Na. KADALA KOMBA GAIRO
Wakulima Wilaya
ya Gairo pamoja Kongwa wamelishukuru Shirika la DASPA Kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania TARI na shirika la kimataifa la Syngenta Foundation sambamba na shirika la Alsem Arusha kwa
kuwapatia Elimu ya uzalishaji wa Mbegu bora za Karanga .
Haya yamejiri wakati wa siku ya mkulima
iliyofanyika katika Wilaya Gairo kijiji cha Kisitwi sambamba na Kongwa kijiji
cha Laikala iliyoandaliwa na shirika la wakulima wazalishaji wa mbegu Mkoani
Dodoma (DASPA)Kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania TARI na kituo cha Kimataifa cha
uboreshaji wa Mahindi na NGano (CIMMYT),AVISA.
Mkulima
kisitwi Denis Rengoliga amesema Elimu waliyopata leo kutoka kwa wawezeshaji juu
kilimo cha kisasa na kutumia mbegu sahihi kwa chakula na kipata itabadilisha maisha
ya wilaya hizo ambazo zimepatiwa mafunzo.
Siku
ya mkulima iliyofanyika katika Kijijicha Kisitwi wilaya ya GAIRO iliyoandaliwa na Shirika la Wakulima wazalishaji wa Mbegu Dodoma (DASPA)
kwa kushirikiana na
Taasisi ya Utafiti
wa Kilimo (TARI), Kituo
cha Kimataifa
cha Uboreshaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT), AVISA na shirika la kimataifa la Syngenta
Foundation.
Afisa
kilimo kijiji cha kisitwi Jofrey Chiduo amesema leo ni siku ya mkulima hivyo
wakulima kutoka vijiji mbalimbali kikiwemo cha kisitwi wamekusanyika kujifunza
kuhusu kilimo cha karanga namna ya kutumia teknolojia za kisasa.
|
Bwana shamba kutoka DASPA PETER akitoa mafunzo kwa wakulima
|
Mkurugenzi Mtendaji wa DASPA, Aithan Chaula alisema kuwa lengo la wakulima kuzalisha mbegu ni
kuwawezesha wazipate kwa urahisi wakati wa msimu wa kilimo.
Alisema Shirika hilo limelipia wakulima 10 kutoka mkoa wa
Dodoma na Singida ili wapate mafunzo ya uzalishaji wa mbegu bora kutoka TOSCI.
“Sheria za mbegu zinataka mkulima wa mbegu awe na shamba
takribani ekari tatu kama ni kikundi lazima kuwe na ekari 10,” alisema
|
Mtafiti kutoka TARI Selian Arusha, Dk Papias Binagwa alisema
kuwa wametoa teknolojia hiyo kwa wakulima
hususan mbegu za karanga katika Wilaya za Gairo mkoani Morogoro na Kongwa
mkoani Dodoma. |
|
Mwenyekiti wa DASPA, Janeth Nyamayahasi alisema kuwa wamekuwa wakifanya tafiti shirikishi za
wazalisha mbegu .
“Tulileta mbegu za aina Nne ambazo ni Tanzanut 2016 , Naliendele, Nari nut na Tanzanite na wakulima walikuwa na mbegu za
asili , mwitikio ni mkubwa, wanawake wanajitokeza sana kujifunza na kufanya
tafiti kwa ajili yakupata mbegu bora zenye uhakika,” alisema |
|
MATUKIO YA PICHA SIKU YA MKULIMA HALMASHAURI YA GAIRO MKOA WA MOROGOGORO KIJIJI CHA KISITWI
|
PICHA ZOTE NA KADALA KOMBA