaji wadogo.
WAKULIMA WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZAO LA MBAAZI ILONGA 14 M-2
Na. Kadala Komba Dodoma
Maonesho ya mwaka huu yaliyobeba kauli mbiu isemayo "Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, mifugo na uvuvi" yalianza tarehe Agosti 01, 2024 na yanategemewa kufika kilele Agosti 08, 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA) Aithan Chaula Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma
"Alisema kuwa mbaazi ni zao linalofanya vizuri baada ya mvua kuisha.
"Mbaazi ni zao la jamii ya mikunde, pia ni chanzo cha viini lishe vya protini kwa binadamu na wanyama, huvumilia ukame na chanzo cha mapato," alisema".
SIKU YA 4 YA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA DODOMA YANAENDELEA VIWANJA VYA NZUGUNI
Na. Kadala Komba Dodoma
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wametembelea Banda la @DASPA. Elimu mbalimbali kuhusu Mbegu bora za Mbaazi,Kunde,Uwele, Karanga na Mtama (small packs) zinatolewa bila malipo hadi tarehe 10, Agosti,Mbegu hizi mazao yake yameongezewa thamani kama vile Siagi ya karanga, mafuta na karanga za kukaanga 2024.@shinenewsblog@wizalayakilimo