Mwezeshaji wa Ushirika wenza kutoka shirika la Compassion International Tanzania Ndg. PF Maximina Goa Alisema Compassion International Tanzania (CIT) ni Shirika la Kimataifa la Kikristo lililojikita katika maendeleo na utetezi wa mtoto anayeishi kwenye umasikini. Tunatekeleza huduma hii kwa Ushirika na washirikawenza ambao ni makanisa kwa kutumia mbinu mtambuka katika kukabiliana na changamoto za maendeleo zinazowakabili watoto wanaotoka familia masikini katika jamii ya Tanzania. Dhamira, ya Compassion International Tanzania ni kushirikiana pamoja na washirikawenza katika kuwakomboa watoto kutoka katika umasikini nchini Tanzania.
Alisema sasa nyakati zimebadilika wazazi wamekuwa Adui wa watoto, wazazi wanawafanyia vitendo vya kikatili mtoto wake mwenyewe haya tunaona kwenye vyombo vya mbalimbali vya Habari mzazi anafanya vitendo vya kikatili mbaya zaidi mzazi anamkatalia mtoto asisome asiende shule ili aolewe au kusaidia kazi za nyumbani, sisi kama serikali hilo jambo alikubaliki.
Picha ya pamoja meza kuu |
PICHA ZOTE NA SHINE PRODUCTION
0 Comments:
Post a Comment