Subscribe Us

WAKULIMA ZAIDI YA 400 WAMEPATIWA MAFUNZO JINSI YA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA KILIMO

 


Na. KADALA KOMBA GAIRO 

Wakulima Wilaya ya Gairo pamoja  Kongwa wamelishukuru  Shirika la DASPA Kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa kilimo  Tanzania TARI   na  shirika la kimataifa la Syngenta Foundation  sambamba na shirika la Alsem Arusha   kwa kuwapatia Elimu ya uzalishaji wa Mbegu bora za Karanga .

 Haya yamejiri wakati wa siku ya mkulima iliyofanyika katika Wilaya Gairo kijiji cha Kisitwi sambamba na Kongwa kijiji cha Laikala iliyoandaliwa na shirika la wakulima wazalishaji wa mbegu Mkoani Dodoma (DASPA)Kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa kilimo  Tanzania TARI na kituo cha Kimataifa cha uboreshaji wa Mahindi na NGano (CIMMYT),AVISA.

Mkulima kisitwi Denis Rengoliga amesema Elimu waliyopata leo kutoka kwa wawezeshaji juu kilimo cha kisasa na kutumia mbegu sahihi kwa chakula na kipata itabadilisha maisha ya wilaya hizo ambazo zimepatiwa mafunzo.




Siku ya mkulima iliyofanyika katika Kijijicha Kisitwi wilaya ya GAIRO  iliyoandaliwa na Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA) kwa kushirikiana na  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Kituo  cha Kimataifa cha Uboreshaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT), AVISA na shirika la kimataifa la Syngenta Foundation.

 


Afisa kilimo kijiji cha kisitwi Jofrey Chiduo amesema leo ni siku ya mkulima hivyo wakulima kutoka vijiji mbalimbali kikiwemo cha kisitwi wamekusanyika kujifunza kuhusu kilimo cha karanga namna ya kutumia  teknolojia za kisasa.



Bwana shamba kutoka DASPA PETER akitoa mafunzo kwa wakulima






 





Mkurugenzi Mtendaji wa DASPA, Aithan Chaula alisema kuwa  lengo la wakulima kuzalisha mbegu ni kuwawezesha wazipate kwa urahisi wakati wa msimu wa kilimo.

Alisema Shirika hilo limelipia wakulima 10 kutoka mkoa wa Dodoma na Singida ili wapate mafunzo ya uzalishaji wa mbegu bora kutoka TOSCI.

“Sheria za mbegu zinataka mkulima wa mbegu awe na shamba takribani ekari tatu kama ni kikundi lazima kuwe na ekari 10,” alisema

Mtafiti kutoka TARI Selian Arusha, Dk Papias Binagwa alisema kuwa wametoa teknolojia hiyo kwa wakulima  hususan mbegu za karanga katika Wilaya za Gairo mkoani Morogoro na Kongwa mkoani Dodoma.


 


Mwenyekiti wa DASPA, Janeth Nyamayahasi alisema kuwa  wamekuwa wakifanya tafiti shirikishi za wazalisha mbegu .

“Tulileta mbegu za aina Nne ambazo ni Tanzanut 2016 , Naliendele, Nari nut na  Tanzanite na wakulima walikuwa na mbegu za asili , mwitikio ni mkubwa, wanawake wanajitokeza sana kujifunza na kufanya tafiti kwa ajili yakupata mbegu bora zenye uhakika,” alisema










MATUKIO YA PICHA SIKU YA MKULIMA HALMASHAURI YA GAIRO MKOA WA MOROGOGORO KIJIJI CHA KISITWI





PICHA ZOTE NA KADALA KOMBA

0 Comments:

Post a Comment